Kwenye ulimwengu wa smartphone apple na samsung zinachuana vikali kimauzo na kiubora wa simu.
Samsung inaongoza kwa kuuza smartphone nyingi.
Apple inashika uskani kwenye mauzo ya simu za hadhi ya juu(High End) ikifuatiwa na Samsung.
Mfano wa simu ya high end ya samsung ni Galaxy S22 Ultra.
Kiubora, inaleta shida kutambua ipi simu bora kati ya Samsung galaxy S22 na iPhone 13 Pro Max.
Kwa sababu simu zote zina kamera kali, processor nzuri, display bora na bodi ngumu kuharibika.
Post hii itazamia ubora wa simu hizi kwenye vipengele muhimu.
Kabla ya kufikia hitimisho, hizi ni sifa za Galaxy S22 Ultra na iPhone 13 Pro Max.
Sifa za Samsung Galaxy S22 Ultra
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Dynamic AMOLED 2X, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 128, 256,512, 1TB na RAM 8GB, 12GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.8inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,768,491/= |
Sifa za iPhone 13 Pro Max
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED |
Softawre |
|
Memori | NVMe,
128GB,256GB,512GB, 1TB na RAM 6GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,538,690/= |
Processor.
Simu iPhone 13 Pro Max ambayo imetoka mwaka 2021 ina processor ya Apple A15 Bionic.
Kwa kipindi ambacho simu ilikuwa imetoka hakukuwa kuna processor ya kushindana nayo.
Mshindani wa A15 Bionic alikuwa ni snapdragon 888+ 5g ambayo ilipitwa mbali.
Lakini mwaka 2022 mambo yameendelea kuwa kama yalivyo.
Snapdragon 8 gen 1 na Exynos 2200 zimeshindwa kuipita Apple A15 Bionic kiutendaji.
App ya GeekBench hutumika kupima nguvu ya processor.
GeekBench huwa inatoa point kulingana na uwezo wa chip upande wa CPU.
Kadri processor inavyofanya kazi kubwa kwa haraka na wepesi ndio inapata point nyingi.
Tayari wazoefu wa simu wamezipima Samsung S22 series kwa GeekBench 5.
Exynos ina point 1108 kwenye core moja
Chip ya Apple A15 Bionic ina point 1717 kwenye core moja.
Wakati Snapdragon 8 gen 1 ina point 1224 kenye core.
App nyingine ya Atuntu ambayo hupima uwezo na ubora wa CPU, GPU na RAM.
Snapdragon 8 gen 1 ina gpu nzuri inayofaa kucheza gemu tena kwa ustadi.
Na pia ina RAM yenye kasi kuliko ya A15 Bionic.
Kwa pafomansi ya ujumla A15 Bionic inaizidi kwa kiasi kidogo Snapdragon 8 gen 1.
Hivyo basi simu iPhone 13 Pro Max kiuwezo wa processor inaizidi Samsung Galxy S22 Ultra.
Network.
Simu zote ya iPhone 13 Pro Max na Samsung Galaxy S22 Ultra zina 5g.
Kuna aina tatu za mtandao wa 5G.
- Lower Band
- Mid Band
- mmWave(Ina kasi kubwa sana)
Aina zote za 5G zipo kwenye simu hizo mbili.
Hivyo spidi ya network simu zinaendana.
Uimara wa simu.
Simu ya samsung galaxy s22 inaweza kuwa imara kuliko iphone 13 Pro Max.
Ukipata nafasi ya kufuatilia majaribio ya kuangusha simu mwaka 2021 Bodi ya iPhone 13 Pro Max ilipasuka kwa haraka kuliko Samsung Galaxy S21 Ultra.
Simu zote mbili zilikuwa zinadoshwa upande wa nyuma, pembeni na mbele kwenye kioo.
Mara nyingi eneo ambalo simu hudondokea huwa ni rafu.
Bodi ya Samsung iliweza kustahamili kupasuka mpaka ilipodondoshwa mara nyingi kwenye kimo cha mita mbili kutoka juu.
Tazama video hii.
https://www.youtube.com/watch?v=1PRb5KFKxI4
Kila wakati iphone 13 pro max ikiangushwa glasi zinaruka kwa maana zinatoka kwa kupasuka.
Matariji ni kuwa Samsung Galaxy S22 Ultra ni imara na inaweza dumu muda mrefu kuliko Pro Max.
Display
Samsung ina vioo vizuri kuliko vya apple.
Kikawaida simu mpya za oppo hutumia vioo vinavyotengezwa na samsung.
