SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ubora wa simu za Tecno Camon 30 na bei zake(Pro, Premier)

Simu Mpya

Sihaba Mikole

June 13, 2024

Tangu mwezi wa nne kampuni ya walitoa matoleo ya Tecno Camon 30

Matoleo ya Camon 30 yapo matatu ambayo ni ya daraja la kati yaani mid range

Ubora wa kiujumla uliopo kwenye simu zote tatu ni kasi kubwa ya kuchaji, mfumo endeshi wa HIOS 14 uliowezesha AI(akili mnemba)

Tutaangalia baadhi ya vitu vilivyomo kwenye hios 14

Na kingine ni kwamba simu zote zinakuja na memori kubwa za kuanzia GB 256

Tuzame kiundani.

Bei za Tecno Camon 30

SIMU BEI(Tanzania)
Tecno Camon 30 690,000/=
Tecno Camon 30 Pro 990,000/=
Tecno Camon 30 Premier 1,250,000/=

Ubora wa software

Simu zote yaani Tecno Camon 30, Tecno Camon 30 Pro na Tecno Camon 30 Premier zinatumia mfumo endeshi wa Android 14

Na pia inaambatana na mfumo wa Tecno wa HIOS 14

HIOS 14 inakuja na vitu vingi vya artificial intelligence yaani akili bandia

Cha kwanza kuna kinaitwa AI Eraser

software hios14

Fikiria upo mtaani unapiga picha, kwenye mtaa kuna watu wanapita kwa nyuma

Ukaja kugundua wapita njia wametokea kwenye picha yako na wewe hutaki

AI Eraser ina uwezo wa kuwaondoa hao watu bila kuharibu uhalisia wa muonekano wa picha

Kitu kingine ni kutengeneza wallpaper unayotaka wewe

ai wallpaper

Unaitengeneza kwa kuifafanulia simu kwa maandishi yanayoelezea muonekano wa wallpaper

Ukishaandika, sehemu itaanza kutengeneza wallpaper kulingana na maelezo uliyotoa

Nguvu ya Processor

Tecno Camon 30 inatumia chip ya Mediatek Helio G99

Wakati huo Tecno Camon 30 Pro na Premier zinatumia chip Mediatek dimensity 8200

Tuangalie uwezo wa kiutendaji wa kila chip

Mediatek helio G99

Utendaji wa mediatek g99 ni wa wastani ila inaweza kufanya vitu vingi

Kwenye core yenye nguvu kubwa helio g99 inatumia muundo wa Cortex A76

Kuna baadhi ya gemu inacheza kwa fps kubwa na kwenye graphics za hd

Zingine ili ucheze vizuri inakulazimu kupunguza ubora wa graphics ili ucheze kwa ultra hd

Kiuhalisia inazidiwa karibu mara mbili na chip ya mediatek dimensity 8200 ambayo ipo kwenye camon 30 pro na premier

Tuangalie sasa 8200 utendaji wake

Mediatek dimensity 8200

Mediatek dimensity 8200 ina ubora mkubwa zaidi ndio maana hata bei za Camon premier na pro ni kubwa

Muundo wake wenye nguvu kubwa unatumia Cortex A78,

Utendaji wa cortex a78 unaweza kusukuma vitu vingi sana vinavyohitaji nguvu kubwa bila kukwama

Ndio maana dimensity 8200 ina alama

Gemu nyingi zinacheza kwa kiwango cha fhd na kwa fremu nyingi

Kwa mantiki hiyo Camon 30 Pro na Camon 30 Premier zitakupa ufanisi stahiki zaidi

Betri na chaji

Simu zote zina betri zenye ukubwa wa 5000mAh na chaji ya wati 70

Kama una haraka ya kwenda sehemu na simu yako haina chaji

Unahitaji dakika 45 kuijaza betri lote kutoka 0 hadi 100

Camon zote zinajitahidi kutunza chaji hata katika matumizi ya intaneti

Kiwastani, na kwa majaribio mbalimbali ukiwa kwenye intaneti simu inakaa karibu masaa 11 kwa kuperuzi

Ila kama ni mchezaji wa gemu utadumu na chaji kwa masaa saba

Ubora wa kioo

Simu zote zinatumia kioo cha Amoled ila kioo cha tecno camon 30 premier ni kizuri zaidi

Tecno Camon 30 na camon 30 premier zinakuja na skrini ya refresh rate inayofika 120Hz

Ila Camon 30 Pro inafika hadi 144Hz

Premier ina ubora wa ziada kwa sababu kioo chake ni cha LTPO AMOLED kikiwa na HDR

Kioo cha namna hii kinadhibiti kiwango cha refresh rate chenyewe na kinaonyesha vitu kwa mkolezo sahihi

Ila Tecno walipaswa waweke angalau HDR10+

Kamera

Tecno Camon 30 Premier inakupa mfumo mzuri wa kamera kuliko camon 30 zingine

Kwa mfano Camon 30 ina kamera mbili moja ina 50MP na OIS huku ya pili ikiwa na 2MP ambayo depth sensor

Depth sensor huwa ni kamera inayopima eneo na kina cha kitu kinachopigwa picha

Hivyo haipigi picha na haina umuhimu kwa sababu teknolojia za PDAF zinafanya hiyo kazi

Camon 30 Premier ina lenzi za ultrawide na wide

Wakati premier ina kamera muhimu za tekephoto, ultrawide na wide

Na Pro na Premier zinarekodi video za 4K

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

display

[VIDEO]: Simu za tecno zenye kamera nzuri zaidi

Tazama ubora wa picha zilizopigwa na simu za Tecno Camon 30, Camon 30 Premier, camon 20 premier na nyininezo

tecno camon 30 thumb

Bei ya Tecno Camon 30 Pro na Sifa Muhimu

Simu ya Tecno Camon 30 Pro ilitangazwa mwezi februari ila imetoka rasmi mwezi wa nne 2024 Ni simu ya daraja la kati(midrange) hivyo bei yake sio sawa na Tecno matoleo […]

tecno camon 30 premier thumbnail

Bei ya Tecno Camon 30 Premier 5G na Sifa zake muhimu

Kwenye matoleo bora ya simu kutoka Tecno, matoleo ya Tecno Camon huja na ubora katika vipengele vingi Hata bei za matoleo ya Camon huzizidi bei za Tecno Spark na Tecno […]

Bei ya Tecno Spark 20 Pro+ na Sifa zake

Simu ya Tecno Spark 20 Pro+ ilitoka rasmi desemba ya mwaka 2023 ila kwa Tanzania imeanza kupatikana miezi ya karibuni Kwa Tanzania bei ya juu kabisa ya Tecno Spark 20 […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company