Mwaka 2023 yapo mateo ya simu yaliyoingia sokoni yakiwa na kamera nzuri na bora kwa kupigia picha na kurekodi video
Kuna simu zenye kamera kali zaidi na mfumo mzuri kwenye nyanja zote
Haziwezi fananishwa na simu zenye kamera nzuri zenye bei ndogo kabisa
Na ndio maana kwenye hii orodha utakuta bei zake karibu zote ni kubwa
Kwenye hii posti utaona ubora wa picha wa kila simu iliyoorodheshwa na upekee wa kamera za simu husika unaojitofautisha na simu zingine
Oppo Find X6 Pro
Oppo Find X6 Pro ni simu mpya ya mwaka 2023 iliyotoka mwezi machi
Ina jumla ya kamera zipatazo tatu
Mfumo mzima wa kamera unaonyesha wazi kuwa ubora wa picha na kurekodi video ni wa kiwango kikubwa
Kwani kamera zake tatu zina teknolojia ya ulengaji ya multi-directional PDAF inayoweza kukitambua kinachopigwa kitu kwa haraka
Hiyo haitoshi, kamera zake zote zina OIS(Optical Image Stabilization) ambayo kazi yake ni kutuliza kamera wakati unarekodi huku ukiwa unatembea
Teknolojia za ulengaji wakati mwingine zinapata shida kulenga kitu kwenye mwanga hafifu ila find x6 pro inatumia teknolojia ya Laser Af
Kamera zake zote zina ukubwa wa megapixel 50
Ubora wa picha wa Oppo Find X6 Pro
Iwe mchana ama usiku kwenye mwanga mdogo, uwezo wa hii ni simu ni kiwango cha juu.
Kamera inajitahidi sana kutoa picha zinazoendana na uhalisia wa muonekano wa kitu
Pia zinabalansi kwa usahihi rangi nyeupe sana na rangi nyeusi
Kwa maana kama eneo lina vivuri basi huonekana bali kuathiriwa na mwangaza mwingi
Hii ni picha moja wapo iliyopigwa kwa kutumia simu ya oppo find x6 pro
Rangi za jengo na nyasi pia muonekano wa rangi anga hazina mkolezo uliopitiliza
Na wala noise(chenga chenga) hakuna na ukizoom vitu ambavyo vipo vinaweza onekana kwa usahihi
Mfano mzuri ni upande wa kuria juu ambao una ngazi
Hii ni ishara kuwa kamera inakusanya data za kutosha ya eneo lote linalostahili kutokea kwenye picha
Samsung Galaxy S23 Ultra
Simu ya Samsung Galaxy S23 Ultra ni toleo la samsung mpya kwa mwaka 2023
Samsung Galaxy S23 Ultra ina jumla ya kamera nne huku kamera kubwa ikiwa na megapixel 200
Kamera ya kubwa inatumia teknolojia ya ulengaji ya multi-directional PDAF na Laser AF kwa ajili ya kwenye mwanga hafifu
Huku kamera zilizozabaki zikiwa zinatumia ulengaji wa dual pixel pdaf
Pia kamera zote zina zina mfumo wa kutuliza kamera wakati wa kurekodi huku ukiwa unatembea yaani OIS
Uzuri mkubwa wa kamera za Samsung ni uwezo mkubwa wa kuchukua kitu ambacho kipo mbali sana
Maana inakuja na kamera ya Telephoto yenye optical zoom yenye uwezo wa kukuza kitu mara 10 bila kupoteza ubora wa pixel
Ubora wa picha
Kwa baadhi,Galaxy S23 Ultra ni simu yenye kamera bora zaidi
Ukitazama picha nyingi zilizopigwa na simu utaona usahihi wa rangi wenye utofautishaji mkubwa
Pia samsung haina swala la “noise”, na muonekano wa vitu usiku unaonekana kwa usahihi
Ukitazama hiyo picha ya paka ambayo imepigwa na Galaxy S23 hasa kwenye jicho la paka
