SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ni nini Maana ya HDR (kwenye simu)?

Miongozo

Sihaba Mikole

May 14, 2022

Inawezekana ukawa umewahi kuona sifa za simu upande wa kioo na kamera

Moja ya kitu utakachokiona kikianishwa ni HDR mfano mzuri ni simu mpya ya Samsung Galaxy S23+

Hivyo ikakufanya kutaka kujua maana ya HDR

Kama unajiuliza hdr ni nini basi hili ndio jibu

HDR ni tekniki (mbinu) ambayo kamera inatumia kutoa picha ambayo ina muonekano unaoendana na jinsi jicho la binadamu linavyoona hiko kitu kwenye mazingira halisi

MAANA YA HDR

Kirefu chake ni High Dynamic Range

Jinsi HDR inavyofanya kazi

Kama kamera ina uwezo wa kuchukua video au picha za HDR, kitu cha kwanza inachofanya ni kupiga picha nyingi kwa wakati kwa nyakati tofauti

Yaani unapobonyeza kitufe cha kupiga picha, kamera hupiga picha nyingi kwa kutofautisha kiasi cha mwanga

Kwa maana viwango vya exposure vintofautiana

Baada ya hapo, simu inaunganisha picha zote ambazo kamera imezipiga

Kuziunganisha picha kwa pamoja kunatengeneza muonekano mpya wa video au picha

maana ya HDR

Hiki kitendo kinafanyika ndani ya sekude chache

Aina za HDR

Mpaka sasa 2022 kuna aina sita za hdr ambazo ni

  1. HDR10
  2. HDR10+
  3. Dolby Vision
  4. HLG
  5. Technicolor
  6. Dolby Vision IQ

Tutazifafanua kwa ufupi HDR10 na HDR10+ pekee

HDR hutumia kitu kinaitwa “metadata” kutambua kiwango cha uangavu kinachohitajika

Hivyo kuna metadata inayotumia kiwango cha uangavu wa aina moja hufahamika kama static metadata

Lakini kuna metadata inayobadilika kulingana na kiwango cha uangavu wa eneo husika hii huitwa dynmic metadata

HDR10 yenyewe inatumia static metadata

Hivyo kama display ina rangi zaidi ya bilioni baadhi ya rangi zinaweza kuonekana zikiwa na giza kiasi

Hilo linarekebishwa na HDR10+ ambayo inapunguza ama kuongeza uangavu kutokana kiasi cha mwanga wa eneo husika

Kitu kinachofanya HDR10+ kuweza kuonyesha rangi nyingi kwa ustadi

Faida za kutumia HDR

Faida kubwa ya HDR ni uwezo wa kurekebisha muonekano wa vitu ambavyo vimepigwa kwenye mwanga hafifu

HDR hubalansi rangi za vitu kwa ustadi

Na inafanya kitu kionekane kwenye simu kama kinavyoonekana kwenye uhalisia wake

Japo kuna nyakati hilo halitokei

Udhaifu wa HDR

Kuna baadhi ya picha za hdr huongeza rangi ambazo hazipo

Kiasi cha kwamba uhalisia wa picha unakuwa haupo

Hii inatokana na hdr kukoreza rangi zaidi ya rangi ya kitu kinavyoonekana

Na baadhi ya vifaa vinachukua picha chache huku ikitumia hdr

Sasa picha ikiwa imechukuliwa kwenye exposure ya aina moja ubandia lazima utokee

Simu zenye kioo na kamera ya HDR

Simu zote za daraja la juu za mwaka 2021 na 2022 huwa na HDR10 au HDR10+

Ila kuna kamera za simu chache ambazo zinaweza kurekodi video za HDR10+

Kiufupi baadhi ya simu hizo ni samsung galaxy s22, iphone 13 pro max, xiaomi 12 pro, vivo x70 pro na  nyinginezo

Gharama za simu za HDR10 na HDR10+

Ukitazama baadhi ya simu zilizotajwa unaweza kujua uhalisia wa bei

Kiuhalisia bei ya simu za HDR10+ ni zaidi ya laki tano

Hakuna simu ya bei rahisi yenye hdr10+

Wazo moja kuhusu “Ni nini Maana ya HDR (kwenye simu)?

  • Kifupi nimependa maelezo yenu mlio fafanua kwa mapana na kwa weledi mkubwa nimependa sana kiufupi nimengi nimepata kujifunza kutoka kwenu hadi vitu ambavyo sikuwahi kutegemea kwamba nitakujaga kivifahamu Ahsante sana.

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram