SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu ya Google Pixel 5 na Sifa Muhimu (2022)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

July 2, 2022

Simu ya Google Pixel 5 ni simu ya Android toleo la 11 iliyotoka mwaka 2020

Pamoja na kuingia sokoni miaka miwili iliyopita bado ni simu inayozizidi simu NYINGI za daraja za kati za mwaka 2022

simu ya google pixel 5

Kitendo kinachofanya bei ya Google Pixel 5 kuzidi shilingi milioni moja kwa Tanzania

Sifa zake zinafikirisha kiasi kama bei yake inastahili kuzidi milioni moja

Ikizingatiwa kuna matoleo mapya yanayoizidi Pixel 5 kwenye nyanja nyingi na ukubwa wa memori

Bei ya Google Pixel 5 ya GB 128 Tanzania

Bei inatofautiana kutokana na hali ya simu

Pixel 5 ya GB 128 ambayo ni used inauzwa kwa shilingi 1,100,000/=

Kwa baadhi ya wauzaji simu unaweza kuipata hata kwa 950,000/=

simu ya google pixel 5 summary

Kama ilivyoelezwa kwenye utangulizi, simu inapatikana kwa pesa kubwa

Sifa zake zinaweza kukushawishi kuinunua

Ila unaweza ukahairisha kuimiliki kama utazipitia sifa za simu ya xiaomi 12 pro ambayo inaendana bei

Sifa za Google Pixel 5

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 765G 5G
  • Core Zenye nguvu sana(1) – 1×2.4 GHz Kryo 475 Prime
  • Core Zenye nguvu(1)- 1×2.2 GHz Kryo 475 Gold
  • Core Za kawaida(6) – 6×1.8 GHz Kryo 475 Silver
  • GPU-Adreno 620
Display(Kioo) OLED, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
Memori UFS 2.1,128GB na RAM 8GB
Kamera Kamera mbili

  1. 12.2MP,PDAF(wide)
  2. 16MP(ultrawide)
Muundo Urefu-6.0inchi
Chaji na Betri
  • 4080mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 1,100,000/=

Ni upi ubora wa simu ya Google Pixel 5

Google Pixel 5 inaweza kuzuia maji kuingia ndani ya simu

Na inatumia kioo chenye kuonyesha vitu kwa ustadi wa juu.

Ni moja ya simu inayoweza kupoekea matoleo mapya ya Android

Ina kimo cha wastani inayofanya simu kuwa nyepesi kubebeka

Ubora mkubwa wa kipekee wa pixel 5 ni kwenye kamera

Ina software inayosaidia simu kutoa picha safi

Utendaji wake ni wa kuridhisha kutokana na aina ya chip inayotumia

Kiuhalisia , ukitazama ubora wa network mpaka software utaona simu ina mapungufu machache.

Fuatilia zaidi

Uwezo wa Network

Pixel 5 ina aina karibu zote za network ikiwemo 5G

Kwa kuwa Tanzania bado hajianza kutumia 5G basi hatutoiangalia bali tutazamia zaidi 4G

Ila sio mbaya ukafahamu: maana ya 5G ni nini

Aina ya 4G iliyonayo ni ya LTE Cat 18 inayopatikana kwenye modem ya X52 ya Qualcomm

Spidi ya juu ya kudownload ya Cat 18 ni 1200Mbps (Ni kubwa)

Ila tia akilini hakuna mtandao wa simu Tanzania unaotoa kasi hii

Japokuwa Google huwa wanalenga nchi zilizoendelea ila simu ina masafa yote ya 4G yaliyopo Tanzania

Ubora wa kioo cha Google Pixel 5

Hii simu inatumia kioo cha OLED

Vioo vya OLED huwa vinasifika kuwa na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi

Ubora wake unachagizwa na kuwa na refresh rate inayofika 90Hz

simu ya google pixel 5 kioo

Refresh rate kubwa huwa inaifanya simu kuwa nyepesi unapokuwa unacheza gemu ama kuperuzi majina au sms

Kioo kinakuwa kinabadirika kwa haraka

Kitu kizuri kingine ni kuwa simu inatumia HDR10+ kitu kinachosaidia kioo kuonyesha vitu vinavyoendana na jinsi vinavoonekana kwenye mazingira.

Resolution yake ya 1080 x 2340 pixels inaongeza ubora mwingine wa kioo

Nguvu ya processor Snapdragon 765G 5G

Katika kitu unachopaswa kukitazama kwa makini unapohitaji kununua simu basi ni processor

Kila kitu unachokifanya kwenye simu kinafanyiwa kazi na processor

Processor ikiwa dhaifu basi jua kuwa una simu mbaya

simu ya google pixel 5 processor

Pitia : Jinsi ya kujua ubora wa processor ya simu

Google Pixel 5 inatumia processor yenye nguvu ya Snapdragon 765G 5G

App ya geekbench inaipa alama 585 kwenye core moja

Ijapokuwa uwezo wake unazidiwa mbali sana Snapdragon 8 gen 1

Ila inaweza kucheza gemu za kila aina zingine kwa resolution kubwa

Nguvu kubwa inatokana na muundo wa chip ambao una core mbili zenye kubwa zinazoitwa Kryo 475 prime na Gold

Uwezo wa betri na chaji

Uwezo wa simu kukaa na chaji ni wa kuridhisha kiasi fulani

Kwa sababu ikiwa inatumia intaneti mfululizo ukaaji wa moto unadumu kwa masaa 12

Ukaaji wa chaji unachangiwa na ukubwa wa betri kuwa ni 4080mAh

Chaji yake inapeleka umeme wa wastani

Kwani kiasi cha umeme kinachopelekwa na chaji ni wati 18

Google Pixel 5 inaweza kutumika kuchaji kifaa kingine

Ina mfumo unaoitwa Reverse Charging

Hivyo unaweza ukachaji simu nyingine kwa kuunganisha waya kuelekea kwenye simu ya google

Ukubwa na aina ya memori

Pixel 5 ina toleo la aina moja pekee

Toleo hilo lina ukubwa wa GB 128 na RAM GB 8

Pamoja na ukubwa huo wa memori, simu hii ya google imewekewa memori aina ya UFS 2.1

UFS 2.1 husafirisha data kwa kasi kubwa inayofikia 1200MBps

Memori za aina ya eMMC 5.1 husafirisha data kwa kasi ndogo

Aina ya memori za UFS huongeza uwezo wa simu kiutendaji

Uimara wa bodi ya Google Pixel 5

Simu ya Google Pixel 5 imetengenezwa kwa glasi za gorilla 6 upande wa nyuma

Na kwenye screen ina Gorilla 6

Gorilla 6 ni vioo stahimilivu kuvunjika

Simu inaweza isipasuke kama ikianguka kwa kimo cha mita 1.2

simu ya google pixel 5 bodi

Japokuwa hilo linategemeana na vitu vingi

Pixel 5 ni moja ya simu isiyopitisha maji kama ukiizamisha kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa nusu saa

Uthibitisho ni kuwa simu ina viwango vya IP68

Lakini pia ni simu inayotumia laini moja pekee na haina sehemu ya kuweka memori card

Lieke akilini hilo

Ubora wa kamera

Pixel 5 ina kamera mbili aina ya wide(kamera kuu) na ultrawide

Ultrawide hutumika kupig picha eneo pana mfano uwanja wa mpira na kutokea eneo lote kwa nyuzi 117

Baadhi ya picha ambazo hii simu imezipiga kwenye mwanga haifiu zimetokea vizuri

Ukiitazama hii picha utaona kuwa,

simu ya google pixel 5 kamera

Kamera inajitahidi sana kuonyesha rangi sahihi za vitu ambavyo vimetokea

Contrast imejitahidi kuweka mlinganyo sahihi wa rangi

Hata nyakati mchana ustadi wa picha unaonekana kwa usahihi ambao hauthiriwi na mwanga mwingi wa jua

Uzuri wa picha unachangiwa na software ya google camera na ulengaji wa dual pixel pdaf

Simu ina kamera zinazoweza kurekodi video za 4K

Ubora wa Software

Simu inakuja na Android 11

Lakini inapokea toleo jipya la android 12

Ukiwa na simu za google pixel utakuwa unapata android yenyewe halisia

Na pia utaweza kuwa unapokea matoleo mapya mara kwa mara

Kumbuka Google wako vizuri sana kwenye swala la software kuliko hardware

Yapi Madhaifu ya Google Pixel 5

Udhaifu mkubwa ni simu kutokuwa na sehemu ya memori kadi

Kwa nyakati za sasa GB 128 inaweza ikawa ndogo

Maana watu wanahifadhi video na magemu makubwa kiasi cha kwamba simu inaweza ikajaa haraka

Lakini ukiwa unarekodi sana video za 4K memori ya simu inaweza kuwahi kujaa

Simu haina sehemu ya kuweka earphone

Hivyo itakulazimu uwe unatumia earphone za bluetooth

Google Pixel 5 inatumia laini moja

Watanzania wengi hupendelea simu inayokubali laini mbili

Neno la Mwisho

Bei ya Google Pixel 5 inaendana na ubora wa simu kwa kiasi kikubwa

Ila kutokuwepo kwa earphone jack, sehemu ya memori card na kutumia laini moja inaweza ikawa sononesha baadhi ya watumiaji

Mbadala mzuri wa simu hii inaweza ikawa Redmi Note 11 Pro+ 5G

Ila hata Infinix Note 12 VIP inaweza ikafaa japo nayo bei si rafki ukilinganisha na ubora

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Related Articles

google pixel 7 pro thumbnail

Bei ya Google Pixel 7 Pro na Ubora wake 2023

Google pixel 7 Pro ni moja ya simu inayosifika kuwa na kamera bora kwenye orodha ya simu mbalimbali Ubora wa kamera unachagiza bei ya Google Poxel 7 Pro kukaribia milioni […]

mtandao aliexpress

Jinsi ya Kununua Simu Mtandaoni (Hatua kwa Hatua)

Kama unataka simu yoyote kwa bei ya chini hasa hapa Tanzania huna budi kujua jinsi ya kununua simu mtandaoni Hapa kuna muongozo unaofafanua hatua za kununua simu kupitita mtandao wa […]

No Featured Image

GPS ni Nini? Maana na Kazi ya GPS

GPS ni mfumo wa utambuzi wa maeneo duniani unaotumia satelaiti ambao unamilikiwa na nchi ya Marekani Mara ya kwanza wakati unaanzishwa ulilenga matumizi ya kijeshi Ila hali ilianza kubadilika mnamo […]

simu ya google pixel 5 5g thumbnai

Simu Nzuri za Google Pixel na Bei Zake (2022)

Kwenye ukurasa huu kuna orodha ya simu kumi za google pixel na bei zake Google Pixel ni simu nzuri za android ambazo huwa zinapiga picha safi na bora Na kiuhalisia […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 624 213 048

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram