SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Tecno Camon 30 Pro na Sifa Muhimu

Sifa za simu

Sihaba Mikole

May 21, 2024

Simu ya Tecno Camon 30 Pro ilitangazwa mwezi februari ila imetoka rasmi mwezi wa nne 2024

Ni simu ya daraja la kati(midrange) hivyo bei yake sio sawa na Tecno matoleo ya Spark ama Pop

Bei ya Tecno Camon 30 Pro 5G kwa Tanzania ni shilingi milioni moja na laki tatu(1,300,000)

tecno camon 30 showcase

Hii ikiwa na ukubwa wa GB 512 na RAM ya GB 12

Ubora mkubwa wa Camon 30 Pro upo sana kwenye kamera, software na utendaji bila kusahau kamera

Kiuhalisia kuna ubora kwenye vipengele vingi kama ukitazama kwa umakini sifa za Camon 30 Pro

Sifa za Tecno Camon 30 Pro

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
 • CPU – Mediatek Dimensity 8200
 • Core Zenye nguvu sana(1) – 1×3.1 GHz Cortex-A78
 • Core Zenye nguvu (3) – 3×3.1 GHz Cortex-A78
 • Core Za kawaida(4) – 4×2.0 GHz Cortex-A55
 • GPU-Mali-G610 MC6
Display(Kioo) Super Amoled, Refresh rate:144Hz
Softawre
 • Android 14
 • HIOS 14
Memori UFS 3.1,256GB,512GB na RAM 12GB
Kamera Kamera nne

 1. 50MP,PDAF(wide)
 2. 50MP(ultrawide)
 3. 2MP(depth)
Muundo Urefu-6.78inchi
Chaji na Betri
 • 5000mAh-Li-Po
 • Chaji-70W
Bei ya simu(TSH) 1,300,000/=

Uwezo wa network

Tecno Camo 30 Pro inasapoti mpaka mtandao wa 5G

Ni simu ya laini mbili ambayo haina uwezo wa eSIM

Aina ya 4G inayotumiwa ni hii simu inaitwa LTE Cat 21 yenye uwezo wa kupakua faili kwa kasi ya 4700mbps

Hata hivyo ni nadra kupata kasi hiyo hapa nchini

Kama ingekuwepo basi mtumiji angekuwa anapakuwa mafaili kwa muda mchache

Ubora wa kioo cha Tecno Camon 30 Pro

Tecno Camon 30 Pro inatumia kioo cha Super Amoled chenye resolution ya 1080 x 2436 pixels

Super Amoled huwa na utofauti wa kiwango cha rangi kwa kiwango kikubwa

Kitu kinachofanya kuwa na uwezo wa kuonyesha rangi kiasi cha kuonyesha vitu vizuri kuliko vioo vya IPS LCD

Ndio maana bei ya vioo vya amled huwa ni kubwa

Kinachoongeza ubora kwenye hii simu ni uwepo wa refresh rate ya 144Hz

Refresh rate kubwa ya kiwango hiki inapendeza sana ukiwa unacheza gemu

Kwani inafanya muonekano kuwa “smooth” yaana kioo kinakuwa chepesi unapotachi

Lakini kumbuka sio kila wakati unahitaji refresh rate kubwa

Bahati mbaya kioo chake sio kama cha Tecno Camon 30 Premier kinachopunguza refresh rate automatiki

Nguvu ya processor Mediatek Dimensity 8200

Kila kitu unachofanya kwenye simu kinachakatwa na processor

Processor yenye nguvu inafanya simu kuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi kwa haraka bila kukwama kwama

Camon 30 Pro inatumia chip ya Mediatek Dimensity 8200,

Ina nguvu japo si kama Apple A17 Bioni au Snapdragon 8 Gen 3

Ila hakuna kitu kitachoshindwa kufanyika kwa ufanisi

Ndio maana inaiacha mbali processor ya Mediatek Helio G99 iliyotumika kwenye Infinix Note 40 4G

Unaweza kufungua app nyingi na nzito kwa wakati bila kukwama

Uwezo wa betri na chaji

Betri yake ni kubwa yenye ujazo wa 5000mAh

Ukaaji wa chaji unaweza kuchukua mpaka masaa 14 kwa matumizi ya hapa na pale

Kwa anayeperuzi intaneti masaa yote betri inaweza kuisha baada ya masaa 12

Kwenye kucheza gemu simu inachukua takribani masaa nane kama ukiwa unacheza gemu muda

Kiujumla utendaji kwenye utunzaji chaji ni mzuri na hata unakaribiana na matoleo ya daraja la juu yanayokaa na chaji masaa

Chaji inayokuja na hii simu inapleka umeme wa wati 70

Umeme huu unajaza betri kwa 100% ndani ya dakika 57 kutoka asilimia sifuri

Ukubwa na aina ya memori

Kuna matoleo ya aina mbili ya Camon 30 Pro upande wa memori

Kuna lenye ukubwa wa GB 256 na GB 512 na zote zinakuja zikiwa na RAM ya GB 12

Hii simu haina sehemu ya kuweka memori kadi

Siku hizi matoleo ya bei kubwa wanaachana na matumizi ya memori kadi

Hata hivyo kwa watu wengi GB 512 inatohsheleza kuweka app nyinngi na mafaili ya kutosha na wakati ikabaki nafasi kubwa

Aina za memori zilizopo kwenye hii simu ni UFS 3.1

Uimara wa bodi ya Tecno Camon 30 Pro

Simu haiji na kioo cha gorilla glass ila skrini imewekewa glasi

Na pia inakuja na skrini protekta ya kioo, hutohitaji kugharamika kununua protekta toka dukani

Kwenye moja ya video za youtube mchambuzi mmoja alitumbukiza hii simu kwenye maji

Na kisha ikawa inafanya kazi, ila muda uliotumika ni mdogo

Hivyo ni ngumu kusema uwezo wake wa kuzuia maji ikizingatiwa haijaainishwa kama simu imejaribiwa kwa viwango IP

Kwa ubora wa camon 30 ilifaa iwekewe uwezo wa kuzuia maji wa kiwango IP67

Yaani maji hayapenyi ndani ya simu hata ikizama kwenye kina cha mita moja

Kwa vyovyote vile, ni muhimu kuwa makini kwenye kila aina ya mazingira

Kwa sababu mwisho wa siku kioo ni kioo na hupasuka

Ubora wa kamera

Katika Tecno zenye kamera bora hii ni moja ya hiyo tecno inayokidhi hiyo nafasi

Katika mazingira yote ya mwanga mdogo na mwanga mwingi kamera kubwa inatoa picha vizrui

Hata ukiizoom picha vitu bado vinaonekana kwa ustadi

Japo kuna kitu kimoja nimekiona kwa kutazama baadhi ya picha zilizopigwa na hii simu

Hasa kwenye nyakati za usiku, kuna changamoto ya overexposure

Kwa maana kuna baadhi ya rangi zinakuwa zinaonekana kwa kiwango kikubwa

Japo si kwa picha zote, ila kiwango cha noise ni kidogo kwa maana hata mwanga hafifu picha inaweza onekana vizuri

Kamera inaweza kurekodi mpaka video za 4K na ina OIS

Ubora wa Software

Tecno Camon 30 Pro inatumia mfumo wa Android 14 ukiwa unaambatana na mfumo wa HIOS 14 wa Tecno

Kwenye HIOS 14 kuna matumizi ya AI(akili mnemba) kwenye maeneo mengi

Mfano kwenye wallpaper

Wallpaper ni zile muonekano unaombatana na picha unaokuwa kwenye skrini yako

Simu nyingi huja na wallpaper lakini sio zote mtumiaji atazipenda na anawezae asizipende kabisa

Camon 30 Pro inakupa nafasi ya kutengeneza picha unayoitaka kwa kuandika maandishi yakielezea namna unavyotaka picha ionekane

Washindani wa Tecno Camon 30 Pro

Tecno Camon 30 Pro inaenda kukumbana na ushindani kutoka simu zipatazo kumi na tano

Hizi ni simu kutoka kwa makampuni ya Vivo, Xiaomi na OPPO bila kusahau Samsung

Simu ambazo zinatishia soko kwa tecno ni Vivo V30 Pro, Samsung Galaxy A55, Oppo Reno 11 Pro

Ni wazi kuwa washindani wa Camon 30 Premier ndio washindani wa Pro

Vivo V30 Pro kwa mfano inafanana kila kitu na Camon 30 premier

Ila Vivo ina teknolojia ya HDR10+ inayoongezea skrini kina cha rangi

Pia vivo v30 pro ina kamera ya telephoto inazoom mara mbili kwa kutumia optical zoom

Neno la Mwisho

Kiujumla bei ya Tecno Camon 30 Pro inaendana kwa kiasi kikubwa na sifa ilizo nazo

Na ni wazi kwa nchi ambapo tecno inapatikana kiurahisi ushindani lazima uwe mkubwa

Kitu cha kuzingatia ni kuwa bei yake haiwezi kupatikana chini ya milioni moja kwa wakati huu

Hivyo mnunuaji inabidi awe na bajeti ya kutosheleza

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

tecno camon premier 30

Ubora wa simu za Tecno Camon 30 na bei zake(Pro, Premier)

Tangu mwezi wa nne kampuni ya walitoa matoleo ya Tecno Camon 30 Matoleo ya Camon 30 yapo matatu ambayo ni ya daraja la kati yaani mid range Ubora wa kiujumla […]

tecno camon 30 premier thumbnail

Bei ya Tecno Camon 30 Premier 5G na Sifa zake muhimu

Kwenye matoleo bora ya simu kutoka Tecno, matoleo ya Tecno Camon huja na ubora katika vipengele vingi Hata bei za matoleo ya Camon huzizidi bei za Tecno Spark na Tecno […]

Bei ya Tecno Spark 20 Pro+ na Sifa zake

Simu ya Tecno Spark 20 Pro+ ilitoka rasmi desemba ya mwaka 2023 ila kwa Tanzania imeanza kupatikana miezi ya karibuni Kwa Tanzania bei ya juu kabisa ya Tecno Spark 20 […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company