SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Google Pixel 8a na Sifa zake Muhimu

Sifa za simu

Sihaba Mikole

June 2, 2024

Kwenye mlolongo wa matoleo ya Google Pixel 8, Google Pixel 8a ndio ina bei ndogo zaidi

Bei ya Google Pixel 8a ya GB 128 ni shilingi za tanzania milioni moja laki tatu na nusu

google pixel 8a showcase

Inashangaza lakini milioni 1.35 ni bei ndogo ukilinganisha na Google pixel 8 au matoleo ya Samsung Ultra

Maeneo makubwa yenye ubora zaidi kwenye hii simu ni

 • Kamera
 • Kioo
 • Nguvu ya processor
 • Ukaaji wa chaji

Kuna vitu vichache vinavyokosekana kwenye hii ila vipo kwenye matoleo mengine ya google pixel 8, lakini kwa kiasi kikubwa hakuna tofauti kwenye sifa nyingi

Sifa za Google Pixel 8a

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
 • CPU – Google Tensor G3
 • Core Zenye nguvu sana(1) – 1×3.0 GHz Cortex-X3
 • Core zenye nguvu(4) – 4×2.45 GHz Cortex-A715
 • Core zenye nguvu(4) – 4×2.15 GHz Cortex-A510
 • GPU-Immortalis-G715s MC10
Display(Kioo) OLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
 • Android 14
Memori UFS 3.1, 256GB,128GB na RAM 8GB
Kamera Kamera MBILI

 1. 64MP,dual pixel PDAF(wide)
 2. 13MP(ultrawide)
Muundo Urefu-6.1inchi
Chaji na Betri
 • 4492mAh-Li-Po
 • Chaji-27W
Bei ya simu(TSH) 1,350,000/=

Uwezo wa network

Google Pixel 8a ni simu inayosapoti mtandao mpaka wa 5G

Inasapoti aina zote za 5G ikiwemo za masafa ya kati yanayopatikana hapa nchini

Upande wa 4G, ina LTE Cat 24 ambayo kasi yake inafika 7300Mbps

Yaani kama unapakuwa muvi ya GB 1, simu itamaliza kupakuwa faili ndani ya sekunde moja

Kasi hii inategemea kama mtandao wa simu una miundombinu ya namna hiyo

Kwa Tanzania ni nadra kupata kasi hii upande wa 4G

Ubora wa kioo cha Google Pixel 8a

Kioo cha google pixel 8a kimeundwa kwa teknolojia ya oled

Oled huundwa kwa matirio yanayotoa mwanga yenyewe pindi umeme ukipita bila kutegmea taa za LED

Inafanya simu kuwa na utajiri mkubwa wa rangi, ukizingatia resolution yake ni kubwa ya 1080 x 2400 pixels

Pia refresh rate inaweza fika hadi 120Hz, na mwangaza mkubwa unaoenda mpaka nits 2000

google pixel 8a display

Ukiwa juani kioo kitaonekana vizuri tu

Ila kwenye kioo google pixel 8a imepungua baadhi ya vitu kama vile hdr10+ na pia hiki sio cha ltpo oled

LPTO  oled hudhibiti matumizi ya refresh rate yenyewe ili kupunguza ulaji wa chaji

Nguvu ya processor ya Google Tensor G3

Google Pixel 8a inatumia chip ya Google Tensor G3 kufanya kazi zake

Tensor G3 ina idadi ya core zipatazo tisa tofauti na processor za mediatek, snapdragon na apple bionic

Lakini hili halifanyi chip ya google kuwa na utendaji mkubwa kuliko Snapdragon 8 Gen 3 ya Samsung Galaxy S24 au Apple A17 Bionic ya iPhone 15 Pro

Hata hivyo nguvu yake ni kubwa ya kufanya chochote bila shida kwenye gemu

Hata ukiangalia alama za app inayopima nguvu za processor utaona kuwa alama zake ni kubwa

Hivyo kwa mpenzi wa magemu ataweza kucheza gemu za kila aina pasipo na shida

Uwezo wa betri na chaji

Betri yake ina ukubwa wa 4492mAh, haijafika mAh 5000 kama ilivyozoelezeka

Lakini inakaa na chaji masaa mengi kama tu simu zingine

Simu inasapoti chaji ya wati 18, kwa chaji ya wati 18 simu inachunkua dakika 129 mpaka kujaa

Sio spidi ya kuridhisha ukilinganisha na simu ya Samsung Galaxy S24 inayojaza betri kwa dakika 75 tu

google pixel 8a betri

Mbali na chaji ya kutoridhisha ila ukaaji wa chaji unaridhisha

Kwani kwa matumizi ya hapa na pale inastahimili mpaka masaa 11

Kwa kucheza gemu pekee muda wote inachukua masaa saba (sio mbaya)

Ukubwa na aina ya memori

Google Pixel 8a inatumia memori aina za UFS 3.1

Kasi ya kusafirisha data huwa ni kubwa kwenye muundo huu wa memori

Kuna matoleo mawili tu ya hii simu upande wa memori

Ambapo kuna ya GB 128 au ya GB 256 na ram za ukubwa wa GB 8

Hiko kiasi kinatosheleza kuhifadhi mafaili mengi

Haina sehemu ya kuweka memori kadi ya ziada

Uimara wa bodi ya Google Pixel 8a

Simu ya Google Pixel 8a ina viwango vya IP67

IP67 inamaanisha simu haipitishi maji kama ikizama kwenye kina kinachofika mita 1.5 kwa muda wa nusu saa

Yaani kama ukiizamisha simu kwenye diaba simu inaweza kuzuia maji kwa muda huo

Uimara wa skrini protekta inayokuja nayo upo sana kwenye kuzuia mikwaruzo

google pixel 8a bodi

Kutokana na kutumia kioo cha gorilla glass 3, hivi huwa ni imara kuzuia mikwaruzo

Kwa hiyo ni muhimu pia kununua skrini protekta kuzuia kupasuka

Ubora wa kamera

Google Pixel 8a inakuja na kamera mbili tu ambapo moja wapo ni ya ultrawide

Kamera kubwa ina megapixel 64 na ulengaji wa kiotomatiki wa dual pixel

Kamera yake inatoa picha zenye usahihi wa rangi kwa kiasi kikubwa

Ina kiwango kizuri cha utofautishaji rangi yaani kama kuna sehemu ina kivuli basi kivuli hakiathiriwi na mwangaza mkubwa kwenye mwanga mwingi

google pixel 8a camera

Hakuna kiwango chengachenga(noises) kinachoonekana kwa picha zilizopigwa nyakati za mchana

Kwa picha zilizopigwa kwenye mwanga hafifu bado vitu vinaonekana kwa ustadi

Kwenye mwanga mdogo sana vitu havionekani

Kamera zake zinarekodi pia video za 4K kwa kasi ya 60fps

Ubora wa Software

Google ndio watengenezaji wa mfumo endeshi wa Android

Hivyo simu inatumia mfumo wa Android 14, kama kuna toleo jipya simu itapokea

Katika android hii kuna maingizo ya matumizi ya AI kwa kiasi kikubwa

google pixel 8a software

Kwa mfano, app ya kamera inakupa uwezo wa kuondoa kitu ambacho hutaki kitokee

Na hata ukiondoa ubora wa picha unabaki kama ulivyo

Washindani wa google pixel 8a

Kuna washindani wengi kwenye hiki kipengele

Ila kwa mwaka huu washindani wakubwa kuna Tecno Camon 30 premier, Samsung Galaxy S4 na hata iPhone 15 bila kusahau Oppo Reno12 Pro

Hizi zina sifa zinazofanana nyingi ila kuna eneo moja pixel inaachwa nyuma pakubwa

Eneo hilo ni upande wa utendaji wa processor

Tensor G3 hazifanyi vizuri ukilinganisha na ubora wa chip za samsung na apple ama mediatek za toleo la juu

Kwa mtu anayetaka simu iliyokamilika kwenye idara zote anaweza akawashawishika kuchukua toleo lingine mbali na google

Ila google ina nguvu katika upande wa kamera

Neno la mwisho

Kiujumla bei ya Google pixel 8a inaendana na vitu inavyoambatana navyo

Ukiwa nayo utafurahi ubora wa picha unaozarishwa na kamera

Utashuhudia mambo mbalimbali ya artificial intelligence yaani kwa kiswahili inaitwa akili mnemba

Pamoja na yote wapo washindani wanaotoa vitu kama hivyo

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

google pixel 8 pro thumbnail

Bei ya Google Pixel 8 Pro na Sifa zake Muhimu

Simu ya Google Pixel 8 Pro imezinduliwa mwezi wa kumi (oktoba) 2023 Ni simu ya daraja la juu kama ilivyo kwa iphone na samsung matoleo ya S-series Kwa maana hiyo […]

google pixel 8 appearance

Google Pixel 8, Simu ya Teknolojia ya Akili Bandia (AI)

Google Pixel 8 na Pro zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi wa kumi tarehe nne Matoleo mapya ya pixel yatatumia toleo la android 14 Android 14 ilitangazwa tangu mwezi wa pili lakini […]

google pixel fold thumbnail

Ubora na bei ya simu mpya ya Google Pixel Fold

Fold ni aina ya simu za kujikunja. Kwa muda mrefu makampuni ya Samsung, Huawei na Oppo wamekuwa wakitengneza simu za aina hii Hivi karibuni tecno na pixel pia zimeingia katika […]

simu za bei rahisi

Simu used za bei rahisi za madaraja ya kati na juu

Kuna simu za bei kubwa ambazo zilizotoka miaka ya nyuma na kwa sasa hazipatikani zikiwa mpya Matoleo yake yalikuwa yanalenga watumiaji wanaopenda vitu vya gharama hivyo kuwa na vitu vingi […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company