SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu ya iPhone 6 Plus na Sifa zake Muhimu (2022)

Bei Nafuu

Sihaba Mikole

June 12, 2022

Simu ya iPhone 6 Plus ni iPhone ambayo ilitoka mwaka 2014

Umri wa miaka minane tangu itoke unaifanya bei ya iPhone 6 plus iwe chini ya laki tatu

Apple walishasitisha kutengeneza hii simu hivyo smartphone hii utaipata ikiwa used

iphone 6 plus

Swali, je simu hii inafaa kutumika kwa mwaka 2022?

Kiuhalisia bei yake na sifa zake zitakupa jibu sahihi.

Fuatilia kila ufafanuzi uliopo kwenye ukurasa huu

Bei ya iPhone 6 Plus Tanzania

Kwa baadhi ya maduka kinondoni bei ya iphone 6 plus ya GB 64 ni shilingi 230,000/=

Wauza simu wengine wanaiuza mpaka 270,000/=

Kwa sasa hii ni moja ya iPhone za bei rahisi

Bei ndogo inasababishwa na sifa zake kuwa na kiwango cha chini kwa nyakati za sasa

Sifa za Simu ya iPhone 6 Plus

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Apple A8 
  • Core za Kawaida(2) – 2×1.4GHz Typhoon
  • GPU-PowerVR GX6450
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
  • iOS 8
Memori  16GB,128GB,64GB na RAM 1GB,
Kamera Kamera MOJA

  1. 8MP,PDAF(wide)
Muundo Urefu-5.5inchi
Chaji na Betri
  • 2915mAh-Li-Po
  • Chaji-11W
Bei ya simu(TSH) 280,000/=

Upi ubora wa iPhone 6 Plus

Hakuna cha kukizungumzia zaidi kuhusu ubora wa iPhone 6 Plus

Kwa sababu ni simu ambayo ipo chini sana kwa nyakati za leo

iphone 6 plus summary

Uzuri mkubwa wa hii simu ni kuwa ndogo na fupi

Hivyo kwa wanaochukia simu ndefu basi iPhone hii inawafaa

Lakini ubora wa vitu kiujumla ni mdogo sana

Uwezo wa Network

iPhone 6 Plus ni simu ya 4G yenye masafa mengi

Hivyo hii simu inakubali mitandao ya simu karibu yote duniani

Ila 4G yake ni aina ya LTE Cat 4

iphone 6 plus network

Spidi ya juu kabisa ya kudownload vitu kwa LTE Cat 4 ni 150Mbps

Japo mpaka sasa hakuna laini ya simu Tanzania yenye inteneti inayoweza kufika spidi hiyo

Pitia hapa uelewe, maana ya 4G

Ubora wa kioo cha iPhone 6 Plus

Kioo cha iPhone 6 Plus ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution ndogo

Kumbuka simu ni ya zamani, mwaka 2014 resolution ya 1080 x 1920 pixels ilikuwa ni kubwa sana

Hii simu haina refresh rate kubwa

Na ubora wa IPS LCD unazidiwa kwa kiasi kikubwa na AMOLED

Hivyo ubora wa uonyeshaji wa picha ni wa kawaida

Nguvu ya processor Apple A8

Apple A8 ndio processor ambayo inaipa nguvu hii simu.

Utendaji wa apple a8 ni mdogo sana

Kwani ina core mbili tu zenye mizunguko michache inayofanya kazi chache

Hivyo usitarajie simu kuweza kufanya kazi kubwa kiufanisi

Kwa mfano app ya geekbench 5 inaipa apple a8 alama 328

Kwa nyakati hizo, hii ilikuwa ni utendaji mkubwa kwani chip ya Samsung Galaxy S5 ina alama 151 kwenye core moja

Kumbuka Galaxy S5 na iPhone 6 Plus zilikuwa zinashindana sokoni

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya iPhone 6 Plus ni dogo sana

Ukubwa wa betri yake ni 2915mAh

Ukubwa huu wa betri unaweza kudumu kwa masaa 24 kama ukiwa unaongea na simu mara kwa mara

Na ukiwa unaperuzi intaneti betri inadumu kwa masaa 9 tu

Kama ukiwa unatazama video za instagram au youtube masaa ya betri yatapungua zaidi

Chaji yake inapeleka umeme mdogo wa wati 11

Ukubwa na aina ya memori

Kuna matoleo matatu ya hii iphone ambayo yote yana RAM ya 1GB

Kuna iphone ya GB 16, 64 na 128GB

Memori za 64gb na 128gb zinaweza kuhifadhi app na mafaili mengi

Kwa bahati mbaya udogo wa RAM unaipa simu kikomo cha kuhimili matumizi ya app nyingi kwa wakati mmoja

Uimara wa bodi ya iPhone 6 Plus

Bodi ya simu ya iPhone 6 Plus imetengenezwa na gorilla glass upande wa mbele

Ila upande wa nyuma simu imewekewa alumiamu

Lakini Gorilla zilizotengenezwa chini ya mwaka 2016 sio imara sana

iphone 6 plus BODI ya simu

Hivyo kuwa na kava na protector ni muhimu sana

Na uzuri kimo cha simu ni inchi 5.5

Hivyo ni nyepesi kubeba na inajaa kwenye mkono

Ubora wa kamera

iPhone 6 plus ina kamera moja tu upande wa nyuma

Na selfie kamera pia ipo moja

Ubora wake wa kamera unazidiwa na matoleo mapya ya simu za daraja la kati kuanzia 2019 hadi sasa

iphone 6 plus KAMERA

Pamoja na hivyo kamera yake inaweza kurekodi video za 4K kwa kasi ya 30fps

Na uzuri simu inatumia OIS kutuliza video wakati wa kurekodi huku ukiwa unatembea

Ubora wa Software

Nyakati za nyuma, app za simu zilikuwa haziwezi kuwasiliana kwenye mfumo wa iOS

Lakini ilipokuja iOS 8 mwaka 2014 hiko kitu kikaanzishwa

Mfumo huo uliwezesha kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja kwenye kifaa kingine

Kwa mfano, ukiwa unaongea na simu ilikuwa ni ngumu kuandika sms

Basi iOS 8 iliwezesha simu kuungana kompyuta ya MAC

Na kisha ukawa unatumia kompyuta kujibu sms na simu ikiwa inatumika kuongea na mtu

Ila ni vitu vya kawaida siku hizi

Lakini pia simu inakubali mpaka iOS toleo la 12

Yapi Madhaifu ya iPhone 6 Plus

Ukilinganisha na simu mpya nyingi za sasa iPhone ina mapungufu mengi

Lakini ni vizuri ukilinganisha iPhone 6 Plus na Samsung Galaxy S5 au S6

Simu haijatumia kioo kizuri cha OLED au amoled

Wakati Galaxy S5 ilitoka kabla lakini tayari ilikuwa na kioo cha amoled

Simu haikuwa na uwezo wa kuzuia maji kupenya

Kwani hakuna sehemu ambayo imeainisha simu kuwa na IP67

Neno la Mwisho

Bei ya iPhone 6 Plus ni ndogo inayoweza kukuvuta kuimiliki simu

Lakini hii simu haipokei maboresho ya kupokea mfumo endeshi mpya wa iOS 15

Huko mbeleni kuna apps nyingi hazitofanya kazi

Kwa mfano app ya Whatsapp haitafanya kazi kwenye matoleo ya iPhone 6 muda si mrefu

Ni vizuri ukaangalia matoleo ya mbele ya iPhone zenye bei ndogo

Maoni 9 kuhusu “Bei ya Simu ya iPhone 6 Plus na Sifa zake Muhimu (2022)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

iphone 15 pro max camera thumbnail

Ubora wa iPhone 15 Pro Max Upande wa Kamera[hatari tupu]

Apple iPhone 15 Pro Max ni simu yenye kamera tatu upande wa mbele na kamera moja ya mbele (selfie kamera) Ukifuatilia ubora wake wa kamera utagundua sababu ya kuuzwa bei […]

iphone 15 pro max thumbnail

Bei ya iPhone 15 Pro Max na Sifa Zake

Apple iPhone 15 Pro Max ni toleo jipya la iphone kwa mwaka 2023 Ni simu ya kwanza kutoka Apple kutumia chaji aina ya USB Type C ambazo hutumika na simu […]

iphone 15 pro thumbnail

Bei ya iPhone 15 Pro na Sifa Zake Muhimu

Kama ilivyotarajiwa hapo awali kuhusu ujio wa simu mpya za iphone kwa mwaka huu 2023 Moja ya simu hiyo ni iPhone 15 Pro ambayo imeongezewa utendaji Kiumuonekano hauwezi kutofautisha sana […]

iphone 15 muonekano

Ujio wa Simu mpya za iPhone 15 Septemba 2023

Kwenye tarehe 12 mwezi wa tisa 2023 kwenye ukumbi wa Steve Jobs makao makuu ya apple kutakuwa kuna uzinduzi wa bidhaa kutoka kwa kampuni ya apple Tukio hili litarushwa moja […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram