eSIM ni aina ya laini ambayo inakuwa ndani ya simu huku ikifanya kazi bila kuwa na laini zilizozoeleka za muundo wa plastiki (PVC)
Kifaa cha mwanzo kuwa na eSIM ni saa ya Samsung Gear S2 Classic 3G mwaka 2016 kabla ya makampuni mengine kuanza kutumia
Umaarufu wa huu muundo umekuwa mkubwa hasa baada ya kampuni ya Apple kuzindua iphone 14 ambazo hazina sehemu ya kuweka laini nchini Marekani.
Umuhimu wake mkubwa hutohutaji kutembea ni kibati cha laini ama kuwa na wasi wa sim card yako kupotea
eSIM inaweza kuhifadhi namba mpaka nane ila zinazotumika huwa ni mbili
Kuna simu nyingi zenye teknolojia hii hivyo jifunze jinsi ya kutazama kama simu yako inasapoti eSIM
eSIM nchini Tanzania
Teknoljia hii inategemea kama mtandao wa simu una mfumo unaokubali kutumia eSIM
Kwa Tanzania kuna kampuni moja mpaka kufika leo april 2023 inayosopati embeded SIM(eSIM)
Kampuni hiyo ni Airtel
Kama ni mteja wa Airtel unaweza kutembelea ofisi zao na kisha wakakupa utaratibu wa kupata huduma hii
Ila usiende kabla ya kuangalia iwapo simu unayotumia inasapoti eSIM
Jinsi ya kutazama eSIM kwenye simu
Kuna njia chache ya kujua kama simu inaweza kutumia aina hii ya laini
Njia ya kwanza ni kwa kupiga namba *#06#
Baada ya kupiga utaona namba nyingi zenye lebo za IMEI, ICCID na EID
EID ni kitambulisho kuwa simu inayo eSIM
Kirefu chake eSIM ID, kama kifaa chako haina hii basi jua kuwa huwezi tumia muundo huu wa laini
Njia ya pili ni kwenda kwenye settings kisha kwenye sehemu ya search andika “IMEI”
Bonyeza sehemu ya imei itakuja sehemu inayoonyesha taarifa za imei zilizopo kwenye simu yako
Moja ya taarifa ya imei inayotakiwa kuwepo ni ya eSIM tofauti na hapo kifaa chako hakina muundo huu
Jinsi ya kuwezesha eSIM
Iwapo umegundua kuwa simu yako inayo, hizi ni hatua unazopaswa kufuata
Kitu cha kwanza lazima upate code kutoka kwenye kampuni ya simu unayotumia
Mara nyingi hizi huwa zipo kwenye muundo wa QR Code
Kisha washa simu yako (kwa upande wa android samsung)
Ingia kwenye Settings na chagua Connection halafu chagua SIM Card Manager
Itatokea orodha ya laini zilizopo kwenye simu ikiwamo eSIM
Kwa chini utaona pameandikwa Add mobile plan bonyeza hiyo sehemu
Simu ita-load ikicheki kama kuna simu kadi baada ya muda itakuja kitufe kinachosema “scan carrier qr code”
Inabidi uichague hiyo sehemu na kisha uanze ku-scan qr code ambayo umepewa na mtandao husika
Kisha kitakuja kitufe kikisema “add and use it now” chagua na hapo utakuwa umeiwezesha simu yako na eSIM
Kwa upande wa iPhone kuna hatua chache.
Nenda kwenye settings halafu data plan kisha chagua add data plan
Baada ya hapo itakuja screen ya kuscan qr code halafu utaendelea na hatua zingine
Simu zenye uwezo wa eSIM
Iwapo umeshafamu kuwa simu yako haina kabisa eSIM hizi ni baadhi ya simu janya unazoweza kuwa nazo
- Google Pixel 3
- iPhone XR
- Samsung Galaxy S20 Ultra
- iPhone 13 Pro Max
- Google Pixel 4
- iPhone 14
- iPhone 14 Pro
- iPhone 14 Pro Max
- Samsung Galaxy S21 Ultra
- Samsung Galaxy S21
- Samsung Galaxy S23 Ultra
- Samsung Galaxy S23 Plus
- Google Pixel 3a
- Google Pixel 4 XL
- Xiaomi 12T Pro
- Google Pixel 6
- Samsung S20 Plus
Yapo matoleo mengi kikubwa ni kuicheki kwa kufuata hatua zilizoelezewa hapa
Jinsi eSIM inavyofanya kazi
Embed Subscriber Identity Module yaani eSIM inakuwa ndani ya simu kama “chip”
Jina la hiyo chip huitwa eUICC inakuwepo ndani ya simu milele na haiwezi kutolewa
Chip ya eUICC inawekewa programu kiwandani programu itakoyoweza kusoma taarifa zinazohitajika na mtandao wa simu
Taarifa hiyo ikiwemo namba yako ya simu
Hivyo simu ikishascan qr code eUICC itazisoma taarifa na kuzihifadhi na kisha kukuanganisha na mtandao husika
Na itaanza kufanya kama laini za kawaida plastiki
Taarifa za laini hii inaweza kuondolewa ama kuongezwa nyingine kikawaida eSIM inaweza kuhifadhi mpaka laini nane
Hitimisho
Natumai maelezo haya mafupi yameweza kukupa mwangaza wa maana ya eSIM
Hutokuwa na haja ya kujiuliza eSIM ni nini isipokuwa kazi kubwa ni kukagua kama kifaa unachotumia kinayo hiyo teknolojia
Maoni 10 kuhusu “eSIM ni nini? Fahamu kama simu yako inayo”
Naomba kuuliza ikiwa simu yangu ina uwezo wa kuingia line moja pekee je naweza kuadd yapili ya esim?
Ndio inawezekana
Nna swali kama simu itapotea laini iliyosajiliwa kwa esim inaweza kufutwa?
Kabisa unaweza ukaiblock
Je kwa simu nyingne janja kama tekno cammon 11 au hizi vivo na xiomi azina hy kitu
Kwa tecno sijabahatika kuona simue yenye esim, kwa xiaomi zipo baadhi kama xiaom 12t pro na vivo ipo vivo x90 pro
Infinix hot 10 lite haina hii eSIM
Haina
Ninaweza kupata sm ya mkopo
Simu ya Aina gani?