Kuna simu zaidi ya tisa zilizotengenezwa na kampuni ya Samsung kutoka
Hapa kuna orodha ya simu kumi mpya za samsung ambazo zimetoka mwishoni mwa mwaka 2023 hadi mwaka 2024
Ni listi yenye samsung za bei ndogo, bei ya kati na bei kubwa
Simu zote zinaanzia laki mbili na nusu kwenda na ubora unatofautiana hasa utendaji
Samsung Galaxy A15
Bei ya Samsung Galaxy A15: 420,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Simu ya Samsung Galaxy A15 iliingia rasmi mnamo mwishoni mwa mwaka 2023 yaani mwezi desemba
Utendaji wake ni wa wastani kutokana na kutumia chip Mediatek Helio G99
Ina kioo kizuri kinachotumia teknolojia ya AMOLED kikiwa na refresh rate ya 120Hz
Yaani ukiwa unatachi kioo kinakuwa chepesi na maridhawa wakati wa kuperuzi kwa ku-scroll
Ubora wa kamera wake haufikii viwango vya simu vya bei kubwa ila ina ubora unaopiga picha za kuridhisha kiasi fulani
Kwa zaidi pitia: Ubora na bei ya Samsung Galaxy A15
Samsung Galaxy A15 5G
Bei ya Samsung Galaxy A15 5G: 500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Hii ni samsung yenye sifa za ziada upande wa network ila kwa kiasi kikubwa inafanana na galaxy iliyotangulia
Na yenyewe ilitoka mwezi desemba kiutendaji haina tofauti na Galaxy A15 isiyo na 5G
Hii inaatokana na simu kutumia muundo mmoja wa Cortex A76
Ila faida ya hii simu unapata mtandao wenye kasi kwa wakazi wanaoishi maeneo yaliyo na mtandao wa 5G
Hii simu ukiwa unaperuzi intaneti betri yake inakaa mpaka masaa 11 (kama unaperuzi)
Ukiwa unacheza gemu muda unapungua zaidi
Samsung Galaxy A25
Bei ya Samsung Galaxy A25: 550,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Samsung Galaxy A25 ni toleo lingine la desemba ya mwaka 2023
Hii simu ina kioo kizuri cha Super AMOLED chenye resolution inayofika 120Hz
Ni kubwa sana ila pamoja na kuwa na betri kubwa ukaaji wa chaji ni wa kiwango cha kawaida
Kwani kwenye kuperuzi betri inadumu kwa masaa tisa
Masaa mawili pungufu ya Samsung Galaxy A25
Hii ni simu ya 5G na utendaji wake ni mkubwa kwani ina muundo wa Cortex A78
Samsung Galaxy S24
Bei ya Samsung Galaxy S24: 2,800,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Samsung Galaxy S24 ilitoka mwanzoni mwa mwaka 2024
Ni simu ya daraja la juu yenye ubora kwenye kila nyanja
Utendaji wake ni mkubwa unaoweza kufungua app za kila aina bila simu kukwama kwama
Ukaaji wa chaji pia unachukua mpaka masaa karibu kumi na moja kwenye matumizi tofauti tofauti
Kamera zake zipo tatu na zote zina ubora mkubwa kwenye upigaji wa picha na uchukuaji wa video
Samsung Galaxy S24+
Bei ya Samsung Galaxy S24+: 2,800,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Samsung Galaxy S24 Plus na lenyewe ni toleo la mwaka 2024
Hii ni simu ya kamera tatu huku kamera kubwa ikiwa na ukubwa wa megapixel 50
Galaxy S4+ inatoa picha yenye uhalisia mkubwa kwa nyakati zote za kwenye mwanga hafifu na mwanga mwingi
Ina kioo cha AMOLED chenye uwezo kubadilisha refresh rate kutokana na aina ya matumizi
Mfumo wa chaji unasapoti chaji ya wati 45
Hiyo ukiwa nayo utakuwa kwenye levo moja na iPhone 15 Pro
Samsung Galaxy S24 Ultra
Bei ya Samsung Galaxy S24: 3,330,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Samsung Galaxy S24 Ultra ndio simu yenye gharama zaidi katika hii orodha
Kwa mtumiaaji anayependa simu yenye kamera nzuri, nguvu kubwa ya kiutendaji, ukaaji wa chaji wa muda mrefu, simu yenye peni(stylus), simu yenye waterproof, kioo kikali, lazima uifikirie Samsung Galaxy S24 Ultra
Kwenye chaji Galaxy S24 Ultra inaweza kuchukua mpaka masaa 11 wakati wa kuperuzi
Na kucheza gemu inadumu kwa muda wa masaa 9
Haya ni masaa yanayofanya mcheza gemu kuchaji simu mara nyingi
Kuna vitu vingi vya msingi juu ya hii simu hasa upande wa matumizi ya Artificial Intelligence(AI)
Samsung Galaxy A55
Bei ya Samsung Galaxy A55: 1,150,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Kwa mpenzi wa Samsung Galaxy A55 mwenye uwezo mdogo wa kumudu matoleo ya S-series Samsung Galaxy A55 inakupa vitu vingi vya premium
Ndio maana hata bei yake imechangamka kidogo japo ni simu ya daraja la kati
Ina utendaji wenye nguvu kutokana na kutumia processor ya Exynos 1480
Na yenyewe ina betri kubwa hivyo chaji inakaa muda mrefu hata kwa kulinganisha na samsung nyingi zilizopo hapa
Kwa mfano kwenye kuperuzi simu inakaribia masaa 12 mpaka betri iishe
Samsung Galaxy A35 5G
Bei ya Samsung Galaxy A35: 950,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Hii ni simu nyingine ya toleo la kati japo bei kubwa lakini ni ya toleo la kati
Inatumia chip zinazoundwa na samsung yenyewe
Betri yake ni kubwa na ina ulinzi wa kuzuia maji kupenya yaani waterproof
Ina kamera tatu upigaji wake ni mzuri
Maoni 5 kuhusu “Simu Mpya za Samsung 2024 (za bei rahisi na ghari)”
Mi Nina Samsung galaxy s24 ultra 5G ila naona kwenye kamera haipo quality
Ulinunua shilingi ngapi?
Naitaji Samsung Galaxy yenye uwezo mkumbwa isiyozid. 300,000
Inategemea
Nahtaji Samsung nzuri Mya isiyozidi laki tatu nitapata