Google Pixel 8 na Pro zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi wa kumi tarehe nne
Matoleo mapya ya pixel yatatumia toleo la android 14
Android 14 ilitangazwa tangu mwezi wa pili lakini bado haijazinduliwa rasmi
Hivyo matoleo ya google mapya yakizinduliwa yatairasimisha android 14
Google Pixel inakuja na teknolojia ya akili bandia(artificial intelligence ) kwenye baadhi ya app
Yaani simu itaweza kutambua vitu kwenye picha, kutafsiri kwa haraka na mengineyo mengi
Sifa za muhimu zinazotarajiwa
Google Pixel 8 na Pro inaangaziwa kuja na memori zenye muundo wa UFS 4
UFS 4 ina ufanisi wa kutumia umeme kidogo na kuwa na kasi kubwa ya kusafirisha data
Kwenye software pixel mpya zitapewa nguvu na Android 14
Kwa watalaam tayari wamekuwa wakiijaribu android 14 tangu mwezi wa pili
Japo simu nyingi zinatoka na android 13, kwa mwaka huu mwishoni simu mpya zitakuwa zinatumia android mpya kabisa
Simu inatarajiwa kuja na kioo cha amoled kilichowezeshwa na teknolojia ya HDR10+ kama ilivyo kwa simu nyingine za daraja la juu
Na vitu vingine vitafafanuliwa pindi ikiingia rasmi sokoni mwezi wa kumi
Akili bandia(AI)
Google wameendelea kuweka mkazo kwenye matumizi ya Artificial Intelligence(kwa maana isiyo rasmi tuite akili bandia)
Simu hii inakuja na kitu kinaitwa Magic Eraser na Photo Unblur
Kwa mfano umepiga picha kwenye eneo la watu wengi
Baada ya kupiga picha kuna watu wakatokea kwenye picha, magic eraser inakupa uwezo wa kuwaondoa watu wote na vitu vingine usivyotaka kuonekana bila kuathiri chochote kwenye picha
Photo Unblur inakuwezesha kurekebisha muonekano wa picha kama imetokea vibaya
Mapinduzi mingine ni kwenye tafsiri ya lugha
Kwa mfano unataka kuchati na mtu ambaye hajui kiswahili anafahamu kichina au kiigeleza pekee
Meseji app ya google inaweza kubadili ujumbe wako ni kuwa kichina hapo hapo na kisha kumtumia meseji mlengwa
Huna haja ya kwenda google search kutafuta maana ya ujumbe unaotaka kutuma
Bei tarajiwa
Bei rasmi haijatajwa kwa sasa
Ila kwa kuangalia mlolongo wa bei za google pixel za miaka ya nyuma, hii simu bei yake itakuwa zaidi ya milioni moja
Google Pixel hutoa simu za madaraja ya juu hivyo bei yake lazima iwe kubwa
Hata ukiangalia sifa zake zinazotarajiwa zinakupa picha ya bei itakavyokuwa
Kama wewe ni mpenzi wa google pixel na unahitaji ikiwa mpya unatakiwa ujipange kama ilivyo kwa simu za iphone au samsung s23
Ushindani sokoni
Kuna Samsung Galaxy S23 ambayo imetoka mapema mwaka 2023
Hivi karibuni apple watazindua toleo la iphone 15
Google kwa miaka mingi imekuwa na shea ndogo sana kwenye soko la simu za tabaka la juu
iPhone zimekuwa zikitawala kwa muda mrefu ikifuatiwa kwa mbali na simu za samsung
Kwa takwimu za mwaka 2022, apple inalishikilia soko la simu za bei ya juu kwa asilimia 75
Wakati Samsung yenyewe inashikilia kwa 17% tu
Hali hii ya soko inatarajiwa kuendelea mwaka huu hasa ujio mpya wa iphone
Mbali ya iphone na samsung kuna kampuni za China zinatoa simu kali kwa bei nafuu kuliko google pixel
Kampuni hizo ni kama Xiaomi na OPPO bila kusahau Vivo
Ukitafuta orodha ya simu zenye kamera nzuri huwezi kukosa hizo brand za china
Kamera ndio kipengele kikubwa kinachoifanya pixel kupendwa duniani
Hivyo kwenye nyanja hiyo ana kazi ya kufanya
Muonekano
Simu za Google Pixel 8 Pro zinatarajiwa kuwa katika rangi tatu kwa mujibu wa picha zilizovuja kwenye mtandao wa Twitter(sasa ni X)
Rangi hizo ni nyeusi, kijivu na bluu
Hizi sio taarifa rasmi ila zinatokana na tetesi za hivi karibuni kutoka kwa watu mbalimbali
Upande wa nyuma kamera zake zitakuwa kwenye mpangilio wa mlalo huku kamera zikiwa zimeongozana kimstari
Ni tofauti na mpangilio wa kamera za iphone ambazo zipo kimuundo wa diaogonal
Na samsung ambazo zenyewe huwa zipo kwenye muundo wa wima
Matarajio
Ujio wa Google Pixel 8 utawapa watu wenye pesa kutosheleza chaguo la ziada kwenye upande wa simu za daraja la juu
Soko litaendelea kuwa kali
Kampuni zingine za simu zitaongeza juhudi kwenye tafiti ili kutoa simu zitakazoendelea kupata shea kwenye soko.
Maoni 3 kuhusu “Google Pixel 8, Simu ya Teknolojia ya Akili Bandia (AI)”
Tunataka video tizione muonekano na jinc inavyofanya kazi kwa ufupi tu
Naomba hizo simu aina Google pixel ziwe na laini mbili
Huwa zina laini moja laini ya pili inakuwa na esim ambapo Kwa tz huduma hii IPO Kwa Airtel na Vodacom na tigo pia