Apple kwa mara ya kwanza wamezindua simujanja za kujikunjua (folding phone)
Imeleta hamsha hamsha nyingi kama ilivyo kawaida
Japokuwa simu za folding zina miaka mingi tangu zilipotoka
Bei yake ni kubwa na ni simu nzuri
Kulikuwa na matarajio iPhone Duo itakuwa bora kuliko simu za folding zingine
Ukifuatilia wachambuzi wa nje walianza kuisifia mapema sana
Lakini walionza kuitumia wameona utofauti
Tutazame sifa zake na tuione changamoto zake
Bei ya iPhone Duo GB 256
Kwa hapa Tanzania iPhone Duo unaweza kuipata kwa shilingi milioni sita (6,000,000)
Hii ni simu ikiwa na RAM ya GB 12
Hii ina maana iPhone Duo iko vizuri kwenye kufungua vitu vingi kwa wakati mmoja

Na kumbuka hata mfumo wa memori ni ule wenye kasi zaidi unaoitwa NMVe
Hizi chini ndio sifa zake za jumla
Sifa za iPhone Duo
| Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
|---|---|
| Network | 2g, 3g, 4g, 5g |
| Processor(SoC) |
|
| Display(Kioo) | LTPO Super Retina XDR OLED, Refresh rate:120Hz |
| Softawre |
|
| Memori | NVMe, 256GB, 512GB, 1TB, 2TB na RAM 12GB |
| Kamera | Kamera TATU
|
| Muundo | Urefu-7.6inchi |
| Chaji na Betri |
|
| Bei ya simu(TSH) | 6,000,000/= |
Uwezo wa network
iPhone Duo inasapoti aina zote za mtandao
Hizi simu zinasapoti laini za eSIM pekee
Kwa maana haziji na sehemu ya kuweka laini
Bali mfumo wake ni wa laini za ndani ambazo ni chip
Na inasapoti aina zote za network
Nguvu ya utendaji
iPhone Duo ina nguvu kubwa kutokana na prosesa mpya iliyopo
Kwenye app ya kupima nguvu za prosesa (geekbench) inaonyesha utendaji wake unazizidi baadhi desktop
Kwa mfano prosesa ya kompyuta Intel Core i3 12100 inaiachwa mbali na Apple A20 Pro
Hii inamaanisha hii simu inaweza kufungua AI za offline bila shida
Na bahati nzuri ina ufanisi mkubwa wa kutumia betri kidogo ila utendaji mkubwa
Kiujumla utaitumia hii simu bila kukwama kwama
Ubora wa kioo
Kiujumla upana na kimo cha kioo ni inchi 7.3
Ni kioo cha kujikunja na kujikunjua
Upande wa nje pia ina kioo

Kwa mantiki hiyo ni kama ina vioo vitatu
Inakupa uhuru wakati ukifungua vitu vinavyohitaji skrini kubwa
Kwa mfano kama unasoma vitabu unaweza kuikunjua skrini na ukaona maandishi makubwa
Ama ukiwa unahitaji kutumia app nyingi kwa wakati mmoja
Skrini yake kubwa inakuwezesha kuzioana app zote
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya iPhone Duo sio kubwa ukilinganisha na simu za Android
Ukubwa wa betri ni mAh 4883, wakati simu za android za kawaida ni 5000
Ila hili lisikutishe
Hii simu inakaa na chaji balaa kuliko hata simu za mAh 5000
Picha ya hapa chini kutoka kwa mtumiaji wa iPhone Duo inaonyesha uwezo wake

Kwa maana iPhone Duo inaweza kukaa na chaji karibu masaa 15 ikiwa inatumika muda wote
Chaji yake inasapoti hadi umeme wa wati 25
Sio spidi kubwa sana maana siku hizi kuna simu hadi za wati 120 upande wa chaji
Uimara wa bodi
Kama ilivyo simu nyingi za daraja la juu huwa na waterproof
Hii pia ina waterproof na inaweza kuzuia maji kama ikizama kaenye kina kikubwa
Kina hiko ni cha mita 1.5 kwa muda wa nusu saa
Hata hivyo skrini yake imeleta changamoto kwa baadhi ya walitoitumia hii simu.
Changamoto za skrini
Kuna wimbi la simu za iPhone Duo zimeibuka zikiwa zimeharibika sehemu ya skrini
Uharibifu huu umesababishwa na bawaba inashikiria skrini mbili
Hii bawaba imesababisha skrini kutuna kwenye maeneo ya skrini

Na simu zingine skrini imeonyesha kuvuja rangi
Kwa sasa unaruhusiwa kubadili na kupewa nyongine

Inaonyesha apple hawajeza kuimasta aina hii ya simu kama ilivyo kwa samsung
Ubora wa kamera
Kamera mpya za iPhone zimewekea kitu kinaitwa variable aperture
Hii inakupa nafasi kuruhusu kiasi cha mwanga kipite kwenye kamera
Kuna mazingira picha itokee vizuri unahitajo mwanga mdogo
Hivyo utabadilisha setting
Tofauri na ilivyozoeleka simu huwa na kiwango kilekile cha aperture
Changamoto za software
Bahati mbaya bado kuna app nyingi hazikatengenezwa kuendana na skrini za kujikungunja
Kuna nyakati app haifiti vizuri kwenye skrini
Kadri muda utakavyosegea maboreaho yatakuja zaidi