SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Zitambue Simu Feki za Samsung Kwa Njia Rahisi

Miongozo

Sihaba Mikole

February 18, 2023

Moja ya changamoto ya ununuaji wa simu nzuri ni kukumbana na wauzaji wasio waaminifu.

Hawa wauzaji wapo wengi maeneo maarufu ya uuzaji simu nchini hasa Dar Es Salaam na ikiwemo mtandaoni

Mara nyingi utakutana na tangazo simu used toka dubai au UK nk

Wanunuaji wa simu za Samsung aina ya S-series mfano wa Samsung Galaxy S20, Samsung Galaxy S23 huathirika zaidi

Hivyo huna budi kujua jinsi ya kuzitambua simu feki za Samsung iwapo unataka kununua samsung za bei ya juu

Zipo njia nyingi lakini hizi ziliowekwa hapa ni baadhi.

Kuangalia Mfumo Endeshi wa One UI

Samsung tangu 2019 zinatumia mfumo endeshi wa One UI ambao una apps za samsung

Hivyo hatua ya kwanza ni kujua kama mfumo endeshi wa hiyo simu ina One UI

Unapaswa kujua taarifa za simu kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo tovuti rasmi ya Samsung

Haihukikishii kuwa simu ni orijino ila ni hatua ya mwanzo kabisa ya kuifuata

Kwa sababu mfumo endeshi wa Samsung wenye android 11 unaweza kuwekwa kwenye simu zingine

Ili kujua toleo la One UI, ingia Settings ->About Phone -> Software Information

Kwenye orodha utaona namba ya toleo kwenye kipengele cha kwanza

Baada ya hapo india kwenye tovuti ya Samsung au GSMArena au SimuNzuri usome sifa za simu

Kisha linganisha kama zinaendana

Kutazama aina ya Processor ya Simu

Mbinu ya pili ni kuweka applikesheni ya CPU Z kwenye simu ya samsung unayotaka kununua

App ya CPU Z inaweza kusoma taarifa zote za simu husika

Taarifa ya muhimu unayoihitaji kuifahamu ni processor iliyotumika

Simu nyingi za Samsung zinatumia chip ya Exynos au Qualcomm Snapdragon

Iwapo taarifa za SoC (System On Chip) zinataarifu tofauti basi jua kuwa simu inaweza kuwa ni feki

Kwa mfano Simu ya Samsung Galaxy S10 toleo la Marekani zina SoC ya Snapdragon 855 na sehemu zingine duniani zinakuja na chip ya Exynos 9820

Hivyo CPU Z inapaswa ikuonyeshe mojawapo kati ya chip hizo mbili

Lakini taarifa za app zikiwa tofauti jua kuwa samsung uliyo nayo ni feki

Hakuna muuzaji atakayekubali uweke app kabla ya kununua lakini simu zote mpya huwa zina warrant

Tumia muda wa warant kuichunguza simu

Kutazama muonekano wa utoaji mwanga wa kioo

Karibu matoleo mengi ya S-Series hutumia vioo vya Amoled

Sifa kubwa ya amoled ni kutotumia taa bali kioo hutoa mwanga wenyewe

Hivyo inafanya rangi nyeusi kuonekana kwa usahihi kabisa

Kiasi cha kwamba kama simu ukiiwasha kwenye giza hakuna mwangaza unaoweza toka kwenye kioo

Ukienda kwa muuzaji muulize aizime na kuiwasha simu kisha aiweke sehmu simu yenye giza

Kioo cha amoled rangi nyeusi huonekana giza totoro

Kutumia IMEI namba

Kirefu cha IMEI ni International Mobile Equipment Identity ambayo inawakilisha namba ya kipekee ya kifaa unacho kimiliki

Kila simu huwa ina namba yake ya utambulisho ndio ukiibiwa simu polisi wanaulizia IMEI ya simu

Ukibonyeza kwenye simu namba *#06# utaona namba yenye tarakimu 15

Inakiri hiyo IMEI namba na kisha na kisha tembelea tovuti zenye mfumo wa kucheki IMEI

Tovuti za namna hiyo zitaitambua aina ya simu na zitakuonyesha taarifa za simu hiyo

Moja ya website hiyo ni, imei checker, unaingiza hizo namba kisha bonyeza check

Kama tovuti inaleta taarifa tofauti kabisa na samsung unayotaka kununua elewa kuwa hiyo simu yaweza kuwa ni feki

Ila njia hii sio ya uhakika sana

Kwa sababu IMEI namba zinaweza kubadirishwa japokuwa TCRA inapiga marufuku mafundi kubadiri IMEI za simu

Kuizamisha simu kwenye maji

Hii ndio njia ya uhakika kabisa japo inaweza kukustajahabisha

Samsung zote za bei kubwa zilizowahi huwa hazipitishi kwenye kina cha mita moja na nusu kwa muda wa nusu saa

Na hata ukiitoa simu nje ya maji simu inaendelea kufanya kazi kama kawaida

Hii inatokana na hizo simu kuwa na viwango vya IP68 vinavyoainisha kuwa simu inaweza kuzuia maji na vumbi

Kwa samsung toleo la S-Series inaweza kustahamili hali hii pasipokuwa na shaka

Kwa hiyo unaweza itumia hii njia baada ya njia zingine zote kuonesha usahihi

Kufuatiliatilia spidi ya chaji

Kasi ya chaji kupeleka umeme mwingi hutegemea na jinsi muundo wa simu ulivyoundwa

Kwenye sifa za simu huwa kunainishwa uwezo wa simu kupitisha chaji

Kwa mfano kasi ya chaji ya Samsung Galaxy S23 Ultra inafika wati 45

Maana yake ni kuwa simu husika inapaswa isome kiwango hiko pidi chaji yenye uwezo wa wati 45 inpowekwa

Kuna app kama AccuBattery ambayo inaweza kuonesha kiwango cha chaji kinachoenda kwenye simujanja

Samsung feki lazima iwe inapeleka chaji kwa kiwango tofauti na kilichoanishwa

Hitimisho

Hizi njia zote zinakuhitaji wewe mtumiaji kuifahamu simu kabla ya kuamua kuinnunua

Ndio maana kwenye tovuti ya simunzuri ikitajwa bei pia kuna maelezo ya simu husika

Usipofuatilia simu unaweza ukajikuta unamiliki samsung feki

Maoni 4 kuhusu “Zitambue Simu Feki za Samsung Kwa Njia Rahisi

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A35 na Sifa zake

Samsung Galaxy A35 ni toleo jipya la samsung lilotoka mwezi machi 2024 Ni simu ya daraja la kati iliyochota baadhi ya sifa muhimu kutoka kwenye galaxy yenye bei kubwa Ndio […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

samsung s24 plus thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy S24+ na Sifa Zake

Kisifa Samsung Galaxy S24 Plus ina sifa nyingi zinazoendana kwa kiasi kikubwa na Samsung Galaxy S24 Ultra Kwa maana Galaxy S24+ ubora wake unazipita simu nyingi na mkubwa, hivyo bei […]

samsung s24 ultra thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy S24 Ultra na Sifa zake

Hivi karibuni simu mpya ya Samsung Galaxy S23 Ultra imeingia sokoni huku bei yake ikiwa haitofautiani sana na Apple iPhone 15 Pro Max Kwenye soko la dunia bei ya samsung […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram