SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Jinsi ya Kutumia GPS kwenye Simu (Hatua kwa Hatua)

Android/iOS

Sihaba Mikole

May 18, 2023

GPS kirefu chake ni Global Positioning System, ni mfumo wa utambuzi wa maeneo ambao unasimamiwa na Marekani

Simujanja karibu zote zina huu mfumo

Una faida kubwa sana hasa kama unajua jinsi ya kutumia gps kwenye simu yako

Inaweza kukulinda na upotevu ama kufuatilia mahala ambapo kifaa chako kipo kama umekipoteza

Pitia: Maana ya GPS na jinsi inavyofanya kazi

Matumizi ya GPS yanahitaji kuwa na app aidha ya ramani au ya kupima umbali, eneo na hata spidi

Hapa utaabarishwa hatua zote muhimu ili uweze tumia gps

Kuwasha GPS

GPS inatakiwa iwe ON ili uweze kuitumia

Kama ikizimwa hakuna app yoyote itakoyeweza pata taarifa za eneo husika

Jinsi ya kuwasha gps ni rahisi

Kwenye simu hutambulika kama “Location

kuwasha gps

Swipe(kutachi) kioo chako cha simu kutokea juu ili ije sehemu yenye machaguo ya kuwasha data, wifi, tochi, bluetooth na mengineyo

Katika hayo machaguo kuna chaguo mojawapo limeandikwa “Location” alama yake ni kamshare kuria upande wa juu

Kama umeweza kuiona itachi sehemu husika na hapo utakuwa umeiwasha

Kujua namna ya kuitumia inategemeana na malengo yako kwa sababu ina matumizi mengi

Na kwa maana utalazimika kutumia apps mbalimbali zinazoweza kufanya kazi unayoitaka kwa kutumia GPS

Hivyo tutafafanua jinsi ya kutumia huu mfumo kwa kuangalia baadhi ya matumizi

GPS Kwenye Ramani(eneo ulilopo)

Baada ya kuwasha fungua applikesheni ya ramani kwenye simu za android huitwa Maps

Simu zote zina applikesheni ya google maps

Ukiifungua kitu cha kwanza ramani itakuonyesha eneo ambalo hupo wakati huo

Hata ukiwa unatembea app inaendelea kuonyesha ulipo yaani inabadilika kutokana na unavyohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine

Google Maps inaweza kukuonyesha majengo yote ambayo upo jirani nayo wakati huo

Na pia kama kuna vituo vya afya na mashule basi app itakuonyesha hizo taasisi

Kama huijui njia applikesheni itakuelekeza

Kutambua spidi ya chombo chako cha usafiri

Pia unaweza kuitumia gps kama kifaa cha kusoma spidi ya chombo chako cha usafiri

Na unaweza kuitumia kufahamu spidi yako ya kutembea, kukimbia na hata kasi ya baiskeli

Hii itakulazimu kutumia applikesheni za speedometer zinazopatikana play store

spidi km

Nenda playstore kisha tafuta applikesheni imeandikwa GPS Speedometer ina nembo(PICHA) ya 84MPH

Ukishaingia kwenye simu ifungue na uipe ruhusa ya kutumia gps

Baada ya kuifungua utaona kitufe kimeandikwa Start Trip

Gusa hiko kitufe baada ya hapo utaona spidi ya chombo ambacho unasafiri nacho

Kujua umbali uliotembea na wa eneo unaloenda

GPS ya simu ina uwezo wa kukujulisha umetembea umbali kiasi gani

Na pia inaweza kukuonyesha umbali kutoka eneo ulilopo mpaka unapoenda

Applikesheni nzuri ya kujua umbali uliotembea ni hiyo hiyo  ya GPS Speedometer

Kwa sababu inaonyesha umbali pamoja na spidi kwa wakati mmoja

Kadri utakavyokuwa unatembea app inaandika kilomita ambazo umetumia

direction selection

Hii inaweza kukusaidia kujua urefu unaotembea ama matumizi ya mafuta ya gari unayotumia kutokana na huo urefu

Kama unasafiri kwenda kwenye mkoa mwingine google Maps inaweza kukujulisha muda uliobaki kufika eneo unaloenda kutokana na spidi yako au ya gari ama chombo chochote

Ili uweze kufanikisha hili yafuatayo unapaswa uyafanye.

  1. Fungua applikesheni ya Google Maps  (Maps)
  2. Upande wa chini kulia kuna alama ya bluu yenye mshale kuelekea kulia, bonyeza hapo
  3. Itakuja sehemu ya kuweka eneo ulilopo na unaloenda, app itatumia gps ya eneo ulilopo(haina haja ya kujaza)
  4. Jaza eneo ambalo unaloenda
  5. Chagua aina ya usafiri (Gari, treni au kwa mguu) hata ukiacha haina shida
  6. Utaona muda na kilomita za eneo husika
  7. Chini yake bonyeza “Start”

Baada ya hapo Google Map itakuwa inakuelekeza uelekeo wa kufuata kama binadamu tena kwa sauti ila ya kiingereza

Na itakwambia hilo eneo ukifika

Kutrack simu

GPS inaweza kutumika kuifuatilia simu mara nyingi kukiwa kuna app

Google map inaweza kutumika kujua eneo ambalo mtu anaweza kutumia

Kutokana na maswala ya haki za faragha, hatotuchimba kiundani kwa kuonyesha aina za app zinazotumika kufanya hiyo kazi

Ila kwenye app ya map unaweza kushea eneo ambapo simu ipo muda wote

Unaweza kufuatilia zaidi kwenye tovuti ya google wameelezea kiundani

Hitimisho

Namna ya kutumia gps ni rahisi na inategemea unaitaka kuitumia gps ikusaidie kitu gani

Unapowasha gps itakulazimu utumie app mbalimbali zinazojishughulisha na kitu

Mara nyingi gps inatumika pamoja na applikesheni za ramani kama Google Maps

Maoni 16 kuhusu “Jinsi ya Kutumia GPS kwenye Simu (Hatua kwa Hatua)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

tecno camon 30 thumb

Bei ya Tecno Camon 30 Pro na Sifa Muhimu

Simu ya Tecno Camon 30 Pro ilitangazwa mwezi februari ila imetoka rasmi mwezi wa nne 2024 Ni simu ya daraja la kati(midrange) hivyo bei yake sio sawa na Tecno matoleo […]

tecno camon 30 premier thumbnail

Bei ya Tecno Camon 30 Premier 5G na Sifa zake muhimu

Kwenye matoleo bora ya simu kutoka Tecno, matoleo ya Tecno Camon huja na ubora katika vipengele vingi Hata bei za matoleo ya Camon huzizidi bei za Tecno Spark na Tecno […]

No Featured Image

Simu Mpya za Samsung 2024 (za bei rahisi na ghari)

Kuna simu zaidi ya tisa zilizotengenezwa na kampuni ya Samsung kutoka Hapa kuna orodha ya simu kumi mpya za samsung ambazo zimetoka mwishoni mwa mwaka 2023 hadi mwaka 2024 Ni […]

Bei ya Samsung Galaxy A25 na Sifa zake

Simu ya Samsung Galaxy A25 ilitoka rasmi mnamo mwezi desemba 2023 Ni simu ya daraja ambayo bei yake kwa Tanzania ni shilingi laki saba (700,000/=), hii ikiwa ni bei ya […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram