SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Jinsi ya Kununua Simu Mtandaoni (Hatua kwa Hatua)

Miongozo

Sihaba Mikole

July 3, 2022

Kama unataka simu yoyote kwa bei ya chini hasa hapa Tanzania huna budi kujua jinsi ya kununua simu mtandaoni

Hapa kuna muongozo unaofafanua hatua za kununua simu kupitita mtandao wa Aliexpress

Nimelazimika kuelezea manunuzi ya vitu mtandaoni kwa sababu watumiaji wa tovuti ya simunzuri.com wamekuwa wakiuliza jinsi ya kupata simu mbalimbali kwa bei nafuu.

Mtandao wa aliexpress una simu za aina nyingi ambazo kwa Tanzania zinapatikana kwa bei ya juu kidogo

Kujiunga na aliexpress

Kitu cha kwanza ni kujiunga na aliexpress

Hivyo unapaswa uwe na email na namba ya simu inayofanya kazi

Kuna njia mbili za kuingia kwenye duka la mtandaoni la aliexpress

  1. Kutumia tovuti
  2. Kutumia applikesheni

Kutumia tovuti kwa maana unatumia Google kuingia kwenye linki ya aliexpress.com

Aplikesheni itakulazimu kuingia Google Playstore kwa android au Apple Appstore kwa simu za iPhone

Kujiunga kwa njia ya tovuti

Tembelea au google aliexpress.com

Ukifungua ukurasa wa tovuti hiyo itakuletea ukurasa unaoonyesha  vitu mbalimbali vinavyouzwa humo

Kwa mtumiaji wa simu muonekano wa tovuti upo hivi

tovuti aliexpress mobile

Na kwa mtumiaji wa kompyuta muonekano utakuwa kama ifuatavyo.

tovuti aliexpress desktop

Kwenye kompyuta bonyeza Register(upande wa kulia) na kwa mtu mtumiaji wa simu bonyeza alama inayowakilisha akaunti

tovuti aliexpress mobile 2

Kisha chagua “register”

Kwenye simu itakuja ujumbe ikikutaka uchague e-mail unayotaka kujisajilia

Na kwenye kompyuta inakuletea ujumbe unaokutaka ujaze nchi uliyopo (Tanzania), email na ujaze password (neno la siri) uitakayo

Kujisajili kwenye simu inachukua muda mchache ukiwa umechagua email au akaunti ya FB kama unayo

tovuti aliexpress mobile imekamilika

Ila ukijisajilia kwa kompyuta, aliexpress watatuma ujumbe kwenye email yako

Utabonyeza linki uliyotumiwa ili kukamilisha usajili

Ni vizuri kuzifanya hatua hizi kwa kutumia simu kama unayo

Hivyo download app ya aliexpress playstore na app ya aliexpress appstore kwa iphone

Hatua za kujisajili ni zile zile

Jinsi ya kutafuta simu unayoitaka

Baada ya kukamilisha, app itakuwa tayari kununua simu na kukufikia mpaka eneo unaloishi

Ili uipate simu unayoitaka, inakubidi uitafute simu kwenye sehemu ya kusachi

Andika jina simu kisha bonyeza kitufe cha kutafuta

aliexpress kutafuta simu

Zitakuja picha za simu mbalimbali

Zipo zinazoendana na unachokitafuta wakati mwingine yatakuja matokeo tofauti (mara chache)

Picha za simu zitaonyesha bei ya simu unayoitafuta na gharama za kusafirisha

Utabonyeza ambaye unaona ana gharama nafuu kwako wewe

Na baada ya kuchagua muuzaji unayemtaka, app ya aliexpress itakuletea ukurasa kwa ajili ya malipo ambao una muonekano huu.

Kufanya manunuzi aliexpress

App ya aliexpress itakupa uhuru wa kuchagua aina ya toleo la simu unalotaka

Kwa mfano simu ya iphone 11 pro max iliyopo kuna ya GB 64 na GB 256

Tumechagua ya GB 64, na pia unapewa nafasi ya kuchagua rangi uitakayo (Color: Black)

Ikimaanisha tumechagua iphone 11 pro max nyeusi

Vile vile unaweza kuchagua kampuni unayotaka ikusafirishie mzigo

kuchagua njia ya malipo

Mara nyingi msafirishaji wa uhakika huwa ni Aliexpress Standard Shipping

Pia wapo wanaosaifrisha bure ila mizigo huwa inachelewa sana

Ukiitazama picha ya pili kwenda juu kuna neno limeandikwa Service 75 day buyer protection

Haya ni makadirio ya siku mzigo unapaswa ukifikie ndani ya kipindi cha siku 75

Iwapo siku zikizidi unaweza kudai urudishiwe pesa yako

Jinsi ya kufanya malipo Aliexpress

Baada ya kujaza taarifa zote za simu hatua inayofuata ni kununua simu husika

Ili ununue simu janja aliexpress itakulazimu kulipa kwa Master Card au Visa Card

Huduma ya malipo kwa njia visa card inaweza kufanyika kwa kutumia M-Pesa Visa Card

M-Pesa Visa Card ndio njia rahisi zaidi kwa ambao hawana akaunti za benk

Jinsi ya kutengeneza kadi ya Visa Card kwa M-Pesa

Hatua za kufuata kwenye simu yako

  1. Bonyeza namba *150*00# kwenye laini ya Vodacom Tanzania
  2. Chagua namba nne (4) malipo kwa m-pesa
  3. Chagua namba sita (6) M-Pesa Visa Card

Itakuja menyu yenye machaguo sita

mpesa visa card ya voda

Utachagua namba moja (1) Tengeneza kadi kama hukuwahi kuwa nayo

Utasubiri sekunde chache kisha utaletewa ujumbe wenye taarifa tatu.

  1. Namba ya visa card
  2. Tarehe ya kadi kuisha muda wake
  3. Namba ya cvv yenye tarakimu tatu

Baada ya kukamilisha zoezi la kuunda kadi ya malipo itabidi uiwekee kadi pesa kutoka kwenye akaunti ya M-PESA

Utafuata hatua za awali, ukifikia kwenye menyu ya visa card, chagua namba 3 (Weka Pesa Kwenye Kadi)

Hakikisha unaweka pesa inayoendana na bei ya simu aliexpress, pesa ya kusafirisha mzigo na makato ya mpesa visa card

Makato ya M-Pesa ni 4.3% ya pesa ya kitu unachokinunua na gharama ya usafiri

Kulipia simu na ujazaji wa anuani ya Makazi

Kitu kinachofuata ni kubonyeza kitufe kilichoandikwa “Buy now”

kununua simu yenyewe

Itakuja peji itakayotaka ufuate hatua tatu za kukamilisha muhamala

Hatua hizo ni kama zifuatazo zinaoonekana kwenye picha

hatua za malipo ya visa

Kama uonavyoona, cha kwanza ni kujaza majina yako kamili kama yanavyoonekana kwenye kitambulisho chako cha URAIA au MPIGA KURA

Sehemu ya pili ni kuiingiza namba ya simu unayoitumia

Sehemu ya tatu ni kuingiza anuani yako ya posta

Kama hauna ingiza jina la WILAYA unayoishi (sio lazima kuwa na sanduku la posta)

Kisha unaweka nchi unayotokea (Tanzania) halafu sehemu inayofuata jaza MKOA unaoishi

Na baada ya mkoa jaza jiji (jina la mkoa tena)

Na sehemu ya mwisho namba ya postal code(posti kodi) ya kata unayoishi

Unaweza kuzipata posti kodi za kila wilaya na kata hapa Tanzania kwenye hii linki

post kodi

Baada ya hapo itakuja ukurasa wa kuthibitisha kuwa unataka kununua hiyo simu

kuthibitisha malipo

Hapo utabonyeza “Place order”

Kisha ukurasa unaotaka kujaza taarifa za viza kadi utakuja ukiwa na muonekano huu

kujaza kadi

Chagua hiyo sehemu iliyoandikwa “Add a new card”

Kisha ukurasa utakaojaza taarifa za kadi utatokea ukiwa na muonekano huu wa chini

taarifa za kadi

Sehemu iliyoandikwa Card number utaweka namba za m-pesa visa card uliyotengeneza ambazo huwa zipo 16

Kwenye Cardholder name utaweka majina yako kamili kama yalivyo kwenye kitambulisho(au kadi ya benki) ulichosajilia simu

Sehemu iliyoainishwa kwa neno MM/YY inachukuwa tarehe ya kuisha kwa kadi (expire date)

Ambapo MM inawakilisha mwezi na YY inawakilisha mwaka

Mwezi na mwaka huandikwa kwa tarakimu mbili

CVV ni tarakimu tatu ambazo zipo kwenye kadi(unatumiwa kwenye sms pia), hizi hutumika kwa ajili ya usalama

Baada ya hapo bonyeza kitufe kilichoandikwa Pay Now

Ukifanikiwa basi kazi yako ni kusubiria mzigo ukufikie

Wapi pa kupokea mzigo kutoka aliexpress?

Mizigo mingi huwa inapokelewa kwa njia ya posta ya wilaya uliyoijaza

Kama unanunua simu mtandaoni kupitia aliexpress mzigo unaenda posta mara nyingi

Swali ni kwamba utajuaje mzigo wako umefika posta?

Posta Tanzania wana mfumo wao ambao unaweza kuutumia kutrack mzigo wako

Na pia mzigo ukiwa umefika wahudumu wa posta watakutaarifu kwenda kuchukua simu yako

Na pia kwenye app ya aliexpress utaweza kutrack simu yako wapi ilipofika

Ukienda posta lazima uwe na kitambulisho na malipo ya shilingi 2350/= ili upewe simu yako

Muda unaotumika mzigo kufika Tanzania

Kikawaida inaweza ikachukua wiki tatu (3) mpaka tano (5) mpaka mzigo ukufikie

Wakati mwingine mzigo unaweza kuchukua mpaka miezi mingi

Ila kama utachagua msafirishaji kuwa Aliexpress Standard Shipping mara nyingi mzigo unakufikia wiki tatu mpaka tano

Epuka kusafirisha mzigo na kampuni kama Canaio au China Post

Huwa wanachelewesha kusafirisha mizigo

Kuna nyakati mzigo unaweza usikufikie kabisa

Ila usiwe na wasi hela yako haitopotea.

Nini cha kufanya kama simu haijakufikia?

Kama nilivyosema wakati mwingine muuzaji wa simu aliexpress anashindwa kukuletea mzigo au anakuletea kitu tofauti

Aliexpress inakupa nafasi ya kudai kurudishiwa pesa yako

Hii inafanyika kwa kufungua malalamiko(open dispute) kwenye mfumo wa aliexpress

Muuzaji atayaona malalamiko yako kisha mtaelewana

Kama hamtofikia maelewaona mfumo wa aliexpress utakurudishia pesa yako ndani ya siku kumi tano

Kikawaida unaponunua kitu aliexpress pesa haiendi moja kwa moja kwa muuzaji

Bali inabaki kwa aliexpress mpaka simu itakapokufikia

Ni salama sana kununua kitu aliexpress ukiwa Tanzania.

Wakala wa Aliexpress Tanzania?

Mtandao wa aliexpress hauna wakala wala tawi hapa Tanzania

Njia pekee ya kufanya mawasiliano na aliexpress ni kwa kupitia app au tovuti yao

Izingatiwe kuwa aliexpress ni soko tu la mtandaoni linalojumuisha wauzaji na wanunuaji

Wauzaji wengi ni kutoka China

Hivyo usihangaike kutafuta wakala wa aliexpress Tanzania kwani hakuna kitu kama hiko

Angalizo

Unaponunua kitu(simu) aliexpress jitahidi kusoma reviews(maoni) ya watu waliowahi kununua kabla

Ni sehemu ambayo kuna matapeli pia na bidhaa feki zinapatikana kule pia

Hivyo kuwa mwangalifu ununuapo chochote

Hitimisho

Huu muongozo umefupishwa lakini umegusa sehemu nyingi

Ufupisho huu umekupa picha kiasi chake ya jinsi ya kununua simu mtandaoni kupitia alixepress

Pia unaweza kuutumia huu muongozo kununua vitu vingine aliexpress unaomilikwa na kampuni ya alibaba

Maoni 23 kuhusu “Jinsi ya Kununua Simu Mtandaoni (Hatua kwa Hatua)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

simu ya google pixel thumbnail

Bei ya Simu ya Google Pixel 5 na Sifa Muhimu (2022)

Simu ya Google Pixel 5 ni simu ya Android toleo la 11 iliyotoka mwaka 2020 Pamoja na kuingia sokoni miaka miwili iliyopita bado ni simu inayozizidi simu NYINGI za daraja […]

No Featured Image

GPS ni Nini? Maana na Kazi ya GPS

GPS ni mfumo wa utambuzi wa maeneo duniani unaotumia satelaiti ambao unamilikiwa na nchi ya Marekani Mara ya kwanza wakati unaanzishwa ulilenga matumizi ya kijeshi Ila hali ilianza kubadilika mnamo […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram