SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ubora wa simu mpya za Infinix Note 50

Simu Mpya

Sihaba Mikole

April 29, 2025

Katika baadhi ya nchi, Infinix walitoa toleo jipya la Infinix Note 50

Matoleo hayo ni

  1. Infinix Note 50 4G
  2. Infinix Note 50s
  3. Infinix Note 50 Pro 4G
  4. Infinix Note 50 Pro+ 4G
  5. Infinix Note 50 Pro+

Na kwa Tanzania simu hizi zinaweza kuja kuzinduliwa muda si mrefu

Kwani hizi zilitangazwa mnamo mwezi machi 2025

Sio mbaya tukapitia sifa za muhimu na ubora uliopo kwenye kila infinix mpya

Infinix Note 50 4G

Infinix Note 50 4G ni infinix ya kamera mbili ambapo kamera kubwa ina megapixel 50 na pia ina OIS

Utendaji wake ni wa wastani kutokana na kutumia chip ya Mediatek Helio G100 Ultimate

Betri yake ina ukubwa wa 5200mAh ambayo inahifadhi umeme mwingi

infinix note 50 4g

Hii simu inasapoti chaji inayopeleka umeme mwingi wa wati 45

Hivyo betri haitochukua muda mrefu kujaa

Itapata matoleo mapya ya android kwa muda wa miaka miwili yaani itapokea Android 17

Infinix Note 50s

Infinix Note 50s inakuja na kamera mbili kubwa ikiwa na megapixel 60 yenye uwezo wa kurekodi video za 4K

Inasapoti mtandao wa 5G, na utendaji wa simu unaweza kufanya vitu vingi vikubwa

Kwani inatumia chip yenye utendaji mkubwa ya Dimensity 7300 Ultimate

infinix note 50s

Pia chaji yake inakubali umeme wa wati 45

Upande wa software inatumia Android 15 na itapokea matoleo mengine kwa miaka miwili mfululizo

Infinix Note 50 Pro 4G

Infinix Note 50 Pro 4G ina kamera mbili tu kubwa ikiwa na megapixel 50

Utendaji wake ni wa wastani kutokana na kutumia processor ya Mediatek G100 Ultimate

Na yenyewe itapata matoleo mapya ya android kwa miaka miwili mfululizo

-infinix note 50 pro

Upande wa chaji simu inakuja na chaji yenye kasi kubwa

Kwani inasapoti chaji ya wati 90, ambapo simu haitochukua dakika nyingi kujaa

Pia ukubwa wa betri yake ni 5200mAh

Infinix Note 50 Pro+

Katika orodha ya matoleo mapya ya Infinix kwa 2025, hii ndio simu bora zaidi

Inakuja na processor yenye nguvu kubwa kiutendaji

Na ina kamera tatu ambapo kamera zina megapixel 50 na nyingine ina megapixel 8

infinix note 50 pro+

Chaji yake inasapoti umeme wa wati 100

Ambao unaweza kujaza simu kwa dakika 30 tu

Betri ni kubwa pia kwani ukubwa wake ni 5200mAh

Maoni 10 kuhusu “Ubora wa simu mpya za Infinix Note 50

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

Ifahamu RAM ni Nini na Inatumikaje kwenye simu

Ukitaka kununua simu kitu kimojawapo utakachoambiwa ni ukubwa wa RAM Utasikia ukubwa wake ni GB 128 na RAM GB 8. Kwa asiyefahamu anaweza kujiuliza RAM ni nini na ina msaada […]

No Featured Image

Bei ya Tecno Spark 50 Pro na Sifa Zake Muhimu

Tecno Spark 50 Pro imekuja na vitu viwili vya kipekee Na ndicho kinachotengeneza utofauti na toleo la tecno spark 40 pro Ila kwa jicho la haraka unaweza kudhani sifa za […]

thumbnail

Bei ya Infinix Hot 70 na Sifa Zilizoboreshwa

Infinix Hot 70 imeundwa katika muktadha wa kuifanya iwe na bei ndogo Ni simu nzuri kutigemeana na aina ya matumizi Kwa sifa zake wapo watakaoona hii simu inawafaa Ila wanaotaka […]

infinix mpya 2026

Simu zote mpya za Infinix na bei za kustaajabisha (2026)

Kuna bei za infinix mpya zinafikirisha Maana zimekuja kitofauti sana kwa namna simu za Infinix zilivyozoeleka Maana kuna infinix inayoenda hadi milioni mbili na nusu kwa Tanzania Ila sifa za […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company