SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

GPS ni Nini? Maana na Kazi ya GPS

Miongozo

Sihaba Mikole

July 2, 2022

GPS ni mfumo wa utambuzi wa maeneo duniani unaotumia satelaiti ambao unamilikiwa na nchi ya Marekani

Mara ya kwanza wakati unaanzishwa ulilenga matumizi ya kijeshi

Ila hali ilianza kubadilika mnamo mwaka 1983 baada ya USSR kulipua ndege ya Korea kusini iliyokuwa inatokea Marekani

Ndege ya Korea Kusini ilingia kwenye anga ya USSR iliyokatazwa bila kutambua

Mpaka mwaka 2000 GPS ilianza kutumika kwa matumizi ya kiraia

Mifumo mingine ya utambuzi wa maneneo ni GLONASS ya Urusi, Galileo ya Ulaya, Baedou ya China

Baada ya kujua GPS ni nini basi ni vizuri ukajua jinsi inavyofanya kazi

Mgawanyo wa GPS katika utambuzi wa Eneo

Ili mfumo wa Global Positioning System utambue eneo kuna vitu vinahitajika kufanya kazi kwa pamoja

  1. Setilaiti
  2. Receiver (simu)
  3. Control Center (kituo cha udhibiti)

Satelati ni kitu chochote kinachoizunguka dunia

Katikamfumo wa GPS kuna idadi ya satelaiti zinazofika 30

Japokuwa kikawaida huwa kunahitajika satelaiti walau nne ili eneo litambulike

Lakini kadri satelaiti nyingi zinavyopatikana ndio usahihi mkubwa wa utambuzi wa eneo unakuwepo

Setilaiti huwa inatuma signal (mawimbi) kwenda kwenye simu

Ndani ya simu kunakuwa na kifaa kinachopokea hayo mawimbi

Kifaa hiko hutambulika kama GPS receiver

Ufuatiliaji wa karibu wa mwenendo wa ufanyaji kazi wa setilaiti unahitajika

Hiyo kazi inafanywa na kituo cha udhabiti (control center)

GPS ina vituo vya aina hiyo vinavyofika 17

Kwa afrika kituo kinapatikana afrika ya kusini pekee kwenye mji wa pretoria

Jinsi GPS inavyofanya kazi kwenye simu

Kila simu janja huwa ina receiver kwa ajili ya utambuzi wa eneo

Receiver ina kazi ya kupokea data kutoka kwenye setilaiti kisha inafanya mahesabu ya kujua latitudo na longitudo ya eneo uliopo

Ili GPS ya simu ionyeshe eneo sahihi inahitaji kupokea data kutoka kwa setilaiti zaidi ya nne

Kisha GPS receiver inakokotoa umbali kati ya setilaiti na simu kwa kila setilaiti inayopatikana

Tofauti ya umbali zitaonyesha taarifa ya eneo ilipo gps receiver ya simu husika

Hivyo eneo ulilopo taarifa zake zinakuwa wazi

Tuchukulie mfano ufuatao.

Kuna mtu A anaishi mwanza na kuna mtu B anaishi dar es salaam

Halafu, tunataka kujua mtu A anaishi wapi

Ukitaka kujua nitamuuliza mtu B umbali kati ya Dar na anapoishi mtu A

Lakini taarifa ya mtu B pekee haitoshi kujua eneo ambalo mtu A anapatikana

Hivyo inahitajika mtu C anayeishi kigoma, mtu D anaeishi Arusha na mtu E anayeishi Mbeya kwa mfano.

Kisha ataulizwa mtu C, D na E umbali kutoka maeneo wanayoishi hadi kwa mtu A

Urefu wa maeneo yote hayao utakuwa unakutana kwenye eneo moja

Kwa staili hiyo mtu A anayeishi atatumbulika eneo lake analoishi ambalo litakuwa ni Mwanza

Kwa sababu upande unaopatikana mwanza utakuwa umejulikana

Hivyo ndivyo GPS receiver ya smartphone inavyoweza kujua eneo ulilopo kwa kupima umbali wa kati ya simu yako na setilaiti zaidi ya nne

Uonyeshaji wa eneo hutumia njia ya ukokotoaji inayofahamika kama trilateration  na Multilateration

Hatutoingia kiundani kufafanua trilateration  na Multilateration ila pitia wikipedia, Global Positioning System 

Jinsi ya kuwasha GPS kwenye Smartphone

Ni rahisi kuwasha gps kwenye simu

Upande wa juu wa screen unaoonyesha tarehe, network ya simu nk

Iguse hiyo sehemu kwa kushusha chini

Utaona machaguo mengi kama kuwasha data, bluetooth, wi-fi, tochi na vitu vingine

GPS hutambulika kama Location

Ukigusa tu basi gps receiver ya simu itaanza  kusoma eneo ulilopo

Na unaweza ukaona eneo ulilopo kwa kufungua ramani ya Google

Itakuonyesha ulipo kwa wakati huo

Usahihi wa GPS kuonyesha Eneo

Mfumo unatoa kwa usahihi mkubwa taarifa za eneo ambalo simu ipo

Ila si kwa usahihi wa asilimia mia

GPS huwa ipo nyuma kwa umbali wa mita tano toka eneo ambalo kifaa cha gps kilipo

Tatizo linakuwepo hasa pale simu inakuwa inapata data kutoka kwenye setilaiti chache

Tatizo hili linalekebeshwa kwa kuiwezesha simu janja kusapoti mifumo kama ya GPS ya nchi zingine

Ndio maana simu nyingi za daraja la kati na juu huwa zina mifumo zaidi ya mmoja ya utambuzi wa maeneo

Utakuta simu moja inakubali Galileo ya umoja wa ulaya, Glonass ya urusi na Beidou ya china

Kama utakuwa na matumizi mengi ya GPS inafaa ukawa na simu inayokubali mifumo mingi

Matumizi ya GPS na Faida Zake

Taarifa za GPS zinaweza kukusaidia kwenye mengi mno

Ukiwa umeiwasha itakusaidia kujua spidi ya chombo chochote cha usafiri unachosafiria ikiwemo baiskeli

Hilo linafanikiswa kwa kutumia aplikesheni

Kuna app nyingi zinazoweza kuonyesha spidi na umbali kutumia gps

Moja ya app iyo inaitwa GPS speedometer

Pia, inaimarisha ulinzi hasa pale simu inapopotea

Kama gps ikiwa imewashwa utaweza kufuatilia eneo ambalo simu ipo

GPS pia hutumika kupima viwanja

Je Ni Salama kuwasha GPS muda wote?

Kiujumla ni salama kama wewe si muharifu

Ubaya wa kuwasha gps mara kwa mara unakuja kwa makampuni makubwa ya teknolojia kama Google, Facebook, Apple nk

Yana tabia ya kuchota taarifa zako pasipo kujua japokuwa wengi hurusu hizo app kuchota data

Haya makampuni hutumia hizo taarifa kwenye biashara zao za matangazo

Mtu akiweka tangazo anaweza kuchagua eneo ambalo tangazo linapaswa lionekane

Kiujumla, ni vizruri GPS ikawa ON muda wote

Inakupa urahisi kuifutalia simu inapopotea

Hitimisho

Ukiwa ni mtu wa kuzingatia faragha itakulazimu kuzima GPS muda mwingi

Ikizingatiwa tayari unafahamu maana ya GPS ni nini na umuhimu wake

Maana kila kilicho na maana hakikosi mapungufu

Lakini jua kuwa huu mfumo unaweza kurekebisha saa ya simu kwa usahihi mkubwa

Kwa sababu gps inasifirisha data zinawakilisha nyakati

Muda unaoletwa na setilaiti ni sahihi zaidi kuliko uliopo kwenye simu

Kwa sababu satelaiti zake zinatumia Atomic Clock kusoma muda

Maoni 16 kuhusu “GPS ni Nini? Maana na Kazi ya GPS

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

google pixel 8 appearance

Google Pixel 8, Simu ya Teknolojia ya Akili Bandia (AI)

Google Pixel 8 na Pro zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi wa kumi tarehe nne Matoleo mapya ya pixel yatatumia toleo la android 14 Android 14 ilitangazwa tangu mwezi wa pili lakini […]

iphone 15 muonekano

Ujio wa Simu mpya za iPhone 15 Septemba 2023

Kwenye tarehe 12 mwezi wa tisa 2023 kwenye ukumbi wa Steve Jobs makao makuu ya apple kutakuwa kuna uzinduzi wa bidhaa kutoka kwa kampuni ya apple Tukio hili litarushwa moja […]

oppo find x6 pro thumbnail

Oppo Yenye Kamera Nzuri na Ubora wa Picha

Kuna matoleo mengi ya simu za oppo zenye ubora tofauti tofauti Zipo ambazo zina ubora wa kati, wa juu na wa chini Katika hizo, nyingi zinajitahidi kuwa na kamera zinazotoa […]

No Featured Image

Simu Mpya za Samsung na Bei Zake 2023

Kama unatafuta samsung mpya kwa mwaka 2023 basi upo sahihi Kwenye hii kuna simu zipatazo saba na maelezo mafupi kuhusu sifa zake Kwenye hii orodha ya simu mpya za samsung […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram