SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu bora duniani na bei zake 2024

Miongozo

Sihaba Mikole

June 11, 2024

Leo tuzungumzie kuhusu simu bora duniani na bei zake kwa mwaka 2024

Kuna matoleo mapya ya simu kali yenye ubora wa kiutendaji na wenye nguvu madhubuti katika maeneo mengi

Ubora mkubwa ambao tumeutazama upo katika maeneo matano,

Simu bora duniani kila mwaka huwa na sifa kubwa na maboresho imara katika vipengele hivyo vitano

Na napendekeza unaponunua simu ni vizuri ukawa unaulizia uimara wa hiyo simu katika hayo maeneo, ambayo nitayafafanua.

Vigezo ambavyo nimevitazama sana kwenye simu bora duniani 2024 ni

  • Software
  • Utendaji na ukaaji chaji
  • Aina ya kioo
  • Uimara wa bodi
  • Ubora wa Kamera

Hivi sio vigezo pekee vya simu bora, vipo vingi kama ni mtembeleaji wa SimuNzuri.com utakuwa unaelewa nini hasa nazungumzia, nakushauri tembelea

Hizi ndio simu zenyewe.

Samsung Galaxy S24 Ultra

Samsung Galaxy S24 Ultra ni simu ya kamera nne na kamera zote zinapiga picha zenye muonekano mzuri kwenye nyakati zote.

Yaani kwenye mwanga mdogo na kwenye mwanga mwingi

Ubora wa kamera unachagizwa na aina ya chip na sensa(lenzi) simu inayotumia na uwepo teknolojia za ulengaji za dual pixel pdaf, laser af, na multi-directional pdaf zinazosaidia simu kukitambua kinachopigwa picha kwa haraka

Inatumia processor yenye nguvu ya Snapdragon 8 Gen 3 yenye muundo wa Cortex X4 kwenye core yenye nguvu zaidi

Hii inafanya simu kuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja bila kukwama ndio maana app geekbench inayopima nguvu za processor za simu, Snapdragon 8 Gen 3  ina alama 2100 na inaweza kufungua peji 198 kwa sekunde moja

samsung s24 ultra thumbnail

Ina waterproof ya kuzuia maji simu izamapo kwenye kina cha mita moja na nusu kwa muda wa nusu saa.

Kwa maana ina viwango IP68, bodi yake ni imara kwani upande wa kioo kunalindwa na vioo vigumu vya Corning Gorilla Armor

Inatumia kioo cha Dynamic LTPO Amoled 2X, faida ya amoled ni kuwa ina utajiri mkubwa wa utofautishaji rangi kwa sasa hivyo kioo kinakuwa na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi na zenye kukolea vizuri

Ubora wa kioo unaongezwa na uwepo HDR10+ na refresh rate ya 120Hz bila kusahau uangavu unafika nits 2600

Yaani hata ukiitumia juani utaweza kuona vitu vizuri kwenye jua, bei yake ni shilingi milioni tatu na nusu

iPhone 15 Pro Max

iPhone 15 Pro Max ni simu ya macho matatu.

Ilitoka mwaka 2023 ila bado ipo katika kundi la simu bora kwa kutazama vipengele vitano nilivyoeleza hapo nyuma

Processor yake ndio chip yenye nguvu mpaka sasa kwa mujibu wa geekbench japo kuna vipengele inaachwa kwa kiasi fulani na snapdragon 8 gen 3 na hata mediatek dimensity 9300

Kamera yake kubwa ina megapixel 48 na ikiwa inatumia ulengaji wa dual pixel pdaf kwenye kamera zote ikiwemo ya periscope telephoto

Periscope telephoto ni kamera kwa ajili ya kupiga picha vitu ambavyo vipo mbali na kamera, kamera yake inaweza kurekodi mpaka video za 4K tofauti na Samsung S24 inayorekodi hadi video za 8K

Simu inatumia mfumo endeshi wa iOS 17 na itakuwa inapokea matoleo mapya ya IOS kwa kipindi cha muda mrefu

Hii simu inakaa na chaji kwa karibu masaa 18 ukiwa kwenye intaneti muda wote kama ukiwa unaperuzi kutumia google chrome

iPhone ni ngumu kupasuka kwani na yenyewe ina vioo vya corninig glass na pia ina viwango vya IP68, vinavyoonyesha uwezo wa simu kuzuia maji kwa kina cha mita 6 ndani ya nusu saa

iPhone 15 Pro Max kioo chake ni cha LTPO Amoled

Oppo Find X7 Ultra

Oppo Find X7 Ultra ni simu ya oppo ya daraja la juu hivyo bei yake haitofautiani sana na matoleo ya samsung au iphone

Kwa sasa bei yake ni shilingi milioni mbii na laki tano

Simu inatumia processor yenye kwenye utendaji, chip inayotumia ni Snapdragon 8 Gen 3 kama ilivyo kwa samsung

Ina jumla ya kamera nne na kiujumla kamera zake zinatoa picha safi zisizo na noises(chengachenga) hata ukiikuza picha

Japo kwa nyakati za usiku chengachenga zinaonekana kwa mbali ukizoom picha ila vitu vinaonekana kwa ustadi na kwa utofoutishaji wa rangi sahihi

oppo find x7 ultra

Hii simu ina viwango vya IP68, ikimaanisha waterproof inaweza kuzuia maji ya kina cha mita moja na nusu kwa muda wa nusu saa

Chaji yake inajaza simu kwa 100% ndani ya dakika 15

Ina kioo cha LTPO Amoled chenye teknolojia mbili za uboreshaji muonekano wa vitu kwenye skrini.

Teknolojia hizo ni HDR10+ na Doldy Vision, hizi zinasaidia kukoreza rangi picha vizuri

Inatumia mfumo endeshi wa Android 14

Pia inakuja na mifumo ya akili bandia breeno smart assistant, breeno inaweza kufungua app kwa kuimbia kwa maneno, huu mfumo unapatikana kwa matoleo a China

Xiaomi 14 Ultra

Bei ya Xiaomi 14 Ultra ni shilingi milioni tatu na laki saba kwa maeneo meneo mengi duniani

Haina tofauti katika maeneo mengi kama simu zilizotangulia

Na yenyewe inakuja na mfumo wa Android 14 ikiambatana na mfumo mpya kutoka xiaomi wa HyperOs

Inakuja na kioo cha LTPO Amoled ikiwa na teknolojia za hdr10+ na dolby vision bila kusahau kiwango cha refresh rate kinachofika 120hz na uangavu unaofika nits 3000(nyingi sana)

xiaomi 14 ultra

Idara ya kamera ina vitu vyote muhimu vya kutoa picha nzuri na video safi, kwani kamera zake zina sensor kubwa ya inchi moja na ulengaji wa mult-directional pdaf, laser pdaf na dual pixel pdaf

Kamera yake zinarekodi mpaka video za 8K

Pia inatumia chip yenye nguvu ya Snapdragon 8 gen 3 hivyo utendaji wake ni wenye nguvu

Inasapoti chaji ya wati  90 kwa maana chaji inajaa ndani ya dakika chache

Ukiondoa hizo kampuni zinazofahamika sana kwa tanzania. Sasa tuangalie kampuni tano ambazo haziimbwi sana.

Google Pixel 8 Pro

Google Pixel 8 Pro huwa zina kamera zinazopiga picha ambazo zinakuwa zinaendana na muonekana halisi kwa kiwango kikubwa.

Simu za pixel kiujumla upande wa kamera huziacha simu nyingi sokoni

Pixel 8 Pro ina jumla ya kamera tatu na zote zinatumia teknolojia ya ulengaji ya dual pixel pdaf, na kamera kuba ina laser af kwa kutambua kitu katika mwanga hafifu

Inatumia kioo cha LTPO AMOLED kikiwa na refresh rate inayofika hatzi 120

Utendaji wake ni mkubwa japokuwa chip yake ya Tensor G3 haifanyi vizuri ukilinganisha na chip za snapdragon 8 gen 3, mediatek dimensity 9300 na apple a17 pro

Kioo chake ni cha LTPO OLED chenye HDR10+

Pia simu haipitishi maji kama ikizama mpaka kwenye kina cha mita moja na nusu, na inatumia vioo imara vya Gorilla glass victus 2 kama skrini protekta

Chaji yake inasapoti mpaka wati 30 na inakaa na chaji kwa takribani masaa nane

Simu inatumia mfumo endeshi wa Android 14 na itakuwa inapokea matoleo kwa miaka saba mfululizo

Bei yake ni shilingi milioni moja na laki nane ya GB 128

Vivo X100 Ultra

Vivo ni simu nyingine ya 5G yenye bodi imara ya kuzuia hata ya kina cha mita moja na nusu kwani ina viwango vya IP68

Na yenyewe inatumia kioo kizuri cha LTPO AMOLED chenye dolby vision pamoja na refresh rate inayoenda hadi 120Hz

Utendaji wake una nguvu kwani na yenyewe inatumia processor ya snapdragon 8 gen 3 kama zilivyo simu zingine za daraja la juu.

vivo x100 ultra

Inakuja na toleo la Android 14 ikiambatana na mfumo wa OriginOs 4, hii itakuwa inapokea matoleo mapya ya android

Kamera yake ya lenzi ya telescope ina megapixel 200 na ulengaji wa pdaf na laser af kwa ajili ya kutambua vitu kwenye mwanga mdogo

Bei yake ni shilingi milioni mbili na laki tano

Huawei Pura 70 Ultra

Katika simu zilizoorodheshwa, Huawei Pura 70 Ultra inauzwa kwa bei kubwa sana kuliko zingine

Bei yake kwa sasa ni shilingi milioni 4 na laki tano

Pamoja na bei kubwa iliyonayo ila kiuhalisia Pura 70 Ultra inaachwa kwa kiwango kikubwa na matoleo mengine yote yaliyopo

Nimeiweka kama kuheshimu juhudi za huawei katika kukabiliana na vikwazo vya marekani dhidi yao

Kwani haikutarajiwa kuwa huawei pura 70 ultra itaweza kuwa na processor yenye nguvu na 5G ambayo ni Kirini 9010

huawei pula

Kamera zake pia zina mfumo mzuri unaosaidia simu kupiga picha vizuri

Ina kioo cha LTPO OLED chenye refresh rate inayofika 120Hz

Hii simu ina viwango vya IP68, ikimaanisha maji hayangii simu ikiwa imezama kwenye kina cha mita 2 kwa muda wa dakika thelathini

Simu za huawei kwa sasa hazitumiii mfumo wa Android bali zinatumia waliotengeneza wao wenyewe harmonyos 4.2 kwa smu za china

Ila kwa masoko ya duniani nje ya china simu inakuja na android 12 core ikiambatana na mfumo wa emui 14.2

OnePlus 12

Japo imetoka desemba 2023 oneplus 12 bado ipo kwenye kundi zenye utendaji wenye nguvu kwa mwaka 2024

Kwani inatumia chip ya Snapdragon 8 Gen 3 ambayo kiutendaji inazidiwa na processor mbili tu.

Ina kioo cha LTPO Amoled na kina teknolojia za hdr10+ na dolby vision bila kusahau refresh rate 120Hz

Ina kamera tatu

Kamera kubwa ni ya lenzi ya telescope ina megapixel 64 na inaweza kuzoom mara 3 kwa kutumia optical lenzi(kuzoom bila kutumia app ya kamera)

Optical lenzi haipotezi ubora wa pixel

Hii simu itakuwa inapokea matoleo mapya android na kwa sasa inatumia android 14

Simu ni imara kwani ina viwango vya IP68, yaani ina waterproof ya kuzuia maji hata kwenye kina cha mita moja na nusu.

Bai ya OnePlus 12 ni shilingi milioni mbii ya GB 256

Sony Xperia 1 VI

Sony Xperia 1 VI ni moja ya simu yenye kamera nzuri ukizingatia Sony ni moja ya kampuni kubwa za uundaji sensa za kamera

Ina kamera za aina tatu na kamera megapixel 48 na ikiwa na ulengaji wa dual pixel pdaf

Kamera zake zinaweza kurekodi video za 4K kwa kiwango cha 120fps(fps inamaanisha idadi ya picha kwa sekunde)

Inatumia processor yenye nguvu ya Snapdraon 8 Gen 3

Kioo chake ni cha aina ya LTPO OLED chenye teknolojia ya uboreshaji wa muonekano wa vitu ya HDR.BT 2020

Inakuja na Android 14 na bila shaka itapokea toleo android 15 linalotarajiwa kutoka mwaka huu

Bei ya Sony Xperia 1 VI ni shilingi milioni tatu na laki tano

Samsung galaxy s24+

Simu ya mwisho ni galaxy 24+, sitoizungumzia kwa sababu ina vitu vingi vinafanana galaxy s24 Ultra

Ila S24 PLUS bei yake ni ndogo kiasi ambayo ni shilingi milioni mbili na laki nane

Kiujumla ukitaka kuchukua simu kali, cha kwanza kabisa angalia aina ya processor inayoambatana nayo.

Processor ndio ubongo wa kompyuta(ikiwemo simu), chip ikiwa nzuri basi uwezekano vitu vingine vitafanya kazi kwa ufanisi

Kama una bajeti ya kutosha kwa sasa hakikisha processor ya simu iwe ni Snapdragon 8 Gen 3, au Apple A17 Pro, au Mediatek Dimensity 9300 au Tensor G3 au Exynos 2400

Pia hakikisha kamera ina ulengaji wa angalau dual pixel pdaf, ama multi-directional pdaf na laser pdaf

Na pia kamera iwe na kamera za aina tatu ama zaidi za lenzi ambazo ni wide, ultrawide na periscope pia

Hakikisha kioo ni LTPO OLED au AMOLED kikiwa na HDR10+ AU dolby vision

Na pia simu iwe na waterproof ya IP68

Note: Listi itakuwa inabadilika badilika kadri simu bora zitakavyokuwa zinatoka

Maoni 8 kuhusu “Simu bora duniani na bei zake 2024

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

No Featured Image

Bei ya Samsung Galaxy A06 na Ubora wake

Samsung Galaxy A06 ina betri inayokaa na chaji muda mrefu na ni simu ya daraja la chini Hii inamaanisha watu wengi kwa hapa Tanzania wanaweza inunua Kwa sababu bei ya […]

No Featured Image

Bei ya iPhone 16 Pro na Sifa zake Muhimu

Kampuni ya Apple imeingiza matoleo mapya ya iphone Moja ya iPhone hiyo ni iPhone 16 Pro, ina ufafanano kwa sehemu ya kimuundo na iPhone 15 Pro Yapo mazuri lakini yapo […]

iphone 16 pro

Simu mpya za iPhone na Bei zake 2024 (matoleo ya iphone 16)

Kila mwezi wa tisa kampuni ya Apple ya Marekani hutangaza simu mpya za iphone Katika uzinduzi apple huanisha vitu vipya simu zinazokuja nazo na bei zake kwa kila toleo Kwa […]

iphone thumbnail

iPhone za bei rahisi za kumiliki kwa sasa(2024-2027)

Katika pitapita zangu na kuchunguza simu bora za bei ndogo na ya chini nimekuja kugundua kitu cha kustahajabisha kidogo Wapenzi wa iPhone wenye bajeti ndogo wananunua iphone used hazipokei maboresho […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company