SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ujio wa Simu mpya za Tecno Camon 40

Simu Mpya

Sihaba Mikole

March 15, 2025

Huu mwezi wa tatu 2025 tecno imetangaza ujio wa matoleo mapya ya Tecno Camon 40

Simu hizo ni

  1. Tecno Camon 40
  2. Tecno Camon 40 Pro 5G
  3. Tecno Camon Pro
  4. Tecno Camon 40 Premier

Kwenye hii post utafahamu baadhi ya sifa za muhimu za kila tecno

Na tecno kali zaidi kati ya zilizotangazwa

Tuzame kiundani na kwa kifupi sana.

Tecno Camon 40

Tecno Camon 40 inakuja na mfumo endeshi wa Android 15

Utendaji wake ni wa wastani kwa sababu inatumia processor ya Mediatek Helio G100 Ultimate

camon 40

Inakuja na memori ya GB 128 na GB 256 na RAM ya GB 8 ama 12

Betri yake kubwa ina mAh 5200

Pia ina kamera mbili kubwa ikiwa na megapixel 50

Tecno Camon 40 Pro 5G

Kioo cha Tecno Camon 40 Pro 5G kina refresh rate ya 144hz ambazo huwa ni smooth

Hii ni tecno iliyowekwa waterproof aina ya IP68 ambayo inaashilia maji hayatoingia kwenye simu ikizama kwenye kina ch mita 2

camon 40 pro 5g

Upande wa kamera, zipo kamera mbili moja ya 8MP na nyingine ya 50MP

Ukubwa wa memori ni GB 256 ila RAM unaweza pata ya GB 8 na GB 12

Kasi yake ya kuchaji ni 45W na betri ukubwa wake ni 5200mAh

Utendaji wake ni wa wastani kwa sababu ya utumiaji wa chip ya Dimensity 7300

Tecno Camon 40 Pro

Tecno Camon 40 Pro ni simu ya daraja la kati

Utendaji wake ni wa wastani kwani processor yake ni Helio G100 Ultimate

Kioo chake ni cha amoled chenye refresh rate ya 120Hz

camon 40 pro

Kasi yake ya kuchaji ni 45W na betri yake ina 5200mAh

Ukubwa wa memori ni wa aina moja ambayo ni GB 256 NA RAM ya GB 8

Ina kamera mbili pekee ambapo kamera kubwa imewezeshwa OIS

OIS hufanya kamera kutulia wakati ukiwa unarekodi video huku unatembea

Tecno Camon 40 Premier

Tecno Camon 40 Premier ndio tecno bora zaidi kati ya zilizotangazwa

Ina kamera tatu na zote ukubwa wake ni 50MP

Kamera ya Periscope Telephoto inasapoti ya optical zoom inayoweza ku-zoom mara tatu

Chaji yake inapeleka umeme wa wati 70 na betri lake lina ukubwa wa 5100mAh

Kioo chake ni cha LTPO AMOLED chenye refresh rate ya 144Hz

Na yenyewe ina waterproof ya IP68

 

Maoni 4 kuhusu “Ujio wa Simu mpya za Tecno Camon 40

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

thumbnail

Bei ya Infinix Hot 70 na Sifa Zilizoboreshwa

Infinix Hot 70 imeundwa katika muktadha wa kuifanya iwe na bei ndogo Ni simu nzuri kutigemeana na aina ya matumizi Kwa sifa zake wapo watakaoona hii simu inawafaa Ila wanaotaka […]

infinix mpya 2026

Simu zote mpya za Infinix na bei za kustaajabisha (2026)

Kuna bei za infinix mpya zinafikirisha Maana zimekuja kitofauti sana kwa namna simu za Infinix zilivyozoeleka Maana kuna infinix inayoenda hadi milioni mbili na nusu kwa Tanzania Ila sifa za […]

Bei ya Tecno Spark 50 na Sifa Zake Mpya

Bei ya Tecno Spark 50 imeongozeka kuliko hata Spark 40 ilipotoka Kwa nini? Kuna sifa mpya mbili ambazo hazipo kwenye toleo lilopita Vitu vipya ni vichache ila vinatengeneza utofauti mkubwa […]

Infinix Hot 60 ni bora kuliko Hot 70?

Infinix Hot 70 ni simu mpya imeingia rasmi sokoni mwezi mei 2026 Kwa Tanzania inatarajiwa kuingia rasmi mwezi huu Juni Sifa zake zinashtua ukiilinganisha na Infinix Hot 60 Utendaji na […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company