SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu Mpya za Samsung na Bei Zake 2023

Brand

Sihaba Mikole

April 20, 2023

Kama unatafuta samsung mpya kwa mwaka 2023 basi upo sahihi

Kwenye hii kuna simu zipatazo saba na maelezo mafupi kuhusu sifa zake

Kwenye hii orodha ya simu mpya za samsung utakutana na matoleo mapya ya A-series na S-series ikiwemo bei zake

A-series inahusisha simu za daraja la mwanzo na S-series ni matoleo ya simu za daraja juu

Hivyo bei zake zinatofautiana kulingana na vigezo vingi

Samsung Galaxy A14

Samsung galaxy ni simu ambayo imeingia sokoni mnamo mwezi machi ya 2023

Ni simu ya 4G inayofanana kwa kiasi fulani na simu ya Tecno Spark 10 Pro

Utendaji wake ni wa kiwango cha kati kwani processor inayotumia ni MediaTek Helio G80

Kioo cha hii simu ni aina ya IPS LCD ambavyo kiubora huzidiwa na vioo vya amoled

Ina betri kubwa la ujazo wa 5000mAh

Mfumo wake wa kamera ni wa kuridhisha na una kamera tatu (unaweza ita samsung macho matatu)

Kasi ya upelekaji wa chaji niĀ  wati 15

Bei ya Samsung Galaxy A14

Bei yake ambayo ina ukubwa wa GB 64 ni shilingi 400,000/= kwa hapa Tanzania

Ipo pia ya ukubwa wa GB 128 na bei yake inakuwa juu zaidi

Kiwango kinaonyesha kuwa hii ndio samsung mpya ya bei nafuu kwa mwaka huu

Samsung Galaxy A14 5G

Samsung Galaxy A14 5G iliingia sokoni mwezi januari mwaka 2023

Hii ilitangulia kabla ya Galaxy 14

Galaxy A14 5G ni simu ya daraja la kati yenye utendaji mkubwa kutokana na kutumia chip Exynos 1330

Kioo chake ni cha aina ips lcd chenye refresh rate kubwa ya 90Hz hivyo kioo kinakuwa chepesi unapotachi

Ni simu ya macho matatu kwa maana kuna idadi ya kamera zipatazo tatu

Kamera kubwa ina megapixel 50

Inakuja chaji kubwa pia ya 5000mAh inayokaa na chaji masaa mengi

Kasi yake ya upelekaji ni wati 15

Kwa kifupi inafanana vitu vingi simu ya mwanzo kinachotofautiana sana ni uwepo wa 5G

Bei ya Samsung Galaxy A14 5G

Bei ya Samsung Galaxy A14 5g hapa Tanzania ni shilingi 490,000/=

Hii ni bei ya samsung ya GB 64 na RAM ya GB 4

Samsung Galaxy A34

Hii ni simu nyingine ya 5G kutoka kwa samsung kwa mwaka huu

Hii simu ilizinduliwa miezi miwili baada ya toleo la Galaxy a14 5G

Galaxy A34 ina ubora kwenye maeneo ukifananisha na matoleo ya A14

Kubwa ni utendaji, galaxy a34 iko fasta kwa sababu ya kutumia chip yenye nguvu ya Exynos 1380

Kioo chake kinaonyesha rangi zilizokolea vizuri zaidi kwani ni cha Super Amoled

Betri yake na yenyewe ni kubwa na ukubwa wa memori unaanzia GB 128 hadi GB 256

Kiujua simu hii kiundani pitia, sifa za samsung galaxy a34

Bei ya Samsung Galaxy A34

Kwa Tanzania, galaxy a34 ya GB 128 na RAM ya GB 6 inauzwa shilingi 750,000/=

Ni bei kubwa kwa wengi ila ubora kwenye maeneo mengi unachangia bei yake kufika huko

Samsung Galaxy A54

Hii ni simu ambayo iliingia sokoni mwezi machi 2023

Kiutendaji inaendana sana na Samsung Galaxy 34 pia ilitoka mwezi huo

Utofauti ni kuwa Samsung Galaxy A54 haipitishi maji na ina eSIM

Pitia: Maana ya eSIM na jinisi ya kujua kama simu yako inayo

Na pia kioo chake ni kizuri sana kina HDR10+, refresh rate ya 120Hz na uangavu unaofika 1000nits

Na kinalindwa vioo vya gorilla 5

Simu inakuja na android 13 ambayo ndio android ya sasa

Na pia ni simu itakayokuwa inapokea matoleo mapya ya android

Tembelea: Sifa za samsung galaxy a54

Bei ya Samsung Galaxy A54

Kwa Tanzania samsung galaxy a54 ya ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 6 inauzwa shilingi 1,300,000/=

Japo simu inawekwa kwenye kundi la daraja la kati lakini hii ni simu ya kundi la daraja la juu

Maana inaiacha mbali sana simu ya Samsung Galaxy Note 10

Samsung Galaxy S23

Simu ya Samsung Galaxy S23 iliingia sokoni mnamo mwezi februari 2023 ikiambatana na matoleo mingi mawili

Hii ni simu yenye kimo kifupi kiasi cha inchi 6.1 na ina betri ya wastani yenye ukubwa wa 3900mAh

Utendaji wa hii simu ni mkubwa sana kutokana na kutumia processor ya Snapdragon 8 Gen 2

Ni samsung ya macho matatu na kamera zake zote zinapiga picha nzuri iwe kwenye mwanga mwingi ama mdogo

Inatumia kioo cha amoled na mfumo wa memori wa wenye kasi wa UFS 4.0

Selfie kamera yake inaweza kupiga picha mpaka za 4K

Ukinunua simu haiji na chaji ila mfumo wake wa chaji unaruhusu mpaka wati 25

Hii ni simu iliyokamilika kila idara

Bei ya Samsung Galaxy S23

Kwa Tanzania bei ya hii simu inauzwa kwa shilingi 2,000,000/=

Galaxy S23 ni simu ya kipekee inachuana na iphone 14

Ni ngumu kuipata kwa bei ndogo kwa nyakati hizi

Hii ni bei ya simu yenye GB 128

Samsung Galaxy S23+

Samsung Galaxy S23+ ina sifa nyingi zinazofanana na S23 na zinatofautiana kidogo

Ukubwa wake kwenye memori unaanzia GB 256

Ina kamera tatu na kamera kubwa ina megapixel 50

Hii ni moja ya simu yenye kamera nzuri kwa mwaka 2023

Kamera zake zinaweza kurekodi video mpaka za 8K

Betri yake ni kubwa na ukaaji wa chaji ni mzuri kwa sababu ukubwa wake wa betri ni 4700mAh

Ni simu ambayo haipitishi maji vilevile

Kuelewa ubora wa hii simu tembele: bei na sifa za samsung galaxy s23+

Bei ya samsung galaxy s23+

Bei ya Samsung Galaxy S23 kwa hapa Tanzania inaanzia 2,500,000/=

Inahitaji kujipanga ukiwa unahitaji kumiliki hii simu

Samsung Galaxy S23 Ultra

Katika simu zote mpya za samsung za mwaka 2023 Galaxy S23 ni ndio kali zaidi

Hii ndio simu yenye kamera kali kushinda simu zingine kwa sasa

Ina jumla ya kamera nne huku kamera moja ikiwa na ukubwa wa megapixel 200

Kamera zote zina teknolojia ya ulengaji za kisasa zinaweza kutambua kitu kitu kinachopigwa picha kwa haraka

Inatumia chip yenye nguvu kama ilivyo kwa matoleo yaliyotoka pamoja

Chip hiyo ni Snapdragon 8 Gen 2

Betri yake ni kubwa na ina ujazo wa 5000mAh

Hivyo ukaaji wa chaji ni kiwango cha juu vilevile

Hapa, kuna maelezo ya kina juu ya ubora wa galaxy s23 ultra

Bei yake

Kwa Tanzania galaxy ya GB 256 inaanzia shilingi 2,900,000/=

Kwa baadhi ya watu wanashangaa kwa nini mtu ununue simu ya bei ya kiwanja

Iwapo unataka utumie simu utakayodumu nayo miaka mingi huna budi kununua simu inafika ama kuzidi milioni

Samsung Galaxy S23 FE

Hii ni simu ambayo bado haijatoka ila ina tarajiwa kutoka mwaka huu 2023

Inatarajiwa kutumia chip yenye utendaji wenye nguvu aina ya Exynoss 2200 kwenye masoko yote duniani

Hii itakuwa samsung s-series yenye bei nafuu kiasi fulani

Ila tarajia kuzidi milioni kama zilivyo zingine

Maoni 26 kuhusu “Simu Mpya za Samsung na Bei Zake 2023

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

iphone thumbnail

iPhone za bei rahisi za kumiliki kwa sasa(2024-2027)

Katika pitapita zangu na kuchunguza simu bora za bei ndogo na ya chini nimekuja kugundua kitu cha kustahajabisha kidogo Wapenzi wa iPhone wenye bajeti ndogo wananunua iphone used hazipokei maboresho […]

[VIDEO]: Simu bora duniani na bei zake 2024

Huu ni muendelezo mwingine wa simu tano ambazo hazitumikii sana na watanzania. Lakini kiulimwengu ni kati ya simu bora duniani kwa mwaka 2024. Hizi ni simu zenye utendaji mkubwa kwenye […]

No Featured Image

Simu Mpya za Samsung 2024 (za bei rahisi na ghari)

Kuna simu zaidi ya tisa zilizotengenezwa na kampuni ya Samsung kutoka Hapa kuna orodha ya simu kumi mpya za samsung ambazo zimetoka mwishoni mwa mwaka 2023 hadi mwaka 2024 Ni […]

Bei ya Samsung Galaxy A25 na Sifa zake

Simu ya Samsung Galaxy A25 ilitoka rasmi mnamo mwezi desemba 2023 Ni simu ya daraja ambayo bei yake kwa Tanzania ni shilingi laki saba (700,000/=), hii ikiwa ni bei ya […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company