Kwenye matoleo bora ya simu kutoka Tecno, matoleo ya Tecno Camon huja na ubora katika vipengele vingi
Hata bei za matoleo ya Camon huzizidi bei za Tecno Spark na Tecno Pop
Na hivyo jua kuwa bei ya Tecno Camon 30 Premier 5G GB 512 kwa hapa Tanzania ni shilingi 995,000/= (laki tisa na elfu tisini na tano)
Ubora mkubwa wa Camon 30 Premier unapatikana kwenye nyanja za
- Kamera
- Utendaji wa processor
- Kioo(skrini)
- Kasi ya chaji
Na pia sifa zingine za hii simu zina ubora mzuri kama inavyoonekana kwenye jedwari
Sifa za Tecno Camon 30 Premier 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | LTPO AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 512 GB na RAM 12GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 995,000/= |
Uwezo wa network
Tecno Camon 30 Premier ni simu inayosapti mtandao wa 5G
Haisapoti eSIM kama ilivyo baadhi ya simu za daraja la kati zilizotoka miaka ya karibuni
Haishangazi sana kwa sababu mwitikio wa matumizi ya eSIM kwa Tanzania na Afrika kiujumla sio mkubwa
Camon 30 premier inaweza kutumia 5G za Stand Alone(SA) na Non Stand Alone(NSA)
Ila kwa hapa Tanzania miundombinu inayotumiwa na mitandao ya simu ni NSA
Aina ya 4G simu inayokuja nayo ni LTE Cat 21 yenye kasi ya kupakua faili inayofika Gbps 4.1
Kama mtandao unasapoti Cat 21 utakuwa unapakuwa mafaili kwa sekunde chache
Ni ngumu kwa Tanzania upande wa 4G
Ubora wa kioo cha Tecno Camon 30 Premier
Kioo cha Tecno Camon 30 Premier 5G ni cha aina ya LTPO Amoled
Kioo chake kina resolution ya 1264 x 2780 pixels
Kwa maana kinaonyesha picha zikiwa mkorezo mzuri wa rangi zenye kuonekana kwa ustadi
Vioo vya Amoled huwa na utajiri wa rangi na huonyesha rangi zenye uhalisia
Kwa mfano, kioo cha amoled huonyesha rangi nyeusi halisi kabisa
Mbali na hayo kioo cha hii simu kina refresh rate ya 120Hz
Refresh rate huchakata fremu nyingi kwa muda mfupi
Hivyo simu inakuwa nyepesi na muonekano mzuri pindi unapo-scroll(kutachi simu kwa kuipeleka juu au chini)
Lakini refresh rate kubwa hula umeme mwingi hivyo kuna njia vioo vya siku hizi hutumia kupunguza refresh pindi ikiwa hahiitajiki
Na hapo ndipo teknolojia LTPO(Low-Temperature Polycrystalline Oxide) inapokuja kudhibiti refresh rate
Nguvu ya processor Mediatek Dimensity 8200 Ultimate
Tecno Camon 30 Premier inatumia processor ya dimensity 8200 ultimate kufanya kazi zake
Dimensity imegawanyika katika sehemu tatu ila sehemu yenye nguvu sana inatumia muundo wa Cortex A78
Cortex A78 inaweza kufanya mizunguko mpaka GHz 3(mizunguko bilioni 3 kwa sekunde), na kila mzunguko mmoja unachakata kazi nne
Ndio maana katika test za app ya geekbench, hii processor inaweza kufungua peji 108 kwa sekunde
Tofauti na processor ya Helio G99 inayofungua peji 50 kwa sekunde, na kwa apple a17 bionic ni 160 kwa sekunde
Kiujumla premier 30 inaweza fanya vitu vingi bila kukwama kwama ikiwemo upande wa magemu
Uwezo wa betri na chaji
Simu inatumia betri ya ukubwa wa 5000mAh
Inakaa na chaji masaa 13 kwenye matumizi tofauti tofauti
Ukiwa unacheza gemu muda wote simu inachukua takribani masaa 8 mpaka betri kuisha
Upande wa kasi ya chaji ni kuwa chaji yake inapeleka umeme mwingi unaofika wati 70
Kiasi hiki cha umeme kinaijaza betri kwa dakika 40 toka asilimia sifuri hadi mia
Kiujumla uwezo wa utunzaji chaji ni mkubwa kiasi cha kukaa masaa mengi kwa matumizi ya kawaida
Na nyakati hizi za umeme kukatika mara kwa mara hutohitaji kusubiri masaa matatu simu ijae
Ukubwa na aina ya memori
Kuna toleo la aina moja tu la Camon 30 Premiere upande wa memori
Na toleo hilo ukubwa wake ni GB 512
Hii ni nafasi kubwa inayochukua mafaili mengi na app za kutosha
Labda ndio maana Tecno na wenyewe wameamua kuondoa sehemu ya kuweka memori kadi
Mtindo wa kuondoa memori kadi uliasisiwa na iPhone, na wengine wakafuata
Aina ya memori ya simu ni UFS 3.1
Kwa maana kama unakopi kitu kwenda kwenye simu kitamalizila kwa muda mfupi
Uimara wa bodi ya Tecno Camon 30 Premier
Kama nilivyotangulia kueleza, simu za Camon ni matoleo bora ya Tecno
Bodi ya hii simu nyuma imewekewa aluminiam na sio plastiki
Pia ni simu yenye viwango vya IP54, ikimaanisha ina uwezo maji ya kiwango cha manyunyu(kuchuruzika)
Ila haiwezi zuia maji kama ikizama kwenye kina kikubwa
Kioo chake kina skrini protekta ya Corning Gorilla Glass 5
Gorilla Glass 5 husifika kwa ugumu wa kutopasuka kirahisi kwenye kimo cha mita mbili
Hata hivyo kuwa na skrini protekta nyingine ni muhimu
Ubora wa kamera
Kama unataka Tecno macho matatu basi hii ni moja wapo
Ina kamera aina za ultrawide, wide na telephoto
Hapa nitazungumzia kamera moja tu ya wide(zingine kwenye mada inayojitegemea ya kamera)
Kamera ya kuu(wide) ina megapixel na upigaji wa picha ni mzuri kwenye mwanga na mwanga mdogo
Kwa nyakati za mchana hakuna kiwango kikubwa cha noise kinachoweza kuonekana kwa uwazi
Muonekano wa rangi unaendana na muonekanao wa vitu kwenye mazingira halisi
Hii inachagizwa na ukubwa wa lenzi pia aina ya processor(ISP) ya simu
Ubora wa Software
Camon 30 premier inatumia Android 14 na HIOS 14
Siku hizi simu zimezidi kuongeza matumizi ya AI(Artificial Intelligence) ama akili mnemba kwa kiswahili
HIOS 14 na yenyewe imefuata mwendo huo hasa kwenye kamera
Kwani imewekwa mfumo wa kuitakasa picha ikiwa haijatokea vizuri
Pia AI yake inamuwezesha mtumiaji kuondoa vitu asivyovitaka kwenye picha
Washindani wa Tecno Camon 30 Premier
Hii ni simu ya daraja la kati hivyo basi ipo kwenye kundi lenye washindani wengi
Kwa mwaka huu wa 2024 kuna matoleo ya Samsung Galaxy A55 na Samsung Galaxy A35, Oppo Reno 11 Pro na bila kusahau Xioami 13T
Bei ya Samsung Galaxy A55, Oppo Reno 11 Pro na Xiaomi 13T hazitofautiani sana na Camon 30 Premier
Ila Samsung Galaxy A55 ndio tishio kwa Tecno zaidi kutokana na aina ya bei
Galaxy A55 bei yake ni milioni moja na laki moja na inazidi premier kwenye maeneo ya kioo(skrini), uimara, ubora wa software na upokeaji wa maboresho ya android kwa miaka minne
Haitoshi pia Samsung A55 ina eSIM
Hivyo kuna vitu vinaweza mshawishi mteja kuchagua samsung kuliko Camon 30 Premier
Neno la Mwisho
Kwa sifa za hii simu kwenye vipengele vingi, inatosha kusema kwamba bei ya Tecno Camon 30 Premier inaendana na ubora wake
Kwa wale ambao wanapendelea tecno zenye kamera nzuri hili ni chaguo zuri
Kikubwa Tecno inabidi waongeze baadhi ya vitu vinavyopatikana kwenye matoleo mengine ya daraja la kati ili kuhimili ushindani
Maoni 11 kuhusu “Bei ya Tecno Camon 30 Premier 5G na Sifa zake muhimu”
Mm nko mkoani naipataje pia mnakopeshs
Unapatikana mkoa gani?
Mikoani zipo tunazitaka hizo simu.
Hiyosimu inakopesheka
Kwa sasa hapana
Kunauwezekano wa kupunguza bei
hello muko wapi namba za simu na ni how much tecno camon 30 Pro
Mwanza
Mimi natumia Simu ya Tecno camon 20 tangu mwaka jana mwezi Julia 2023.
Nauliza naweza kuirudisha nikabadirisha nikapewa Tecno camon 30pr?
Mimi ni mteja wa Tecno tangu mwaka 2012 Hadi Leo hii situmii kampuni nyinyine
Mimi nipo kilindi naipataje
Mimi BAKARI MOHAMEDI MTINGITA
Natumia cim kampuni ya TECNO kuanzia mwaka 2010 kwakweli TECNO naipenda sasa nashida na TECNO camoni 30 5g naipataje?