SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu ya Samsung Galaxy S23 Ultra na Sifa Zake

Simu Mpya

Sihaba Mikole

February 6, 2023

Kampuni ya Samsung toka Korea Kusini imekuja na toleo jipya la simu za galaxy s-series

Matoleo hayo yapo matatu ikiwemo Samsung Galaxy S23 Ultra

Samsung Galaxy S23 Ultra ni simu ya daraja la juu iliyoingia sokoni mwezi februari mwaka 2023

samsung galaxy s23 ultra

Kikawaida matoleo ya S-Series huwa na ubora kila nyanja kitu kinachofanya bei ya Samsung Galaxy S23 Ultra kuwa zaidi ya milioni mbili

Hii ni simu inayoizidi simu ya Apple iPhone 14 Pro kwenye nyanja nyingi upande wa kamera

Ni moja ya simu bora za samsung kwa kutazama sifa zake zilizofafanuliwa hapa

Bei ya Samsung Galaxy S23 Ultra ya GB 256

Kwa bei ya sasa kwenye masoko ya dunia Galaxy S23 Ultra inapatikana kwa kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tisa (2,900,000/=)

Kwa Tanzania bei inazidi kidogo na kuwa zaidi ya shilingi milioni tatu

Hii ni simu ambayo inachuana na matoleo ya iPhone na baadhi ya simu zingine zenye utendaji mkubwa.

samsung galaxy s23 ultra summary

Ukitazama sifa za simu ya iphone mpya utazikuta pia kwenye samsung s23

Mfano, Galaxy S23 Ultra haipitishi maji ikidumbukia kwenye kina kirefu kwa muda wa nusu saa

Na pia utendaji wake una nguvu kutokana na kutumia chip mpya kutoka qualcomm

Ubora wa kila kifaa na mfumo mzima wa software unachangia sana bei kuwa kubwa kuliko simu zingine za android kwa sasa

Fuatilia kila kipengele uone utofauti wa Samsung Galaxy S23 Ultra na kampuni zingine za simu kama Tecno Phantom X2 Pro

Sifa za Samsung Galaxy S23 Ultra

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
 • CPU – Snapdragon 8 Gen 2
 • Core yenye nguvu sana(1) – 1×3.36 GHz Cortex-X3
 • Core Zenye Nguvu (2) – 2×2.8 GHz Cortex-A715
 • Core Zenye Nguvu Wastani (2)-2×2.8 GHz Cortex-A710
 • Core Zenye Nguvu Ndogo (3)-3×2.0 GHz Cortex-A510
 • GPU-Adreno 740
Display(Kioo) Dynamic AMOLED 2X, Refresh rate:120Hz
Softawre
 • Android 13
 • One UI 5.1
Memori UFS 4.0, 256GB,512GB,1TG na RAM 8GB, 12GB
Kamera Kamera nne

 1. 200MP,Multi-directional PDAF(wide)
 2. 12MP(ultrawide)
 3. 10MP(Telephoto)
 4. 10MP(Periscope Telephoto)
Muundo Urefu-6.8inchi
Chaji na Betri
 • 5000mAh-Li-Po
 • Chaji-45W
Bei ya simu(TSH) 2,900,000/=

Upi ubora wa Samsung Galaxy S23 Ultra

Ni simu yenye kiwango kikubwa cha kuzoom ambayo haipotezi ubora wa picha

Inauwezo wa kuzuia maji kupenya ndani ya simu

Ni simu inayokuja na peni (S pen)

Ina bodi ngumu na kioo kigumu kupasuka

Utendaji wake umeongezeka ukilinganisha na samsung matoleo ya 22

Inakuja na betri kubwa linalokaa na chaji muda mrefu

Inatumia mfumo mpya kabisa wa android

Kiufupi, ni simu bora kama sifa zake zinavyoonekana kwenye makala hii

Uwezo wa Network

Galaxy S23 Ultra ni simu ya 5G inayoweza kutumia aina zote za 5G ikiwemo ya Vodacom Tanzania

Mbali na 5G simu ina uwezo wa kutumia mtandao wa 4G aina ya LTE Cat 24

LTE Cat 24 ina spidi ya kupakua mafaili inayofika 2500Mbps ambayo ni sawa na 312MBps

samsung galaxy s23 ultra network

Spidi hii inamaanisha kuwa faili la ukubwa wa 312MB litapakuliwa kwa sekunde moja tu

Ila kasi hii inategemea sana na nguvu ya mtandao wa simu unaotumia

Kwani kwa hapa nchini hata 5G inayopatikana haiwezi kufikia kasi hiyo

Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy S23 Ultra

Kioo cha Samsung S23 ni aina ya Dynamic Amoled ambacho kina refresh rate 120Hz

Kioo chake kinaoonyesha vitu kwa ubora na rangi halisi huku kikiwa chepesi na kinachoitika haraka unapokuwa unagusa

Hii inasababishwa na refresh rate kubwa

Lakini kumbuka kuwa refresh rate inapoongezeka sana inakuwa inatumia betri kwa kiwango kikubwa

samsung galaxy s23 ultra display

Samsung kioo chake kimewekewa LTPO ambacho kinadhibiti matumizi ya refresh rate

Kama matumizi ya hayaitaji refresh rate kubwa LTPO itapunguza kiwango chake

Kioo kinachagizwa na uangavu mkubwa unaifika nits 1700

Hii inasaidia kioo kuonyesha vitu vizuri hata kwenye mwanga mkali wa jua

Na pia kioo kina uwezo wa kuboresha muonekano wa vitu kwa sababu ya uwepo wa teknolojia HDR10+

Nguvu ya processor Snapdragon 8 Gen 2

Matoleo mapya yote ya Samsung 2023 ya S-Series yanatumia chip aina ya Snapdragon 8 Gen 2

Kwa miaka ya karibuni samsung wamekuwa wakiweka chip za Exynos kwa simu zinazouzwa Ulaya na Afrika

Chip za exynos zimekuwa na tatizo la kupata moto sana na utendaji wa chini

Kwenye app ya Geekbench Snapdragon 8 Gen 2 ina alama 1400, hizi ni alama nyingi inayotoa ishara kuwa processor ina nguvu kubwa sana

Samsung galaxy s23 ultra processor scores

Hakuna gemu yoyote itakayoshindwa kuchea kwenye hii simu

Na uzuri magemu mengi yanacheza kwa fremu zaidi ya 60fps inafanya gemu murua

Kw mfano gemu nzito kama Genshin Impact inacheza kwa fremu 60fps bila kuganda ganda wala simu kupata moto

Kiuhalisia Snapdragon 8 Gen 2 inaicha kwa kiasi flani chip iliyotumika kwenye simujanja ya iphone 14 plus

Uwezo wa betri na chaji

Kwa mujibu wa majaribio ya Tomsguide, Galaxy S23 Ultra imeweza kukaa na chaji kwa muda wa masaa 13 ikiwa inatumia intaneti ya 5G muda wote

Intaneti ya 5G ina kasi kubwa na hivyo inatumia umeme mwingi

Simu inayostahamili masaa zaidi ya 10 ni simu inayotunza chaji sana

samsung galaxy s22 ultra charge

Kwa mfano huu ni kuwa betri yake ya 5000mAh itaweza kukaa muda mrefu na chaji hata kwenye kucheza magemu

Simu inasapoti chaji yenye kupeleka kasi mpaka wati 45

Inachukua nusu saa simu kujaa kwa 65%

Ukubwa na aina ya memori

Samsung Galaxy S23 Ultra inatumia mfumo mpya wa memori aina ya UFS 4.0

UFS 4.0 inaweza kusafirisha data kwa kasi inayofika 42000MBps

Memori yenye kasi kama hii huwa zinaifanya simu kufungua apps kwa haraka na pia kuwaka kwa sekunde chache

Memori zake zinaanzia GB 256 mpaka TB 1 na hakuna sehemu ya memori ya ziada

Hivyo kama unahifadhi kwenye simu mafaili makubwa itakulazimu pia kuhifadhi mafaili kwenye mtandao

Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy S23 Ultra

Galaxy S23 Ultra ina bodi ngumu na ndefu inayofika inchi 6.8

Upande wa nyuma imewekewa kioo cha Gorilla Victus na mbele pia ina kioo hiko

Simu ina IP68 kwa maana ina uwezo wa kuzuia maji kupenya iwapo ikidumbukia kwenye maji ya kina cha mita 1.5 ndani ya nusu saa

samsung galaxy s23 ultra bodi

Hivyo kama simu ikizidi muda huo basi maji yanaweza ingia kwenye simu

Simu ni nzito kiasi kutokana  na kuwa na uzito wa gram 234 na pia inakuja na peni ya stylus

Ubora wa kamera

Samsung Galaxy S23 Ultra inaweza kuwa ni simu yenye kamera nzuri kwa sasa

Ina kamera nne huku mbili zikiwa za Telephoto maalumu kupiga vitu ambavyo vipo mbali sana

Kamera yake inauwezo wa kuzoom kitu mara 120 na kitu kikaonekana vizuri

samsung galaxy s23 ultra kamera mchana

Kwenye mwanga hafifu kamera zake zinaonyesha vitu kwa ufanisi na kwa noise(vitu visivyoitajika) ndogo sana

samsung galaxy s23 ultra kamera usiku

Ni simu nzuri kurekodi video huku ukiwa unaongea

Kwani mfumo wake unaondoa makelele yasiyoitajika na kufanya sauti yako isisikike vizuri

Hata wakati wa kurekodi huku ukiwa unatembea kamera hutulia sana

Na kamera zake zinaweza kurekodi video mpaka za 8K kwa kiwango cha 30fps, hili ni boresho kubwa

Ubora wa Software (Android 13 na One UI 5.1)

Samsung mpya ya 2023 inatumia mfumo endeshi wa Android 13 na mfumo wa One UI 5.1

Kwenye Android 13 unapata uwezo wa kuchagua lugha tofauti tofauti kwa kila app

Kwa mfano, unaweza ifanya facebook kuwa inatumia kiswahili wakati huo instagram iwe inatumia kiingereza

Miaka ya nyuma lugha utakayochagua kwenye mfumo ndio itatumika kwa app zote

samsung galaxy s23 ultra software

Maboresho yapo mengi, mengine unaweza yasoma zaidi kwenye kurasa ya Android 13

Mfumo wa One UI 5.1 una maboresho yake hasa kwenye app ya gallery.

Gallery ya One UI 5.1 imewezesha mfumo wa AI(“akili bandia”) unaotambua picha zenye kasoro

Inaweza kutambua picha zenye resolution ndogo na kuzirekebisha bila kupoteza uhalisia

Hii simu itakuwa inapokea matoleo mapya ya Android kwa kipindi cha miaka minne (4)

Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy S23 Ultra

Simu haiji na chaji hivyo mnunuaji atalazimika kununua chaji ya ziada

Autofocus ya kamera inachelewa kiasi kwenye mwanga mdogo kitu kinachoweza kusababisha kitu kinachotembea kwa kasi kutokea vibaya

Haina sehemu ya memori na pia sehemu ya earphone

Samsung Galaxy S23 Ultra camera

Mtumiaji atalazimika kununua earphone za bluetooth

Baadhi ya earphone za bluetooth hazikai muda mrefu na chaji hasa za china

Earphone zinazotunza zinauzwa bei ghari

Neno la Mwisho

Samsung Galaxy S23 Ultra ni moja ya simu bora kwa mwaka huu 2023

Imekamilika kila idara na itadumu muda mrefu kwa sababu ya kupokea Android mpya hadi 2027

Kama una bajeti ya kutosha hii ni simu ya kuwa nayo vinginevyo simu ya Oppo Reno8 inaweza kuwa mbadara

Maoni 24 kuhusu “Bei ya Simu ya Samsung Galaxy S23 Ultra na Sifa Zake

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

No Featured Image

Simu Mpya za Samsung 2024 (za bei rahisi na ghari)

Kuna simu zaidi ya tisa zilizotengenezwa na kampuni ya Samsung kutoka Hapa kuna orodha ya simu kumi mpya za samsung ambazo zimetoka mwishoni mwa mwaka 2023 hadi mwaka 2024 Ni […]

Bei ya Samsung Galaxy A25 na Sifa zake

Simu ya Samsung Galaxy A25 ilitoka rasmi mnamo mwezi desemba 2023 Ni simu ya daraja ambayo bei yake kwa Tanzania ni shilingi laki saba (700,000/=), hii ikiwa ni bei ya […]

samsung galaxy a15 thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A15 na Sifa Muhimu

Mwezi wa desemba 2023 ni mwezi ambao Simu ya Samsung Galaxy A15 ilizinduliwa Ni simu ya daraja la kati ambayo ina vitu vichache vinavyopatikana kwenye samsung za bei kubwa Ndio […]

samsung a55 showcase

Bei ya Samsung Galaxy A55 na Ubora wake

Samsung Galaxy A55 imetoka mwezi machi mwaka 2024 na ni simu ya daraja la kati Bei ya Samsung Galaxy A55 kwa Tanzania ni shilingi milioni moja na laki moja na […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram