SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu Nzuri Za Tecno na Bei Zake 2022

Brand

Sihaba Mikole

February 14, 2022

Tecno ni kampuni ya china ambayo imjikita sana kwenye soko la nchi zinazoendelea.

Kuna baadhi ya simu za tekno ni nzuri lakini sio ubora wa kufananisha na brandi kubwa za za simu kama samsung au xiaomi.

Izingatiwe tekno hutengeneza simu za kiwango cha kati na cha chini(lower-end).

Simu nzuri za tekno mara nyingi hutumia processor(SoC) ya Mediatek Helio G-series.

Ni processor nzuri kwa matumizi ya kawaida.

Pia inafaa tu kwa kiasi chake kucheza gemu.

Simu za tekno zinasifika kukaa na chaji.

Hii inachangakiwa na specifications(sifa) zake ambazo utazifahamu kwa kusoma mada yote.

Hizi hapa chini ni baadhi ya simu bora za tekno zenye bajeti ya kawaida.

Kila simu ya tekno iliyopo kwenye orodha ina sifa tofauti.

Ukifahamu aina ya matumizi yako unaweza fanya chaguzi sahihi kuchagua tecno ipi ya kuwa nayo.

Ni vizuri kufahamu sifa ya kila simu.

TECNO PHANTOM X

Tecno phantom x ni moja ya simu bora ya tecno.

Ubora wa tecno phantom x upo kwenye screen(display) kwa kiasi kikubwa.

Kioo cha tecno phantom x ni super amoled chenye refresh rate ya 90Hz.

Super amoled ni kioo ambacho kina raangi zaidi ya bilioni.

Picha zinazoonekana kwenye super amoled hazipotezi uhalisia ukilinganisha na vioo vya IPS LCD.

amoled-vs-ips-lcd

SoC inayoipa nguvu phantom x ni MediaTek Helio G95.

Ni chip yenye ubora wa kati ambayo inafanya vitu vingi vikubwa.

Memori ina ukubwa wa 256GB na RAM ya 8GB.

Haitumii memori ya kasi kwa sababu Helio G95 husapoti memori za UFS 2.1 kama kiwango cha juu.

Simu ina 4G na haina 5G.

simu-nzuri-tecno-phantom-x

Hii inaweza isiwe tatizo ukizingatia hakuna miundombinu ya 5G afrika mashariki kwa sasa.

Tecno phantom haina waterproof ila kioo chake kina protector ya Gorilla toleo la 5.

Hiki kioo huwa ni kigumu kuvunjika kama simu ikidondoshwa mara nyingi kwa kimo cha mita 1.2 toka juu [reference]

Simu hii ina fast chaji ya wati inayochaji betri lake la 4700mAh kwa asilimia 70 ndani ya dakika 30(kwa mujibu wa tecno).

Kamera yake ni nzuri japo haina OIS.[Internal Link For OIS Explaination].

Simu inakosa ulinzi pindi maji yakipenya kwa maana haina IP68.

Sifa za TECNO pantom X kwa ufupi.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio G95
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.05 GHz Cortex-A76
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G76 MC4
Display(Kioo) Super AMOLED, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
  • HIOS 7.6
Memori  256GB na RAM 8GB
Kamera Kamera tatu

  1. 50MP,PDAF
  2. 13MP
  3. 8MP
  4. 48MP(Selfie Camera)
Muundo Urefu-6.7inchi
Chaji na Betri
  • 4700mAh-Li-Po
  • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) 1,234,359.26/=

TECNO POVA 5G

Simu ya tecno pova 5G ina urefu wa nchi 6.9.

Ni simu pana na ndefu.

Tecno pova 5g inatumia processor bora ya mediatek dimensity 900.

MediaTek dimensity 900 ina uwezo wa kufungua apps kubwa bila kukwama.

simu-nzuri-tecno-pova-5g

Na intaneti yake ikiwemo ya 4G ina kasi kubwa.

Memori ya simu ina uwezo wa kuhifadhi vitu vingi.

Ina ukubwa wa 128GB na RAM ya 8GB.

Storage yake ina kasi(1200Mb/s) kubwa ya kuhifadhi vitu UFS 3.1. 

Kwa mfano,  ukikopi faili la 1GB kwenye simu, simu litamaliza kukopi faili ndani ya sekunde 7.[Reference].

Kamera zake tatu hazina OIS huku kamera kuu ikiwa na megapixel 50.

Mfumo wa kamera tekno pova 5g si wa kuridhisha, hakuna hdr10.

Inatumia display ya IPS LCD ambayo kwa sasa inaenda kupitwa na wakati.

Simu imeundwa kwa plastiki na haina waterproof(IP68).

Ukiingiza kwenye maji, maji yanapenya.

Mfumo wake wa chaji unapeleka chaji kwa haraka lakini kwa umeme mdogo wa wati 18.

Na betri yake 6000mAh inachukua muda wa zaidi ya masaa matatu kujaa.

Betri hii kubwa hutunza chaji muda mrefu.

Sifa za Tecno Pova 5G kwa ufupi.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek  Dimensity 900 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.4 GHz Cortex-A78
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G68 MC4
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 11
  • HIOS 8.0
Memori  128GB na RAM 8GB
Kamera Kamera tatu

  1. 50MP,PDAF
  2. 2MP
  3. QVGA
  4. 16MP
Muundo Urefu-6.9inchi
Chaji na Betri
  • 6000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 709,100/=

TECNO SPARK 8P

Tecno spark 8P ina urefu na upana wa inchi 6.6.

Ni simu iliyotengenezwa kwa ajili ya watumiaji wenye matumizi madogo ya simu.

Kwa maana inatumia processor ya kiwango cha chini ya Mediatek Helio G70.

Memori yake ni kubwa lakini ni zile zenye kasi ya kawaida.

Zinatumia teknolojia ya zamani ya eMMc 5.1

simu-nzuri-tecno-spark-8p

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh.

Mfumo wake chaji unapeleka umeme mdogo wa 10W(wati 10).

Hii inafaya simu kuchukua muda mrefu kujaa(si chini ya masaa matatu).

Kwa mpenzi wa kamera simu haimfai pamoja na kuwa kamera kuu yake ina 50 megapixel.

Lakini haina hdr10 na kuendelea wala OIS.

Hdr10 hufanya kamera kutoa picha mzuri kwenye mwanga mdogo.

Haina 5G bali ina 4G yenye spidi ndogo ya kudownload ambayo ni 100Mbps.

Simu pia haina protector ya gorilla wala waterproof.

Bado ni simu matumizi ya kawaida.

Na inatumia display yenye rangi chache ya IPS LCD.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Helio G70
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.0GHz kryo 460
  • Core Za kawaida(6) – 6×1.8GHz kryo 460
  • GPU-Adreno 619
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 11
  • HIOS 7.6
Memori eMMc 5.1, 64GB,128GB,256GB na RAM 4GB
Kamera Kamera tatu

  1. 50MP,PDAF(Main, wide)
  2. 2MP(depth)
  3. VGA
  4. 8MP(Selfie Camera)
Muundo Urefu-6.6inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-10W
Bei ya simu(TSH) 261,796.00/=

TECNO CAMON 18 PREMIER

Hukuipenda tecno spark 8P?

Basi kuna Tecno camon 18 premier yenye ubora wa kioo, chaji, betri kubwa, kamera na memori kubwa yenye kasi.

Tecno camon 18 premier inatumia processor ya MediaTek Helio G96.

Ni processor yenye ubora wa kati na uwezo wa kufanya kazi kubwa nyingi tu.

simu-nzuri-18-premier

Kioo cha Tecno camon 18 premier ni cha super amoled.

Vioo vya super amoled husifika kuonyesha picha na video kwa uhalisia kutokana na uwezo wa kuonyesha rangi zaidi bilioni 1.

Mfumo wa kamera una kamera tatu.

Kamera ya ultrawide(inapiga eneo kubwa) pekee ina OIS.

Kamera zingine ukiwa unachukua video huku unatembea video inatingishika(haitulii). 

Kamera yake ina uwezo wa kuchukua video ya 4k kwa spidi ya kawaida.

4k huwa zinaonyesha picha clear(safi) sana kwa sababu ya resolution kubwa ya 4000pixels.

Betri ya camon 18 premier ina ukubwa wa 4750mAh.

Kama simu ikiachwa bila kuwasha data, betri linakaa na chaji masaa 112.

Chaji yake hupeleka umeme mwingi wa wati 33.

Umeme huu hujaza simu kwa asilimia 64 ndani ya nusu saa.

Ina memori kubwa na yenye kasi aina ya UFS 2.1

Ina ukubwa wa 256GB na RAM ya 8GB

Sifa za tecno camon 18 premier kwa ufupi.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio G96 
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.05 GHz Cortex-A76
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G57 MC2
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
  • HIOS 8.0
Memori UFS , 256GB na RAM 8GB
Kamera Kamera TATU

  1. 64MP,PDAF(wide)
  2. 8MP(telephoto)
  3. 12MP(ultrawide)
  4. 32MP
Muundo Urefu-6.7inchi
Chaji na Betri
  • 4700mAh-Li-Po
  • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) 1,021,004.40/=

TECNO CAMON 18P

Simu ya camon 18P ina kioo ambacho ni chepesi(smooth) sababu ya refresh rate ya 120Hz.

Kwa bahati mbaya kioo kinatumia IPS LCD na sio AMOLED hivyo ubora wa picha si mkubwa sana.

Ila kioo si ang’avu sana maana kina nits 500.

Chaji yake ina chaji simu kwa kasi kubwa kwa sababu ya kupeleka umeme wa wati 33.

simu-nzuri-camon-18p

Betri ya inatunza moto muda mrefu japo lina ukubwa 5000mAh.

Processor inayoipa nguvu camon 18P ni Helio G96.

Inaweza kuchezi gemu nzito kwa ufanisi mkubwa.

Simu sio imara kwenye upande wa kuzuia maji(haina waterprooof)

Simu ina 4g bila network ya 5G.

Helio g96 modem yake ni ya 4g.

Memori yake inaweza kuhifadhi faili mengi na kuweka apps nyingi.

Storage yake ina ukubwa wa 128GB na RAM ya 8GB.

Hii ni memori ambayo haina kasi kubwa.

Kamera za tecno camon 18P zina ubora wa chini, hazina OIS wala HDR10.

Sifa za tecno CAMON 18P kwa ufupi

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio G96
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.05 GHz Cortex-A76
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G57 MC2
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 11
  • HIOS 8.0
Memori 128GB na RAM 8GB
Kamera Kamera TATU

  1. 48MP,PDAF(wide)
  2. 13MP(telephoto)
  3. 2MP(depth)
  4. 16MP(selfiecamera)
Muundo Urefu-6.8inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) 523,592.00/=

TECNO SPARK 8 PRO

Tecno spark 8 pro ni simu nzuri kwa mtu anayeanza kutumia smartphone.

Na inafaa kwa mtu mwenye matumizi ya kawaida ya simu.

Matumizi kama kuingia mitandaoni, kupiga simu na si kucheza gemu kubwa kubwa.

Inatumia processor yenye uwezo wa kati ya MeidaTek Helio G85

simu-nzuri-tecno-spark-8-pro

Simu ina bodi ya plastiki na kioo chake hakijalindwa na glasi za Gorilla.

Kioo kinatumia IPS LCD, teknolojia ya kioo inayoonyesha rangi chache.

Ina Fast chaji yenye kupeleka umeme wa 33W.

Hivyo betri lake la ukubwa wa 5000mAh linajazwa kwa haraka sana chini ya masaa mawili.

Simu haina 5G wala waterproof bali ina 4G.

Bado kasi yake ya intaneti inaridhisha.

Upande wa kamera kuna kamera kubwa ya megapixel 48 ambayo haina OIS.

Kiujumla kuna kamera tatu lakini simu haina kamera ya MACRO

MACRO ni kamera inayopiga vitu vidogo na ambavyo havipo mbali sana na kamera.

Sifa za Tecno Spark 8 Pro kwa ufupi.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Helio G85 
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.0 GHz Cortex-A75
  • Core Za kawaida(6) – 6×1.8 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G52 MC2
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 11
  • HIOS 7.6
Memori eMMc 5.1, 64GB,128GB na RAM 6GB,4GB
Kamera Kamera TATU

  1. 48MP,PDAF(wide)
  2. 8MP(depth)
  3. 8MP(Selfie Camera)
Muundo Urefu-6.8inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) 323,769.58/=

TECNO POVA 2

Ubora wa tecno pova 2 upo kwenye ujazo mkubwa wa betri.

Ujazo wake unaweza kutunza chaji kwa kipindi cha masaa mengi (zaidi ya 14 kimakadirio) data ikiwa imewashwa.

Ni simu inayotunza chaji ila ina kioo kinachotumi IPS LCD.

Ubora wa picha wa vioo vya IPS LCD si mkubwa sana kulinganisha na AMOLED.

simu nzuri tecno pova 2

Baadhi ya vitu rangi zake zinaweza zisionekane kwa uhalisia.

Chip ya simu ya Tecno Pova 2 ni MediTek Helio G85 yenye ubora wa kati.

Kama ni mcheza magemu sana unaitaji simu zaidi ya hii.

Pamoja na kuwa na betri kubwa mfumo wa chaji wake unapeleka umeme mdogo sana kulinganisha na betri.

Umeme wa wati 18 unachelewa kujaza betri ya hii simu kwa takribani masaa zaidi ya matatu.

Intaneti yake ina 4G yenye kasi ya kawaida.

Kamera zake nne zote hazina HDR10 na haziwezi rekodi video ya 4k.

Tarajia ubora wa kawaida pindi unapopiga picha na picha zisizo onyesha vizuri pale unapotumia kamera kwenye mwanga hafifu.

Bado ni simu nzuri kwa matumizi ya kawaida.

Na ina memori yenye ukubwa wa 64GB yenye RAM ya 4gb na 128GB yenye Ram ya 6GB.

Sifa za simu ya tecno pova 2 kwa ufupi

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Helio G85
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.0 GHz Cortex-A75
  • Core Za kawaida(6) – 6×1.8 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G52 MC2
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 11
  • HIOS
Memori UFS 2.1, 64GB,128GB na RAM 6GB
Kamera Kamera NNE

  1. 48MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(macro)
  3. 2MP(depth)
  4. 2MP(depth)
Muundo Urefu-6.9inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 356,146.54/=

TECNO CAMON 17

Smartphone ya tecno camon 17 ni moja ya simu inayokaa na chaji muda mrefu.

Hilo linatokana na kutumia hardware ambazo hazina vitu vingi vya msingi ambavyo hutumika sana kwenye simu za gharama.

Kioo kina resolution ndogo(720×1600) kulinganisha na simu zilizotangulia.

Kioo cha namna hii huwa hakitumii umeme mwingi lakini huonyesha picha kwa ubora wa kawaida sana.

simu-nzuri-tecno-camon-17

Na pia kioo hakina HDR+

Kamera zake sio nzuri kutokana na kutokuwepo kwa OIS na HDR10.

Lakini wakati wa mchana picha zinatokeo vizuri.

Processor yake ni Helio G85 ambayo imetumika kwenye simu nyingi zilizopo kwenye hii orodha.

Mfumo wa chaji unapeleka moto kidogo wa 18W.

Hii inachelewesha simu kujaa.

Ina 4g na haina 5g.

Kiufupi ni simu nzuri kwa wenye matumizi ya kawaida.

Sifa za tecno camon 17 kwa ufupi.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Helio G85
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.0 GHz Cortex-A75
  • Core Za kawaida(6) – 6×1.8 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G52 MC2
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
  • HIOS 7.6
Memori , 128GB na RAM 6GB,4GB
Kamera Kamera TATU

  1. 48MP,PDAF
  2. 2MP
  3. 16MP(Selfie camera)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 427,620.20/=

TECNO SPARK 7

Simu ya tecno spark 7 haina vitu vikali vingi mbali na kuwa na betri kubwa ya 6000mAh.

Simu haina nguvu ya kutumia app nzito mfano wa gemu.

Kwa sababu processor inayotumika Helio A25.

Intaneti yake ya 4G ina spidi ndogo ya kudownload 150MB/s.

simu-nzuri-tecno-spark-7

Mfumo wake wa kamera ni kawaida kama sio wa chini hazina HDR10 wala OIS.

Kioo kina resolution ya 720×1600 ni HD lakini si bora sana.

Simu ina kamera mbili ambazo haziwezi kupiga picha ya 4K

Picha ikipigwa kwenye mdogo inaweza isionekane vizuri.

Haina fast chaji.

Hii simu inafaa kwa wenye bajeti ndogo.

Sifa za tecno Spark 7 kwa ufupi

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Helio A25
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×1.8 GHz Cortex-A53
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.5 GHz Cortex-A53
  • GPU-PowerVR GE8320
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
  • Android 11
  • HIOS 7.5
Memori eMMc 5.1, 32GB, 64GB na RAM 2GB,3GB,4GB
Kamera Kamera mbili

  1. 16MP,PDAF
  2. 8MP(Selfie Camera)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 6000mAh-Li-Po
  • Chaji-
Bei ya simu(TSH) 235,191.11/=

TECNO CAMON 18T

Simu ya tecno camon 18t ni simu screen kubwa ya kiasi cha inchi 6.8

Ni simu inayokaa kwa muda mrefu na chaja.

Betri ni kubwa yenye ujazo wa 5000mAh.

Processor ni nzuri lakini si nzuri sana kwa kutumia kwenye app kubwa kubwa.

Inatumia processor ya MediaTek Helio G85.

simu nzuri camon-18t

Mfumo wake wa chaji unapeleka umeme wa wastani.

Hivyo Betri inaweza chukua muda wa zaidi ya masaa matatu kujaa.

Chaji yake inapeleka umeme wa 18W.

Ina kamera tatu zinazopiga picha za HD(1080p).

Kamera zake si nzuri kwa maana hazichukui video za 4k.

Na hazina OIS.

Kioo chake si ang’avu na ubora wa kawaida ambacho ni IPS LCD.

Ina memory ya 128GB na RAM 4GB.

Memori haina kasi sana.

Inatumia 4G yenye spidi ndogo ya 150Mbps kwa kudownload.

Kiujumla Tecno camon 8T ni simu nzuri kwa mtumiaji asiye na matumizi makubwa ya simu.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Helio G85
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.0 GHz Cortex-A75
  • Core Za kawaida(6) – 6×1.8 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G52 MC2
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
  • Android 11
  • HIOS 8
Memori 128GB na RAM 4GB
Kamera Kamera TATU

  1. 48MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(macro)
  3. 2MP(depth)
  4. 48MP(selfie camera)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 392,694.00/=

Maoni 5 kuhusu “Simu Nzuri Za Tecno na Bei Zake 2022

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

Bei ya Tecno Spark 20 Pro+ na Sifa zake

Simu ya Tecno Spark 20 Pro+ ilitoka rasmi desemba ya mwaka 2023 ila kwa Tanzania imeanza kupatikana miezi ya karibuni Kwa Tanzania bei ya juu kabisa ya Tecno Spark 20 […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

Bei ya Tecno Spark 20 na Sifa Zake Muhimu

Tecno Spark 20 ni toleo la Tecno lilotoka mwishoni mwa mwaka 2023 hivyo ni simu inayofaa hata kwa mwaka 2024 Bei ya Tecno Spark 20 yenye ukubwa wa memori ya […]

No Featured Image

Bei ya Tecno Spark 4 na Spark 3 Pro na sifa muhimu 2023

Simu za Tecno Spark 4 na Spark ni simu za daraja la chini za mwaka 2019 Spark 3 ilitangulia kabla ya spark 4 Kiteknolojia, hazina vitu vizuri na hivyo basi […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram