SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu Oppo Reno8 5G na Sifa Zake

Sifa za simu

Sihaba Mikole

January 30, 2023

Oppo Reno8 ni simu ambayo imetoka katikati ya mwaka 2022 ila ni simu shindani 2023

Ni simu ya daraja la kati hivyo sifa zake zina ubora unaoendana na matoleo ya simu za hivi karibuni kama Tecno Phantom X2 Pro

oppo reno8 showcase

Kwa maana hiyo bei ya Oppo Reno8 inazidi milioni kutegemeana na ukubwa wa memori

Hii posti ina maelezo ya kina juu ya bei yake kwa Tanzania, ubora na madhaifu ya hii simu

Kiufupi ni maelezo yanayosaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu Reno 8

Bei ya Oppo Reno8 ya GB 256

Kwa Tanzania, Reno8 ya GB 256 inapatikana kwa shilingi 1,260,000/=

Pamoja na kuwa simu za oppo huwa zina bei kubwa ila kwa simu hii bei inaendana na ubora

oppo reno 8 summary

Oppo hii inatumia chip yenye nguvu na uwezo wa kutumia kamera mpaka ya Megapixel 200

Chip yenye nguvu ndogo haiwezi kuchakata lenzi yenye pixels nyingi mfano mzuri ni simu ya Samsung Galaxy 04

Baadhi ya sifa zake zinaashiria simu ina mapungu machache kwenye hii posti

Sifa za Simu ya Oppo Reno8

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Dimensity 1300
  • Core yenye nguvu sana(1) – 1×3.0 GHz Cortex-A78
  • Core Zenye Nguvu (3) – 3×2.6 GHz Cortex-A78
  • Core Za kawaida(4) – 4×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G77 MC9
Display(Kioo) AMOLED, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 12
  • ColorOs 12.1
Memori UFS 3.1, 256GB,128GB na RAM 8GB
Kamera Kamera TATU

  1. 50MP,PDAF(wide)
  2. 8MP(ultrawide)
  3. 2MP(macro)
Muundo Urefu-6.4inchi
Chaji na Betri
  • 4500mAh-Li-Po
  • Chaji-80W
Bei ya simu(TSH) 1,260,000/=

Upi ubora wa Oppo Reno8

Reno8 inawahi kujaza betri kwa muda mchache kutokana na kuwa na chaji yenye kasi

Ina kioo (display) kinachoonyesha picha kwa uzuri sana

Betri yake inakaa na chaji masaa mengi hata data ikiwa imewashwa

Utendaji wake wa chip unaipa simu uwezo wa kutumia app yoyote hata zile zinazohitaji nguvu kubwa

Kiuwezo inaachwa mbali na simu ya iphone 14 plus ila bei yake inavumulika

Kuilewa hii simu kiundani itakubidi upitie kipengele kimoja baada ya kingine kwenye maelezo yaliyopo

Uwezo wa Network

Simu karibu zote za daraja la juu huja na mtandao wa 5G

Oppo Reno8 pia inatumia aina hii ya mtandao

Na inakubali 5G aina ya NSA na SA, ambapo hapa Tanzania NSA ndio hutumika na mtandao wa Vodacom

NSA kirefu chake ni Non Stand Alone ikimaanisha ni 5G inayotumia miundo mbinu ya 4G

oppo reno8 network

Unaweza kupitia maelezo zaidi: Maana ya 5g na Aina Zake

Simu inatumia 4G ya LTE Cat 21 yenye kasi inayofika ya 1400Mbps ambayo ni sawa na 175MBps

Ukipakua faili la MB 175 simu italidownload kwa sekunde moja

Lakini hilo linategemea aina ya mtandao na uwezo wa kampuni ya simu unayotumia

Ubora wa kioo cha Oppo Reno8

Oppo Reno 8 inatumia kioo cha AMOLED chenye resolution ya 1080 x 2400 pixels

Kiasi hiki cha resolution kinasababisha simu kuonyesha kwa mkorezo wa rangi ulio sahihi

Ukizingatia AMOLED zimetengenezwa kuwa na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi

oppo reno8 display

Kioo chake kinalindwa na vioo vigumu vya Gorilla 5

Uhitaji wa kuweka protekta sio mkubwa sana ila ni muhimu kuchukua tahadhari

Pia simu imewezeshwa kuwa na refresh rate inayofikia 90Hz

Hivyo kioo kinakuwa chepesi wakati wa kutachi

Ukitumia kwenye mwanga mkali yaani juani kioo kitaonyesha vizuri kutokana na uangavu kufika nits 800

Nguvu ya processor Dimensity 1300

Simu inatumia chipset ya Mediatek Dimensity 1300 yenye idadi ya core 8

Core hizi zimegawanyika katika makundi matatu

  • Core zenye nguvu sana
  • Core Zenye nguvu kiasi
  • Core zenye nguvu ndogo

Core kubwa zaidi ina kasi kufanya mizunguko bilioni tatu kwa sekunde (3.0GHz)

oppo reno8 processor

Ni sehemu ya processor ambayo inaifanya simu kuweza kufanya kazi nyingi na kubwa wakati mmoja kwa wepesi

Simu ikiwa na core zote zenye nguvu huwa inakumbana na shida ya kucheza gemu kubwa kama gemu ya mpira ya Dream Soccer

Na pia kadri muda unavyoenda na mafaili yanapokuwa mengi simu inakuwa nzito

Hilo haliwezi linatokea kwenye Oppo Reno8 kwa sababu ya utendaji mkubwa wa processor.

Kwenye GeekBench dimesnity 1300 ina alama 915, hivyo kiuwezo inazidiwa karibu mara mbili na chip ya Apple A16 Bionic

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya oppo Reno8 ina ukubwa wa 4500mAh

Betri ni kubwa na inakaa na chaji kwa karibu masaa 16 iwapo simu ipo kwenye intaneti muda wote bila kuzima data

Unaweza pitia ripoti ya betri hapa: Ukaaji chaji wa Oppo Reno8

Inakuja na chaji inayopeleka umeme unaofika 80W

oppo reno 8 chaji

Kiwango ambacho kinajaza simu kwa dakika 28 tu

Oppo pia ina uwezo wa kuchaji kifaa kingine kwani imewezeshwa na teknolojia ya Reverse Charging (kuchaji kinyume nyume)

Ukubwa na aina ya memori

Utendaji wa simu unachangiwa pia na aina ya memori

Memori yenye kasi ndogo ya kusafirisha data husababisha simu kuwa nzito, kuchelewa kuwaka wakati wa kuwasha na pia app kuchelewa kufunguka

Oppo Reno8 inatumia memori aina ya UFS 3.1

Hizi ni memori zenye kasi sana, usafirishaji wake unafikia 2400MBps

Kwenye upande wa memori kuna reno8 za aina mbili tu na zenye RAM ya GB 8

Kuna reno8 ya GB 128 na ya GB 256 na haina sehemu ya kuweka memori kadi

Uimara wa bodi ya oppo Reno8

Simu imewekewa kioo cha gorilla 5 upande wa mbele kwenye screen

Na upande wa nyuma imeundwa kwa plastiki

Gorilla 5 ni kioo kigumu kuchunika na kuanguka

Kama ukiweka sarafu mfukoni pamoja na simu ni ngumu kioo cha simu kupata michubuko

oppo reno8 bodi

Gorilla 5 hustahamili mipasuko pale inapoanguka kwa kimo cha mita mbili

Simu itapasuka kama ikianguka kwenye sehemu mbaya sana na kwa kimo kikubwa

Kwa bahati mbaya simu haina viwango vya IP mfano wa IP67 au IP68

Hivi ni viwango vinavyoonyesha uwezo wa simu kutopitisha maji wala vumbi

Ubora wa kamera

Simu ina kamera tatu (unaweza iita Oppo macho matatu)

Kamera ya tatu aina ya macro ina ubora mdogo sana

oppo reno8 5g camera

Kamera moja tu ndio ina ulengali wa PDAF tena iliyoboreshwa aina ya Omidirection PDAF

Omidirection PDAF hukitambua kitu kinachopigwa picha kwa muda mchache

Hivyo inaifanya kamera kuipata picha kwa usahihi mkubwa hata kitu kikiwa kinatembea kwa kasi

oppo reno8 5g camera photo quality night

Kwenye video, kamera inaweza kurekodi mpaka video za 4K

Ubora wa Software

Oppo Reno8 inatumia mfumo endeshi wa Android 12 na ColorOs 12.1

ColorOs 12.1 ina app zinazounganisha simu na laptop, utaweza kuhamisha mafaili kati ya vifaa viwili bila kuwa na apppliksheni ya ziada

oppo reno 8 software

Kitu kingine utakachokikuta kwenye ColorOs 12.1 ni muonekano wa kipekee wa emoji

Emoji za oppo huwa zipo tofauti na oppo wenyewe huziita Omoji

Yapi Madhaifu ya Oppo Reno8

Oppo hawajaweka kioo cha Gorilla upande wa nyuma kama ilivyo simu ya iPhone 14 pro

Simu inaweza kuingia maji kama ikidumbukia kwenye maji ya kina cha mita 1.2

Huwezi kuweka memori ya ziada kwenye Reno8 kwani hakuna sehemu ya memori kadi

Kwa wasikilizaji radio, simu haina radio hivyo utalazimika kuetegemea intaneti pekee

Neno la Mwisho

Kiujumla Reno8 ni simu nzuri kwa mwaka 2022 na hata 2023

Ila bei ya Oppo Reno8 inaweza kuingia kwenye ushindani na simu za brand ya Xiaomi na Redmi na hata Realme

Mfano mzuri Xiaomi 12

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

thumbnail oppo

Simu mpya 12 nzuri za Oppo na bei zake 2024

Tangu mwishoni mwa mwaka 2023 mpaka sasa 2024 tayari kampuni ya OPPO toka china wametoa simu zaidi ya 15 za madaraja mbalimbali Hapa utakutana na orodha ya simu mpya za […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

No Featured Image

Bei ya sasa ya Oppo A17K na Sifa Zake

Oppo  A17K ni simu iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2022 mnamo mwezi oktoba Ni simu ya daraja nafuu ambayo haihitaji bajeti kubwa kuimiliki Kwani bei ya oppo A17K haizidi laki tatu […]

google pixel 8 appearance

Google Pixel 8, Simu ya Teknolojia ya Akili Bandia (AI)

Google Pixel 8 na Pro zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi wa kumi tarehe nne Matoleo mapya ya pixel yatatumia toleo la android 14 Android 14 ilitangazwa tangu mwezi wa pili lakini […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram