Apple mnamo mwezi wa tisa walizindua simu kali sana
Simu kali zinamaanisha ubunifu
Ila kwenye iPhone 18 hakuna upekee kwenye ubunifu
Tutafafanua huu mtazamo wetu baadae
Ila . . . .
Apple walizindua simu aina za iPhone 18, iPhone 18 Pro na iPhone Duo
Hizi iphone mpya za 2026 zina utendaji mkubwa na maboresho mengine
Hizi ndio sababu za msingi kwa nini apple wameishiwa ubunifu
Wamekopi wa Samsung
Kwa mara ya kwanza iPhone imekuja na simu za kujikunja
Simu hiyo ni iPhone Duo
Ina skrini mbili ndani na moja nje
Ila hii simu haijaja kimapinduzi tofauti na mwaka 2007
Mwaka 2007 iPhone 1 ilizinduliwa
Wakati huo smartphone zilikuwepo hasa blackberry
Ila iPhone 1 ilitengeneza standard mpya ya namna simu janja inavyoonekana leo
Lakini hii samsung duo sio simu ambayo imeleta upekee japo yapo maboreshoi
Utofauti mdogo kiujumla
Ukiilinganisha iPhone 17 Pro na iPhone 18 Pro utastaajabu
Simu mbili hizi zina muonekano unaofanana
Kitu kinachotofautisha simu hii na iliyopita ni utendaji
Maana utendaji wa iPhone 18 Pro umeengezeka na betri pia
Ila kwa mtumiaji wa kawaida ambao ni wengi hawezi kuona utofauti
Na uzuri iPhone 17 Pro inaweza kupata toleo jipya
Apple wamekuwa watu kuvizia
Zama za Steve Jobs kampuni ya apple ilijikita sana kwenye utafiti
Bidhaa kama iPod ilileta mageuzi makubwa sana kwenye mp3 player
Kiasi cha kuitoa kwenye reli sony na bidhaa zao za walkman
Walkman ilikuwa inatumia kanda za tep, wakati apod ilifanikiwa kutumia memori za flash
Hivyo ipod ikawa inaweza kuhifadhi audio nyingi (lilikuwa jambo kubwa)
Ila siku hizi apple imekuwa ikisikilizia ubunifu wa kampuni zingine kwanza
Baada ya kuona uwezekano wa teknolojia kufanikiwa ndio apple huja sasa na maboresho kadhaa
Mfano mzuri ni hizi simu za folding (kujikunja)
Samsung ndio kampuni ya kwanza kuja na simu ya mtindo huu
Simu ya kwanza ni Samsung Galaxy Fold mwaka 2019
Ilikuwa na mapungufu lakini simu za aina hii ziliendelea kuimalika
Baada ya miaka saba (7) apple ndio wakaja na iPhone Duo
Kwa maana wamepata taarifa za kutosha kupitia kampuni zingine
Wapo nyuma kwenye AI
Apple wameshindwa kuja na AI yao wenyewe
Mfumo wao wa AI unategemea chatgpt na gemini kwa kanzi ngumu zaidi
Na kuna tetesi kuwa apple wameilipa Google kutumia mifumo yao AI
Hitimisho
Kikubwa apple bado ni moja ya kampuni bora ya kiteknolojia
Lakini apple tangu mwaka 2011 wameshindwa kuleta bidhaa zinazoleta mapinduzi
Hivyo kwa sasa simu za Android ndio zinakuja na ubunifu mwingi zaidi
Na apple wao wanavizia na kuziweka baada ya miaka mingi