Moja ya simu ambayo Xiaomi wameachia mwaka 2022 ni Redmi 10C
Ni simu inayoingia kwenye kundi la kati la chini kutokana na sifa zake
Bei ya Redmi 10C kwa maeneo mengi ya Tanzania inazidi laki tatu na nusu
Lakini ni simu ya bei ndogo inayoendana na ubora wa simu ila sio kama iPhone 11 Pro Max
Unaweza ukatembelea linki iliyopo inayoonyesha ubora na bei ya iPhone 11 Pro Max
Katika uchambuzi uliopo utafahamu bei halisi ya Xiaomi Redmi 10C katika masoko ya dunia na sifa zake kiundani
Bei ya Redmi 10C ya GB 64 na GB 128
Redmi 10C yenye ukubwa wa GB 64 bei yake ni shilingi 330,000/=
Na ile ambayo memori yake ni GB 128 inaenda mpaka shilingi 415,000/=
Hizi ni bei za aliexpress ya China, na inajumuisha gharama zote mpaka usafirishaji
Lakini gharama zinaweza kubadilika kutokana na mabadiliko ya shilingi ya Tanzania na dola
Hii simu haina sifa kubwa sana lakini inaizidi simu ya oppo a54 ambayo bei yake ni kubwa kiasi
Pitia hapa: Sifa muhimu na bei ya OPPO A54
Kisha linganisha kwa kutazama sifa za redmi kwenye jedwari
Sifa za Simu ya Redmi 10C
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2,128GB,64GB na RAM 3GB,4GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 330,000/= |
Ni upi ubora wa Redmi 10C?
Ubora mkubwa wa hii simu ni kutumia memori ambazo zinasafirisha data kwa kasi kubwa
Ni moja ya simu inayokaa na chaji muda mrefu
Pia kamera zake zinatoa picha za kuvutia
Inakuja na memori zinazoweza kuhifadhi appilkesheni nyingi
Ina bei inayovumilika
Ila simu za kundi la kati huwa zina mazuri mengi na mapungufu mengi pia
Fuatilia vitu vyote vya redmi iliyopo kuanzia network mpaka ubora wa software hapa
Uwezo wa Network
Redmi 10C ni simu ya 4G yenye masafa yapatayo 12
Hivyo kila laini ya simu inayosapoti 4G itakubali Tanzania
Aina ya 4G inayotumia ni LTE Cat 13
Fahamu kiundani : maana ya 4G na aina zake
Smartphone yenye LTE Cat 13 inaweza kudownload kwa kasi inayofikia 300Mbps
Ukiwa nchini marekani na ukawa unatumia mtandao wa AT&T utaweza kuifikia hii spidi lakini sio Tanzania
Kasi 300Mbps inaweza kupakua faili la 1500MB kwa sekunde 40
Ubora wa kioo cha Redmi 10C
Simu haina kioo kizuri kutokana na kuwa na resolution ndogo ya 720 x 1650 pixels
Japokuwa vitu vitaonekana vizuri lakini si kwa ubora wa kama vioo vya amoled
Kwa bahati mbaya kioo cha redmi 10c ni ips lcd
Kirefu cha ips lcd ni in-plane switching liquid crystal display
Hivi vioo huwa vina contrast ndogo
Kwa maana vina uwezo wa kuonyesha rangi chache
Na huwa vinapata shida kuonyesha rangi nyeusi sahihi
Gharama na bei ya kioo cha lcd huwa ni ndogo
Ndio maana na simu imekuwa na bei nafuu kiujumla
Nguvu ya processor Snapdragon 680 4G
Redmi 10C inatumia chip ya Snapdragon 680 4G katika kufanya kazi zake
Kila kitu unachokifanya kwenye simu kinachakatwa na processor
Chip ikiwa na nguvu kubwa itaweza kufanya kazi nyingi kwa haraka na kwa ufanisi
Snapdragon 680 ina core nane ila utendaji wake ni wastani kama sio wa chini
Hii inazidiwa na chip ya mwaka 2017 iliyopo kwenye Samsung Galaxy Note8
Katika applikesheni inayopima nguvu ya processor ya GeekBench Snapdragon 680 ina alama 376 kwenye core moja
Kiasi cha magemu mengi kucheza kwa resolution ndogo
Hii inatokana na core nne zenye nguvu kutumia muundo wa Kryo 265 Gold
Kryo 265 Gold huwa una mizunguko michache na kufanya kazi chache kwa sekunde
Kama utaitumia simu kucheza gemu sana basi tegemea simu kuwa inachemka mara kwa mara
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Redmi 10c ni kubwa
Hivyo simu inaweza kukaa na chaji kwa masaa yanayozidi 14 ukiwa unatumia intaneti muda wote
Hii inatokana na ujazo wa betri kuwa 5000mAh
Chaji yake inapeleka umeme wa wati 18
Hivyo simu inaweza ikachukua masaa takribani matatu kujaa
Inatokana na betri kuwa kubwa sana kitu kinachosababisha betri kujaa taratibu
Ukubwa na aina ya memori
Hii simu ina matoleo ya aina tatu
Bei ya redmi 10c zinaoongezeka kadri ukubwa wa RAM na ROM unayoongezeka
Simu ipo ya GB 64 inayotumia RAM ya GB 3 au GB 4
Pia ipo ya GB 128 na RAM ya GB 6
Cha kuvutia ni kuwa aina memori simu iliyonayo ni UFS 2.2
Kasi ya kusafirisha data ni 1200MBps
Hii huwa inafanya simu kufungua applikesheni kwa sekunde chache ukilinganisha simu zenye memori za eMMC 5.1
Uimara wa bodi ya Redmi 10C
Mara nyingi simu za bei nafuu huwa inaundwa kwa bodi za plastiki upande wa nyuma
Hii simu haina kioo cha Gorilla kwenye screen
Na pia haina uwezo wa kuzuia maji kupenya
Hivyo ni muhimu kuweka kava ya simu na screen protector
Bila hivyo rangi ya simu upande wa nyuma inaweza ikawa inachunika mara kwa mara
Ama simu kupasuka kirahisi
Ubora wa kamera
Ubowa wa kamera ya Redmi 10C sio mkubwa sana
Kwani aina ya ulengaji inayotumia ni PDAF
PDAF inaweza kukitambua kitu kinachopigwa picha kama haraka ila sio kama dual pixel pdaf
Simu janja hii ina kamera mbili ambazo ni wide(kamera kuu) yenye 50MP na depth yenye 2MP
Hii kamera ya depth huwa haina maana kwa sababu haipigi picha na simu yenye camera PDAF
Kazi kubwa ni kupima kiasi cha eneo kinachostahili kuonekana kwenye picha
Na pia kutengeneza ukungu ukungu(brul) nyuma ya kitu kinachopigwa picha
Kamera zake zinaweza kurekodi video za full hd pekee
Ubora wa Software
Mfumo endeshi ambao simu inatumia ni Android 11
Xiaomi bado hawajaainisha kama redmi 10c inaweza kupokea android 12
Xiaomi ni tofauti kidogo na simu za google pixel upande wa kupokea matoleo mapya ya android mara kwa mara
Mbali na hilo redmi inakuja na mfumo wa MIUI 13
MIUI 13 ina mfumo mzuri wa ku-screenshot
Kwani inakupa chaguo la ku-screenshot kitu kwa urefu unaotaka
Na pia kamera yake ina scanner inayoweza kuscani dokumenti mbalimbali
Yapi Madhaifu ya Redmi 10C
Simu hii ni nzuri kiasi chake ila ukilinganisha na simu za huawei utagundua simu ina madhaifu mengi
Kioo chake cha IPS LCD kina resolution ndogo na uangavu mdogo
Utendaji wake ni wa kiwango cha chini hasa kwenye uchezaji gemu
Chaji inapeleka umeme kidogo unaojaza betri masaa mengi
Redmi 10c haina kamera ya ultrawide wala telephoto
Simu haiji na toleo jipya la android 12 ambalo limeboreshwa kiusalama
Neno la Mwisho
Madhaifu unayoyaona yanafanya bei ya simu ya Redmi 10C kuwa ndogo
Simu za daraja la juu huwa zina kasoro chache sana
Na aina ya simu hizo bei yake huwa ni kubwa
Yote ya yote Redmi 10C ni simu nzuri ya daraja la kati yenye bei inayovumilika na inayoendana na ubora wake
Maoni 4 kuhusu “Bei ya Simu ya Redmi 10C na Sifa Muhimu (2022)”
Nzuri
Simu nime ipenda kweli hiyi
Simu zangu pendwa daima ni Redmi
Simu zangu pendwa daima