Bei ya Tecno Spark 50 imeongozeka kuliko hata Spark 40 ilipotoka
Kwa nini?
Kuna sifa mpya mbili ambazo hazipo kwenye toleo lilopita
Vitu vipya ni vichache ila vinatengeneza utofauti mkubwa
Kiuhalisia hata kwa mtumiaji wa Tecno Spark 40 anaweza kuona tofauti
Hii ndio bei yake kwa Tanzannia
Bei ya Tecno Spark 50 ya GB 128
Kuipata hii simu inakulazimu uwe na takribani laki nne (400,000)
Bei hii inakupa Spark 50 ya ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 4
Zipo matoleo yenye ukubwa wa GB 256 na RAM GB 8
Hizi bei zake ni kubwa zaidi ambayo ni shilingi laki tano
Hivyo unapaswa kutathmini mahitaji yako ujue bajeti na mahitaji yako
Sifa za Tecno Spark 50
| Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
|---|---|
| Network | 2g, 3g, 4g |
| Processor(SoC) |
|
| Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
| Softawre |
|
| Memori | 128GB, 256GB na RAM 4GB,6GB, 8GB |
| Kamera | Kamera moja
|
| Muundo | Urefu-6.78inchi |
| Chaji na Betri |
|
| Bei ya simu(TSH) | 400,000/= |
Kwenye sifa zote ni sifa mbili pekee zimeleta utofauti mkubwa
Tuanze na sifa hizo MBILI halafu tuendee inayofuata
Utendaji
Utendaji wa Tecno Spark 50 umeiacha mbali Spark 40
Tofauti ya utendaji imeonekana hata kwa matoleo mapya ya Infinix
Tofauti ya uharaka unapotumia hii simu utaiona kama unatumia Spark 40 au Spark 30
Utendaji wa ziada unaletwa na kutumika chip ya Mediatek Dimensity 6400
Hata ukitazama app za kupima ubora, utofauti ni wa kiwango kikubwa
Na sifa inaambatana na ukaaji wa chaji
Ukubwa wa Betri
Ukubwa wa betri ya Tecno Spark 50 ni mAh 6500
Betri ya aina hii inaweza kukaa na chaji kwa takribani masaa 14
Kama muda mwingi upo kwenye intaneti simu hii inafaa
Uwezo wa chaji umebaki vile vile
Kwa maana chaji inaweza kupeleka mpaka hadi wati 45
Muda wa kujaa chaji unatofautiana na spark 40
Spark 40 inawahi wakati Spark 50 inachelewa kwa sababu betri lake ni kubwa
Uwezo wa network
Spark 50 ni simu ya 4G
Japokuwa chip yake inakubali 5G ila hii simu haijawekewa
5G inahitajika kama unapenda kucheza gemu mtandaoni na unapenda kupakuwa vitu vingi sana
Maana spidi ya 5G huwa ni kubwa
Lakini kwa kazi ya kuperuzi na kuangalia video mtandaoni bado 4G ni chaguo sahihi kwa sasa
Na ukizingatia ni simu inayomlnega mtumiaji wa matumizi ya kawaida
Ubora wa kioo
Kioo cha Tecno Spark 50 hakina mkolezo mkubwa wa rangi
Kwa maana inatumia kioo cha IPS LCD na sio AMOLED
Vioo vya amoled huwa na kina kikubwa cha rangi
Hivyo muonekano wa vitu unakuwa na uangavu mzuri zaidi
Faida ya kioo cha IPS LCD havina bei kama kikiharibika
Hata hivyo kwa sasa ni nadra simu ya laki nne kuwa na kioo cha amoled
Ubora wa kamera
Tecno Spark 50 ina kamera moja pekee
Na kamera hiyo ina megapixel 50
Upigaji wa picha ni kuridhisha
Na katika mazingira ya mwanga mwingi muonekano wa vitu ni mzuri pia
Kwa bahati mbaya kamera yake inarekodi mwisho wa video za full hd+
Uimara wa simu
Simu ni himilivu kama ikianguka kwenye kimo cha mita 1.5
Kwa maana simu ikianguka usawa huu kioo chake kinaweza kisiharibike
Pia ina waterproof inayoainishwa na uwepo wa cheti cha IP64
Inamaanisha ina uwezo wa kuzuia maji ya kiwango cha kutiririka
Ila kama ikizama kwenye maji mengi simu inaharibika ndani ya muda mfupi
Kwa namna yoyote unalazimika kuwa muangalifu ili simu iwe idumu muda mrefu
Ubora wa software
Tecno Spark 50 inakuja na mfumo endeshi wa android 16
Android 16 inatumia AI katika swala la usalama
Kwa maana kuna nyakati inaweza kutambua meseji ya kitapeli
Imeongezwa mambo mengine ambayo mengine yalikuwepo katika simu
Mbali na Android 16 simu inaendeshwa pia na mfumo wa HIOS 16
HIOS 16 imeweka mifumo mingi ya AI kwa jumla wanaita tecno AI
Mojawapo ni kufupisha ujumbe
Washindani
Pamoja na upekee wa vitu vikubwa vya awali, spark 50 bado ina ushindani na spark 40
Kwa maana utofauti na vitu vingine mdogo vingi vinafanana
Neno la mwisho
Kwa hii bei, simu imepanda ukilinganisha na toleo lilopita
Kisifa hii ni simu ya laki tatu na nusu
Ila kuna kitu kimoja kinaendelea kwa sasa
Bei za memori zimepanda sana kutokana na kupanuka kwa AI
Hivyo simu zitakazo toka kwa sasa zitakuwa na bei kubwa