SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu ya Infinix Hot 12 na Sifa Zake Muhimu

Sifa za simu

Sihaba Mikole

June 3, 2022

Simu ya infinix hot 12 ni simu ya android ambayo imetoka mwezi april mwaka 2022

Bei ya infinx hot 12 inaanzia shilingi laki nne kwa maduka mengi Tanzania

Bei yake ni kubwa ukilinganisha na bei ya simu ya infinix hot 11

muonkano wa infinix hot 12

Ila ukitazama vitu vinavyochangia simu kuwa na bei kubwa inafanya Hot 12 kuwa na bei kubwa kuliko uwezo

Pitia hapa kufahamu vitu vinavyofanya simu kuwa ghari na nzuri

Hata hivyo simu hii inaweza kukuvutia kwa kutazama bei yake kwa kuangalia ukubwa wa memori na sifa zake zote.

Bei ya Infinix Hot 12 ya GB 128

Bei ya infinix hot 12 yenye ram ya GB 6 na memori ya GB 128 ni shilingi 415,000/= kwa baadhi ya maduka Kariakoo

Simu ina baadhi ya sifa zinazoizidi simu ya Infinix Hot 12i.

Kitu kinachoifanya hot 12i kuwa na bei ndogo kuliko Hot 12 kwa mwaka huu 2022

Ifuatilie kila nyanja ya hii infinix kwenye jedwari lifuatalo linaloelezea ubora wake

Sifa za Infinix Hot 12

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Helio G85
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.0 GHz Cortex-A75
  • Core Za kawaida(6) – 6×1.8GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G52 MC2
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 12
  • XOS 10.6
Memori 128GB na RAM 8GB,6GB
Kamera Kamera tatu

  1. 13MP, AF(wide)
  2. 2MP
  3. QVGA
Muundo Urefu-6.82inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 420,000/=

Upi ubora wa Infinix Hot 12

Ubora mkubwa wa infinix hot 12 ni kuwa na memori kubwa

Memori ambayo inaiwezesha simu kuhifadhi app nyingi na mafaili ya kutosha

Lakini pia simu ina ukaaji mkubwa wa chaji

infinix hot 12 kwa ufupi

Kwa sababu ina betri lenye ujazo mkubwa

Pia simu ina upelekaji wa chaji wa wastani

Vitu vingine vina ubora wa wastani ama wa chiniĀ  kama utakavyoona mbeleni

Uwezo wa Network

Hot 12 inasapoti mtando wa 4G lakini haina 5G

Aina ya 4g simu inayotumia ni LTE Cat 7

Spidi ya kudownload kwa simu ya LTE Cat 7 inafikia 300Mbps

Infinix Hot 12 network

Japokuwa si rahisi kupata mtandao wa simu unaokupa spidi hii hapa nchini

Uzuri ni kuwa simu ina masafa ya mtandao wa 4G yapatayo 12

Yakiwemo yanayotumika na mitandao ya simu Tanzania

Hivyo intaneti ya 4G inakubali kwa laini zote za simu

Ubora wa kioo cha Infinix Hot 12

Kioo cha infinix hot 12 ni cha aina IPS LCD chenye resolution ndogo

Resoltion ya kioo chake ni 720 x 1600 pixels

Pia unagavu si mkubwa sana kitu kichofanya simu kutoonyesha vizuri ukiwa unaitumia juani

Lakini kioo cha hii simu ni chepesi wakati wa kutachi

Kwa sababu kina refresh rate inayofikia 90Hz

Refresh ya ukubwa inafanya screen kwenda haraka ukiwa unatafuta majina ya kwenye simu au ukiwa unasoma kitabu

Kiujumla kioo cha hot 12 si kizuri ukilinganisha na simu ya infinix note 11

Kioo cha infinix note 11 ni cha Amoled na resolution yake ni kubwa

Nguvu ya processor MediaTek Helio G85

Infinix hot 12 inatumia processor ya mediatek helio g85 katika kufanya kazi zake zote

Helio G85 ni processor ya simu yenye uwezo wa kati

Inaweza kucheza gemu nyingi ila zile gemu kubwa za simu inacheza resolution za chini na kwa FPS chache

Kwa mfano gemu ya Fortnite inacheza kwa 21 FPS na kwa resolution ndogo

Infinix Hot 12 helio g85

Hivyo kuna uwezekano simu ikawa inapata moto sana kama ukicheza gemu kila wakati

Hii ina sabababishwa na core kubwa za Helio G85 kuwa ni aina ya Cortex A75 na sio Cortex A77 auĀ  Cortex A78

Cortex A75 spidi yake ya juu kabisa 2.0 GHz (mizunguko bilioni mbili kwa sekunde)

Cortex Ranking

Na kila mzunguko unaweza kufanya kazi tatu

Kitu kinachofanya processor kuwa na nguvu ya wastani

Na ndio maana app ya kupima nguvu ya chip, GeekBench inaipa alama 358 kwenye core moja

Wakati Helio G96 inapewa alama 541 kwa core moja

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya Infinix Hot 12 ina ukubwa wa 5000 mAh na ni aina ya Li-Po

Ukubwa huo wa betri unaifanya infinix kukaa na chaji kwa wastani wa masaa yanayozidi 14 simu ikiwa kwenye intaneti

Simu nyingi zenye betri la 5000 mAh hutunza chaji

Infinix Hot 12 chaji

Chaji yake inapeleka umeme wa wasatani upatao wati 18

Kiasi hicho cha umeme kinafanya simu kuchelwa kujaa kwa sababu betri yake ni kubwa

Hivyo inaweza kuchukua masaa zaidi ya matatu simu kujaa kwa 100%

Ukubwa na aina ya memori

Kuna toleo moja tu la Hot 12 upande wa memori

Ni toleo ambalo lina ukubwa wa GB 128 na RAM y a GB 6

Infinix hawajaainisha aina ya memori

Lakini chip ya Helio G85 inasapoti memori aina ya eMMC 5.1 na UFS 2.1

Kama infinix hot 12 inatumia UFS 2.1 basi utendaji wake ni mkubwa kiasi

Uimara wa bodi ya Infinix Hot 12

Bodi ya simu ya infinix hot 12 ni ndefu na nzito kiasi

Na pia ni bodi iliyoundwa kwa plastiki

Bodi za plastiki zina kawaida ya kuchunika rangi kadri inavyotumika muda mrefu

Infinix Hot 12 bodi

Kuna ulazima wa kununua kava ya simu na pia kuweka screen protector

Kwa sababu simu haitumii kioo cha gorilla

Vioo vya gorilla huwa ni vigumu kuchunika na kuvunjika hasa Gorilla 5

Ubora wa kamera

Infinix Hot 12 ni infinix macho matatu yenye kamera zenye ubora wa chini

Ubora wake wa kamera unapitwa mbali sana na infinix zero x pro au Redmi Note 10

Kamera zake zina teknolojia ya ulengaji ya kawaida aina ya AF

Autofocus ya AF inalenga vitu kwa taratibu na utoaji wa picha kwenye mwanga mdogo ni wa chini

Infinix Hot 12 Camera

Kibaya kuhusu kamera zingine ni kuwa na resolution ndogo za 2MP na nyingine ni QVGA

Kamera ya QVGA (Quarter Video Graphics Array) ni teknolojia ya kizamani

Kwani ni kamera inayozalisha picha ya upana wa 320p na urefu wa 240p

Ndio maana kamera za hot 12 haziwezi kurekodi video za 4K

Pitia hapa kujua, maana ya 4K na umuhimu wake

Kiujumla simu ya infinix hot 12 haina kamera nzuri

Ubora wa Software

Infinix hot 11 inakuja na mfumo endeshi wa Android 12 unaotumia sofatware ya XOS 10.6

XOS 10.6 ni mfumo mpya kabisa ambao una maboresho kadhaa

Moja ya kitu cha kuvutia kuhusu XOS 10.6 ni kukupa uwezo wa kurudisha picha ulizozifuta kwenye simu

Infinix wanadai mfumo mpya una kitu kinaitwa AI Gallery

AI Gallery unaweza kurudisha picha zote zilizofutwa kwa dakika 30

Ila kitu kibaya kuhusu XOS ni kuwa na matangazo mengi yanayotokea mara kwa mara

Haya matangazo huwa yanakera

Yapi Madhaifu ya Infinix Hot 12

Infinix hot 12 ni simu ya daraja la chini hivyo mapungufu yapo mengi

Kwanza bei yake inaweza kununua simu ya daraja la kati ya Redmi Note 10 Pro

Wakati huo Redmi Note 10 Pro inaizidi infinix kwenye nyanja nyingi

Mfumo wa kamera wa hot 12 hauna OIS wala PDAF

Lakini pia simu inakosa ulinzi wa kulinda simu kutopitisha maji

Kioo chake kina resolution ndogo hivyo uoneshaji wa picha si wa kuvutia

Neno la Mwisho

Kama unapenda simu inayohifadhi vitu vingi basi infinix hot 12 inafaa sana

Ila kama unapenda simu yenye utendaji mkubwa wa kamera na kila kitu kuna machaguo mengi mazuri

Hayo machaguo yana bei inayoendana na bei ya infinix hot 12

Maoni 2 kuhusu “Bei ya Simu ya Infinix Hot 12 na Sifa Zake Muhimu

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Related Articles

No Featured Image

Bei ya Infinix Hot 20i na Sifa Zake Muhimu

Kampuni ya infinix iliingiza sokoni simu ya Infinix hot 20i mnamo mwezi septemba 2023 Hivyo bado simu changa na ni bei ya infinix hot 20i ni ndogo kwa sababu ni […]

Jinsi ya Kutumia GPS kwenye Simu (Hatua kwa Hatua)

GPS kirefu chake ni Global Positioning System, ni mfumo wa utambuzi wa maeneo ambao unasimamiwa na Marekani Simujanja karibu zote zina huu mfumo Una faida kubwa sana hasa kama unajua […]

No Featured Image

Bei ya infinix hot 8 na Sifa Zake 2023

Infinix Hot 8 kwa sasa imekuwa simu ya kitambo kwa sababu ilitoka mwaka 2019 Kutokana na kutoka muda mrefu, simu inauzwa kwa bei ndogo sana hivyo ni nafuu kwa wenye […]

samsung fold 4 camera

Simu 10 Zenye Kamera Nzuri na Bora 2023

Mwaka 2023 yapo mateo ya simu yaliyoingia sokoni yakiwa na kamera nzuri na bora kwa kupigia picha na kurekodi video Kuna simu zenye kamera kali zaidi na mfumo mzuri kwenye […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 624 213 048

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram