SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ubora na Bei ya Simu ya Redmi Note 10 (2022)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

April 18, 2022

Mwaka 2021 simu ya redmi note 10 iliingia katika kundi la simu bora za android za uwezo wa kati

Ubora wake unachangiwa na chpset, kioo, kamera na ukaaji wa chaji wa kuridhisha.

muonekano wa simu ya redmi note 10

Na bei ya redmi note 10 ilikuwa ni chini ya laki tano kwa zenye memori chini ya 128GB

Ila bei yake imekuwa ikibadilika badilika kulingana na wapi inapopatikana

Bei ya Redmi Note 10 Tanzania

Redmi yenye ukubwa wa 128GB na 6GB inafika 590,000/= kwa baadhi ya maduka karikaoo

Wakati simu inatoka bei ya simu ya 128GB ilikuwa haizidi 500,000/= aliexpress

Lakini kwa nyakati za leo bei ni kubwa.

Zitazame sifa za redmi note 10 ujue kwa nini simu haistahili kuuza bei hii

Sifa za Redmi Note 10

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
 • CPU – Snapdragon 678
 • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.2GHz kryo 460 Gold
 • Core Za kawaida(6) – 6×1.7GHz kryo 460 Silva
 • GPU-Adreno 612
Display(Kioo) Super Amoled,
Softawre
 • Android 11
 • MIUI 12.5
Memori UFS 2.1, 128GB, 64GB na RAM 6GB, 4GB
Kamera Kamera nne

 1. 48MP,PDAF(wide)
 2. 8MP(ultrawide)
 3. 2MP(macro)
 4. 2MP(depth)
Muundo Urefu-6.43inchi
Chaji na Betri
 • 5000mAh-Li-Po
 • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) 590,000/=

Upi ubora wa Simu ya Redmi Note 10?

Ubora wa simu aina ya redmi note 10 ni kuwa na chaji inayojaza betri kwa dakaka chache

Kioo chake kinaonyesha vitu kwa ustadi mkubwa

sifa za redmi note 10

Simu ina betri kubwa inayokaa na chaji masaa mengi

Ni simu inayoweza kupokea toleo jipya la android 12

Uwezo wa Network

Redmi note 10 inasapoti mitandao ya aina yote isipokuwa 5G

4G yake ni aina ya LTE Cat 12.

network ya redmi note 10

Kama kuna mtandao wenye kasi ya LTE Cat 12, simu itaweza kudownload faili kwa kasi kubwa ya 600Mbps

LTE za mitandao yote inashika vizuri hapa Tanzania.

Kwani katika network bands 12 za 4G zipo ambazo zinatumiwa na makampuni ya simu nchini

Ubora wa kioo cha Redmi Note 10

Linapokuja kwenye swala uoneshaji picha, basi simu ina kioo kinachoonyesha vitu kwa uhalisia sana.

Kwa sababu kioo cha redmi note 10 ni aina ya Super Amoled.

Super amoled vinatengeneza rangi nyingi kutokana na kuwa na contrast kubwa

Wingi wa rangi wa hii simu unachangiwa na resolution kubwa ya pixels 1080 x 2400

Kwa bahati mbaya redmi hii ina refresh rate ndogo

Nguvu ya processor Snapdragon 678

Ubongo wa simu ya redmi note 10 ni snapdragon 678

Processor ya snapdragon 678 ina uwezo wa wastani sana.

Kwani gemu zenye graphic kubwa kama Fortnite inacheza kwa resolution ya chini na kwa spidi ndogo.

Hii inasababishwa na aina ya core kubwa mbili na uwezo wake.

Kitu kinachopelekea chip kupata alama za wastani kwenye geekbench zinazofikia 528 kwenye core moja

Uwezo wa core kubwa.

Processor ya simu hii ina core kubwa mbili zenye spidi inayofika 2.2GHz kwa core moja

Core zake zimeundwa kwa muundo wa Kryo 460 Gold

Muundo wa Kryo 460 Gold ni muundo wa Cortex A76 ulioboreshwa

Kiuhalisia uwezo wa uchakataji wa data ni wa kiwango cha kati unaofanyika katika njia nne

Pamoja na uwezo wastani wa chip ila matumizi yake ya chaji ni makubwa kidogo ukilinganisha muundo wa Cortex A78

Uwezo wa core ndogo

Processor ina core ndogo zipatazo sita.

Hizi zina spidi ndogo isiyovuka 1.7GHz

Muundo ambao umetumika ni Kryo 460 Silva ambao ni Cortex A55.

Kryo 460 Silva ni core zinazotumika wakati simu ikiwa inafanya kazi ndogo.

Na ina matumizi madogo ya umeme kutokana na kuwa na spidi ngogo isiyofika 1.8GHz

Uwezo wa betri na chaji

Redmi note 10 inaweza kukaa na chaji masaa 110 simu ikiwa inatumika mara chache

Na masaa takribani 14 simu ikiwa kwenye intaneti masaa mengi mfululizo

Uwezo mkubwa wa kukaa na chaji unachangiwa na betri kubwa ya simu.

Kwani betri yake ina 5000mAh.

Chaji yake ina wati 33

Umeme unaojaza betri chini ya dakika 80 kwa 100%

Ukubwa na aina ya memori

Aina ya memori iliyotumika ni UFS 2.1

Hii ni memori inayofungua applikesheni nyingi kwa haraka

Kwani kasi ya kusfirisha data ya UFS 2.1 inafika 1200MBps

Kuna matoleo matatu ya redmi note 10 upande wa memori.

Na ukubwa wake unaanzia 64GB mpaka 128GB.

Na RAM inaanzia 4GB na nyingine 6GB

Memori inaweza kuweka apps, video, audio na picha nyingi

Uimara wa bodi ya Redmi Note 10

Bodi ya redmi note 10 haina bodi imara japo inaweza kuzuia maji tiririka.

Uimara mdogo unasababishwa na simu kuwa na plastiki upande wa nyuma.

Japokuwa upande wa mbele una kioo cha Gorilla Glass 3

Gorilla Glass 3 vina uwezo wa kuzuia mikwaruzo ya kioo na sio kupasuka

Simu ina IP53, inayoonyesha uwezo wa simu kuzuia vumbi na maji yanayotiririka

Ubora wa kamera

Simu ina kamera nne ambapo kamera kubwa ina 48MP

Kamera zake zinaweza piga eneo pana kwa nyuzi  118

macho manne ya redmi note 10

Na pia ina kamera maalumu kwa kupiga vitu kwa ukaribu sana

Upande wa ulengaji inatumia PDAF

PDAF ina spidi ndogo kutambua kitu kinachpigwa picha ukilinganisha dual pixel pdaf

Kamera zake pia zinaweza kurekodi video za 4k na full hd kwa spidi inayofika 60fps

Hii ni simu ninayoitumia, inapiga picha nzuri nyakati za mchana, ila kwenye mwanga mdogo sana ubora wa picha si mkubwa sana

Ubora wa Software

Simu inakuja na android 11 na mfumo wa MIUI 12.5

MIUI 12.5 ina app inayoweza kuscreenshot kitu kwa urefu unaotaka

Kama unataka kuscreen shot ukurasa mzima kwa pamoja simu inaweza kufanya hivyo

Kitu kizuri, ni kuwa redmi note 10 inakubali toleo jipya la android 12

Kama utakuwa na data za GB 3 utapata android 12

Yapi Madhaifu ya Redmi Note 10

Uwezo wa simu kiutendaji ni mdogo usioendana na bei yake.

Kioo chake hakina refresh rate kubwa.

4G yake ina network bands chache

Kamera hazijawekewa OIS wala gyro-EIS kwa ajili ya kutuliza video wakati wa kurekodi

Simu haina bodi imara kutokana na kuwa na plastiki

Simu haina kamera ya telephoto hivyo inategemea digital zoom inayopunguza ubora wa picha

Neno la Mwisho

Redmi note 10 ni simu sahihi kama utaipata kwa bei ya chini ya laki tano

Kama utaipata kwa bei ya mwaka 2022 hapa tanzania ni vizuri ukaangalia machaguo mbadala

Na washindani wazuri ni simu za iphone za bei rahisi zilizotumika

Maoni 3 kuhusu “Ubora na Bei ya Simu ya Redmi Note 10 (2022)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

xiaomi 14 ultra

Simu 13 mpya na kali za Redmi na Xiaomi 2024

Kampuni ya Xiaomi sio ngeni kwa wengi Ni kampuni ya china inayotengeneza simu za madaraja yote kwa brandi za Xiaomi, Redmi na Poco Hapa kuna orodha ya simu mpya za […]

No Featured Image

Bei ya Redmi Note 13 na Sifa Zake Muhimu

Redmi Note 13 5G ni simu kutoka Xiaomi ya China ambayo bei yake kwa sasa ni shilingi laki nane Hii ni bei ya toleo lenye ukubwa wa GB 256 na […]

redmi 10a thumbnail

Bei ya Sasa ya Redmi 10A na Sifa Muhimu

Simu ya Redmi 10A iliiingia sokoni mwaka 2022 Ni aina ya simu inayolenga watu wenye matumizi ya kawaida kama sio machache Hivyo bei ya Redmi 10A ni chini ya laki […]

Jinsi ya Kutumia GPS kwenye Simu (Hatua kwa Hatua)

GPS kirefu chake ni Global Positioning System, ni mfumo wa utambuzi wa maeneo ambao unasimamiwa na Marekani Simujanja karibu zote zina huu mfumo Una faida kubwa sana hasa kama unajua […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram