SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu ya Samsung Galaxy Note8 na Sifa Zake (2022)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

June 22, 2022

Mwaka 2017 ulikuwa una simu ya daraja la kwanza aina ya Samsung Note8

Simu ya samsung galaxy note8 ni simu ya android ambayo kwa sasa ina miaka karibu mitano tangu ilipoingia sokoni

Umakini wa kuifahamu sifa zake utakusaidia kujua kama simu inafaa kwa mwaka 2022

samsung note8 muonekano

Kwa sababu kuna simu za daraja la kati ambazo zinapatikana kwa bei nafuu zaidi

Kwani bei ya Samsung Galaxy note8 iliyotumika(used) inazidi laki nne na nusu

Hivyo ni vizuri ukafahamu sifa zake, washindani wake na bei yake kulingana na ukubwa wa memori kabla ya kutoa pesa

Bei ya Samsung Galaxy Note8 ya GB 64

Kwa maduka ya Dar Es Salaam simu inauzwa kwa shilingi 490,000/=

Ni Galaxy Note8 used ambayo RAM yake ni GB 6 na memori ni GB 64

Hivyo basi bei itakuwa kubwa kama utahitaji note8 yenye memori kubwa

Ukilinganisha sifa za samsung note8 na Redmi Note 10 utaona kuwa samsung ipo chini

samsung note8 summary

Zitazame hapa sifa za redmi note 10 halafu tazama sifa za galaxy note 8 kwenye jedwari kisha fananisha sifa na bei

Sifa za simu ya Samsung Galaxy Note8

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 835
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.35 GHz Kryo 280
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.9 GHz Kryo 280
  • GPU-Adreno 540
Display(Kioo) Super AMOLED,
Softawre
  • Android 7.1.1
Memori UFS 2.1, 256GB,128GB,64GB na RAM 6GB
Kamera Kamera mbili

  1. 12MP, dual pixel PDAF(wide)
  2. 12MP, AF(Telephoto)
Muundo Urefu-6.3inchi
Chaji na Betri
  • 3300mAh-Li-Po
  • Chaji-15W
Bei ya simu(TSH) 490,000/=

Ni upi ubora wa Samsung Galaxy Note8

Ubora mkubwa wa samsung hii ni kuwa na kioo cha amoled

Hivi vioo huwa vinauwezo wa kuonyesha rangi nyingi

Na uweoz kutopitisha maji ndani ya simu

Vitu vingine ni vya kawaida hasa kutokana na simu kali zilizotoka hivi karibuni ambazo bei zake ni chini ya laki tano

Uwezo wa Network

Note8 inatumia network ya 4G aina ya LTE Cat 16

Kasi ya juu kabisa ya kudownload ni 1000Mbps

Kama ilivyo kawaida mitandao ya simu Tanzania haitoi kasi hii

samsung note8 network

Simu nyingi mpya zinazouzwa laki nne kwenda juu huja na mtandao wa 5G

Lakini galaxy hii ni simu ya mwaka 2017 wakati ambao 4G ndio ilikuwa inatawala

Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy Note8

Samsung galaxy note8 inatumia kioo aina ya super amoled chenye resolution ya 1440 x 2960 pixels

Hii ni resolution inayoonyesha vitu kwa usahihi mkubwa

Uwepo wa amoled unaifanya simu kuonyesha rangi za vitu kwa uhalisia mkubwa kama vinavyoonekana na jicho la mwanadamu

Na huo usahihi wa rangi unachangiwa na kioo kuwa na HDR10

Pitia hapa kujua: maana ya HDR upande wa simu

Japokuwa android za sasa zinakuja na HDR10+ au Dolby vision ila HDR10 bado inaboresha pia uwezo wa screen kuonyesha vitu vizuri

Kiuhalisia simu chache zinazokuwa na HDR10

Hata infinix note 12 vip haina hiyo teknolojia

Nguvu ya processor Snapdragon 835

Simu ya Samsung Galaxy Note8 inatumia processor ya snapdragon 835 katika kufanya kazi zake

Hii ni processor yenye idadiĀ  ya core nane

Core zenye nguvu kubwa zipo nne zinazotumia muundo wa Kryo 280

Kryo 280 ni muundo wa Cortex A73 ulioboreshwa na kampuni ya Qualcomm

Utendaji wake ni wa wastani ambao unazidiwa na chip ya MediaTek Helio G95 ambayo hutumika na baadhi ya simu za infinix

Kwenye app ya geekbench snapdragon 835 ina alama 385 kwenye core moja

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya hii simu ni ndogo kitu kinachofanya simu kukaa na chaji masaa machache

Betri yake ya ukubwa wa 3300mAh inafanya simu kukaa na chaji masaa kumi ikiwa inaperuzi intaneti

Lakini muda unaweza kupungua zaidi kama mtu ataangalia video na intaneti kwa pamoja

Na chaji haipeleki umeme mwingi sana

Kwani kiasi chake ni wati 15 tu

Umeme huo unaweza kufanya simu kuchukua msaa zaidi ya mawili kujaa

Lakini betri ya simu ni dogo hivyo simu itawahi kujaa

Ukubwa na aina ya memori

Samsung note8 ina matoleo matatu upande wa memory

Kadri memori inavyokuwa kubwa na bei ndio inaongezeka

Uzuri ni kuwa simu inatumia memori za UFS 2.1

Ambzo husafirisha data kwa kasi kubwa

Uwezo wa memori kusafirisha data nyingi kunaongeza utendaji wa simu

Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy Note8

Bodi ya galaxy note8 ni ngumu kupasuka na kuchunika rangi kirahisi

Bodi ya simu inatumia kioo cha Gorilla 5

Majaribio mengi ya kuvunja simu zenye gorilla 5 yameonyesha simu kutokupasuka ikiangushwa kwa kimo cha mita moja kutoka juu

samsung note8 bodi

Huatopata wasi simu inapozama kwenye maji

Kwa sababu ina IP68

Hii huwa inaonyesha uwezo wa simu kuzuia maji na vumbi

Hivyo, maji hayatopenya ukiizamisha note8 kwenye kina cha maji ya kimo mita 1.5

Ubora wa kamera

Hii simu ina kamera mbili tu

Kamera hizo ni aina ya wide na ultrawide

Kamera zinatumia ulengaji aina ya dual pixel autofocus

samsung note8 kamera

Na zinaweza kurekodi video mpaka za 4K

Hata ukiwa unarekodi video huku ukiwa unatembea, video itatokea bila kutikisika

Kwa sababu kwenye kamera kuna EIS na OIS

Ubora wa Software

Ubora wa software haundani tena na nyakati za sasa

Kwa mara ya kwanza ukiinunua utakuta Android 7

Lakini unajua kuwa kuna Android 12 wakati huo Android 13 inagonga mlangoni?

galaxy note 8 software

Bahati mbaya simu za “premium” za samsung za zamani zilikuwa zinapokea maboresho miaka miwili tu

Tofauti na simu za iphone ambazo mara nyingi hupokea maboresho miaka karibu mitano

Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy Note8

Simu haitumii network ya 5G

5G ni muhimu kwa sababu hata Tanzania inaweza ikaja siku za mbeleni

Haiwezi kupokea toleo jipya la Android 12

Inapokea toleo la android 9 pekee

Hakuna kamera aina ya ultrawide

Kama utalenga kupiga eneo pana la nyuzi 120 basi galax note8 haitoweza

Kwa mwaka 2022, utendaji wake ni mdogo

Ukicheza gemu zinazotumia nguvu nyingi simu inawea ikawa inachemka

Neno la Mwisho

Ni bora kununua matoleo mapya ya android yaliyopo kwenye kundi la kati

Kwa maana bei ya Samsung Galaxy Note8 inakupa simu ya 5G ya Redmi Note 10 5G na chenji inabaki

Ila kama wewe ni mpenzi wa samsung basi hii ni smartphone nzuri ya kuwa nayo ya bei ndogo

Maoni 12 kuhusu “Bei ya Simu ya Samsung Galaxy Note8 na Sifa Zake (2022)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

samsung galaxy a15 thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A15 na Sifa Muhimu

Mwezi wa desemba 2023 ni mwezi ambao Simu ya Samsung Galaxy A15 ilizinduliwa Ni simu ya daraja la kati ambayo ina vitu vichache vinavyopatikana kwenye samsung za bei kubwa Ndio […]

samsung a55 showcase

Bei ya Samsung Galaxy A55 na Ubora wake

Samsung Galaxy A55 imetoka mwezi machi mwaka 2024 na ni simu ya daraja la kati Bei ya Samsung Galaxy A55 kwa Tanzania ni shilingi milioni moja na laki moja na […]

thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A35 na Sifa zake

Samsung Galaxy A35 ni toleo jipya la samsung lilotoka mwezi machi 2024 Ni simu ya daraja la kati iliyochota baadhi ya sifa muhimu kutoka kwenye galaxy yenye bei kubwa Ndio […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram