SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya iPhone 14 Pro na Sifa Zake (Ubora)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

February 5, 2023

Ikiwa unatafuta simu nzuri kwa mwaka 2023 basi iPhone 14 Pro bado inafaa

Japokuwa ni simu iliyotoka mwaka 2022, ila itaenda kushindana na matoleo mapya ya Samsung Galaxy S23 ambayo yatazinduliwa mwezi huu februari 2023

iphone 14 pro showcase

Kwa Tanzania bei yai iphone 14 pro ni zaidi ya shilingi milioni mbili ikitegemea na ukubwa wa memori

Bei yake itakushangaza ila ubora wake uliofafanuliwa kwenye kurasa huu unaweza kukushawishika kuwa simu inastahili kuwa ghari.

Bei ya iPhone 14 Pro ya GB 128

iPhone 14 Pro yenye ukubwa wa GB 128 inauzwa shilingi 2,600,000/=

Kiujumla bei inaweza ikawa kubwa zaidi kutoka duka moja Hadi jingine

Bei nafuu inawezekana kama ukinunua simu mtandaoni kwenye mtandao wa Amazon na AliExpress.

iphone 14 pro summary

Unaweza jifunza hapa, jinsi ya kununua vitu mtandaoni

Ukifuatilia ubora wa iphone 14 pro kuanzia kamera mpaka uimara wa bodi yake utakutana na vitu vingi vilivyoundwa kwa teknolojia zinazoisaida simu kudumu muda mrefu

Mfano mzuri ni chip yake ya apple A16 Bionic Ina utendaji unaozizidi karibu chip zote za Qualcomm ambazo hutumika Sana na Samsung, Xiaomi, Sony na simu zingine za Android

Fuatilia makala yote uilewe iphone hii kiundani

Sifa za iPhone 14 Pro

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Apple A16 Bionic
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×3.46 GHz Everest
  • Core Za kawaida(4) – 6×1.8GHz kryo 460
  • GPU-Apple GPU (5-core graphics)
Display(Kioo) LTPO Super Retina XDR OLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • iOS 16
Memori  NVMe, 256GB,128GB,512GB,1TB na RAM 6GB
Kamera Kamera tatu

  1. 48MP,dual pixel PDAF(wide)
  2. 12MP(telephoto), dual pixel pdaf
  3. 12MP(ultrawide)
Muundo Urefu-6.1inchi
Chaji na Betri
  • 3200mAh-Li-Ion
  • Chaji-
Bei ya simu(TSH) 2,600,000/=

Upi ubora wa iPhone 14 Pro

Kitu Cha kwanza ni utendaji wenye nguvu unaoweza kufungua app nyingi kwa wepesi

Ni simu  ambayo inakuja na uwezo wa kufanya mawasiliano kwa njia ya setilaiti.

Setilaiti itatumika wakati mtandao wa simu ukiwa haupatikani

Ni simu ambayo haipitishi maji hata ikiwa imedumbukia kwenye kina Cha MITA SITA

Ina kamera tatu zenye uwezo wa kupiga eneo Pana Sana na kitu ambacho kipo mbali bila kupoteza ubora.

Ni simu yenye urefu wa wastani na hivyo inapendeza kwa watu wasiopenda simu ndefu Sana.

Kiuhalisia, unaweza usione mapungufu ya hii simu lakini yapo kama utakavyoona mbeleni.

Uwezo wa Network

iPhone 14 pro ni simu ya 5G inayokubali 5G za aina zote.

Kwa maana simu inafanya kazi kwa Masafa ya kati, mafupi na Masafa ya juu

Masafa ya juu Huwa yana spidi kubwa ya intaneti

Ila kwa hapa Tanzania hakuna mtandao unaotumia 5g aina ya mmWave bali kuna NSA ya Vodacom.

iphone 14 pro satellite connection

Pia simu inatumia mtandao wa 4g wenye kukubali Masafa yote ya kampuni za simu nchini.

