SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Infinix Hot 60 ni bora kuliko Hot 70?

Miongozo

Sihaba Mikole

June 8, 2026

Infinix Hot 70 ni simu mpya imeingia rasmi sokoni mwezi mei 2026

Kwa Tanzania inatarajiwa kuingia rasmi mwezi huu Juni

Sifa zake zinashtua ukiilinganisha na Infinix Hot 60

Utendaji na betri pia chaji ndio kumetengeneza utofauti huu unaostaajabisha

Utofauti

Infinix Hot 70 na Infinix Hot 60 zinatofautiana kwenye maeneo kama manne

Hot 60 ina network inayosapoti mtandao wa 5G

Wakati Infinix Hot mpya ya 2026 inasapoti mpaka mtandao wa 4G

Kwa mantiki hiyo utendaji wa Hot 60 ni mkubwa kuliko hot 70

Vitu vilivyoongezeka

Japokuwa Infinix Hot 70 inakosa utendaji mkubwa ila ina sifa za ziada

Kwanza inakuja na betri kubwa

Betri yake ina mAh 6000

Hivyo ukaaji wa chaji unaweza kufika masaa 14

Hii simu ina NFC, haikuwepo kwwnye toleo lililopita

NFC hutumika kufanya malipo malipo bila kuhitaji kadi

Malipo ya kadi kwa Tanzania hayasambaa hivyo hata matumizi ya NFC yanaweza yasitumiwe na wengi

Kitu kingine Infinix Hot 70 inasapoti chaji hadi ya wati 45 kutoka wati 15

Pia saizi ya hii simu ni kubwa kidogo ukifananisha na toleo hilo la nyuma

Ufanano

Kwa zaidi ya 80% hizi simu mbili zinafanana

Infinix hot 70 imeongozewa uwezo wa betri na chaji

Ila utendaji umepungua

Kwa maana inatumia prosesa ya Mediatek helio g100 ultimate

Ambayo ni prosesa zisizo na utendaji wa kutisha

Kwa hiyo kwa muhitaji wa mtandao wa 5G hana haja ya kununua Infinix Hot 70

Ila kama swala la ukaaji wa chaji ni kitu, huna kununua hii infinix mpya

 

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

infinix note 60 pro

Bei ya Infinix Note 60 Pro na Sifa Zake za Kishindani

Infinix Note 60 Pro ni bonge la simu inayozitoa “knock out” simu shindani nyingi Ukilinganisha na matoleo ya infinix yaliyopita, Infinix Note 60 Pro imeboreshwa pakubwa sana Ni simu ya […]

samsung a57

Bei ya Samsung Galaxy A57 na Sifa Zinazotofautiana na Galaxy A56

Samsung Galaxy A57 ina sifa nyingi za kubwa Hata hivyo ina vitu vingi sana vinavyofanana na Samsung Galaxy A56 Bei ya Samsung Galaxy A57 inatofautiana kulingana na ukubwa wa memori […]

Bei ya Infinix Smart 20 na Sifa Zilizoongezwa

Kiuhalisia Infinix Smart 20 ni simu moja na Infinix Smart 10 Sifa karibu zote zinafanana ila utofauti upo maneneo matatu Hizi tofauti zinaweza kuonekana kuwa ndogo lakini zinaweza leta upekee […]

Hizi ndizo Simu 100 za Bei Ndogo Kabisa (ipi kali zaidi?)

Una bajeti ndogo na unataka simu ya kukidhi mahitaji yako? Basi hii ni orodha ya simu zipatazo mia moja ambazo za bei nafuu zaidi Hii orodha inaorodhesha simu kutoka kampuni […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company