SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Jinsi ya kujua ubora wa simu (simu kali na mbaya)

Miongozo

Sihaba Mikole

April 9, 2022

Huu ni muongozo mfupi unaofafanunua vitu vya kuzingatia kujua ubora wa simu

Kujua ubora wa simu itakusaidia kutambua simu nzuri na simu mbaya

Na hautopoteza pesa yako kununua simu isiyokidhi mahitaji yako

Ukivijua hivyo vitu utapata ufahamu sababu ya baadhi ya simu kuwa na gharama sana

Na utaweza kununua simu kwa kuzingatia sifa na sio brand ya simu

Chipset ya simu

Chipset ni kifaa kinachochakata kazi zote simu inayofanya.

Kwenye chipset kuna cpu(processor), gpu, ram, ram, modem, wifi, isp nk

Simu kali huwa na processor yenye nguvu

Nguvu ya processor utaijua kwa kuangalia spidi na aina ya core(muundo)

Spidi chini ya 2.0GHz huwa ni kwa ajili ya processor yenye nguvu ndogo

Spidi kubwa zaidi ya 2.0GHz hutumika na core zenye nguvu.

Lakini kitu muhimu zaidi ni muundo wa processor.

Utakutana na miundo imeandikwa Cortex, Kryo au avalanche upande wa Apple

Miundo ya Cortex

Miundo ya cortex yenye nguvu huanza na 7 mfano Cortex A73, Cortex, Cortex A77 nk

Na miundo mingine huwa ni Cortex X1 na Cortex X2

Na cortex zenye nguvu ndogo huanza na 5 mfano Cortex A53 na Cortex A55

Ukiona sifa za simu kwenye processor ina Cortex A53 au Cortex A55 pekee basi hiyo simu ina uwezo mdogo

Jifunze: Aina ya processor za simu zenye nguvu

Hivyo ukichagua simu yenye processor nzuri kila kitu kitakuwa na utendaji mkubwa

Miundo ya Kryo

Kryo ni miundo ya Cortex iliyoboreshwa na kampuni Qualcomm Snapdragon.

Miundo yenye nguvu ya kryo huitwa gold na yenye nguvu ndogo huitwa Silva

Matoleo ya Kryo yenye utendaji mkubwa huanzia Kryo 400 na kuendelea.

Chini ya hapo ni processor zenye nguvu ndogo.

Miundo ya iPhones(Avalanche na Billzard)

Bei Ya Simu

Lazima uingatie bajeti yako.

Hakuna simu yenye uwezo mkubwa wa processor itakayouzwa chini ya laki tatu

Ukiona simu ya hivyo jua kuw ni mbovu au kuna chembechembe za utapeli.

Na tegemea simu iliyokamilika idara nyingi kwa bei ya juu ya laki nne.

Tazama ubora na bei ya iphone 13 pro max na itel a58

Utofauti ni mbingu na ardhi.

Aina ya Network

Mpaka sasa kuna aina tano za network za simu

  1. GPRS
  2. 2G(second generation)
  3. 3G(third generation)
  4. 4G(fourth generation)
  5. 5G(fifth Generation)

Simu bora hukubali aina zote za network

Simu yenye nguvu ya network hukubali network bands nyingi za 3G na 4G na hata 5G

Simu yenye network bands chache hitakataa kufungua intaneti za baadhi ya laini za simu

Ni vizuri ukafahamu network bands za simu na mtandao unaotumia

Network Bands za mitandao ya simu Tanzania

Vodacom  4G Bands– 3, na 3G Bands-B1(2100 MHz)

Tigo 4G Bands– 20 na 3, 3G Bands- B1 (2100 MHz), B8 (900 MHz)

Airtel 4G Bands-28, na 3G Bands- B1 (2100 MHz), B8 (900 MHz)

Halotel 4G Bands-7, na 3G Bands-B1 (2100 MHz)

TTCL 4G Bands-3 na 40, na 3G Bands- B1 (2100 MHz)

Kama simu inakosa hizo bands basi kuna mitandao haitokubali intaneti

Aina za 4G na 5G

Simu nzuri upande wa network inasapoti aina zote za network za 4G.

Network ya 4G yenye spidi kubwa ya kudownload inaanzia LTE Cat 12

Ukiona taarifa ya simu  inaonyesha 4G yake ni LTE Cat 4 ujue kuwa ina spidi ndogo ya 4G

Kuna aina tatu za msafa ya 5G

  1. Masafa ya mafupi
  2. Masafa ya kati
  3. Masafa marefu

5G ya masafa ya kati na marefu yana spidi kubwa

Simu nzuri ya 5G inapaswa iwe na masafa yanayoanzia 3.5GHz-6GHz(masafa ya kati)

Tofauti na apo unaweza ukwa unapata spidi ya 5G inayotofautiana kidogo na 4G

Moja ya simu inayosapoti aina zote za 4G na 5G ni samsung galaxy s22 ultra

Kioo cha Simu

Simu zenye ubora hutumia vioo vya simu aina ya amoled au oled.

