Kuna bei za infinix mpya zinafikirisha
Maana zimekuja kitofauti sana kwa namna simu za Infinix zilivyozoeleka
Maana kuna infinix inayoenda hadi milioni mbili na nusu kwa Tanzania
Ila sifa za Infinix kwa mwaka 2026 nyingi ni za kiushindani
Ndio maana kuna tofauti kubwa sana kati ya Infinix Note 60 Pro na Infinix Note 50 Pro
Hizi ndio simu zenyewe na sifa zake
Zitazame kama zinaendana na bei na kama inakufaa
Infinix Note 60 Pro
Bei ya Infinix Note 60 Pro ya GB 256 na RAM ya GB 8 ni shilingi milioni 1.2 (1,200,000)
Ubora mkubwa wa hii simu ni utendaji ulioimarishwa na betri kubwa
Tofauti na simu ya mwaka uliopita
Infinix Note 60 Pro imepata maboresho kwenye skrini, esim, chaji ya wati 90
Na hata kamera yake ni nzuri na ina fingerprint ya kwenye kioo
Hivyo sifa zake zinaendana kabisa na bei ya simu
Infinix Note 60
Infinix Note 60 ya GB 256 ni shilingi laki tisa (900,000)
Hii simu pia ina utendaji mkubwa wa kusuma kila aina ya app na kwa haraka
Ni simu ya 5G yenye kusapoti laini za aina ya eSIM
Kwa sasa bado haijaingia rasmi kwa Tanzania
Na yenyewe ina betri kubwa la mAh 6500
Ukaaji wake wa chaji ni mkubwa na ina kioo himilivu simu inapoanguka
Infinix Note 60 Ultra
Bei ya Infinix Note 60 Ultra ni shilingi milioni mbili na nusu (2,500,000)
Kwa sehemu inafanana na Infinix Note 60 Pro
Ila hii ina maboresho ya ziada katika vipengele vifuatavyo
Kamera zipo tatu na ina kamera ya telephoto, nzuri sana kurekodi ukiwa mbali na unayemrekodi
Mfumo wake wa memori una kasi hivyo utendaji wake ni mkubwa zaidi
Betri lake ni kubwa lina mAh 7000, hapa chaji inakaa mpaka masaa 20 ukiwa kwenye intaneti
Kwa kifupi hii ndio infinix bora zaaidi kwa 2026
Infinix Hot 70
Bei ya Infinix Hot 70 ni shilingi 330,000 ya GB 128 na RAM 4
Ni simu maalum kwa matumizi ya kawaida ya kila siku
Kwa maana haina utendaji mkubwa na kamera kali kama za Infinix Note 60
Kwani ina kamera moja tu ya ukubwa wa megapixel 8
Kama ilivyo ada, betri ni kubwa ina mAh 60000
Infinix Smart 20
Simu ya Infinix Smart 20 inauzwa shilingi 350,000 ya GB 128
Kwenye hii linki kuna maelezo zaidi: infinix smart 20
Kiujumla ni simu inayomfaa mtumiaji mwenye mahitaji machache ya simu
Infinix Note Edge
Bei ya Infinix Note Edge ni shilingi laki saba na nusu (750,000)
Hizi ndio sababu za simu kuuzwa zaidi ya laki saba
Ina utendaji mkubwa wa kuruhusu kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja
Betri yake ni kubwa ina mAh 6500 na chaji ya wati 45, hivyo inakaa muda mrefu na wakati wa kuchaji haichukui muda kujaa