Kama ukiwa eneo ambalo halishiki mtandao wowote, simu inaweza kutumia setilaiti kutumia meseji

Huduma ni kwa ajili ya nchi ya Marekani na Kanada

Ubora wa kioo cha iPhone 14 Pro

Kioo Cha iphone 14 pro ni aina ya LTPO OLED chenye resolution ya 1179 x 2556 pixels

Na pia kina refresh rate inayofika 120hz.

Refresh rate ikiwa kubwa inafanya kioo chepesi Sana ukiwa unagusa

Kwa bahati mbaya refresh rate kubwa inakula Sana chaji

iphone 14 pro display

Ila vioo vyenye LTPO (Low-Temperature Polycrystalline Oxide) vinaoongeza ama kupunguza refresh rate kulingana na matumzi.

Kama kitu unachokifanya kinahitaji refresh rate kubwa basi LTPO itaongeza kiwango na kinyume chake.

Kioo Cha hii simu kimewezeshwa hdr10 na Dolby vision

Hizi ni teknolojia zinazoboresha muonekano wa vitu na kuonekana wa rangi zake halisi kwa kiwango cha juu.

Nguvu ya processor Apple A16 Bionic

Apple A16 Bionic ndio chip ambayo imetumika kwenye iphone za 2022 japo si zote.

Hii ni processor yenye nguvu na uwezo wa kufanya vitu vingi vikubwa kwa urahisi

iphone 14 pro processor

Kwenye app ya Geekbench chip alama nyingi kuliko chip za kampuni nyingine

Unaweza kuisoma kiundani hapa: Uwezo wa  A16 Bionic kwenye iphone 14 pro max

Uwezo wa betri na chaji

iPhone 14 Pro haiji na chaji kitu kinachomlazimisha mnunuaji kununua chaji yake kama hakuwahi kumiliki iphone

Mfumo wake wake wa chaji unapeleka wati 25 sio kubwa kama Tecno Phantom X2 Pro

Betri ya iPhone 14 Plus inaizidi betri ya iPhone 14 Pro kwa ukubwa wa asilimia 25% kwenye ujazo

iphone 14 pro charge

Lakini iPhone 14 Pro inakaa na chaji masaa karibu 20 ikiwa inatumia intaneti wakati mwenzio inakaa na chaji masaa 16

Unaweza kustaajabu inawezekanaje betri ya 3200mAh kuizidi betri ya 4323mAh.

Ukaaji wa chaji kwenye simu uaathiriwa kwa kiasi kikubwa na aina ya chip(processor) simu inayotumia

Hii simu inatumia chip mpya Apple A16 Bionic ambayo ina ufanisi mkubwa katika matumizi ya nishati ya betri hata ikiwa inafanya kazi kubwa

Ukubwa na aina ya memori

Hii iphone imegawanyika katika sehemu tatu upande wa memori huku zote zikiwa na RAM ya GB 6

Ukubwa wa memori unaathiri bei ya iphone 14 pro kwa kiasi kikubwa

Kwani ya GB 512 yaani GB kule amazon inafika shilingi  milioni 3.8

Hii inamaanisha ya TB 1 yaani GB 1020 inazidi milioni 4.5 kwa hapa Tanzania

Yenye unafuu wa bei ni ile ya GB 128 lakini kwa wingine ukubwa huu hautosholezi kuhifadhi mafaili mengi ya kutosha

Uimara wa bodi ya iPhone 14 Pro

iPhone 14 Pro ni simu inayoweza kudumu muda mrefu na haipitishi maji

Inaweza kuzuia maji kupenya kwa muda wa nusu saaa iwapo ikidumbukizwa kwenye kina cha mita 6

Simujanja za kundi la chini kama Samsung Galaxy A04 hazina uwezo wa kuzuia maji kwa muda na urefu wa kina uliotajwa

Pia simu inatumia kioo cha Gorilla upande wa mbele na nyuma japo haijatajwa aina ya toleo

Ila kava ya simu na protekta sio muhimu sana

Uimara wa bodi unampa mtumiaji uhakika wa kutumia simu hata kwenye mvua kwenye bwawa la kuogelea

Ubora wa kamera

Mfumo wa kamera wa hii hauna tofauti na iPhone 14 Pro Max

Ubora wa hizi simu mbili unafanana kwani kamera ni zilezile.

iphone 14 pro camera

Unaweza tembelea tovuti ya gsmarena kutazama ubora wa picha wa iphone hii mpya

Kiujumla simu ina kamera tatu (macho matatu) ambazo zina lenzi za wide, telephoto na ultrawide

Kamera zake zinarekodi video mpaka za 4K pia zina HDR10 na Dolby Vision teknolojia zinazoboresha muonekano wa vitu na kuvifanya vionekane kama vinavyoonekana kwenye mazingira halisi

Ubora wa Software

Simu inatumia mfumo endeshi mpya wa iOS 16 kama ilivyo kwa iPhone 14 Pro Max

Kuuelewa huu mfumo, tembelea taarifa kuhusu iphone 14 pro max

Yapi Madhaifu ya iPhone 14 Pro

Hii simu imekosa sehemu ya kuwekea memori kadi hivyo kama simu imejaa itakulazimu kulipia “cloud storage” kuhifadhi vitu vyako mtandaoni

Haiji na redio bali mtumiaji atalazimika kutumia intaneti kusikiliza redio uitakayo

Ukininua iPhone 14 Pro Marekani utakuta simu haina sehemu ya kuweka laini

Kwani yenyewe inatumia eSIM

Huduma ya kutumia setilaiti haijasambazwa nchi zote duniani

Simu hii inaongeza gharama za kununua chaji kwa sababu iphone siku hizi haziambatani na chaji

Wenyewe wanadai ni kwa ajili ya utunzaji wa mazingira

Neno la Mwisho

Sifa za iPhone 14 Plus zinaifanya simu kuuzwa kwa bei ghari sana kiasi cha kwamba ni watu wachache kwa Tanzania wanaweza kununua

Bei yake inaenda kushindana na Toleo jipya la Samsung Galaxy 23 ambalo limezinduliwa februari 2023

Hivyo kabla ya kutoa pesa kwa ajili ya iPhone 14 fikiria pia Galaxy 23

 

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

iphone 15 pro max camera thumbnail

Ubora wa iPhone 15 Pro Max Upande wa Kamera[hatari tupu]

Apple iPhone 15 Pro Max ni simu yenye kamera tatu upande wa mbele na kamera moja ya mbele (selfie kamera) Ukifuatilia ubora wake wa kamera utagundua sababu ya kuuzwa bei […]

iphone 15 pro max thumbnail

Bei ya iPhone 15 Pro Max na Sifa Zake

Apple iPhone 15 Pro Max ni toleo jipya la iphone kwa mwaka 2023 Ni simu ya kwanza kutoka Apple kutumia chaji aina ya USB Type C ambazo hutumika na simu […]

iphone 15 pro thumbnail

Bei ya iPhone 15 Pro na Sifa Zake Muhimu

Kama ilivyotarajiwa hapo awali kuhusu ujio wa simu mpya za iphone kwa mwaka huu 2023 Moja ya simu hiyo ni iPhone 15 Pro ambayo imeongezewa utendaji Kiumuonekano hauwezi kutofautisha sana […]

iphone 15 muonekano

Ujio wa Simu mpya za iPhone 15 Septemba 2023

Kwenye tarehe 12 mwezi wa tisa 2023 kwenye ukumbi wa Steve Jobs makao makuu ya apple kutakuwa kuna uzinduzi wa bidhaa kutoka kwa kampuni ya apple Tukio hili litarushwa moja […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram