SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Orodha ya Simu Mpya za Infinix na bei zake 2023

Brand

Sihaba Mikole

July 4, 2023

Kwa mwaka 2023 infinix wameingiza matoleo mapya ya simu zipatazo tisa

Matoleo hayo yamegawanyika katika makundi kama matatu kwa kuzingatia bei zake na ubora wake

Utakutana na infinix zenye ubora wa chini, kati na ubora wa juu

Hivyo kwenye hii orodha kuna simu mpya za infinix za mwaka 2023 na bei zake kwa Tanzania

Infinix Note 30 Pro

Infinix note 30 Pro ni simu ya daraja la kati ambayo imetoka mwezi mei

Ina urefu wa inchi 6.67 na ina kioo kizuri aina ya amoled chenye refresh rate ya 120Hz

Hii ni simu inayoweza kuchaji kwa njia ya wireless kwa maana unachaji simu bila kutumia waya wa usb

infinix note 30 pro software

Fahamu Zaidi: Ubora na uwezo wa infinix note 30 Pro

Kamera yake ina lenzi kubwa ya megapixel 108 na upigaji wa picha ni wa kuridhisha

Betri yake inakaa na chaji muda mrefu kwani ukubwa wake ni 5000mAh

Na pia inakuja na chaji yenye wati 68 inayoweza kujaza simu kwa 80% ndani ya nusu saa

Bei ya Infinix Note 30 Pro

Kwa Tanzania simu inauzwa kiasi cha shilingi 700,000/=

Kwa maeneo mengine inaweza kupatikana chini ya bei tajwa

Bei yake inaendana na ubora wa simu kiujumla

Infinix Note 30

Simu ya Infinix Note 30 imetoka pamoja na note 30 pro kwa maana zote ni za mwezi mei

Utendaji wa note 30 ni wa wastani kwa sababu inatumia processor ya Helio G99

Ina kio aina ya IPS LCD chenye refresh rate inayofika 120Hz

Ubora wa kamera sio mkubwa sana kama simu iliyotangulia

 

Kasi ya chaji ni wati 45 na yenyewe inajaza  betri yake ya 5000mAh ndani ya muda mfupi

Unaweza kupata infinix ya GB 128 au ya GB 256 kwenye upande wa memori

Hii ni simu ya 4G, haina 5G kama ilivyo kwa note 30 5g

Hapa, kuna maelezo ya kina kuhusu infinix note 30

Bei ya Infinix Note 30

Infinix Note 30 ya GB 256 inapatikana kwa kiasi cha shilingi laki sita

Kama hiki kiwango ni kigumu kulipa kwa mkupuo yapo maduka ambayo yanakopesha

Ila lazima utoe kianzio ili ukopeshwe

Infinix Note 30 5G

Simu nyingine ya Infinix iliyotoka mwezi mei mwaka 2023

Ni simu ya 5G

Kwa haraka haraka unaweza kudhani Infinix note 30 5G ni bora zaidi kutokana na utendaji mkubwa kuliko infinix note 30 pro

Kiuhalisia infinix note 30 pro ni nzuri zaidi

Kwa sababu note 30 5G inatumia kioo cha ips lcd, ina kamera yenye megapixel 64

infinix mpya 2023 note 30 5g

Inakuja na chaji yenye wati 45 ambayo inajaza betri kwa muda mfupi pia

Ila haina mfumo wa kuchaji simu bila kutumia waya

Bei ya Infinix Note 30 5G

Bei ya Infinix Note 30 5G ni shilingi 450,000/= kwa hapa Tanzania

Simu nyingi za 5G bei huanzia laki nne, hizi ni zile zenye kiwango cha kawaida

Infinix Note 30 VIP

Katika matoleo ya note 30 toleo la infinix note 30 VIP ndio toleo bora zaidi

Kwani infinix note 30 vip inatumia processor yenye nguvu kubwa hivyo inaipa uwezo wa ziada

Kwa mfano kamera yake inaweza kurekodi mpaka video za 4K ambazo huo na muonekano mzuri na uliokorea vizuri

Na yenyewe ina mfumo wa wireless chaji kwa maana kuchaji bila kutumia waya

Kasi ya wireless chaji ni kubwa sana humu kutokana na uwezo wa kupeleka chaji kwa wati 50

Hii inafanya simu iweze kuchaji kwa 50% ndani ya nusu saa

Chaji nyingi za wireless huwa zinapeleka kiwango kidogo ila infinix wamejitahidi

Kiufupi simu ina vitu bora vingi na hii ni simu nzuri zaidi ya infinix mpaka sasa

Unaweza kuijua zaidi kwa kutazama hii video ya Youtube.

Bei ya Infinix Note 30 VIP

Kwa kuwa ubora wa infinix note 30 vip unazizidi simu nyingi zilizopo humu hivyo bei yake lazima iwe kubwa kiasi

Infinix Note 30 VIP inauzwa kwa shilingi 860,000 ya GB 256

Kwa kuringanisha simu na bei naweza nikasema ni bei rafiki kwa kiasi kikubwa

Infinix Hot 30

Infinix Hot 30 ni simu yenye uwezo wa wastani ambayo imetoka mwezi machi 2023

Ina jumla ya kamera zipatazo mbili ambapo kubwa ina megapixel 50 ila kiubora wa picha sio wa kiwango kikubwa

Betri lake ni kubwa lina 5000mAh

infinix hot 30 showcase

Chaji yake inapeleka umeme wa wati 33 ambayo inajaza simu kwa 50% ndani ya nusu saa

Inatumia kioo cha ips lcd chenye refresh rate ya 90Hz

Na pia inakuja na android toleo la 13 ambalo bado ni jipya kwani android 14 bado haijatoka rasmi

Bei ya Infinix Hot 30

Infinix Hot 30 ya GB 256 kwa Tanzania inauzwa kwa shilingi 450,000

Hata hivyo kuna toleo moja tu upande wa memori ambalo lina RAM ya GB 8 na memori ya GB 256

Infinix Hot 30i

Hii ni simu nyingine ambayo imetoka mwezi machi pamoja na hot 30

Simu mbili zina ufanano wa kiwango kikubwa utofauti upo kwenye sehemu chache

Hot 30i ina kamera yenye kiwango cha chini na ukubwa wake ni megapixel 13

Pia inatumia android 12 na hakuna uhakika wa kupata toleo lifuatalo la android 13

infinix hot 30i showcase

Memori yake ni GB 128 na RAM yake ni GB 4

Ni ndogo ukilinganisha na hot 30 lakini bado upo uwezekano wa kuhifadhi mafaili mengi ya kutosha

Pia chaji ina kasi ya kawaida ambayo umeme wake ni wati 18

Bei ya Infinix Hot 30i

Kwa kuwa tayari umeona kuna vitu vimepunguzwa hivyo bei yake hii ni ndogo zaidi

Infinix Hot 30i inauzwa kwa kiasi cha shilingi 350,000 kwa Tanzania

Infinix Hot 30 play

Unataka simu yenye betri kubwa sana lenye 6000mAh bila kujali mambo mengine?

Basi Inifinix Hot 30 Play inakupa suruhisho hilo

Hivyo utakuwa na simu inayokaa na chaji kwa muda mrefu kama sio masiku

hot 30 play

Kiutendaji simu haina nguvu kubwa kwani processor yake ni ndogo ambayo ni Mediatek Helio G37

Kioo chake kina reslution ndogo ya 720 x 1640 pixels na aina ya IPS LCD ila refresh rate yake inafika 90Hz

Pia inatumia toleo la sasa la android ambayo ni android 13

Na chaji yake inapeleka umeme wa kiwango cha wastani cha wati 18

Bei ya Infinix Hot 30 Play

Bei ya Hot 30 Play kwa hapa Tanzania ni shilingi 380,000/=

Kiuhalisia hii inaizidi kidogo hot 30i

Infinix Smart 7

Simu ya infinix smart 7 iliingia sokoni mwezi wa pili mwaka 2023

Hii ni simu ya daraja la chini hivyo haina vitu vingi vizuri kama ilivyo kwa matoleo ya note na hot

Utendaji wa smart 7 ni mdogo kwa sababu inatumia processor yenye nguvu ndogo

Kamera zipo mbili na inarekodi video za full hd

Ila kiubora wa kamera ni kiwango cha kawaida kama sio cha chini

Ina betri kubwa na inakaa na chaji masaa mengi kwa sababu simu haitumii nguvu kubwa

Ila chaji yake inapeleka kiwango kidogo cha umeme wa wati 10

Kwa maana tegemea betri kuchukua masaa mengi mpaka kujaa

Bei ya Infinix Smart 7

Infinix Smart 7 ni infinix ya bei nafuu kwenye hii orodha iliyopo

Inauzwa shilingi 220,000/= hapa Tanzania

Ni simu inayofaa kwa mtumiaji anaejali matumizi ya chaji

Infinix Smart 7 Plus

Simu nyingine yenye betri kubwa ya 6000mAh ni Infinix Smart 7 Plus

Hii simu inafanana vitu vingi smart 7

Hivyo hakuna vitu vingi vya kuvifafanua kiundani

Kwani pia ni simu ya kundi la daraja la chini

Bei ya Infinix Smart 7 Plus

Bei ya Infinix Smart 7 Plus ya GB 3 na memori ya 64 ni shilingi 210,000/=

Bei hazitofautiani sana

Hitimisho

Una machaguo tisa upande wa infinix kwa mwaka 2023

Uchaguzi wa moja ya simu itategemeana na kiasi cha pesa kilichopo mfukoni

Ukiwa na bajeti ya kutosha unapata infinix nzuri tofauti na apo utapata infinix ya kusukuma siku

Kubwa zaidi ni aina ya matumizi ndio itakupa muongozo wa simu ipi ya infinix ya kununua mwaka 2023

Maoni 17 kuhusu “Orodha ya Simu Mpya za Infinix na bei zake 2023

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

infinix mpya thumbnail

Simu za Infinix zinazotamba na bei zake (2024)

Mwishoni mwa mwaka 2023 na mwanzoni mwa 2024 kuna matoleo mapya ya infinix yalitoka Matoleo hayo mengi ni ya daraja la kati na la chini yaani yamegusa kila mtu kulingana […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

No Featured Image

Bei ya Infinix Hot 40 Pro na Ubora wake

Simu ya Infinix Hot 40 Pro ni simu janja ya daraja la kati ambayo imetoka pamoja na simu ya infinix hot 40 Hot 40 Pro ina ubora wa ziada kwenye […]

infinix hot 40

Bei ya Infinix Hot 40 na Sifa Zake Muhimu

Kuelekea mwishoni mwa mwaka 2023 infinix walitoa toleo jingine la simu aina ya Infinix Hot 40 Hili ni baada ya toleo la infinix hot 30 ambvalo limetoka mwaka 2023 pia […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram