Samsung Galaxy A55 imetoka mwezi machi mwaka 2024 na ni simu ya daraja la kati
Bei ya Samsung Galaxy A55 kwa Tanzania ni shilingi milioni moja na laki moja na nusu
Hii ikiwa na ukubwa wa GB 128, yenye GB 256 bei yake inazidi hapo
Nini hasa cha kipekee na thamani vinavyopatikana kwenye Galaxy A55
Ubora wa hii simu umejikita hasa kwenye utendaji, ubora wa kamera na kioo kizuri
Utaelewa kiundani ukifuatilia vipengele vyote vilivyofafanuliwa hapa kwa kutazama pia sifa zake
Sifa za Samsung Galaxy A55
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Amoled, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB na RAM 8GB,12GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,150,000/= |
Uwezo wa network
Samsung Galaxy A55 inasapoti laini za eSIM ambazo zinaruhusu kushika network ya mtandao bila kuwa na laini zile za plastiki
Pia hii ni samsung ya 5G ambayo inasapoti aina zote tatu za 5G
Kwa mkazi wa baadhi ya maeneo ya Dar na Dodoma, mtandao wa 5G unapatikana kwa laini za Airtel, Tigo na Vodacom
Chaguo ni lako
Upande wa 4G simu inasapoti 4G aina ya LTE Cat 18
LTE Cat 18 inaweza kupakua faili kwa kasi inayofika 5000Mbps
Hata hivyo hii spidi ni kubwa sana kwa mitandao ya hapa nchini upande wa 4G
Ubora wa Kioo cha Samsung Galaxy A55
Kioo cha Samsung Galaxy A55 ni cha aina ya Super Amoled
Hivi vioo vya amoled huwa vina utajiri wa rangi kitu kinachofanya kioo kuonyesha vitu kwa rangi zenye kuendana na uharisia kwa kiwango kikubwa
Kwa mfano rangi nyeusi kwenye vioo vya Amoled yaani vinaonekana ikiwa nyeusi kweli
Uzuri wa kioo cha hii unaongezewa na uwepo wa HDR10+ ambayo inaongeza kina cha rangi
HDR10+ huwa inafanya utofoutishaji mzuri sana wa rangi kwenye maeneo yanye mwanga mwingi na mwanga mdogo
Refresh rate ya kioo chake inafika 120Hz hivyo inakuwa “smooth” wakati ukiwa unatachi
Hata hivyo sio mara zote utahitaji refresh rate kubwa maana huwa inakula chaji nyingi
Nguvu ya processor Exynos 1480
Galaxy A55 inatumia chip ya Exynos 1480 katika kufanya kazi zake mbalimbali
Hii chip imegawanyika katika sehemu mbili ambapo sehemu yenye nguvu kuna core nne zinazotumia muundo wa Cortex A78
Cortex A78 inaweza fanya kazi nne kwa mzunguko wakati kuna mizunguko mingi kwa sekunde moja
Kwa maana hii processor nguvu yake ya kufanya nyingi na nzito ni kuridhisha
Ndio maana hata app geekbench inayopima uwezo wa processor inaipa hii chip alama 1168
Kwa mpenzi wa magemu atafurahia muonekano wa graphics za gemu
Uwezo wa betri na chaji
Ukiwa unacheza magemu muda wote betri ya hii simu itadumu kwa wastani wa masaa saba
Na ukiwa unaperuzi intaneti mara kwa mara bila kupumzika itakuchukua karibu masaa 12 mpaka chaji iishe
Kwa maana hiyo kwa mtumiaji mkubwa wa intaneti atalazimika kuchaji simu mara mbili kwa siku
Na kwa mchecha gemu atalazimika kuchaji simu zaidi ya mara tatu kwa siku
Uzuri ni kuwa chaji yake inasapoti wati 25 ambayo inachukua muda mfupi kujaa kwa asilimia mia
Kiwastani ukaaji wa chaji wa Samsung Galaxy A55 ni wa kuridhisha
Ukubwa na aina ya memori
Upande wa memori samsung zipo za matoleo mawili, ambazo kuna zenye GB 128 na GB 256
Na pia katika mgawanyo wa RAM zipo za aina tatu ambazo ni GB 8 na 12
Yenye RAM kubwa ndio inafaa zaidi kwani inakuwezesha kufungua app nyingi kwa wakati mmoja bila kukwama kwama
RAM ndogo huwahi kujaa hasa kama simu imefungua applikesheni nyingi kwa wakati mmoja kitu kinachosababisha simu kuwa nzito
Hii simu inatomia memori za aina UFS 3.1 ambazo huwa zina kasi kubwa ya kusafirisha data
Yaani kama unakopi video ya MB 500 kwenda kwenye simu utaona imemalizika fasta
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A55
Samsung Galaxy A55 ni simu yenye waterproof kwa maana ina IP67
IP67 ni viwango vinavyoashiria kuwa simu haiwezi kuingiza maji ikiwa imezama kwenye kina cha mita 1 kwa muda wa nusu saa
Hata kioo ambacho kimewekwa kwenye skrini ni imara na kigumu kupasuka
Kwa sababu kimewekewa kioo cha Gorilla Glass Victus+
Hata hivyo ni muhimu kuwa makini kwani Gorilla Glass Victus+ pia huchunika
Umakini ni muhimu kioo ni kioo, hupasuka
Ubora wa kamera
Hii simu ina jumla ya kamera tatu ambapo kamera kubwa ina megapixel na inaweza kurekodi video za 4K
Muonekano wa video za 4K huwa na kuvutia na angavu kutokana na kuwa na pixel nyingi
Utafurahi ukirekodi video ya 4K na kuitazama kwenye TV inavosapoti 4K
Kitu kingine ni kuwa hii kamera ina OIS ambayo huwa inatuliza mtikisiko wakati ukirekodi huku ukiwa unatembea
Ubora wa picha ni mzuri kwenye mazingira yote yaani ya mwanga hafifu na kwenye mwanga mwingi
Ubora wa Software
Samsung Galaxy A55 inakuja na toleo jipya la mfumo endeshi ambalo ni Android 14 na pia One UI 6.1
Kwenye One UI 6.1 kuna mifumo mingi ya akili bandia
Kwa mfano unaweza ukawasiliana na mtu anaeongea lugha nyingine ambayo wewe huwelewi
Lakini mfumo one ui 6.1 unaweza kutafsiri maongezi na kuyabadirisha kuwa kwenye lugha unayoielewa
Na kuna mambo mengine
One UI 6.1 ni moja mifumo ya Android ambayo ni mizuri ukilinganisha na mengine
Washindani wa Samsung Galaxy A55
Kwenye masoko ya nchi zinazoendelea kama hapa kwetu Tanzania kuna matoleo mengi ya simujanja kutoka China
Baadhi ya kampuni kama Oppo na Redmi zinatengeneza simu nyingi za daraja la kati na zenye bei nafuu kuliko Galaxy A55
Mfano mzuri tu simu ya Oppo Reno11 Pro ambayo na yenyewe bei yake ni shilingi milion 1.15
Oppo Reno11 Pro inaizidi Samsung Galaxy A55 katika maeneo mengi karibu yote ukitoa upande wa software
Hivyo kitu kama hicho kinaweza kumuhamisha mteja kununua Oppo
Hapo bado matoleo ya Redmi, Tecno na Infinix bila kusahau Realme na OnePlus
Ushindani ni mkubwa kwa samsung kutoka kwa matoleo ya simu za China
Neno la Mwisho
Kwa wapenzi wa Samsung ambao hawawezi kununua matoleo ya Samsung Galaxy S24 hawapaswi kuwaza sana
Kwani bei ya Samsung Galaxy A55 ni ndogo na pia inakupa baadhi ya vitu vinavyopatikana kwenye Samsung za madaraja ya juu
Kwa maana utakutana na toleo jipya la android na utakuwa unapata update za mara kwa mara kuipa simu yako uhai na kutunza thamani yake kwa muda mrefu
Maoni 7 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy A55 na Ubora wake”
Nimeipenda sana hii aina ya simu A55
Je nailataje simu hii???
Wewe unapatikana wapi
A55 iko powa kimaelezo nimependa sana. niulize hivi simu za a series mbona zina shida ya vioo sana .nipe ushauri ni samsung gani ambayo iko vzr iwe daraja la kati au la daraja la juu
Mm napenda simu nzuri ila ushauri ni samsung ipi ni nzuri katika sehem zote
Samsung s24 ultra Ila bei yake kubwa sana
Ni simu bomba
Hii ni nzuri Kwa maelezo, jinsi ya kuupata Sasa