Na kioo huwa ni resolution ya kuanzia 1080 x 2400 pixels na kuendelea

Na kioo chepesi huwa kina refresh rate inayofikia 90Hz kwenda mbele

Vioo vya simu vizrui ni vile vyenye uangavu wa kuanzia 500nits kwenda juu

Ili kioo cha simu kionyeshe picha na video kwa ustadi zaidi, HDR10 au Dolby Vision ni ya muhimu

Kama simu inatumia kioo cha IPS LCD inapaswa resolution kubwa na dynamic range ya angalau HDR10

Teknolojia za Kamera

Kwanza simu nzuri huwa ina kamera za macho matatu zenye resolution ya walau 12MP

Kamera tatu au nne hizo zinaweza kuwa kamera za ultrawide, wide, telephoto, Macro au periscope Teleohoto

Ukiona aina ya kamera ni QVGA, hiyo kamera ni mbaya kwa sababu resolution yake ni ndogo sana

Kamera bora huwa na teknolojia ya OIS(Optical Image Stabilization)

Na huwa na Teknolojia safi ya ulengaji ya dual pixel pdaf au Laser AF

Aina ya Memori

Kwenye simu kuna aina kama tatu hivi za memori

Aina za memori zinatofautiana spidi ya kusafirisha data

Baadhi ya memori hizo ni NVMe, eMMC, na UFS

Na kwenye ram kuna kuna LPDDR4X na LPDDR5

Mfumo wa memori wa NVMe na UFS ina kasi kubwa ya usafirishaji kuliko eMMC

eMMC hutumiwa sana na simu za bei rahisi

Simu bora ya nadroid inapswa itumie memori za UFS na iPhone hutumia NVMe

Simu kali lazima iwe na RAM ya kutosha kuanzia 4GB kwenda juu na ROM ya 64GB na kuendelea

Mfumo Endeshi(Software)

Simu nzuri hutumia matoleo mapya ya mfumo endeshi.

Hata kama simu imekuja na toleo la zamani inapaswa iwe na uwezo wa kudownload toleo jipya.

Kwa mfano sasa hivi kuna toleo jipya la Android 12

Baadhi ya simu haziwezi tumia android 12 kwa sababu hazina sapoti ya software

Lakini kuna simu zinaweza kubadirisha toleo jipya la android kila linapotoka

Uwezo wa betri na chaji

Simu yenye betri kubwa na matumizi mazuri ya umeme hukaa na chaji muda mrefu.

Mara simu zenye uwezo mkubwa zinaweza kukaa na chaji masaa zaidi ya 80 ikiwa haitumiki.

Na zinapswa kukaa na chaji kwa masaa zaidi ya 13 endapo simu ikiwa kwenye intaneti kwa masaa mengi mfululizo

Chaji ya simu bora huweza kupeleka umeme wa wati 25 na kuendelea

Umeme unaochaji na kujaza betri ya simu kwa dakika chini ya 75

Na betri ya simu bora huwa na ukubwa wa 4300mAh kwenda juu

Bodi ya simu

Bodi ya simu kali haipitishi maji hata ikidumbukia kwenye kina kirefu cha mita moja mpaka sita

Simu nzuri hulindwa na vioo vigumu kupasuka aina ya gorilla glass kuanzia toleo la tano

Simu inapaswa iwe na bodi ya glasi upande wa nyuma kuepusha kuchunika kwa rangi

Simu inapswa iwe na uzito wa wastani wa chini ya gramu 228

Na simu inapaswa iwe na upana na urefu wa inchi 6.4 kwenda juu

Mifumo ya Mawasiliano(Bluetooth, Wifi, etc)

Bluetooth ya simu inapaswa iweze kusendi fiaili umbali wa zaidi wa mita 100 kwenye eneo la wazi.

Na mita 40 kwa eneo lisilowazai.

Kwa maana simu inatakiwa iwe na bluetooth 5.0 na kuendelea.

Simu bora huwa na mifumo ya gps zaidi ya mitatu

Wapi pa kupata taarifa za simu?

Sehemu ya kwanza kupata taarifa za simu ni ukurasa wa mtandao husika

Kama unataka kufahamu kuhusu vivo t1 5g tembelea tovuti rasmi ya vivo kutazama sifa zake

Sehenu ya pili ni website ya GSMArena, inaorodhesha karibu vitu vyote vya simu

Taarifa za processor ya simu zinapatikana kwenye tovuti ya nanoreview na notebookcheck

Hata hapa(simunzuri.com) unaweza zipata baadhi ya taarifa lakini si kiundani sana

Maoni 8 kuhusu “Jinsi ya kujua ubora wa simu (simu kali na mbaya)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

display

[VIDEO]: Simu za tecno zenye kamera nzuri zaidi

Tazama ubora wa picha zilizopigwa na simu za Tecno Camon 30, Camon 30 Premier, camon 20 premier na nyininezo

tecno camon premier 30

Ubora wa simu za Tecno Camon 30 na bei zake(Pro, Premier)

Tangu mwezi wa nne kampuni ya walitoa matoleo ya Tecno Camon 30 Matoleo ya Camon 30 yapo matatu ambayo ni ya daraja la kati yaani mid range Ubora wa kiujumla […]

tecno camon 30 thumb

Bei ya Tecno Camon 30 Pro na Sifa Muhimu

Simu ya Tecno Camon 30 Pro ilitangazwa mwezi februari ila imetoka rasmi mwezi wa nne 2024 Ni simu ya daraja la kati(midrange) hivyo bei yake sio sawa na Tecno matoleo […]

tecno camon 30 premier thumbnail

Bei ya Tecno Camon 30 Premier 5G na Sifa zake muhimu

Kwenye matoleo bora ya simu kutoka Tecno, matoleo ya Tecno Camon huja na ubora katika vipengele vingi Hata bei za matoleo ya Camon huzizidi bei za Tecno Spark na Tecno […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company