Samsung Galaxy Note 10 ilitoka kwa mara ya kwanza mwaka 2019
Inaenda miaka minne na kuna matoleo mengi na mazuri yametoka ya simu kama Oppo A78
Pamoja na umri mkubwa bado Galaxy Note 10 inachuana na kuziacha nyuma simu nyingi
Ndio maana bei ya samsung galaxy note 10 kwa Tanzania bado ni kubwa na inazidi laki saba dukani
Hapa utaelewa nyanja ambazo zinaendelea kuziweka hizi simu kwenye chati hasa ukiangalia sifa zake
Bei ya Samsung Galaxy Note 10 ya GB 256
Kwa Dar Es Salaam simu inauzwa kwa shilingi 750,000 ambayo memori yake ni GB 256
Ukitazama bei yake inaendana na simu ya na simu Tecno Camon 19 Pro 5G ila kisifa samsung iko vizuri maeneo mengi
Kuanzia kamera, kioo mpaka uwezo wa 4G ni wa kasi kubwa
Kitu utakochokosa kwenye hii simu ni 5G na betri yake ambayo sio kubwa
Ila ni simu inayoweza kukidhi haja nyingi za mtumiaji kwa mwaka 2023 pasipo kuwa na shida
Sifa za Samsung Galaxy Note 10
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Dynamic Amoled |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.0, 256GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.3inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 750,000/= |
Upi ubora wa samsung galaxy note 10
Ni simu ambayo haipitishi maji kama ikizama kwenye kina kikubwa
Ina kioo kinachoonyesha vitu kwa uzuri na kwa rangi sahihi kwa kiwango kikubwa
Ina mgawanyo wa kamera unaokupa machaguo wa kupiga picha za umbali tofauti tofauti
Ubora wa picha bado ni mkubwa ukilinganisha na simu nyingi za hivi karibuni
Inapokea matoeo ya hivi karibuni ya android
Ina mfumo wa memori unaosafirisha data kwa kasi hivyo simu kuwa nyepesi
Chaji yake ina peleka umeme mwingi
Kiufupi simu ina kasoro chache ambazo zinasababishwa na hatua kubwa iliyopigwa hivi karibuni kwenye simujanja
Tuitazame kiundani kwenye nyanja zingine muhimu
Uwezo wa Network
Hii simu inasapoti mtando mpaka wa 4G aina ya LTE Cat 20
Kasi ya LTE Cat 20 ni 2000Mbps ambayo ni sawa na 250MBps
Kwa mfano kama ukipakuwa applikesheni ya whatsapp, simu itachukua chini ya sekunde moja kumaliza kudownload
Kwa bahati mbaya sio rahisi kuipata kasi hii kwa hapa Tanzania
Inakubali masafa yote ambayo yanatumika hapa nchini
Kwa kuwa simu ilikuwa ni ya 2019 basi 5G haiwezi kutumika humu
Ila kama unatamani 5G kuna samsung galaxy a54 yenye sifa nzuri zaidi ya hii
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy Note 10
Kioo cha Galaxy Note 10 ni aina ya Super Amoled ambacho kina reoslution kubwa ya 1080 x 2280 pixels
Kiwango cha resolution kinazidi baadhi ya simu mpya za 2023 ambazo hutumia 720 x 1660 pixels
Pixels nyingi huongeza uangavu na muonekano safi wa picha na video zinazonekana kwenye kioo
Uzuri mwingine wa kioo cha hii simu ni kuwa kina HDR10+
HDR10+ husaidia kioo kuweza kutofautisha kwa uzuri kati ya rangi nyeusi kama vile kivuli na rangi nyeupe kama vile jua
Kitu kinachosababisha muonekano wa vitu huendane na mazingira halisi ya kitu kinavyoonekana
Ni nadra hata kwa simu za daraja la kati za 2023 kukuta walau HDR10
Mara nyingi huwa wanaweka refresh rate kubwa
Nguvu ya processor Exynos 9825
Simu inatumia chip ya Exynos 9825 kwa zile ambazo zilikuwa zinauzwa nje ya Marekani na China
Kwa soko la china na USA walikuwa wanapata samsung zinazotumia chip ya Snapdragon 855
Chip zote zina mfanano kwani zimegawanyika katika sehemu tatu, sehemu mbili zinatumia muundo wa Cortex A75 isipokuwa core kubwa zina kasi inayofika 2.73GHz
Kwa miaka ya hivi karibuni muundo wa cortex a75 haiwezi kuchukuliwa kuwa na nguvu
Kwani kuna miundo mipya kama Cortex A78 ambayo inapiga kazi kubwa na kwa matumizi madogo ya betri ya simu
Hata hivyo bado inaweza kufungua app nyingi kwa wakati mmoja na kucheza magemu mengi bila tatizo
Kama utendaji ni msisitizo mkubwa kwako ni vizuri ukaangalia simu kama Tecno Phantom X2 Pro yenye processor yenye nguvu kuliko hii
Ila bei pia lazima ipande
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Samsung galaxy note 10 ina ukubwa wa wastani tu wa 3000mAh
Ni betri ndogo hivyo ukaaji wa chaji sio mkubwa kwa sababu ya betri
Chaji inapeleka umeme wa wati 25 kiwango cha juu ambayo inajaza betri kwa haraka
Ukizingatia kuwa betri sio kubwa hivyo simu itawahi kujaa tu
Ukiwa unaperuzi intaneti muda wote simu inaweza kuchukua masaa takribani 11 kuisha chaji
Siku hizi simu nyingi zinakuja na betri kubwa na betri na zenye wastani wa ukaaji wa chaji wa masaa zaidi ya 15 ikiwa kwenye intaneti
Ukubwa na aina ya memori
Upande wa memori simu ina toleo moja tu
Toleo hilo lina ukubwa wa GB 256 na RAM ya GB 8
Na aina ya memori simu iliyonayo ni UFS 3.0 ambayo kasi yake ya usafirishaji wa data ni 2400MBps
Kiwango hiki kinafanya app kufunguka kwa haraka na simu kuwahi kuwaka pindi ukiwasha
Ukubwa wa memori ni wa kutosheleza kuhifadhi mafaili mengi na applikesheni za kutosha
Ukitaka kuongeza memori kadi hutoweza kwa sababu simu haina sehemu ya kuweka memori kadi
Hivyo tumia simu vizuri ila GB 256 ni kubwa pia
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy Note 10
Samsung Galaxy Note 10 haina bodi ndefu sana kutokana na urefu wake kuwa ni inchi 6.3
Upande wa nyuma na mbele imewekewa vioo aina ya gorilla 6 kutoka kampuni ya Gorilla ya marekani
Hivi huwa ni vioo vigumu kuchunika, hataka ukiweka sarafu pamoja na hii simu mfukoni sio rahisi kwa mikwaluzo kutokea
Simu imethibitishwa na viwango vya IP68 ambavyo humaanisha kuwa simu haiwezi kupitisha maji iwapo itazama kwa kina cha mita moja na nusu kwa muda wa dakika 30
Kwa mantiki hiyo bodi ya galaxy note 10 ina bodi imara inayosaidia simu kukaa muda mrefu
Ubora wa kamera
Simu ina mfumo mzuri wa kamera kwani kuna lenzi ya telephoto kwa ajili ya kupiga kitu kilichopo mbali na kamera
Pia lenzi ya Ultrawide kwa ajili ya kupiga eneo kwa upana mkubwa mfano mkutano wa hadahara
Na pia kamera ya kawaida na kamera zote zina megapixel 12 ila ultrawide ina megapixel 16
Kumbuka kuwa simu yenye kuanzia megapixel 8 inaweza kupiga picha yenye ubora mkubwa na kurekodi video za 4K
Inategemea kama vitu vingine vinapatikana kwenye kamera kuanzia ulengaji kama dual pixel pdaf, ois, mpaka ubora wa app inayopiga picha
Kwenye mwanga mwingi galaxy note 10 inapiga picha na rangi sahihi za vitu bila kuathiriwa na mwangaza mwingi wa jua
Japo kuna kuzidisha fulani kwa rangi ya anga na kufanya kuonekana ya bluu sana
Kiwang cha chengachenga (noises) ni ngumu kuonekana
Pia simu inaweza kurekodi video mpaka za 4K ambazo huwa na ubora mzuri unapotazama kwenye tv ya 4K
Ubora wa Software
Kama simu ikiwa mpya inakuwa na Android 9
Ila inasapoti mpaka toleo la miaka ya hivi karibuni la Android 12
Kuna simu nyingi tu za mwaka 2023 zinakuja na Android 12, hii ina maana simu itaendelea kutumia apps nyingi bila shida yoyote kwa miaka mingi ijayo
Mbali na android simu pia ina mfumo wa One UI 4.0
Ni mfumo mwepesi usiokuwa na matangazo kama baadhi ya kampuni zingine zinavyofanya
Washindani wa Samsung Galaxy Note 10
Kuna machaguo mbadala na yenye sifa zinazoendana na Galaxy Note 10
Kiujumla karibu sote mpya za laki nane ni washindani wa hii samsung
Lakini kwa kuzingatia muktadha wa mwaka simu iliyotoka washindani sahihi ni Apple iPhone XS, Xiaomi Mi 9, OnePlus 7 Pro na Samsung Galaxy S10
Hizi simu zina vitu karibu vyote vilivyopo kwenye note 10
Na baadhi ya hizo zinapatikana kwa bei ya chini
Neno la Mwisho
Pamoja na uzuri wa hii simu ila jua kwa sasa nyingi ni simu used na sio mpya
Kama ukifanya maamuzi ya kuimilii weka akilini kuwa hutoweza kuipata hii simu ikiwa mpya kwa sasa
Hivyo unavyonunua jaribu kuichunguza simu kwa makini kuhakikisha hununui kitu kibovu kitakachokusumbua mbeleni
Maoni 6 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy Note 10 na Ubora wake 2023”
Nimeusubiri uchambuzi wa Hii simu kwa muda lakini nikaona kimya nikashawishika kuamia kampuni ya Xiaomi kwa sasa,nlitaka kununua hii simu ila,baada ya kuona simu hizi nyingi ni used nimeachana nazo
Ila asante kwa uchambuzi wako unatufundisha mengi
Naweza kununua simu za Samsung Galaxy Kwa kulipia kidogo kidogo?.Na ni njia ipi naweza kuitumia kujua fake na original Samsung Galaxy?
Nataman nimiliki sim ya Samsung ila naogopa sim used itakuja kunisumbua baadaye
kiujumla samsung ni sim bora na kwangu bado iko namba moja na sio mimi tu wa kusema hivo bali ni watanzania kwa ujumla
Natamani sana nije kufanya kazi na Samsung na hii professional yangu ya PRO, ili niitangaze duniani zaidi
Mimi naitumia ni muda sasa hadi leo.
Natafuta fundi wa kubadili kioo chake cha ndani ilipata hitilafu
Nataka nijue bei na fundi alipo.
Asante