Infinix Hot 70 imeundwa katika muktadha wa kuifanya iwe na bei ndogo
Ni simu nzuri kutigemeana na aina ya matumizi
Kwa sifa zake wapo watakaoona hii simu inawafaa
Ila wanaotaka simu iwe kamili kweli Infinix Hot 70 inaweza isiwavutie
Maana bei yake ukilinganisha na simu zingine za bei ya kundi lake inaleta maswali kidogo
Bei ya Infinix Hot 70 ya GB 128
Kwa Tanzania Infinix Hot 70 ya GB 128 inauzwa shilingi laki nne (400,000)
Hii ikiwa na ukubwa wa RAM ya GB 8
Kuepuka simu kuwa nzito mbeleni RAM kubwa itakuokoa
Zipo mpaka za RAM ya GB 4 ila simu zinaambatana na mifumo mingi ya AI
Hii mifumo hutumia memori nyingi kufanya kazi
Tazama sifa zake kamili zote uone maboresho kama yanastahili laki nne
Sifa za Infinix Hot 70
| Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
|---|---|
| Network | 2g, 3g, 4g |
| Processor(SoC) |
|
| Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
| Softawre |
|
| Memori | 128GB, 256GB na RAM 12GB, 8GB |
| Kamera | Kamera mbili
|
| Muundo | Urefu-6.78inchi |
| Chaji na Betri |
|
| Bei ya simu(TSH) | 400,000/= |
Uwezo wa network
Infinix Hot 70 inatumia mtandao wa 4G
Inasapoti laini mbili lakini haiji na laini za eSIM
Kwa maana utalazimika kutumia laini tu hizi za kawaida
Pia kama 4G iko imara, hii simu inaweza kupakua app ndani ya muda mchache
Yaani kama una-download gemu ya GB 1, ndani ya sekunde 13
Siri ni kuwa 4G yake ni LTE Cat 13 ila ni nadra hiyo spidi kufikiwa kama hakuna 5G kwa hapa Tanzania
Ubora wa kioo
Kutokana na ukweli kuwa hii sio simu ya daraja la kati, basi ubora wa kioo sio mkubwa
Kwani inatumia kioo cha IPS LCD na sio kioo cha AMOLED
AMOLED huwa inaonyesha vitu vizuri na kwa rangi zenye kina kikubwa
Bahati mbaya resolution imekuwa ni ndogo ukilinganisha urefu wa skrini
Resolution yake ni 720p, urefu wa kioo ni 6.78 hivyo muonekano wa vitu unakuwa na changamoto kidogo
Hata hivyo refresh rate 120Hz inaifanya kioo na uharaka na mwitikio mkubwa unapotachi
Nguvu ya utendaji
Utendaji wa Infinix Hot 70 ni wa wastani
Ila ina uwezo wa kusukuma vitu vingi kama magemu makubwa
Hii inatokana na kutumia chip ya mediatek helio g100
Hata hivyo sio nzuri kufungua mafaili mengi kwa wakati mmoja
Lakini RAM kubwa na mfumo wake wa memori wa UFS unaiongezea spidi kiasi fulani
Uimara wa bodi
Uimara wa bodi wa Infinix Hot 70 upo katika kuzuia maji
Ni yale maji ya kiwango cha kutililika
Ikizama kwenye maji ya kutulia na kina kirefu simu itaharibika
Pia ustahimilivu wa kutopasuka ni pale ikiangua kwenye kimo cha usawa wa kiuno cha mtu mzima
Na hapo inategemea na eneo inapoangukia
Yote ya yote umakini wa kina unahitajika
Ubora wa kamera
Simu ina kamera mbili
Kamera yake kubwa ina megapixel 50
Na inajitahidi kiasi fulani kupiga picha vizuri
Katika kurekodi video inaweza kurekodi mpaka video za 1444p (full hd+)
Ukitazama video za full hd+ muonekano wake ni mzuri na unaweza usione tofauti na 4K
Ila kama una tv ya 4K ndio utaona video ya 4K ilivyo nzuri
Tofauti na hapo unaweza usione utofauti wowote
Uwezo wa betri na chaji
Hii simu ina betri kubwa yaani unaweza simu karibu masaa 15 ukiwa kwenye intaneti
Betri yake kubwa inaweza kuchelewa kujaa kama chaji ina spidi ndogo
Uzuri Infinix Hot 70 inakuja na chaji ya wati 45
Hii ni fast chaji, hivyo chini ya dakika 90 simu inajaa
Kwa mantiki hiyo utakuwa ni mizunguko michache ya kuchaji simu
Unajua simu ukiwa unaichaji mara kwa mara huwahi kuharibika
Ubora wa software
Simu inakuja na mfumo endeshi wa Android 16
Huu mfumo unafanya kazi pamoja na XOS 16
Kubwa zaidi ni matumizi ya AI
Ambapo kwenye hii simu imeunganisha mifumo ya gemini, chatgpt, deepseek nk
Kwa hiyo unakuwa unachagua moja wapo unapouliza maswali
Simu Mbadala
Mshindani wa kwanza wa infinix hot 70 ni Infinix Hot 60
Kwa maelezo zaidi pitia hii post: infinix hot 60 vs Infinix Hot 70
Lakini pia hii simu inaingia kwenye ushindani na Samsung Galaxy A07, Tecno Spark 50 na Redmi 15C
Neno la mwisho
Uwekezaji wa AI umechangia sana ongezeko la bei za simu
Miundombinu ya AI inakula kiwango kikubwa cha memori
Hivyo memori zimepanda bei
Ukiangalia bei ya Infinix Hot 70 safari hii imekuwa kubwa
Tofauti na ilivyotoka Infinix Hot 60