Kampuni ya Xiaomi sio ngeni kwa wengi
Ni kampuni ya china inayotengeneza simu za madaraja yote kwa brandi za Xiaomi, Redmi na Poco
Hapa kuna orodha ya simu mpya za xiaomi na redmi kwa mwaka 2024 na bei zake
Listi imekusanya xiaomi za bei ndogo, ya kati na bei kubwa
Hivyo kuna uwanda mpana wa kuchagua simu kulingana na kiasi cha pesa ulicho nacho
Xiaomi Pad 6S Pro 12.4
Bei ya Xiaomi Pad 6S Pro: 2,000,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Xiaomi Pad PS Pro 12,4 ni kishikwambi kilichotoka mwaka 2024 mwezi februari
Ina mfumo wa chaji unaopekea umeme wa wati 120
Hivyo betri yake yake kubwa ya 10000mAh inajaa ndani ya lisaa moja
Utendaji wak ni kutokana na kutumia chip ya Snapdragon 8 Gen 2
Xiaomi Redmi A3
Bei ya Xiaomi Redmi A3: 250,000/= ,Ukubwa wa Memori: 64GB, RAM: 3GB
Redmi A3 ni xioami ya bei nafuu iliyotoka mwezi februari 2024
Haina kamera nzuri ila ina kioo kikubwa chenye refresh rate ya 90Hz
Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh ila kasi ya chaji yake sio kubwa
Inafaa kwa mtumiaji mwenye matumizi ya kawaida kwani inakaa na chaji muda mrefu
Redmi Note 13 Pro 4G
Bei ya Redmi Note 13 Pro 4G: 600,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 8GB
Simu ya Redmi Note 13 Pro 4G inatumia kioo chenye uonteshaji mzuri wa vitu
Kioo hicho kinatumia teknolojia ya AMOLED
Chaji yake ina uwezo wa kupeleka chaji kwa kiwango cha wati 67
Kwa maana hiyo betri yake ya mAh 5000 haiwezi chukua muda mrefu kujaa
Ila hili ni toleo ambalo halina 5G ni kwamba ina 4G kama mtandao wenye kasi zaidi
Redmi Note 13 4G
Bei ya Redmi Note 13 4G: 500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Hii ni simu nyingine ya daraja la kati yenye sifa nzuri upande wa kioo, kamera, na utendaji wa wastani
Processor yake ina nguvu ya wastani, chip hiyo ni Snapdragon 685
Ina betri yenye ukubwa wa 5000mAh kama ilivyo kwa simu nyingi
Kamera yake kubwa ina megapixel 108 na inaweza kurekodi mpaka video za FULL HD
Hii sio kama Redmi Note 10 ambayo kamera yake inarekodi mpaka video za 4K
Redmi Note 13
Bei ya Redmi Note 13: 700,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Hii ni Redmi Note 13 yenye 5G na inatumia processor tofauti na ile yenye utendaji
Redmi Note 13 inatumia chip ya Mediatek Dimensity 6050
Ukiondoa uwepo wa 5G sifa zingine zote zinaendana na redmi note 4G
Hakuna tofauti kwenye vipengere vingine
Xiaomi Poco X6 Pro
Bei ya Poco X6 Pro: 890,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Kioo cha Poco X6 Pro kina HDR10+ kitu kinachosaidia kuwa na utajiri wa rangi na kuonyesha vitu vingi kwa rangi zake halisi
Hii simu inatumia mfumo mpya wa Xiaomi unaitwa HyperOS badala MIUI
Ina kamera tatu huku kamera kubwa ikiwa na megapixel 64
Chaji yake inapeleka umeme kwa kiwango cha wati 67
Ina betri kubwa pia na ukaaji wa chaji ni wa kuridhisha
Xiaomi Poco X6
Bei ya Poco X6: 750,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Hii simu ina kamera zipatazo tatu ambapo kamera kubwa inaweza kurekodi video za 4K kwa kiwango cha 30fps
Ina processor ya Snapdragon 7s Gen 2 ambayo nguvu yake kiutendaji ni kubwa pia
Betri ina ukubwa wa 5100mAh, ongezeko la 100mAh ukilinganisha na simu nyingi za siku hizi
Chaji yake ya wati 67 inaweza kujaza betri hili kwa dakika 44
Xiaomi Poco M6 Pro
Bei ya Poco M6 Pro: 610,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Simu ya Poco M6 Pro iliingia sokoni mnamo mwezi januari 2024
Hii ni poco yenye 4G kwani kuna Poco M6 Pro 5G ya mwaka 2023 mwezi august
Hii ina kioo kizuri cha AMOLED chenye uangavu unaofika nits 1000
Inatumia chip ya daraja la kati Mediatek Helio G99
Na yenyewe chaji yake ina wati 67 hivyo betri itajaa kwa haraka
Xiaomi Poco M6
Bei ya Poco M6: 300,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Xiaomi Poco M6 ni simu ya bei nafuu ambayo ina vitu vilivyopunguzwa ukilinganisha na Poco M6 Pro
Kwa mfano, skrini ya POCO M6 sio ya amoled bali ni IPS LCD japo refresh rate yake ni kubwa
Siku hizi app nyingi zinachukua nafasi kubwa ya simu kitu kinachochangia RAM kujaa
Hivyo kuwa na simu yenye RAM ya GB 4 inaweza kuwa changamoto
Hata hivyo, utendaji wa Poco M6 ni wa wastani unaoweza fanya vitu bila tatizo
Ila itafaa zaidi kwa matumizi ya wastani pia
Redmi 13R
Bei ya Redmi 13R: 370,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Hii ni simu yenye utendaji wa wastani na simu ya daraja la kati
Inatumia processor yenye nguvu ya wasatani ambayo ni Dimensity 6100+
Kioo chake ni vile vyenye resolution 720 na ni cha aina ya IPS LCD
Kasi ya chaji yake ni 18W, hii inachukua muda kidogo kujaza simu
Ina kamera moja yenye megawati 50 na ulengaji wa PDAF
Redmi 13C 5G
Bei ya Redmi 13C 5G: 370,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Simu ya Redmi 13C 5G ni toleo lingine la simu ya 5G ya bei nafuu
Sifa zote za Redmi 13C 5G zinalingana na Redmi 13R
Kinachotofautisha ni hiyo teknolojia ya mtandao wenye kasi zaidi kwa sasa
Kwa hiyo mnunuaji ana uwanda wa kuchagua simu aitakayo kati ya hizi mbili
Redmi K70
Bei ya Redmi K70: 970,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 12GB
Simu ya redmi k70 ni moja ya simu kali amabayo imetoka novemba 2023
Ila inatazimiwa kuwa ni toleo litakaloendana kiushandani na matoleo mapya ya 2024 yanayotarajiwa kutoka mbeleni
Redmi K70 inapewa nguvu na chip kutoka kwa kampuni Qualcomm ambayo ni Snapdragon 8 Gen 2
Ina kamera tatu na kamera moja inapiga picha hadi za 8K
Kitu kingine kitakachokufurahisha ni aina ya chaji iliyo nayo
Chaji yake inaweza kupeleka umeme kwa spidi mpaka ya 120w
Hii inajaza simu kwa muda wa dakika 28
Xiaomi 14 Ultra
Bei ya Xiaomi 14 Ultra: 4,200,000/= ,Ukubwa wa Memori: 512GB, RAM: 16GB
Xiaomi 14 Ultra ni simu mpya kabisa na imeingia rasmi sokoni mwezi februari 2024
Katika hii orodha, hii ndio simu mbayo imekamilika kila idara na ubora mwingi
Kamera zake tatu za wide, ultrawide na telephoto zote zina mfumo mzuri wa upigaji picha
Simu inatumia processor yenye nguvu kubwa kiutendaji aina ya Snapdragon 8 Gen 3
Hii ina maanisha Xiaomi 14 Ultra ipo kundi moja na Samsung Galaxy S24 Ultra na iPhone 15 Pro Max
Kwa bahati mbaya bei yake ni kubwa na ni maalumu kwa wenye uwezo wa kununua simu kwa bei ya milioni nne
Maoni 6 kuhusu “Simu 13 mpya na kali za Redmi na Xiaomi 2024”
Nahitaji Simu Redmi pro+ yenye GB 512 Ram 12 bei gani
Milioni moja na laki moja
Nahitaji simu ya redmi pro+ GB128 bei gani?
simu ya redmi note 13 bei kama ukinunua china ni bei gani
simu ya redmi note 13 plain bei gani kama ukinunua china
Bei gali