SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Sifa za simu ya iPhone 13 Pro Max

Sifa za simu

Sihaba Mikole

March 1, 2022

Simu ya iPhone 13 Pro Max ni simu iliyowekewa vitu vingi vinavyofanya simu kuwa na ufanisi mzuri.

Ukizifuatilia sifa za simu ya iPhone 13 Pro Max utagundua kuwa ni simu yenye nguvu kubwa, imara, software nzuri, kamera bora, display inayoonyesha vizuri, inakaa na chaji muda mrefu na mengine mengi.

Kiuhalisia hata simu ya samsung s22 ultra iliyozinduliwa mwaka 2022 inapitwa kwa kiasi fulani na simu ya iPhone 13 Pro Max.

Swali la kujiuliza kwa nini?

Jibu lipo kwenye hii linki : simu bora kati ya samsung s22 ultra na iphone 13 pro max

Sifa za iPhone 13 Pro Max kwa ufupi.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
 • CPU – Apple A15 Bionic
 • Core Zenye nguvu(2) – 2×3.22 GHz Avalanche
 • Core Za kawaida(4) – 4×2.0 GHz ¬†Blizzard
 • GPU-Apple GPU(5-core)
Display(Kioo) Super Retina XDR OLED
Softawre
 • iOS 15
Memori NVMe,

128GB,256GB,512GB,

1TB na RAM 6GB

Kamera Kamera nne

 1. 12MP,dual pixel PDAF(main),
 2. 12MP(telephoto)
 3. 12MP(ultrawide)
 4. TOF 3D LiDar Scanner(depth)
 5. 12MP(selfie camera),SL 3D(biometric sensor)
Muundo Urefu-6.7inchi
Chaji na Betri
 • 4352mAh-Li-Po
 • Chaji-27W
Bei ya simu(TSH) 2,538,690/=

Ubora wa simu y iphone kwa kutazama jedwari upo katika pande nane.

 1. Network
 2. Processor (Chipset au SoC)
 3. Software
 4. Bodi ya simu
 5. Kamera
 6. Mfumo wa chaji na betri
 7. Memori
 8. Display

Ukitaka kujua ubora wa simu yoyote zingatia hizo sifa.

Network

iPhone 13 pro max inasapoti mtandao wa 5g.

Modem iliyopo kwenye pro max inakubali aina zote za 5G.

Mtandao wa 5G umegawanyika katika sehemu tatu.

 1. Lower Band
 2. Mid Band
 3. mmWave.

Kwa hiyo kama simu inatumika kwenye maeneo yenye 5G zenye kasi ndogo simu itaendelea kufanya kazi.

Kwa bahati mbaya Tanzania bado inatumia 4G na hakuna 5G.

Lakini hilo lisikutishe kwa sababu hata 4G ya iphone 13 pro max ina kasi kubwa.

Processor ya simu ya iPhone 13 Pro Max

iPhone 13 Pro Max inatumia processor yenye core sita yaani Hexacore.

Core zilizoundwa kwa ajili ya kuchakata kazi kubwa zipo mbili ambazo zinafahamika kama Avalanche.

Na core ambazo zimeundwa kwa ajili ya kazi za kawaida zipo nne hizi hufahamika kama Blizzard.

Core ya Avalanche ina spidi kubwa ya 3.223GHz

Wakati Core ya Blizzard ina spidi ya wastani ya 1.82GHz

Chipset ya iphone 13 pro max inajulikana kama Apple A15 Bionic.

Apple wanadai ISP(Image Signal Processor) ya A15 Bionic inachakata picha zinazopigwa na kamera kwa ubora.

Ni processor yenye nguvu na uwezo wa kusukuma aina yoyote ya application kwa wepesi.

Platform mojawapo maarufu na inayoominika katika kupima nguvu za processor ni geekbanch.

Kwenye GeekBench 5 a15 bionic ina point zaidi ya 1700.

Ni point nyingi ukilinganisha processor karibu zote za simu.

Upande wa GPU chipset inatumia Apple GPU 5-core.

Moja ya sifa kubwa ya Grapic Card ya simu yenye ni kucheza gemu kwenye resolution kubwa bila kukwama.

Na pia kucheza gemu kwa spidi kubwa ambayo inafahamika kama Frame Rate ambayo hupimwa kwa Frame rate per second(fps).

Kikawaida video huwa ni mkusanyiko wa picha ila kwa jicho la binadamu haliwezi kuzitambua hizo picha.

Hizo picha hufahamika kama frames, na hizo frames zinabadilika kwa sekunde ndio maana hatuwezi kuziona.

Apple GPU 5-core inaweza onyesha video na kucheza gemu kwneye resolution kubwa kwa spidi ya 60FPS.

Gemu kama la PUGB Mobile 2018 linacheza kwa resolution kubwa.

Memori ya iPhone 13 Pro Max

Simu za iphone hutumia memori aina ya NVMe.

Mfumo wa NVMe huwa unasafirisha data kwa kasi kuliko mifumo ya UFS na EMMc.

Memori inapokuwa na kasi simu huwaka kwa haraka na application inafunguka kwa haraka vilevile.

Nadhani umeshawahi shuhudia simu zinazowaka taratibu au application kuandika Application Not Responding.

Mara nyingi ni mfumo wa memori wenye kasi ndogo husababisha.

iPhone 13 pro Max zipo za aina nne.

Kuna iphone za 1TB, 512GB, 256GB na 128GB.

Simu inakosa sehemu ya kuwekea memori.

Kama unahitaji memori ya ziada itakupasa utumie iCloud kuhifadhi mafaili mbalimbali ambayo inahitaji intaneti ku-upload mafaili.

Ambayo itafanya gharama kuongezeka.

Simu hii ya iphone ina RAM ya 6GB.

Ram yake ni ya channel 4x aina ya LPDDR4x

Kirefu cha LPDDR4x ni Low Power Double Data Rate.

Ni ram zinazotumia umeme mdogo na kasi kubwa ya kubwa ya kupeleka data.

Bodi ya iPhone 13 pro Max.

Bodi ya iphone 13 pro max inaundwa na glass za gorilla upande wa mbele na nyuma.

Katika moja ya kitu kikubwa upande wa sifa za simu ya iphone 13 pro max ni ugumu wake wa maji kupenya.

Simu haiwezi pitisha maji hata punje ikiwa imedumbukia kwenye kina cha maji cha mita sita muda wa nusu saa.

Hii inatokana na simu kuwa na IP68 ambayo hutambulisha uimara wa simu kupenyeza maji.

Simu ina uzito wa gramu 249.

Na urefu wa inchi 6.7 kutoka juu kushoto kwenda chini kuria.

Simu ni ndefu.

Bodi yake ni imara pia kupasuka.

Baadhi ya majaribio yameonyesha ugumu wa simu kupasuka ikiwa imeangushwa kwa kimo cha mita 2 kutoka juu.

Na eneo ambalo simu imeangukia ni eneo lenye uso wa rafu.

Upande wa michubuko vitu kama chuma haviwezi kukwangua kioo cha iphone 13 pro max

Kwa kuzingatia vipimo vya mohs scales kioo cha apple kinaweza kuchubuka ikiwa kitu kinachochubua kioo ni jamii ya topaz(sio wembe).

Kamera ya iPhone 13 Pro Max

iPhone 13 pro max ni simu yenye kamera nzuri kuanzia hardware na software.

Upande wa kamera za nyuma simu ina kamera nne.

Aina za kamera za simu hii ni wide, telephoto, ultrawide(nyuzi 120) na TOF 3D LiDAR scanner(depth).

Kamera tatu za mwanzo zina megapixel 12.

Kamera ya ultrawide hupiga picha na video za eneo pana kwa nyuzi 120.

Telephoto inapiga picha na video kwa umbali mrefu.

Kamera ya telephoto inaweza kuzoom mara tatu kama unatumia optical zoom ambayo inazoom kwa kutumia sensor na sio app ya kamera.

Lakini pia ina OIS na dual pixel PDAF.

Na kamera zingine pia ukiachalia ya TOF zina dual pixel na OIS.

Ukiwa unapiga picha ama video ya kitu kinachotembea mfano ndege, dual pixel PDAF inafanya simu ilenge kwa usahihi sana na kutokea vizuri.

Simu inaweza ikawa na mfumo mzuri wa kamera na megapixel nyingi lakini application yake ya kamera inaweza isiwe nzuri.

App ya kamera iphone ni nzuri kiujumla.

Kwa upande wa chaji, display na softaware ya iOS, pitia kurasa zifuatazo.

Simu Nzuri za iPhone na Bei Zake 2022

Ipi Simu Bora: Samsung Galaxy S22 Ultra vs iPhone 13 Pro Max

 

Maoni 3 kuhusu “Sifa za simu ya iPhone 13 Pro Max

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

thumbnail

[VIDEO]:Simu zote za iPhone za bei ndogo na zinazofaa

Kabla ya kununua iphone za bei rahisi ambazo mara nyingi huwa ni used, kitu cha kwanza cha kuangalia ni kama itakuwa inapata sapoti ya kupokea mfumo endeshi wa iOS Tofauti […]

iphone thumbnail

iPhone za bei rahisi za kumiliki kwa sasa(2024-2027)

Katika pitapita zangu na kuchunguza simu bora za bei ndogo na ya chini nimekuja kugundua kitu cha kustahajabisha kidogo Wapenzi wa iPhone wenye bajeti ndogo wananunua iphone used hazipokei maboresho […]

iphone 15 pro max camera thumbnail

Ubora wa iPhone 15 Pro Max Upande wa Kamera[hatari tupu]

Apple iPhone 15 Pro Max ni simu yenye kamera tatu upande wa mbele na kamera moja ya mbele (selfie kamera) Ukifuatilia ubora wake wa kamera utagundua sababu ya kuuzwa bei […]

iphone 15 pro max thumbnail

Bei ya iPhone 15 Pro Max na Sifa Zake

Apple iPhone 15 Pro Max ni toleo jipya la iphone kwa mwaka 2023 Ni simu ya kwanza kutoka Apple kutumia chaji aina ya USB Type C ambazo hutumika na simu […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company