SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Tecno Spark 10 na Sifa Zake

Sifa za simu

Sihaba Mikole

April 7, 2023

Tecno Spark 10 ni toleo lingine jipya inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi april ya mwaka 2023

Ni toleo linalotoka pamoja na toleo zuri kiasi la Tecno Spark 10 Pro

tecno spark 10 showcase

Bei ya Tecno Spark 10 inazidi laki nne kwa Tanzania

Ni simu ya kawaida yenye vipengele vichache vya kuvutia

Vipengele ambavyo vinaweza kukuvutia kununua hii simu

Bei ya Tecno Spark 10 ya GB 128

Tecno ya ukubwa huu inauzwa kwa kiasi cha shilingi 350,000/= kwa maduka mengi Tanzania

Ukubwa wa memori na bei yake inamaanisha ni simu ya bei nafuu

Maana simu nyingi zenye GB 128 huuzwa kwa zaidi ya laki nne

Japo bei kubwa husababishwa na sifa zingine nzuri za ziada zinazoweza kukosekana kwenye tekno hii

Fuatilia sifa zake uelewe kiundani kuhusu spark 10

Sifa za Tecno Spark 10

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – 
  • Core Zenye nguvu(2) –
  • Core Za kawaida(6) –
  • GPU-
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 13
  • HIOS 12
Memori 128GB, na RAM 8GB
Kamera Kamera MBILI

  1. 50MP,PDAF(wide)
Muundo Urefu-6.6inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 350,000/=

Upi ubora wa simu ya Tecno Spark 10

Simu ina betri kubwa hivyo kuna uhakika wa kuitumia muda mrefu

Kioo chake kina refresh rate kubwa

tecno spark 10 summary

Inakuja na RAM kubwa na memori ya kutosheleza kiasi

Spark 10 inatumia toleo jipya la android 13 kama ilivyo kwa simu ya samsung galaxy 23 plus

Vitu vingine ni vya kawaida sana ukizingatia ni simu ya bei ndogo

Uwezo wa Network

Hii simu ina uwezo wa kutumia mtandao wa 4G na 3G bila kusahau 2G

Haina teknoljia mpya ya 5G

tecno spark 10 network

Kutokana na kutoainishwa na aina ya processor simu inayotumia, ni ngumu kuelezea kasi ya kiwango cha juu ya 4G YAKE

Kwa maana si rahisi kufahamu aina ya LTE kama hujui chip iliyomo ndani ya simu

Kikubwa ni  kuwa utaweza kutumia intaneti ya 4G ya mtandao wowote kwa sababu simu ina masafa yanayotumika na mitandao ya simu hapa Tanzania

Ubora wa kioo cha Tecno Spark 10

Tecno Spark 10 ina kioo cha kawaida aina IPS LCD

Hivyo simu ikipasuka bei ya kioo haitokugharimu sana

Ila ubora wa vioo vya IPS LCD sio mkubwa katika uonyeshaji wa rangi ukilinganisha na vioo vya AMOLED kama kilichopo kwenye simu ya Samsung Galaxy A54

Ukizingatia resolution ya kioo cha tecno spark 10 ni ndogo ambayo ni 720 x 1612 pixels

Ila spark 10 ina refresh rate inayofika mpaka 90Hz

Video chini inaonyesha utofauti wa refresh rate ya 60Hz, 90Hz na 120Hz

https://www.youtube.com/watch?v=IW8VWZJOGEE

Hii inamaanisha simu inakuwa fasta wakati wa kutachi, na mnato(animation) za kuvutia

Na refresh rate kubwa huwa inasaidia sana magemu kuchezeka vizuri

Vitu vingine vinavyopendezesha kioo simu haina

Nguvu ya processor

Tecno hawajaainisha chip simu inayotumia hata ukitembelea kurasa rasmi.

kurasa rasmi  ya tecno:

Ila sifa zilizoorodheshwa kwenye jedwari zinaonyesha wazi kuwa simu ina processor yenye nguvu ndogo

Hasa ukiangalia kiasi cha resolution kilichopo kwenye kioo

Mara nyingi kampuni za simu huweka resolution kubwa iwapo chip ikiwa na nguvu ya kutosha

Kivyovyote vile, spark 10 ni simu inayomlenga mtumiaji mwenye matumizi ya kawaida, anayependa simu inayokaa na chaji muda mrefu

Uwezo wa betri na chaji

Hii simu inakuja na betri ya ukubwa wa 5000mAh

Ukubwa huu wa betri simu inaweza kukaa na chaji kwa zaidi ya masaa 12 ikiwa kwenye intaneti

Ikizingatiwa inatumia kioo cha kawaida ambacho kinatumia umeme kidogo

Chaji yake ina kasi ya wastani ambayo ni wati 18

Ni spidi inayoweza kufanya betri kujaa kwa muda mrefu

Ukubwa na aina ya memori

Tecno spark 10 ipo ya aina moja tu upande wa memori

Memori yake ina ukubwa wa 128GB na RAM GB 8

Ni kiasi kinachoweza kutosheleza kuhifadhi mafaili mengi

Hata kama simu imejaa utaweza kuongeza memori kwa kuweka memori kadi

Ni tofauti na simu za siku hizi nyingi kama iPhone 14 Pro Max ambazo huondoa sehemu ya memori kadi

Uimara wa bodi ya Tecno Spark 10

Upande wa nyuma simu imewekewa kioo lakini sio cha gorilla

Kioo kinasaidia gamba ;a nyuma kutochunika kwa urahisi tofauti na simu zenye plastiki

tecno spark 10 body

Kwa mbele haina screen protekta ya kioo

Kiusalama zaidi itakulazimu kununua kava ya na pia protekta

Urefu wa simu ni inchi 6.6, kwa wapenda simu ndefu hili pia ni chagua sahihi

Ubora wa kamera

Mfumo wa kamera wa Tecno Spark 10 sio wa kuvutia sana

Fuatilia: simu zenye kamera nzuri za bei ndogo, uone utofauti

Ukianza upande wa kamera za nyuma kuna kamera mbili pekee

Kamera moja kubwa ina megapixel 50 na inatumia ulengaji wa PDAF

tecno spark 10 camera

PDAF huwa inaifanya simu itambue na kukilenga kitu kinachopigwa picha kutokana na muelekeo wa kamera

Kasi yake si kubwa kama zile zenye dual pixel pdaf hasa kwa vitu vinavyotembea

Kamera ya pili haijulikani ina lenzi ya aina gani, ni ngumu kuielezea

Upande wa selfie(kamera ya mbele) ipo moja tu yenye megapixel 8

megapixel 8 sio mbaya lakini hii kamera haina PDAF

Kamera zake zinarekodi video za full hd pekee yake na hakuna OIS

Hivyo kama unarekodi huku ukiwa unatembea utahitajika kutuliza mkono

Ubora wa Software

Simu inakuja na Android 13 ikiwa inatumia mfumo wa HiOS 12 kutoka tecno

HiOS 12 inatoa uwezo wa kuongeza kiwango cha RAM ya simu

Mfumo wa android huwa unahitaji kiwango kikubwa cha RAM

Na pia kuna apps zinakula memori kubwa ya ram unapozifungua

RAM ya GB 8 ni kubwa ila unapokuwa na apps nyingi zinazohitaji memori kubwa zinasababisha memori kujaa

Kujaa kwa memori kunaweza kupunguza utendaji wa simu na mwishowe ukajikuta simu inakuwa nzito

Hivyo kuongeza ram kunasaidia kiasi

Yapi Madhaifu ya Tecno Spark 10

Tecno Spark 10 simu ya daraja la chini hivyo changamoto ni nyingi ikitegemeana na aina ya matumizi

Mfumo wa kamera sio mzuri kiujumla

Chaji yake haipeleke kwa kasi kubwa na kwa viwango vya kisasa

Kasi ya chaji ya simu za siku hizi ni wati 25

Kioo inatumia teknolojia ya IPS LCD huku ikiwa na resolution ndogo

Simu haina teknolojia mpya ya mawasiliano ya 5G ikizingatiwa baadhi ya mitandao wameanza kuweka 5G nchini

Neno la Mwisho

Tecno Spark 10 ni tecno ya bei ndogo yenye baadhi ya sifa nzuri

Kwa mtumiaji anaepedna simu inayokaaa na chaji tu na kioo chenye uitikaji wa haraka, hili ni chaguo sahihi

Iwapo sifa zilizopo kwenye hii simu hazijakuvutia utalazimika kutafuta mbadala

Na mbadala maana yake itakulazimu kuongeza bajeti ya simu kwa sababu kitu bora huwa kinahitaji bajeti ya uhakika

Maoni 25 kuhusu “Bei ya Tecno Spark 10 na Sifa Zake

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

display

[VIDEO]: Simu za tecno zenye kamera nzuri zaidi

Tazama ubora wa picha zilizopigwa na simu za Tecno Camon 30, Camon 30 Premier, camon 20 premier na nyininezo

tecno camon premier 30

Ubora wa simu za Tecno Camon 30 na bei zake(Pro, Premier)

Tangu mwezi wa nne kampuni ya walitoa matoleo ya Tecno Camon 30 Matoleo ya Camon 30 yapo matatu ambayo ni ya daraja la kati yaani mid range Ubora wa kiujumla […]

tecno camon 30 thumb

Bei ya Tecno Camon 30 Pro na Sifa Muhimu

Simu ya Tecno Camon 30 Pro ilitangazwa mwezi februari ila imetoka rasmi mwezi wa nne 2024 Ni simu ya daraja la kati(midrange) hivyo bei yake sio sawa na Tecno matoleo […]

tecno camon 30 premier thumbnail

Bei ya Tecno Camon 30 Premier 5G na Sifa zake muhimu

Kwenye matoleo bora ya simu kutoka Tecno, matoleo ya Tecno Camon huja na ubora katika vipengele vingi Hata bei za matoleo ya Camon huzizidi bei za Tecno Spark na Tecno […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company