SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Google Pixel 7 Pro na Ubora wake 2023

Sifa za simu

Sihaba Mikole

February 27, 2023

Google pixel 7 Pro ni moja ya simu inayosifika kuwa na kamera bora kwenye orodha ya simu mbalimbali

Ubora wa kamera unachagiza bei ya Google Poxel 7 Pro kukaribia milioni mbili

google pixel 7 pro showcase

Hii ni simu ambayo ipo kwenye kundi moja na matoleo ya Samsung Galaxy S23 au iPhone 14 Pro Max

Ni simu yenye utendaji mkubwa na utunzaji chaji wa muda mrefu kama ilivyofafanuliwa humu

Bei ya Google Pixel 7 Pro ya GB 128

Kwa kuzingatia bei ya ebay, google pixel 7 pro inauzwa shilingi 1,700,000/= yaani milioni moja na laki saba

Kwa hapa Tanzania bei yake lazima izidi na inaweza kufika zaidi ya milioni mbili

Sababu ya bei kubwa ni ubora kwenye sifa karibu zote kuanzia kamera, utendaji, display(kioo), chaji, betri bila kusahau upokeaji wa matoleo mapya ya Android

google pixel 7 pro summary

Kupata android mpya na aina ya vifaa ambavyo simu inavyo inaifanya simu kuweza kutumika muda mrefu

Kiasi cha kwamba inakuwa inaweza kuuzika hata baada ya miaka mingi tofauti na baadhi ya simu

Maana inaweza kusahangaza kwa nini Tecno Phantom X2 Pro ina bei ndogo kuliko Pixel 7 Pro

Kuna mengi ifuatilie zaidi.

Sifa za Google Pixel 7 Pro

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g na 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Google Tensor G2
  • Core Zenye nguvu ya ziada(2) – 2×2.85 GHz Cortex-X1
  • Core Zenye Nguvu(2)-2×2.35 GHz Cortex-A78
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.80 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G710 MP7
Display(Kioo) LTPO AMOLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 13
Memori UFS 3.1, 256GB,128GB,512GB na RAM 8GB,12GB,
Kamera Kamera TATU

  1. 50MP, multi-directional  PDAF(wide)
  2. 48MP(telephoto)
  3. 12MP(ultrawide)
Muundo Urefu-6.7inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-23W
Bei ya simu(TSH) 1,700,000/=

Upi ubora wa Google Pixel 7 Pro

Kitu cha kwanza kabisa ni upande wa software kwani inakuja na Android yenyewe kabisa

Ina kamera inayopiga picha vizuri kwenye kila aina ya mazingira

Utendaji wake ni mzuri kutokana na kuwa chip yenye nguvu

Ina mfumo wa chaji wenye kasi ya kujaza simu kwa haraka

Ni simu isiyopitisha maji

Inakuja na mifumo ya akili bandia inayorahisisha matumizi ya simu zaidi

Uwezo wa Network

Google Pixel 7 Pro ni simu ya 5G inayokubali aina zote za 5G

Moja ya 5G yenye kasi sana ni mmWave ambayo haipatikani kwenye simu zote za 5G

Ukiwa kwenye nchi yenye miundombinu hii utakuwa unapakuwa mafaili kwa muda mfupi sana

google pixel 7 pro network

Pia simu inakuja na uwezo  wa 4G aina ya LTE Cat 24 yenye uwezo wa kudownload kwa spidi inayofika 2Gbps

Ila hata kama unayo hii simu si rahisi kwa Tanzania kupata kasi hiyo

Utapata kasi ya kawaida kulingana na aina ya mtandao unaotumia

Hii simu inakuja na uwezo wa eSIM ambayo unaweza tumia bila laini lakini kwa Tanzania bado hii kitu

Ubora wa kioo cha Google Pixel 7 Pro

Kioo cha Google Pixel 7 Pro ni cha aina ya LTPO Amoled kama ilivyo kwa simu nyingi za google pixel

Ni kioo chenye resolution 1440 x 3120 pixels na refresh rate ya 120Hz

Kiwango hiki cha refresh rate pia kinaweza kusababisha kioo kutumia betri kwa kiwango kikubwa

google pixel 7 pro display

Ila LTPO inadhibiti kiwango cha refresh rate inayohitajika

Kama matumizi yanahitaji kiwango kidogo basi LTPO

google pixel 7 pro display 2

Umuhimu wa refresh rate unafanya kioo cha simu kuwa na mwitikio mkubwa na unaovutia wakati unapokuwa unagusa

Amoled huwa inafanya vitu vikolee kwa kuzingatia rangi halisia za vitu husika

Nguvu ya processor Google Tensor G2

Miaka ya hivi karibuni Google wameanza kutumia chip wanazounda wenyewe aina ya Tensor G2

Google Tensor G2 ni chip yenye nguvu ambayo imewezeshwa uwezo wa akili bandia (Artificial Intelligence)

Inaweza kufanya kila kitu kinachohitajika kwenye simu ikiwemo kucheza magemu

google pixel pro processor

Japokuwa ina nguvu ila bado inaachwa nyuma na Apple A15 Bionic ya iphone 13 au Dimensity 9000 ya Tecno Phantom X2 Pro

Kiujumla Google Tensor G2 imegawanyika katika sehemu tatu

Yaani sehemu (core) zenye nguvu sana, sehemu zenye nguvu kubwa kiasi na core zenye nguvu ndogo

Mgawanyo huu unakuhakikishia utendaji mkubwa wenye matumizi ya wastani ya umeme

Hivyo simu inaweza kudumu na chaji muda mwingi

Uwezo wa betri na chaji

Chaji ya Google Pixel 7 Pro inaweza kupeleka umeme mpaka wati 23

Kwa mujibu wa GSMArena, simu inajaa kwa 46% baada ya nusu saa

google pixel 7 pro chaji

Ni kiwango hafifu ukilinganisha na Samsung Galaxy S23 Ultra au simu ya Xiaomi 12 Pro ambayo muda huo inakuwa imejaa kwa 100%

Kwa bahati simu haiji na chaji hivyo utalazimika kununua chaji kama hauna

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh, kiasi kinachotosha kabisa kukaa na chaji muda mwingi

google pixel 7 pro chaji

Lakini ukaaji wake wa chaji  ni wa kawaida kwani inatumia masaa takribani 12 ikiwa inatumia intaneti muda wote

Ijapokuwa swala la ukaaji wa chaji hutegemea sana na matumizi ya mtumiaji

Ukubwa na aina ya memori

Aina ya memori ambayo Google Pixel 7 Pro inatumia ni UFS 3.1

Hii ni memori yenye kasi ya kusafirisha na kuhifadhi data inayofika 2400MBps

Kasi hiyo inaifanya simu kuhifadhi vitu kwa haraka ukiwa unakopi ama kudownload mafaili

Lakini pia inasaidia simu kuwahi kuwaka na kufungua appliksheni kwa haraka

Kuna matoleo matatu ya google pixel 7 pro upande wa memori

Unaweza ukanunua ya GB 128, GB 256 au GB 512.

Kikubwa uwezo wako kipesa kwani bei inapanda kulingana na ukubwa wa memori

Na upande wa RAM kuna GB 8 na GB 12

Uimara wa bodi ya Google Pixel 7 Pro

Google Pixel 7 Pro ina bodi imara yenye uwezo wa kuzuia maji kupenya

Iwapo hii simu ikizama kwenye kina cha mita 1.5 haiwezi ingiza maji kwa muda wa nusu saa

Na ukiitoa simu inaendelea kufanya kazi vizuri, ni tofauti sana na simu kama Samsung Galaxy A04

google pixel 7 pro bodi maji

Display yake inalindwa na glasi ya Corning Gorilla Glass Victus, na upande wa nyuma pia hivyohivyo

Corning Gorilla Glass vinaweza kustahimili kupasuka kwa kimo cha mita 1.5 kama simu ikianguka kwenye sakafu

Umuhimu wa kava si mkubwa sana ila ni muhimu kama kuweka tahadhari

Ubora wa kamera

Google Pixel 7 Pro ina jumla ya kamera tatu ambazo ni wide, ultrawide na telephoto

Kamera zote zinapiga picha vizuri bila kupoteza ubora

Nyakati za mchana ni hakuna kabisa chengachenga kwa maana noise

gogle pixel 7 pro kamera 2

Pia nyakati za usiku kwenye mwanga hafifu vitu vinaonekana kwa ustadi na noise kwa kiwango cha chini sana

Simu hii inaweza kurekodi video za 4k tena bila video kutikisika

Kwa sababu simu ina teknolojia OIS ambayo hutuliza kamera wakati ukirekodi huku ukiwa unatembea

Kamera zake zote zina HDR, ambazo huboresha muonekano wa vitu uendane na jinsi vinavyoonekana kwenye mazingira halisi

gogle pixel 7 pro kamera

App ya google camera inakupa uwezo wa kuondoa vitu ambavyo hutaki vionekane kwenye kamera

Kwa nfano upo ufukweni umepiga picha kisha kwenye picha watu wepembeni wakatokea

Basi kwa kamera hii, unaweza kuwaondoa wale wasiohitajika

Kiuhalisia ubora wake kwenye kamera huwezi linganisha na kamera za simu za bei rahisi hata kidogo

Ubora wa Software

Google Pixel 7 Pro inakuja na android mpya kabisa yaani Android 13

Kwenye android hii, utaweza kujibu meseji kwa kuongea bila kuandika kwa kutumia keyboard

Kwa maana unaweza ukawa unachati na mtu, wakati unaongea app ya meseji itakuwa inageuza maneno kuwa maandishi

google pixel pro software

Kwa bahati teknolojia hii inahitaji kutumia kiingereza

Kitu kingine Android 13 inaweza kukopi rangi ya wallpaper ni kuiweka vitu vingine vyote vya simu

Mfumo endeshi uliopo kwenye hii simu unafanya kazi kwa ufanisi na kwa haraka mno

Yapi Madhaifu ya Google Pixel 7 Pro

Simu haiji na chaji kitu kinachoongeza gharama nyingine bila kutarajia

Madai wanayoyasema ni kuwa wanatunza mazingira

Hii simu haiji na redio hivyo utalazimika kutumia intaneti kusikiliza redio

Simu hii haina sehemu ya kuweka memori

Ukaaji wake wa chaji ni wa wastani ukilinganisha na ukubwa wa betri

Neno la Mwisho

Kwa wapenzi wa kamera na software zilizo nyepesi Google Pixel 7 Pro ni moja ya simu bora kuwa nayo kwa mwaka 2023

Japokuwa kuna makampun kama oppo na simu ya oppo reno8 5G ila kiubali bado ipo nyuma ya pixel 7 Pro

Maoni 12 kuhusu “Bei ya Google Pixel 7 Pro na Ubora wake 2023

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

huawei mate

Simu Bora 15 Duniani 2024 (na zitakazotamba 2025)

Kwa mwaka 2024, soko la simu janja yaani smartphone duniani lilitawaliwa na makampuni ya Apple, Samsung, Xiaomi, Vivo na Oppo Kwa hapa Afrika kampuni ya Samsung inaongoza kwa mauzo ikifuatiwa […]

pixel 9 pro fold

Simu Mpya za Google Pixel 2024 na bei zake

Kuna matoleo yapatayo manne ya simu mpya za google ambayo yametoka mwaka 2024 Matoleo yote yanatofoautiana kwa kiasi fulani kwenye muundo na baadhi ya vitu kama utakavyoona Hivyo, bei zake […]

No Featured Image

Bei ya Google Pixel 9 na Sifa zake muhimu

Google Pixel 9 ni simu mpya kabisa ya pixel kwa mwaka 2024 Ni simu kali sana upande wa utendaji, kamera na software hasa katika matumizi ya AI(akili mnemba) Maboresho makubwa […]

pixel 8a thumbnail

Bei ya Google Pixel 8a na Sifa zake Muhimu

Kwenye mlolongo wa matoleo ya Google Pixel 8, Google Pixel 8a ndio ina bei ndogo zaidi Bei ya Google Pixel 8a ya GB 128 ni shilingi za tanzania milioni moja […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company