SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu ya Samsung Galaxy A04 na Sifa Zake

Bei Nafuu

Sihaba Mikole

November 15, 2022

Simu ya Samsung Galaxy A04 ni simu ya daraja la chini ambayo imetoka oktoba 2022

Ni simu ya kawaida kwenye vitu vingi hivyo bei ya samsug galaxy A04 ni chini ya shilingi laki nne

Ukizifuatilia sifa za Samsung A04 utagundua kuwa simu inafaa iwe bei ya chini zaidi

Kwani inaenda moja kwa moja kwenye ushindani na simu za Redmi 10C na Infinix Hot 12

Fuatalia kiundani sifa zote kuanzia bei mpaka utendaji wake ufahamu kama ni simu janja inayofaa kuwa nayo

Bei ya Samsung Galaxy A04 ya GB 64

Kwa Tanzania, simu galaxy A04 inauzwa shilingi 345,000/= ikiwa na ukubwa GB 64 na RAM ya GB 4

Kikawaida bei za samsung huwa juu kulingana na ubora wa simu husika

Simu ya Galaxy A04 haiwezi kuwa sawa na Samsung Galaxy S22 kisifa

Ndio maana S22 bei yake huwa ni kubwa sana ila A04 ina bei ndogo

Kwa maana usitarajie ubora uliopo kwenye Samsung S22 kuukuta kwenye hii simu mpya

Sifa za Samsung Galaxy A04

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Helio P35
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.3GHz Cortex A53
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.8GHz Cortex A53
  • GPU-IMG PowerVR GE8320
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
  • Android 12
  • One UI Core 4.1
Memori eMMC 5.1, ,128GB,64GB,32GB na RAM 3GB,6GB,4GB
Kamera Kamera MBILI

  1. 50MP,AF(wide)
  2. 2MP(depth)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
Bei ya simu(TSH) 345,000/=

Ni Upi Ubora wa Samsung Galaxy A04

Hii ni moja ya samsung inayokaa na chaji masaa mengi kutokana na kuwa na betri kubwa

Ni simu ndefu na inayopatikaa kwa bei inayovumilika

Ina kamera yenye sensa kubwa hivyo vitu vitaonekana kwa uzuri

Inakuja na matoleo ya aina nyingi kweye upande wa memori

Na yenye memori kubwa inakupa nafasi ya kuhifadhi mafaili mengi

Kwenye nyanja zingine simu ina viwago vya kawaida au vya chini kama utakavyoona kwenye posti hii

Uwezo wa Network

Hii ni simu inayosapoti mitandao yote kasoro mtandao wa 5G

Kama unataka simu ya 5G basi kuna Infinix Zero Ultra japo inahitaji bajeti kubwa

Aina ya 4G iliyopo kwenye Samsung A04 ni LTE Cat 7

Kwa maana mtandao wake unaweza kupakua faili kwa spidi inayofikia 300Mbps

Kwenye 4G hapa Tanzania ni nadra kupata mtandao wa simu unaotoa kasi hii

Kama kungekuwepo na kasi hii basi faili la ukubwa wa 750MB lingemalizika kudownload kwa sekunde 20

Ni spidi ya chini sana kama ukifananisha hii simu na simu ya Apple iPhone 14 Pro Max

Zingatia pia kasi ya intaneti mara nyingi huathiriwa na eneo na idadi ya watu wanaotumia intaneti wakati huo

Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A04

Kio cha Samsung Galaxy A04 sio cha amoled au oled isipokuwa inatumia kioo aina ya IPS LCD

Kutokana na simu kutumia chip yenye nguvu ndogo kioo kimewekewa resolution ya 720 x 1600 pixel ambayo ni kiwango cha kawaida kwa simu mpya nyingi

Kwa kifupi, simu ina kioo chenye ubora wa kawaida kwa sababu hakina refresh rate kubwa na hdr

Ukichukua simu ya iPhone 14 Pro Max na hii samsung 04 utashuhudia utofauti mkubwa katika muonekano wa vitu

Nguvu ya processor MediaTek Helio P35

Simu ya Samsung Galaxy 04 inalenga watumiaji wanaoanza kutumia simu janja na wale ambao wana bajeti ndogo

Hivyo simu imeundwa kwa chip yenye nguvu ndogo inayoweza kuhimili matumizi ya kawaida

Inatumia processor ya MediaTek Helio P35 ambayo ina idadi ya core zipatazo nane

Core zote zinatumia muundo wenye utendaji unautumi umeme mdogo, muundo huo ni Cortex A53

Cortex A53 hutumia chaji kidogo lakini utendaji wake kwenye vitu kama magemu aina makubwa si mzuri

Ukiangalia taarifa za app ya geekbench inayopima nguvu za processor za simu. Helio P35 ina alama 169

Hii inamaanisha simu ya Infinix Hot 12 inaizidi ubora Samsung A04

Hapa kuna malezo ya kina kuhusu ubora na udhaifu wa infinix hot 12

Uwezo wa betri na chaji

Smsung A04 ina betri kubwa yenye kiwango cha 5000mAh

Hivyo ukaaji wa chaji utachukua masaa mengi

Ikizingatiwa kuwa simu inatumia chip yenye nguvu ndogo ya uchakataji data

Hii inamaanisha matumizi ya betri yatakuwa ni ya chini

Kikawaida betri za simu zenye 5000mAh huweza kukaa na chaji kwa masaa zaidi ya 14

Kwa bahati mbaya simu haina fast chaji kitu kinachosababisha betri kuchukua muda mrefu kujaa

Ukubwa na aina ya memori

Galaxy 04 ina matoleo karibu sita (6) upande wa ukubwa wa memori na RAM

Kuna ambazo zina GB 32, 64 na 128 pamoja na RAM za 3GB, 4GB, 6GB na 8GB

Simu ikiwa na ram kubwa na memori ya kutosha itahifadhi mafaili mengi na kuwa na uwezo wa kufungua mafaili mengi kwa wakati mmoja

Izingitiwe bei zake zinatofautina, kadri memori inavyokuwa na bei inapanda

Kumbuka kuwa simu inatumia chip (processor) yenye nguvu ndog na hivyo haiwezi kuhimili memori aina ya UFS zinazosafirisha data kwa kasi

Hii inamaanisha samsung galaxy 04 inatumia memori aina ya eMMC

Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A04

Simu imetengenezwa kwa bodi ya plastiki upande wa nyuma na upande wa pembeni

Kwenye screen kuna kioo (glass) lakini sio vioo imara vya gorilla

Kutokana na simu kuwa na bodi ya plastiki ni muhimu kuwa na kava ya simu

Na pia kuweka protekta na kuepuka kuingusha kwenye maji

Kwa sababu simu haina uwezo wa kuzuia maji kupenya ndani ya simu kama ilivyo kwa Samsung Galaxy S21 Ultra

Ubora wa kamera

Hii simu ina kamera mbili tu huku kamera kubwa ikiwa na 50MP

Kamera kubwa haina ubora kutokana na kukosekana kwa teknolojia ya ulengaji wa PDAF

Kwani yenyewe inatumia AF (ambayo imepitwa na wakati)

Kamera nyingine haipigi picha bali hupima eneo linalopaswa kuonekana kwenye picha kutokana na ulengaji wako

Hii kamera huitwa Depth, simu za daraja juu huondoa haina hii ya kamera kwani haina umuhimu mkubwa

Ubora wa Software

Samsung Galaxy A04 imewezeshwa na Android 12 na ikiwa inatumia mfumo wa One UI Core 4.1

One UI Core 4.1 ni mfumo wa samsung ambao hutmika kwenye simu za sasmung zenye nguvu ndogo

Ni mfumo unaoifanya simu kuwa fasta kutokana na kupunguzwa kwa baadhi ya vitu vimepunguzwa

App kama Samsung pay na samsung health hazipo kwenye One UI Core 4.1

Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy A04

Madhaifu ya hii simu yapo mengi ambayo asingetazamwa kiundani kutokana na bei ya galaxy 04 na aina ya watu inaowalenga

Lakini kwa kufananisha na simu ya Redmi 10C inafanya samsung 04 kuwa simu ya bei ghari inayokosa baadhi ya vitu muhimu

Vitu ambavyo vipo kwenye simu ya bei nafuu zaidi ya Redmi 10C

Hili toleo jipya la samsung halina fast chaji, kamera sio ya kuridhisha sana, haina kioo cha gorilla na utendaji wa processor ni mdogo sana

Neno la Mwisho

Kama unatafuta simu mpya ya samsung ya bei nafuu samsung Galaxy A04 inaweza kukufaa

Ila ni simu inayomfaa mtumiaji mweny matumizi ya kawaida

Kwa mtu anaependa picha nzuri hii simu sio chaguo sahihi

 

Maoni 18 kuhusu “Bei ya Simu ya Samsung Galaxy A04 na Sifa Zake

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company