SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Sera ya Faragha

Sihaba Mikole

SimuNzuri imejifunga kuhakikisha matumizi mazuri ya taarifa ambazo tovuti inakusanya pindi unapotembelea tovuti yetu.

Katika uendeshaji wa simunzuri.com zipo taarifa ambazo tunakusanya kwa lengo la kuboresha maudhui tunayoyatengeneza.

Tovuti zinazomilikiwa na WebAppLabs zinaheshimu taarifa za mtembeleaji.

Hakuna taarifa ya mtumiaji wa simunzuri.com itakayotumiwa kinyume ama kuuzwa.

Taarifa tunazokusanya toka kwako.

Katika uboreshaji wa huduma taarifa zifuatazo zinaweza kukusanywa.

Baadhi ya taarifa zitahitaji ruhusa yako na nyingine simunzuri.com inakusanya bila kukutaarifu.

  1. Eneo ulilopo
  2. Kifaa unachotumia kutembelea tovuti yetu
  3. Barua pepe
  4. Namba ya simu
  5. Akaunti za mitandao ya kijamii
  6. Muda unaotumia kusoma kurasa zatu
  7. IP Address

Jinsi tunavyotumia taarifa zako

Ukusanyaji wa taarifa ni wa eneo kwa ajili ya kukuletea makala nzuri zaidi.

IP Address

IP ni namba inayopatiwa kifaa chako kwa ajili ya kutumia intaneti

Ukiwa unakomenti hii namba inaonekana na inabaki katika seva zetu

SimuNzuri haitoshea namba ya IP kwa mtu yoyote

Ukusanyaji wa IP unatusaidia kuweza kujua maroboti yanayoweka komenti zisioendana na maadhui kwa maana spam

Kwa nini tunataka eneo ulilopo?

Lengo kubwa ni kufahamu eneo kwa kuzingatia idadi ya watembeleaji.

Dhumuni kuu ni kuweza kutafiti upatakinaji wa simu mbalimbali katika eneo ulipo.

Hivyo tunapoona idadi kubwa ya watembeleaji kutoka eneo fulani inatupa nafasi ya kuelezea upatikanaji wa bidhaa kwenye eneo ulilopo.

Pia inatusaidia kujua upatikanaji wa tovuti yetu maeneo mbalimbali.

Kwa nini tunataka kujua kifaa unachotumia?

Inatusaidia kujua kama simunzuri.com inafunguka vizuri kwenye aina nyingi ya vifaa.

Kwa mfano kuna baadhi ya simu hazionyeshi vizuri kurasa zetu.

Ili kurekebisha tatizo tovuti inalazimika kufahamu aina ya simu na browser unayotumia.

Tukishapata data tunaanza kuiunda upya tovuti ili iweze kufunguka vizuri kwenye simu na aina nyingine ya vifaa vya kiielektroniki.

Barua pepe, namba ya simu na mitandao ya kijamii

SimuNzuri.com itakuomba barua pepe, namba ya simu au akaunti za mitandao ya kijamii pale ambapo kuna kampeni inaendeshwa.

Ni hiyari yako kutupatia e-mail yako na namba zako za simu pamoja akaunti za mitandao ya kijamii.

SimuNzuri.com ikihitaji taarifa hizi itakuomba ruhusa yako.

Ukikataa wala haitokulazimisha.

E-mail unayotupa haitotumika popote mbali na tovuti yetu

Unaruhusia kusitisha huduma yoyote ambayo inakutumia messeji kwenye barua pepe au kwenye namba yako.

Taarifa zako zote zinahifadhiwa kwenye server salama yenye ulinzi madhubuti.

Kama ukiandika maoni kwenye kurasa zetu utahitajika kutumia email yako

Email zinabaki kwenye database zetu

Kwa nini tunataka kujua muda unaotumia kwenye tovuti yetu?

Muda unaotumia kusoma makala zetu unatujurisha ubora wa maudhui yanayoandikwa na SimuNzuri.com

Tunapoona umetumia muda mfupi kwenye kurasa zetu tunajiuliza kwa nini?

Swali linalotulazimisha kutathmini kiundani tovuti yote na mada zake.

Tathmini inayotupa majibu wapi pa kurekebisha.

Kwa mtindo huo simunzuri.com inakuwa inatengeneza maudhui yanayokidhi mahitaji ya msomaji.

Cookies

Cookie ni mafaili yanayohifadhiwa kwenye kompyuta.

SimuNzuri.com inatumia cookies kukusanya takwimu za mtembeleaji.

Pia simunzuri.com inaweza kufanya kazi mfanyabiashara(advertiser) anayetumia cookie.

Cookie ambazo zimehifadhiwa kwenye kompyuta yako au simu inasaidia tovuti kukuwekea matangazo yanayoendana na kile ambacho unapendelea.

Baadhi ya cookie za simunzuri.com zinatoka Google Analytics.

Google Analytics na Google search console zinasaidia kukusanya taarifa ambazo tovuti yetu inazihitaji kwa ajiri ya kuboresha huduma zetu.

Unaweza kusitisha cookie wakati wowote kwenye browser unayotumia.

Kwa mtumiaji wa chrome, jinsi ya kuzima cookie

Tovuti ya nje

Pindi usomapo makala zetu unaweza ukakutana na linki zitazokupeleka kwenye kurasa zingine.

SimuNzuri.com haina mamlaka juu ya aina ya taarifa zinazokusanywa na tovuti za nje ya simunzuri.com

Ni vizuri ukasoma sera za faragha za tovuti husika.

SimuNzuri.com haitohusika na uharibifu wa aina yoyote utakaofanywa na tovuti ambayo link yake umeikuta humu

Zingatia

Sera zetu za faragha zinaweza kubadilika wakati wowote bila kukutaarifu

Tunaomba, msomaji wetu kupitia ukurasa huu mara kwa mara upatapo nafasi

Maboresho

Kwa sasa tunakusanya mpaka namba za whatsapp pindi ukiwasiliana nasi

Endapo ukipewa namba ya muuzaji simu kutoka kwetu hatutohusika na lolote kati yako na muuzaji

Ni vizuri ukawa makini kabla ya kutoa hela

Mawasiliano

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 624 21 30 48

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company