Vioo vya apple wamevibrand kwa jina la Super Retina XDR OLED.
Wakati samsung vioo vyao wanavibrand kwa jina Dynamic Amoled 2x
Dynamic Amoled 2x ni kioo angavu sana kuliko Super Retina.
Uangavu wa xdr oled unafikia kiwango cha juu cha 1200nits.
Ni kiasi kidogo kwa sababu samsung kioo chake kinafikia 1750nits.
Hii inamaanisha nini?
Screen ya Samsung s22 itaonyesha vitu vizuri sana endapo simu inatumika kwenye jua.
Dynamic Amoled 2x inaweza kuonyesha video za HDR10+
Picha na video HDR10+ huwa ni ang’avu na zenye usahihi mkubwa wa rangi.
Kama sehemu ina rangi nyeusi basi rangi nyeusi itaonekana vizuri kama ilivyo.
Kwa kifupi HDR ni teknolojia inayojaribu kuwasilisha picha kwa jinsi jicho la binadamu linavyoona kwenye mazingira halisi.
Galaxy S22 ultra ina kioo bora kuliko iphone 13 pro max.
Kamera.
Kwa sasa unaweza kusema simu yenye kamera kali ni Galaxy S22 ultra.
Ili ujue ubora ni lazima upate picha zilizopigwa kwenye mazingira halisi kuliko kutazama sifa za kamera.
Ukitazama megapixel pekee yake unaweza kusema kamera ya iphone inazidiwa na kamera za tecno
Kwa kuzingatia tathmini upande wa iliyofanywa na mchambuzi maarufu wa simu youtube MrWhoTheBoss.
Samsung inatoa picha safi kabisa ambazo zinapigwa kwenye mwanga hafifu.
Utulivu wa kamera ya samsung ni mkubwa ukilinganisha na iphone 13 pro max.
Zoom ya pro max haionyeshi picha hasa ukipiga ghorofa ya juu ya jengo refu.
Hii inamaanisha telephoto ya Samsung galaxy inaweza kupiga kitu cha mbali kwa ustadi.
Mbali na hayo kuna mengi ambayo yanafanana kwenye kamera.
Kamers za simu zote zinaweza kupiga video za 4k na 8k.
Selfie ya apple ni nzuri kwa kufungua simu kutumia sura.
Ina kamera mbili ambayo moja ina sensa.
Betri na Mfumo wa Chaji.
Samsung galaxy s22 ina mfumo wa chaji unaepeleka umeme mwingi kuliko iphone 13 pro max.
Chaji ya S22 ultra inaweza kujaza betri kwa haraka sababu inatoa umeme wa 45W ambapo iphone pro max yenye 13W.
Betri ya iphone ni ndogo kuliko la samsung.
Pamoja na udogo huo betri ya iphone 13 pro max inakaa na chaji muda mrefu kuliko samsung galaxy 22 ultra.
Pitia kwenye page phonearena kutazama uwezo wa simu kukaa na chaji muda mrefu kati iphone 13 pro max na samsung galaxy s22 ultra.
Mawazo yangu yalidhani kuwa Samsung electronic watakuwa wameboresha simu zao upande wa betri kwa kuzingatia simu mpya za samsung zinatumia mfumo mpya wa kupooza simu.
Lakini hali ni tofauti.
Ukitumia intaneti kwenye s22 ultra simu inawahi kuisha kuliko kwenye iphone 13 pro max.
Kwa data chache toka kwenye test zilizofanywa na tovuti phoneArena, iphone 13 pro max pro max inaweza kukaa na chaji masaa 18 ukiwa unatumia intaneti wakati samsung ni masaa ni masaa 13.
Hivyo upande wa chaji ipjone ina mfumo mzuri wa chaji zaidi ya samsung.
Memori.
Apple hutumia memori zenye teknolojia ya NVMe.
Wakati samsung inatumia U.F.S 3.1
Kwa rekodi za sasa mfumo wa memori wa NVMe una kasi kubwa ya kuhifadhi data kuliko UFS.
Kinadharia NVMe inaweza kupeleka spidi mpaka ya 32Gbps, ni mara sita ya spidi ya memori aina UFS.
Hivyo apple ina memori nzuri.
Hitimisho.
iPhone 13 pro max inaendeleo kuwa simu bora samsung 22 ultra.
Ukiwa na simu yenye processor nzuri basi simu inakuwa nzuri kwenye nyanja nyingi
Wazo moja kuhusu “Ipi Simu Bora: Samsung Galaxy S22 Ultra vs iPhone 13 Pro Max”
Ila kwangu mimi bado nabaki na Samsung