Kwenye ukurasa huu kuna orodha ya simu kumi za google pixel na bei zake
Google Pixel ni simu nzuri za android ambazo huwa zinapiga picha safi na bora
Na kiuhalisia simu za zamani kama iPhone 6 Plus hazifiki simu za zamani za pixel kama 3a
Katika hii orodha kuna pixel za kuanzia mwaka 2019 hadi 2021
Mpaka mwezi juni 2022 google ilitangaza toleo jipya moja
Baadhi ya simu kali za Google Pixel
Google Pixel 6
Google Pixel 6 ni toleo jipya kabisa la pixel ambalo lilitoka 2021 mwezi wa kumi
Matoleo ya Pixel 6 yanatumia processor ambazo google wamezibuni wenyewe
Chip hizo ni Google Tensor
Google Tensor utendaji wake una nguvu kwa sababu core zenye nguvu zinatumia Cortex X1 na Cortex A76
Ubora wa kioo pia ni wa kuvutia kutokana na kutumika kwa Amoled
Kioo cha pixel 6 kina HDR10+
HDR10+ huboresha muonekano wa vitu ili viendane na jinsi vinavyoonekana kwenye mazingira halisi
Simu inatumia kamera ambazo zinapiga picha kali
Pamoja na simu hii ya google kuwa na betri yenye 4614mAh, ukaaji wake wa chaji sio mkubwa sana
Kwani simu ikiwa inaperuzi intaneti inachukua masaa 12 kuisha chaji
Bei ya Google Pixel 6 Tanzania
Katika masoko ya dunia google pixel 6 yenye GB 128 na RAM GB 8 inauzwa shilingi 1,235,430.00/=
Ukiitazama simu hii kiundani, ina vitu vingi ambavyo wake ni mkubwa
Vitu ambavyo si rahisi kuvikuta katika simu zinazouzwa chini ya laki nne
Google Pixel 6 Pro
Simu ya Google Pixel 6 Pro ni simu ya android ya daraja la juu.
Katika orodha ya simu zenye camera nzuri Google Pixel 6 Pro ipo
Na yenyewe uwezo wake wa kufungua app na kucheza gemu ni wa kuridhisha sana
Hii inatokana na simu kutumia chip ya Google Tensor
Kioo cha Google Pixel 6 Pro ni cha LTPO AMOLED chenye refresh rate 120Hz na resolution ya 1440 x 3120 pixels
Hii inamaanisha ustadi wa kioo kuonyesha rangi halisi ina usahihi mkubwa
Ni moja ya simu za 5G zinazotumia toleo jipya la Android 12
Google Pixel 6 Pro ina betri kubwa lenye ujazo wa 5003mAh
Ila ukaaji wa chaji unazidiwa na simu ya iPhone 13 Pro Max
Pixel 6 Pro inadumu na chaji masaa 12 tu simu ikiwa kwenye intaneti masaa yote
Bei ya Google Pixel 6 Pro Tanzania
Pixel yenye memori ya GB 128 na RAM ya GB 8 ni 1,864,800.00/=
Kwa Tanzania tarajia pesa kuwa zaidi ya milioni mbili
Bei yake kiuhalisia ni kubwa
Kiasi hiki cha bei kinaepeleka simu kwenye ushindani na Samsung Galaxy S22+ 5g
Samsung Galaxy S22+ 5g inaicha pixel 6 pro kwa sehemu kubwa
Google Pixel 6a
Simu ya Google Pixel 6a ni simu mpya ya pixel ambayo imetangazwa hivi karibuni mwezi mei
Inatarajiwa kuingia sokoni ifikapo mwezi julai
Hivyo hakuna taarifa za bei yake kwa wakati huu
Lakini inatarajiwa kutumia chip ya Google Tensor, kioo cha amoled, memori aina ya UFS
Pia uwezo wa kuzuia maji kupenya ndani simu
Kwa Taarifa zaidi kuhusu pixel 6a, pitia sifa za simu ya pixel 6a kwenye tovuti ya GSMArena
Google Pixel 5
Moja ya simu ambayo Google waliizindua 2020 ni simu ya Google Pixel 5
Hii ni smartphone yenye viwango vya IP68
Kwa maana maji ya kina cha mita moja hayawezi ingia ndani ya simu
Kioo chake ni kizuri linapokuja uangavu na uonyeshaji wa vitu kwa rangi zake halisi
Ubora wa rangi unachagizwa na kioo cha oled, refresh rate ya 90Hz na HDR10+
Pitia hapa kuelewa, maana ya hdr na jinsi inavyofanya kazi
Ina idadi ya kamera zipatazo mbili ambapo kamera kubwa inatumia dual pixel pdaf
Lakini ukaaji wa chaji sio wa kuridhisha
Inatunza moto kwa muda wa masaa 12 wakati wa kuperuzi
Ila chaji ianpeleka umeme wa wastani wa wati 18
Hivyo betri ya 4000mAh inaweza chukua modo kujaa
Bei ya Google Pixel 5
Kwa sasa simu inapatikana kwa bei ya 1,1655,00.00/=
Bei hii ni kubwa hasa kama utailanginisha na simu za xiaomi
Lakini pixel 5 ni simu inayopokea toleo jipya la Android 12
Google Pixel 5a 5G
Google Pixel 5a 5G ni simu ya 5g ambayo inatumia chip ya snapdragon 765G 5G
Hii chip ina nguvu inayoifanya simu kuwa na utendaji mkubwa na wa haraka
Simu inakuja na Android 11 lakini inaweza kupokea toleo la Android 12
Kioo cha google pixel 5a 5G ni cha oled chenye resolution ya 1080 x 2400 pixels
Hii ni simu nyingine isiyopitisha maji kutokana na kuwa na IP67
Betri ya google pixel 5a 5G ina ukubwa wa 4680 mAh
Ila ukaaji wa chaji ni kiwango kikubwa ukilinganisha na pixels nyingi
Ukiwa unaperuzi intaneti simu inachukua masaa 18 mpaka chaji kuisha
Huu ndio muda ambao iPhone 13 Pro Max inatumia kwenye intaneti mpaka kuisha chaji
Bei ya Google Pixel 5a 5G
Pixel 5a 5G yenye ukubwa wa GB 128 na GB 6 ni shilingi 933,200.00/=
Maamuzi ya kununua simu hii yanaweza kukwama kama utakutana na sifa za xiaomi 12 pro
Ilinganishe hapa bei ya hii simu na ubora wa simu ya xiaomi 12 pro
Google Pixel 3a
Google Pixel 3a ni simu ya mwaka 2019 hivyo inakuja na Android 9.0
Na inaweza kupokea toleo la Android 12
Ni moja ya simu ya bei nafuu ya pixel inayoweza kununuliwa na Watanzania wengi
Uzuri ni kuwa unafuu huo wa bei unakupa pixel yenye kioo cha oled, memori ya GB 64 kamera inayoweza kurekodi video za 4K
Angalizo,
Usitarajie makubwa sana kwenye Google Pixel 3a
Kwani ina kamera moja, inatumia memori za eMMC, betri yake ni dogo
Na hata kasi yake ya kuchaji simu ni ndogo pia kwani ni wati 18
Bei ya Google Pixel 3a
Bei halisi ya pixel 3a ni shilingi 320,000/=
Kwenye mtandao wa aliexpress unaweza kuipata chini ya laki tatu
Ila kwa Tanzania bei yake inafika laki tatu na nusu
Google Pixel 4 XL
Kwa sasa Google Pixel 4 XL ni moja pixel ambazo unaweza kuipata kwa bei nafuu
Wakati ilipotoka mwaka 2019 ilikuwa ni simu ya kundi la juu
Hii ni kwa sababu simu inatumia processor yenye nguvu katika kufanya kazi
Chip inayotumi pixel 4 xl ni Snapdragon 855
Na pia ina kioo cha oled chenye refresh rate 90HZ
Refresh rate kubwa huwa inafanya simu kuwa nyepesi wakati wa kutachi na kuperuzi
Ila sasa betri yake lina ukubwa 3700mAh hivyo usitarajie ukaaji wa chaji wa kiwango kikubwa
Simu ina kamera aina ya wide na Telephoto
Kamera ya wide ina OIS na dual pixel pdaf
Kitu kinachoongeza ufanisi wakati wa kurekodi video na kupiga picha
Bei ya Google Pixel 4 XL
Kuna google pixel 4 xl ya GB 64 ambayo bei yake kwa sasa ni 839,880.00/=
Kwa Tanzania bei inaweza ikawa kubwa
Ila kama ni used bei inaweza kuwa chini
Google Pixel 4
Simu ya Google ina vitu vingi vinavyofanana na pixel 4 xl
Ikiwemo processor, kioo, aina za kamera
Ila pixel 4 ina betri dogo sana la ukubwa wa 2800mAh
Hii inafanya simu kukaa na chaji masaa machache kama ukiwa unatumia intaneti
Japokuwa inakuja na android 10 aimu inaweza kupokea toleo la 12
Bei ya Google Pixel 4
Bei ya Google Pixel 4 ya GB 64 ni shilingi 613,579.00/=
Kwenye mtandao wa aliexpress simu inapatikana kwa bei ya chini zaidi
Google Pixel 4a
Pixel 4a ni simu nyingine nzuri yenye kamera moja yenye kupiga picha kwa usahihi
Google Pixel 4a iliingia sokoni mwaka 2019
Imepita miaka mitatu ila ni simu inayochuana na simu nyingi za mwaka 2021 na 2022
Hilo linasababishwa na simu kutumia kioo cha oled chenye resolution ya 1080 x 2340 pixels
Pia simu kuwa na protector ya Gorilla 3 ambapo simu kama infinix note 12 vip haina
Lakini pia kamera yake kuwa na Dual Pixel Pdaf na OIS
Kuna simu za oppo mpya ambazo hazina OIS
Betri yake pia sio kubwa hivyo ukaaji wa chaji ni wa masaa machache
Bei ya Google Pixel 4a
Kwenye mtandao wa Aliexpress bei ya hii simu ni shilingi 676,570.00/=
Hii ni bei ya pixel 4a ya GB 64
Kwa wauzaji wa Tanzania bei inaweza kuzidi laki saba
Google Pixel 3
Simu ya Google Pixel 3 ni simu ya Android 9 iliyotoka mwaka 2018
Kisifa inafanana na pixel 3a
Ila hii na yenyewe ina betri dogo
Ni simu ambayo haina sehemu ya kuweka earphone
Utendaji wake ni wa wastani kwa nyakati za sasa
Japokuwa inatumia chip ya Snapdragon 845 ambayo ilikuwa ni moja ya chip yenye nguvu nyakati hizo
Chaji yake ina kasi ndogo ya wati 18
Bei ya Google Pixel 3
Kutokana na simu kuwa na ubora katika sehemu chache inafanya kuwa na bei ndogo
Kwani bei yake ya GB 64 ni shilingi 373,280.00/=
Inaweza ikawa ni bei kubwa kwa baadhi ya watu ila hii ni bei ndogo ukizitazama pixel nyingi zilizomo
Maoni 6 kuhusu “Simu Nzuri za Google Pixel na Bei Zake (2022)”
Inapokeamoto lakin haipeleki chaji
Ninahamu ya kutumia simu ya Google ila bei ni Kali sana
Nilikuwa naomba bei za matoleo yote ya google pixel
Naomba bei za Google pixel kwa matoleo yote
Nahitaji pixel 4
Naitaj pixel 6