Simu ya Samsung Galaxy A25 ilitoka rasmi mnamo mwezi desemba 2023
Ni simu ya daraja ambayo bei yake kwa Tanzania ni shilingi laki saba (700,000/=), hii ikiwa ni bei ya GB 128
Ila kama unaweza kuagiza kutoka nje bei yake ni chini ya hapa
Sifa zake nyingi ni za kiwango cha wastani ila upande wa kamera na skrini kuna ubora wenye viwango vya “premium”
Kabla ya kujiuliza sana kuhusu bei yake ni vizuri kuzitazama sifa za samsung galaxy a25 kinaga ubaga kufahamu iwapo sifa zake zinaendana na mahitaji yako
Sifa za Samsung Galaxy A25
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Amoled, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB na RAM 8GB,6GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 700,000/= |
Uwezo wa network
Samsung Galaxy A25 inatumia laini za kawaida na haisapoti eSIM
Kama unataka eSIM ya samsung yapo machaguo mengine kama Samsung Galaxy A55
Ni galaxy ya 5G na inasapoti aina zote za 5G ikiwemo ya masafa ya kati inayotumiwa na mitandao ya simu mingi nchini
Pia si tu 5G hata 4G inakama vizuri kwa masafa ya hapa nchini
Aina ya 4G ni LTE Cat 18 yenye kasi ya kupakuwa faili ya 2550Mbps
Kiuhalisia hakuna mtandao wa simu kwa hapa nchini kwa sasa unatoa spidi hii
Labda mbeleni hasa upande wa 5G
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A25
Kioo cha Galaxy A25 kinatumia teknolojia ya Amoled na resolution yake ni 1080 x 2340 pixels
Kitu cha kufurahisha kwenye kioo ni uangavu wenye nits zinazofika 1000 na refresh rate inayosogea hadi 120Hz
Kiwango hiki cha nits kinasaidia sana kutumia simu hata ukiwa juani na kioo kikawa kinaonyesha picha vizuri
Refresh rate kubwa inafanya kioo kuwa fasta ukiwa unaperuzi ama muonekano mzuri ukiwa unacheza gemu
Ila kioo cha hii simu sio kama cha Galaxy A55 kwani hakina HDR10+
HDR10+ huongeza kina cha rangi kitu kinachofanya vitu vingi kuonekana kwa rangi zenye kuondana na uhalisia
Nguvu ya processor Exynos 1280
Galaxy A25 inapewa nguvu na processor ya Exynos 1280
Kiuwezo Exynos 1280 ina nguvu ya kufanya kazi nyingi hata zile zinazotumia nguvu kubwa kubwa
Hii inatokana na simu kutumia muundo wa Cortex A78
Kitu kinachoifanya exynos 1280 kuwa na alama zaidi ya 800 kwenye app ya kutesti nguvu za processor
Kwa mfano kwa sekunde moja exynos inaweza kufungua kurasa zaidi ya 50
Hii ni tofauti na chip ya mediatek helio g35 inayofungua kurasa 25 kwa sekunde
mediatek helio g35 imetumika kwenye simu za daraja la chini kama Nokia G20 na Redmi 9C
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Galaxy A25 ukubwa wake ni 5000mAh
Changamoto ukaaji wake wa betri uko chini ya standard ukilinganisha na simu nyingi zenye betri ya 5000mAh
Ukiwa unaperuzi intaneti simu inachukua mpaka masaa 9 na dakika 30 kuisha chaji
Simu nyingi huweza kumudu hadi masaa 12
Kwa samsung zinazotumia chip ya exynos huwa hazina ufanisi mkubwa wa matumizi ya betri ukilinganisha na snapdragon
Chaji yake ina wati 25 ambao ni umeme mwingi wa kuchaji simu kwa dakika chache
Inaichukua simu dakika 84 tu kujaa kutoka 0 hadi 100%
Ukubwa na aina ya memori
Aina ya memori simu inayotumia ni UFS 2.2 kama ilivyo kwa simu nyingi za daraja la kati
UFS husafirisha data kwa kasi kwa maana ukiwa unakopi faili kwenda kwenye simu linawahi kumalizika
Simu imegawanyika katika makundi mawili zipo za GB 128 na GB 256 na mgawanyo wa RAM ni GB 6 na GB 8
Ni vizuri kununua yenye RAM kubwa kama ili uweze kutumia vitu vingi bila kwa wakati mmoja
Ukiwa unacheza gemu RAM hujaa kitu kinachoweza kusababisha kuganda ganda
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A25
Bodi ya Samsung Galaxy A25 ni ya plastiki upande wa nyuma na mbele
Na haina viwango vyovyote vya IP, kwa hiyo sio simu imara kuzuia maji kwani hakuna waterproof
Hivyo unapotumia kwenye mazingira yenye maji au kwenye mvua unapaswa uwe makini ili isikutane na maji
Kwa sababu kama ikizama kwenye kina kirefu haitochukua muda mrefu simu kuanza kuharibika
Kama unajari juu ya muonekano mzuri wa simu kwa muda mrefu huna budi kutumia kava
Ubora wa kamera
Hii ni samsung ya macho matatu kwa maana ina kamera ya wide, ultrawide na macro
Kamera kubwa ina megapixel 50 na ikiwa na OIS na ulengaji wa PDAF
Ubora wa picha hasa kwenye mwingi ni mzuri kwani kamera inapiga picha zenye vitu kwa ustadi
Kama ukizoom picha iliyopigwa na kamera kubwa utaona kiwango kidogo cha noise
Ila ukiacha tu hivi kawaida kwa jicho la kawaida utakuwa na wakati mgumu kutofautisha ubora wa kamera kwenye simu zingine za bei kubwa
Hii kamera inaweza kurekodi mpaka video za 4K
Mara nyingi kamera zinazoweza kurekodi 4K hupiga picha nzuri kwa kiasi kikubwa
Ubora wa software
Samsung Galaxy A25 inakuja na Android 14 na One UI 6
One UI 6 inaambatana na app zingine kama facebook, tiktok, Temu nk
Hizi zote unaweza kuziondoa kama huzihitaji tofauti na simu zingine za daraja la chini
One UI 6 imeepuka kuweka matangazo(ads) ambazo baadhi ya watumiaji hawafurahishwi nayo
Pia one ui 6 ina autoblocker ambayo inazuia app zinazotaka kuingia kwenye simu bila ridhaa yako
Kuna hali kama hiyo kwenye simu za android
Washindani wa Samsung Galaxy A25
Kwa hapa Tanzania bei ya Samsung Galaxy A25 ni kubwa tofauti ne bei halisi inayouzwa huko duniani
Kwani bei yake ni dola 200 ambayo ni kama laki tano na thelathini
Kwa maana hiyo washindani wa samsung galaxy a25 ni matoleo ya zamani ya Samsung S-series mfano Samsung Galaxy S10
Japo kwa sasa Samsung Galaxy S10 utapata used ila ina baadhi ya vitu vinavyokosekana kwenye galaxy a25 kama HDR10+ na waterproof
Washindani wengine ni kutoka kwa kampuni za China kama poco x6 neo, poco m6 pro na motorola edge 40
Poco x6 neo inakuja na waterproof ya kuzuia maji yenye kasi ndogo na pia ina screen protekta ya kioo cha Gorilla Glass 5
Kwa bahati mbaya au nzuri Poco X6 Neo inauzwa chini ya laki tano
Neno la mwisho
Kwa mpenda kamera asiye na uwezo wa kununua Samsung Galaxy S24 Ultra, Galaxy A25 ni mbadala mzuri
Inakupa baadhi ya vitu vichache vinavyopatikana kwenye matoleo ya daraja la juu
Japo haiwezi ikakupa utendaji wa juu kama simu za bei ghari, ila chaguo madhubuti kwa bajeti ndogo
Maoni 2 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy A25 na Sifa zake”
Kwann Samsung galaxy A25 inapata joto sana ukiwa unatumia.?
Inawezekana Betti imeanza kuharibika