Ni kuwa kiini cha macho hakiaathiriwa na sehemu nyingine ya jicho
Rangi ya kiini ni nyeusi na ndio muonekano unavyoonekana kwenye picha husika
Xiaomi 13 Ultra
Xiaomi 13 Ultra ni simu nyingine ya kamera nne
Kamera zote nne zina megapixel 50 huku kamera kubwa ikitumia teknolojia ya ulengaji ya multi-directional PDAF
Na kamera zilizobaki zinatumia dual pixel pdaf
Uzuri ni kuwa kamera zake zote zina OIS hivyo hutowaza wakati ukirekodi video ukiwa unatembea
Kamera zake zinaweza kurekodi video mpaka za 8k
Ubora wa picha wa Xiomi 13 Ultra
Xiaomi kama ilivyo simu zingine kwenye orodha inatoa picha nzuri na usahihi mkubwa wa rangi
Rangi mbalimbali zinaonekana kama vinavyoonekana kwenye mazingira halisi kwa kiwango kikubwa
Na pia kwenye mwanga hafifu utaweza kuviona vitu kwa uzuri
iPhone 14 Pro Max
iPhone 14 Pro Max ilitoka kwenye robo ya mwisho ya mwaka 2022, kwa sasa hakuna toleo jingine zaidi ya hili
Ina jumla ya kamera tatu huku kamera kubwa ikiwa na megapixel 50
Kwneye swala la ulengaji iphone inatumia dual pixel pdaf ambapo kwa sasa simu nyingi za bei kubwa wameanza kuachana nayo.
Kamera zake zinaweza kurekodi mpaka video za 4K kwa kiwango kinachofikia 60fps
Pia zina OIS kama ilivyo kwa simu nyingi
Ubora wa picha wa iPhone 14 Pro Max
Moja ya kitu unachoweza kukiona kwenye iPhone ni picha kali ila kuna kukolea kwa rangi kulikopitiliza
Rangi ya anga imekuwa ya bluu sana na hata jengo rangi zimezidi kiasi fulani
Hata hivyo usahihi wake kwenye rangi ni wa kiwango kikubwa
Vivo X90 Pro+
Kama hujui basi ni kuwa vivo ni moja ya simu zenye kamera hasa haya matoleo ya Vivo X
Kwenye orodha ya simu kali zenye kamera nzuri vivo lazima utaikuta
Basi jua kuwa Vivo X90 Pro+ ni vivo yenye kamera nzuri zaidi kwa sasa
Idadi ya kamera kwenye Vivo X90 Pro+ zipo nne huku kamera ya Telephoto ikiwa na 60 megapixel na zingine ni megapixel 50
Na yenyewe kamera yake inaeza kurekodi mpaka video za 8K kwa kiwango cha 30fps
Ubora wa kamera yake ya kupiga vitu vya mbali haufikii samsung galaxy s23 ultra kwani yenyewe inaweza kukuza mara tatu tu
Aina ya ulengaji ambayo simu inatumia ni Dual Pixel PDAF, na yenyewe inatambua umbali wa kitu kinachopigwa kwa haraka pia
Ubora wa picha
Kwenye mwanga mwingi inatoa muonekano mzuri wa kinachopigwa picha
Kiasi cha kwamba unaweza usione kasoro yoyote
Japo kuna kiwango cha noise kwa mbali hasa kwa kitu kinachopigwa kikiwa kinatembea
Honor Magic5 Pro
Honor ilikuwa ni tawi ya kampuni ya Huawei ila kwa sasa imeuzwa kama njia ya kuepuka vikwazo vya USA
Honor Magi5 Pro ina jumla ya kamera zenye ukubwa wa megapixel 50 huku kamera kuu ikiwa inatumia ulengaji wa multi-directional PDAF
Kanera zake zinaweza kurekodi mpaka video za 4K na pia kamera mbili zina OIS, kamera ya tatu(ultrawide) haina.
Kwenye orodha hii, honor ndio yenye mfumo wa kamera za kawaida (pixel 7 pro ilifaa iwekwe?)
Hata hivyo ni simu inayotoa picha safi kabisa hata ukizoom mara nyingi vitu vinaonekana kwa kiwango kidogo cha noise
Uhalisia wa rangi hasa kwenye mwanga mwingi ni wa kiwango cha kuridhisha ila si kiwango kikubwa sana
Motorola Edge 40 Pro
Motorola Edge 40 Pro ni simu ya macho matatu ambayo imetoka mwezi wa nne 2023
Kamera mbili zina megapixel 50 na moja ikiwa na megapixel 12
Kamera kuu ina multi-directional PDAF na OIS zingine hazina
Hivyo ukiwa unarekodi video kwa kutumia kamera za ultrawide, video itatokea ikiwa inatikisika kama hutulizi mkono
Ubora wa picha
Ukilinganisha na simu ya Horo Magic5 Pro, usahihi wa rangi Motorola Edge 40 Pro ni mkubwa
Vitu vinaonekana vizuri nyakati za mchana na kwenye mwanga hafifu
Ukichukua picha za hili eneo na ukalinganisha na zilizopigwa na kamera zingine kwenye eneo hilo hilo utaona huawei inatoa picha halisi kwa kiwango kikubwa zaidi
Huawei P60 Pro
Huawei P60 inaweza kuwa nido simu yenye kamera nzuri zaidi kwenye hii orodha
Mfumo wake wa kamera ni wa kawaida ila ubora wa picha ni mkubwa
Ukichukua picha za hili eneo na ukalinganisha na zilizopigwa na kamera zingine kwenye eneo hilo hilo utaona huawei inatoa picha halisi kwa kiwango kikubwa zaidi
Rangi ya anga, majani na jengo vinaendana na uhalisia
Hata picha ukiikuza mara nyingi vitu vinaonekana na unaweza usigundue kuwa kuna chengachenga
Kamera za hii simu zinaweza kurekodi mpaka video za 4K kwa kiwango cha 60fps
Na ulengaji wa kamera uliotumika kwenye simu ni dual pixel pdaf
Samsung Galaxy S23 Plus
Ubora wa picha upande wa samsung Galaxy S23 Plus unaendana na mkubwa wake yaani samsung ultra
Simu ina jumla ya kamera tatu huku kamera kubwa zaidi ina megapixel 50
Na kamera mbili zimewekewa mfumo wa OIS
Pia hizi kamera zinaweza kurekodi video za 8K kwa kiwango cha juu cha 30fps
iPhone 14 Pro
Apple iPhone Pro ina kamera tatu na kamera kubwa zaidi ina megapixel 48
Ubora wa kamera unaendana sana na iPhone 14 Pro Max
Kamera mbili zinatumia teknolojia ya ulengaji ya dual pixel pdaf nyingine inatumia PDAF
Na zina uwezo wa kurekodi video mpaka za 4K
Simu Zingine
Matoleo yapo mengi yanayopiga picha nzuri
Moja ya simu ambayo imeachwa kwenye orodha ni Google Pixel 7 Pro
Haikuwekwa kwa sababu simu za google pixel kiujumla huwa wanatoa simu zenye kamera nzuri
Maoni 10 kuhusu “Simu 10 Zenye Kamera Nzuri na Bora 2023-2024”
Je Samsung galaxy A53 sofa zake zikoje tafazali
Iko vizuri pia
Nafulaia sana elimu yako nimekua nikitembelea maranyingi kujifunza mambo mbalimbali hongera sana sihaba mikole. Naomba niulize tafadhari nina tsh 400k je naweza pata sim gani usd yenye kamera nzuri na bettri kubwa na utendaji mkubwa memor ufs
Pixel 4
Pixel kubwa kabisa bei gani
Naitaji kujuwa bei ya
Xiom13 ultre na
Honor magic5 pro tafadhari
Xiaomi 13 Ultra ni mil 2.7
Honor magic5 pro ni mil 2.7
Naitaji kufaham kuhus pixel 5. Ubora wake wa camera na Matumiz mengine ikoje.
Ina kamera nzuri na inapokea updates za android na utendaji wake wa kuridhisha
Je samsung s24 bei gani na ni GB Ngapi samahan lakini