Simu ya infinix hot 12 ni simu ya android ambayo imetoka mwezi april mwaka 2022
Bei ya infinx hot 12 inaanzia shilingi laki nne kwa maduka mengi Tanzania
Bei yake ni kubwa ukilinganisha na bei ya simu ya infinix hot 11
Ila ukitazama vitu vinavyochangia simu kuwa na bei kubwa inafanya Hot 12 kuwa na bei kubwa kuliko uwezo
Pitia hapa kufahamu vitu vinavyofanya simu kuwa ghari na nzuri
Hata hivyo simu hii inaweza kukuvutia kwa kutazama bei yake kwa kuangalia ukubwa wa memori na sifa zake zote.
Bei ya Infinix Hot 12 ya GB 128
Bei ya infinix hot 12 yenye ram ya GB 6 na memori ya GB 128 ni shilingi 415,000/= kwa baadhi ya maduka Kariakoo
Simu ina baadhi ya sifa zinazoizidi simu ya Infinix Hot 12i.
Kitu kinachoifanya hot 12i kuwa na bei ndogo kuliko Hot 12 kwa mwaka huu 2022
Ifuatilie kila nyanja ya hii infinix kwenye jedwari lifuatalo linaloelezea ubora wake
Sifa za Infinix Hot 12
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | 128GB na RAM 8GB,6GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.82inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 420,000/= |
Upi ubora wa Infinix Hot 12
Ubora mkubwa wa infinix hot 12 ni kuwa na memori kubwa
Memori ambayo inaiwezesha simu kuhifadhi app nyingi na mafaili ya kutosha
Lakini pia simu ina ukaaji mkubwa wa chaji
Kwa sababu ina betri lenye ujazo mkubwa
Pia simu ina upelekaji wa chaji wa wastani
Vitu vingine vina ubora wa wastani ama wa chiniĀ kama utakavyoona mbeleni
Uwezo wa Network
Hot 12 inasapoti mtando wa 4G lakini haina 5G
Aina ya 4g simu inayotumia ni LTE Cat 7
Spidi ya kudownload kwa simu ya LTE Cat 7 inafikia 300Mbps
Japokuwa si rahisi kupata mtandao wa simu unaokupa spidi hii hapa nchini
Uzuri ni kuwa simu ina masafa ya mtandao wa 4G yapatayo 12
Yakiwemo yanayotumika na mitandao ya simu Tanzania
Hivyo intaneti ya 4G inakubali kwa laini zote za simu
Ubora wa kioo cha Infinix Hot 12
Kioo cha infinix hot 12 ni cha aina IPS LCD chenye resolution ndogo
Resoltion ya kioo chake ni 720 x 1600 pixels
Pia unagavu si mkubwa sana kitu kichofanya simu kutoonyesha vizuri ukiwa unaitumia juani
Lakini kioo cha hii simu ni chepesi wakati wa kutachi
Kwa sababu kina refresh rate inayofikia 90Hz
Refresh ya ukubwa inafanya screen kwenda haraka ukiwa unatafuta majina ya kwenye simu au ukiwa unasoma kitabu
Kiujumla kioo cha hot 12 si kizuri ukilinganisha na simu ya infinix note 11
Kioo cha infinix note 11 ni cha Amoled na resolution yake ni kubwa
Nguvu ya processor MediaTek Helio G85
Infinix hot 12 inatumia processor ya mediatek helio g85 katika kufanya kazi zake zote
Helio G85 ni processor ya simu yenye uwezo wa kati
Inaweza kucheza gemu nyingi ila zile gemu kubwa za simu inacheza resolution za chini na kwa FPS chache
Kwa mfano gemu ya Fortnite inacheza kwa 21 FPS na kwa resolution ndogo
Hivyo kuna uwezekano simu ikawa inapata moto sana kama ukicheza gemu kila wakati
Hii ina sabababishwa na core kubwa za Helio G85 kuwa ni aina ya Cortex A75 na sio Cortex A77 auĀ Cortex A78
Cortex A75 spidi yake ya juu kabisa 2.0 GHz (mizunguko bilioni mbili kwa sekunde)
Na kila mzunguko unaweza kufanya kazi tatu
Kitu kinachofanya processor kuwa na nguvu ya wastani
Na ndio maana app ya kupima nguvu ya chip, GeekBench inaipa alama 358 kwenye core moja
Wakati Helio G96 inapewa alama 541 kwa core moja
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Infinix Hot 12 ina ukubwa wa 5000 mAh na ni aina ya Li-Po
Ukubwa huo wa betri unaifanya infinix kukaa na chaji kwa wastani wa masaa yanayozidi 14 simu ikiwa kwenye intaneti
Simu nyingi zenye betri la 5000 mAh hutunza chaji
Chaji yake inapeleka umeme wa wasatani upatao wati 18
Kiasi hicho cha umeme kinafanya simu kuchelwa kujaa kwa sababu betri yake ni kubwa
Hivyo inaweza kuchukua masaa zaidi ya matatu simu kujaa kwa 100%
Ukubwa na aina ya memori
Kuna toleo moja tu la Hot 12 upande wa memori
Ni toleo ambalo lina ukubwa wa GB 128 na RAM y a GB 6
Infinix hawajaainisha aina ya memori
Lakini chip ya Helio G85 inasapoti memori aina ya eMMC 5.1 na UFS 2.1
Kama infinix hot 12 inatumia UFS 2.1 basi utendaji wake ni mkubwa kiasi
Uimara wa bodi ya Infinix Hot 12
Bodi ya simu ya infinix hot 12 ni ndefu na nzito kiasi
Na pia ni bodi iliyoundwa kwa plastiki
Bodi za plastiki zina kawaida ya kuchunika rangi kadri inavyotumika muda mrefu
Kuna ulazima wa kununua kava ya simu na pia kuweka screen protector
Kwa sababu simu haitumii kioo cha gorilla
Vioo vya gorilla huwa ni vigumu kuchunika na kuvunjika hasa Gorilla 5
Ubora wa kamera
Infinix Hot 12 ni infinix macho matatu yenye kamera zenye ubora wa chini
Ubora wake wa kamera unapitwa mbali sana na infinix zero x pro au Redmi Note 10
Kamera zake zina teknolojia ya ulengaji ya kawaida aina ya AF
Autofocus ya AF inalenga vitu kwa taratibu na utoaji wa picha kwenye mwanga mdogo ni wa chini
Kibaya kuhusu kamera zingine ni kuwa na resolution ndogo za 2MP na nyingine ni QVGA
Kamera ya QVGA (Quarter Video Graphics Array) ni teknolojia ya kizamani
Kwani ni kamera inayozalisha picha ya upana wa 320p na urefu wa 240p
Ndio maana kamera za hot 12 haziwezi kurekodi video za 4K
Pitia hapa kujua, maana ya 4K na umuhimu wake
Kiujumla simu ya infinix hot 12 haina kamera nzuri
Ubora wa Software
Infinix hot 11 inakuja na mfumo endeshi wa Android 12 unaotumia sofatware ya XOS 10.6
XOS 10.6 ni mfumo mpya kabisa ambao una maboresho kadhaa
Moja ya kitu cha kuvutia kuhusu XOS 10.6 ni kukupa uwezo wa kurudisha picha ulizozifuta kwenye simu
Infinix wanadai mfumo mpya una kitu kinaitwa AI Gallery
AI Gallery unaweza kurudisha picha zote zilizofutwa kwa dakika 30
Ila kitu kibaya kuhusu XOS ni kuwa na matangazo mengi yanayotokea mara kwa mara
Haya matangazo huwa yanakera
Yapi Madhaifu ya Infinix Hot 12
Infinix hot 12 ni simu ya daraja la chini hivyo mapungufu yapo mengi
Kwanza bei yake inaweza kununua simu ya daraja la kati ya Redmi Note 10 Pro
Wakati huo Redmi Note 10 Pro inaizidi infinix kwenye nyanja nyingi
Mfumo wa kamera wa hot 12 hauna OIS wala PDAF
Lakini pia simu inakosa ulinzi wa kulinda simu kutopitisha maji
Kioo chake kina resolution ndogo hivyo uoneshaji wa picha si wa kuvutia
Neno la Mwisho
Kama unapenda simu inayohifadhi vitu vingi basi infinix hot 12 inafaa sana
Ila kama unapenda simu yenye utendaji mkubwa wa kamera na kila kitu kuna machaguo mengi mazuri
Hayo machaguo yana bei inayoendana na bei ya infinix hot 12
Maoni 5 kuhusu “Bei ya Simu ya Infinix Hot 12 na Sifa Zake Muhimu”
Infinix hot12i inakaa na chaji siku ngapi?
masaa 15 yana fika betri yake ni 5000mah, na haina vitu vinavyokula chaji sana ila inategemea na matumizi
Mnapatikana sehemu gani tanzania? Naomba kujua bei halisi ya hot 12 toka kwenu nimeipenda hiyo sim asante.
Nahitaji simu ya infinix hot 12 price in india yenye macho matano 5 na iwe ngumu haimalizi haraka chaji
Nahitaji simu