Kuna simu za bei kubwa ambazo zilizotoka miaka ya nyuma na kwa sasa hazipatikani zikiwa mpya
Matoleo yake yalikuwa yanalenga watumiaji wanaopenda vitu vya gharama hivyo kuwa na vitu vingi vizuri
Vitu vingine havipo kwenye matoleo ya simu za miaka ya karibuni
Kwenye orodha hii kuna simu kali used za bei rahisi ambazo zilitamba miaka ya nyuma na zinaweza kutumika mpaka sasa bila tatizo
Utafahamu na bei ya kila simu
1- Apple iPhone 11
Simu ya apple iPhone 11 ni simujanja ya mwaka 2019
Ipo kwenye kundi la daraja la kwanza kwa wakati huo iliokuwa inatoka
Pamoja na kuwa ina miaka minne uwezo wa utendaji ni mkubwa
Na pia ina eSim kitu ambacho hakipo kwenye simu nyingi mpya za 2023
Pitia hapa, kujua maana ya esim na ufanyaji kazi wake
Inatumia processor yenye nguvu inayoweza kufungua kwa wepesi gemu nyingi nzito
Processor yake ya Apple A13 Bionic inazizidi simu nyingi za android mpya ikiwemo simu zote mpya za infinix 2023
Hii simu inaweza kupokea mfumo mpya kabisa wa iOS 17 hivyo maisha yake ni marefu
Bei ya iphone 11 used kwa hapa Tanzania ni shilingi 700,000 kwa ya GB 64
2- Apple iPhone 11 Pro
Simu ya Apple iPhone 11 Pro pia ilitoka miaka minne iliyopita
Kiuwezo inashindana na kuzizidi simu nyingi za android toka makampuni mbalimbali za uundaji wa simu
Inatumia chip yenye nguvu pia ya Apple A13 Bionic
iPhone 11 Pro haipitishi maji kama ikizama kwenye kina mpaka cha mita 4 kwa muda wa nusu saa
Imeundwa kwa bodi ngumu inayotumia kioo cha Gorilla
Na pia ina uwezo wa kutumia eSIM
Kioo chake ni aina cha OLED chenye HDR10 na Dolby Vision
HDR10 na Dolby Vision huboresha muonekano wa vitu kwa kuipa skrini uwezo kuonyesha rangi nyingi kwa kila pixel moja ya kioo
Kama ukitazama simu ya Redmi Note 12 ya 2023 huwezi kukuta teknolojia hii
Hivyo bei ya iphone 11 pro used imechangamka kidogo kwani infika shilingi 1,200,000
3- Apple iPhone X
Simu ya iPhone X ni ya mwaka 2017 kwa maana ina miaka zaidi ya mitano tangu itoke
Ni simu ya 4G na yenye water proof kwani inaweza kuzuia maji kupenya kwa muda wa nusu iwapo imezama kwenye kina cha mita 1
Kamera zake zinatoa picha nzuri na zinaweza kurekodi video za 4k kwa fremu 60
Yapo matoleo ya daraja la kati ya 2023 yenye kamera ambazo zinarekodi video za full hd pekee bila 4K mfano Tecno Spark 10 Pro
Hii inaifanya iphone x kuwa bado inaendana na teknolojia za sasa pamoja na umri mkubwa
Changamoto yenyewe inapokea toleo la iOS 16 haiwezi kupata iOS 17
Hata iOS 16 ni kama bado mpya maana ilikuja na iPhone 14 Pro Max hivyo uhai wake bado ni mkubwa
Bei ya iPhone X ya GB 256 ni shilingi 650,000 na ya GB 64 inauzwa laki tano
4- Apple iPhone XR
Kiubora iPhone X ni nzuri kuliko Apple iPhone XR iliyotoka mwaka 2018
Hata hivyo iPhone XR bado ni simu nzuri kwa mwaka 2023 ukilinganisha na bei yake na simu zingine za android
Kioo cha XR ni cha IPS LCD chenye resolution ya 828 x 1792 pixels
Ukiangalia ni resolution ndogo
Upande wa memori kuna ya GB 64, 128 na 256 huku RAM yake ikiwa ni GB 3
Kiuhalisia kiwango cha RAM ni kidogo ila processor yake ina nguvu kubwa
Kamera yake ipo moja ambayo kiuwezo kwa simu za sasa inaendana na simu nyingi zenye kamera nzuri za bei rahisi
Bei ya iphone xr used ya GB 64 ni shilingi 550,000
5- Samsung Galaxy S10
Samsung Galaxy S10 ni simu ya 4G ya mwaka 2019
Ni smartphone yenye memori ya GB 128 hadi GB 256 na ya GB 6 AU 8
Ina viwango vya IP68 vinavyoashilia uwezo wa kuzuia maji kuingia ndani ya simu kama ikizama
Kioo chake kina resolution kubwa na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi kwa usahihi kwani ni cha amoled
Betri yake ni ndogo kwa viwango vya sasa kwani ina 3400mAh hivyo ukaaji wa chaji sio mkubwa kivile
Kamera zake ni nzuri kutokana na uwepo wa teknolojia kama ya dual pixel pdaf inayofanya simu kulenga kitu kwa ustadi
Pia kamera za galaxy S10 zinarekodi video za 4K, na kioo chake pia kina HDR10+
Kitu kinachofanya muonekano wa vitu kuwa wa uharisia sababu ya usahihi wa kiwango kikubwa cha rangi
Inakuja na toleo la android 9 ila inaweza kupokea mpaka toleo la android 12 pekee
Hii simu inaizidi Oppo Reno7 ya mwaka 2022
Bei ya Samsung Galaxy S10 used ya GB 128 ni shilingi 600,000
6- Samsung Galaxy S10+
Simu ya Samsung Galaxy S10+ ni ya mwaka 2019 na yenyewe pia
Ina ufanano na galaxy s10 isipokuwa samsung s10 plus ni ndefu na betri yake ni kubwa na ina ubora wa ziada kwenye kamera
Na memori zake zinaenda mpaka 1TB(gb 1000)
Kamera yake inaweza kurekodi video za 4K kwa kutumia hdr10+
Uwepo wa HDR10+ inafanya muonekano wa kitu kinachopigwa picha kuwa na uharisia kwa kiwango kikubwa
Fahamu: Maana ya HDR na matumizi yake
Ukubwa wa betri ya samsung galaxy s10+ ni 4100mAh
Simu za madaraja ya kati zinaweza izidi hii simu kwenye kasi ya kuchaji
Kwani kasi ya galaxy s10 plus ni wati 15
Bei ya Samsung Galaxy S10+ used ni shilingi 650,000
7- Samsung Galaxy S10 5G
Samsung Galaxy S10 5g ndio simujanja ya kwanza kuwa na 5G mwaka 2019
Betri yake ni kubwa lenye ujazo wa 4500mAh hivyo ukaaji wa chaji ni mkubwa
Inatumia kioo cha amoled kama ilivyo kwa samsung zingine za bei kubwa
Kwenye kamera na mambo mengine inaendana na Samsung S10 Plus
Tofauti kubwa ni network kwa maana ina 5G na betri pia ukubwa wa kimo kwa sababu ina inchi 6.7
Bei ya samsung galaxy s10 5g used ni shilingi 650,000
8- Google Pixel 3
Google Pixel 3 ni simu ya mwaka 2018 kutoka kwa kampuni ya Google
Ukubwa wa betri ni 2915mAh hivyo haikai sana na chaji
Pamoja na ukweli kuwa ni simu ya kitambo ila upande wa kamera ina mfumo mzuri
Kamera ipo moja yenye megapixel 12.5 na ina teknolojia ya dual pixel pdaf inayofanya kamera kulenga kitu vizuri hata kikiwa kinakimbia
Hii kamera inaweza kurekodi video za 4K na ina OIS inayotuliza kamera wakati wa kurekodi
Kasi ya chaji ni wati 18
Upande wa memori unaweza ipata ya GB 64 au GB 128
Hii simu inakubali mpaka android 12 ambayo pia inatumiwa na baadhi ya simu za mwaka 2023
Bei ya Google Pixel 3 used kwa sasa ni shilingi 285,000, ni bei ukizingatia simu za google pixel huwa na kamera nzuri
9- Google Pixel 3a
Simu ya Google Pixel 3a ilitoka mwaka 2019 baada yaa pixel 3
Ni simu inayotumia kioo chenye ufanisi wa kuonyesha vitu kwa rangi sahihi
Hii inatokana na kioo chake kuwa cha OLED ambacho kina resolution ya 1080 x 2220 pixels
Betri yake na yenyewe sio kubwa kwani ina 3000mAh hivyo ukaaji wa chaji sio wa kiwango kikubwa
Utendaji wake ni wastani kwa sababu chip inayotumia ni Snapdragon 670
Ila ina toleo la aina moja tu upande wa memori ambayo ni GB 64
Hata Google Pixel 3a inazidiwa ubora na mtangulizi wake pixel 3
Bei ya Google Pixel 3a used ni shilingi 265,000
10- Google Pixel 4
Simu ya Google Pixel 4 ni simu iliyoingia sokoni mnamo mwaka 2019
Ni simu ya 4G ambayo kwenye kioo imewekewa kioo kigumu cha Gorilla Glass 5
Ina viwango vya IP68 vinavyoonyesha uwezo wa simu kuzia maji kupenya ndani ya simu kama ikizama
Skrini ni ya oled yenye refresh rate ya 90Hz hivyo unapotashi simu inafanya vitu kwa haraka
Kwa mara ya kwanza simu inakuja na android 10 ila inapokea Android 13 ambayo ndio toleo jipya zaidi kwa sasa
Upande wa memori kuna matoleo mawili ya GB 64 na 128 na RAM ya GB 6
Simu ina kamera mbili na zinaweza kurekodi video za 4K
Hivi ni vitu vichache ambavyo baadhi ya simu mpya za samsung hazina
Kwa sasa bei ya Google Pixel 4 used yenye GB 64 ni shilingi 400,000
Hitimisho
Kununua simu mpya kuna changamoto zake na unapaswa uzitilie maanani
Ubora wa simu used zozote bila kujali bei sio sawa na simu ikiwa mpya
Hivyo kuna uwezekano ukanunua bidhaa itakayokuja kukusumbua kama hufahamu namna ya kuchunguza
Ni vizuri ukauliza au kama huwezi matoleo mengi ya daraja la kati yanaweza kukupa vitu ambavyo vipo kwenye hizi simu za zamani za tabaka la juu
Maoni 5 kuhusu “Simu used za bei rahisi za madaraja ya kati na juu”
Nataka kununua iphone 11 pro Nini nizangatie katika kununua
Asanteni
Kikubwa owe orijino Kwa maana simu iendane na sifa halisi pia afya ya betri owe nzuri
Itapendeza sana ikiwa ni products imara sana.
nataka samsung galaxy A14 used zipo?
nahitaji google pixel 3a used ipo na mpo sehemu gani