SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu ya Tecno Spark 8C na Sifa Zake Zote

Bei Nafuu

Sihaba Mikole

June 26, 2022

Katika simu nyingi zilizozinduliwa na Tecno mwaka 2022 mojawapo ni Tecno Spark 8C

Hii ni simujanja inayoingia moja kwa moja kwenye kundi la daraja la chini

simu ya tecno spark 8c muonekano

Kitu kinachofanya bei ya Tecno Spark 8C kuwa chini ya laki tatu

Bei ndogo inasababishwa na simu kuwa na sifa za chini NYINGI ukilinganisha na simu zingine kama Redmi 10C

Bei ya Tecno Spark 8C ya GB 64

Kwa maduka mengi ya simu dar es salaam wanaiuza simu kwa bei ya 240,000/=

Sifa zake zinazidiwa kwa kiasi kikubwa na iPhone 6 Plus ya mwaka 2014

simu ya tecno spark 8c summary

Itazame: ubora na bei ya iPhone 6 Plus 2022

Hivyo spark ilifaa iuzwe chini ya bei ya sasa kwa kulinganisha na sifa za iphone 6

Fuatailia sifa za tecno hii kwenye jedwari

Sifa za Simu za Tecno Spark 8C

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • Hakuna Taarifa
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 11 (Go Edition)
  • HiOS 7.6
Memori eMMC 5.1, 64GB, na RAM 2GB,3GB,4GB
Kamera Kamera mbili

  1. 13MP,(wide)
  2. QVGA
Muundo Urefu-6.6inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
Bei ya simu(TSH) 245,000/=

Ni upi ubora wa Tecno Spark 8C

Hii ni simu ya daraja la chini hivyo kuna ubora kwenye sehemu chache

Ubora mkubwa ni simu kuja na memori inayoweza kuchukua vitu vingi

Pia ni simu ambayo inakaa na chaji masaa mengi

Ikizingatiwa inatumia memori na processor inayotumia umeme mdogo

Kwenye nyanja zingine hakuna ubora mkubwa kama utakavyoona.

Uwezo wa Network

Hii ni tecno ya bei nafuu inayosapoti mtandao wa 4G

Tovuti rasmi ya Tecno haijainisha processor iliyotumika kwenye simu

Hivyo inakuwa ngumu kujua spidi ya juu na aina ya 4G iliyotumika

simu ya tecno spark 8c network

Ndio, 4G imegawanyika katika makundi mengi kulingana na kasi

Ufafanuzi wa 4G upo hapa: Aina za 4G na maana yake

Lakini pia kuna Spark 8C zinatengenezwa kwa ajili ya soko la India

Hivyo kuwa makini na aina ya masafa ya 4G kama yapo ya Tanzania

Ubora wa kioo cha Tecno Spark 8C

Karibu simu zote zinazouzwa chini ya laki tatu hutumia vioo vya IPS LCD

Hiki kioo kinaoonyesha picha vizuri zaidi kama resolution yake itakuwa kubwa

Ila Spark 8C ina resolution ndogo ya 720 x 1612 pixels

Kiufupi, ubora wa kioo wa ips lcd huwa unaachwa nyuma na vioo vya AMOLED katika uonyeshaji wa vitu kwa rangi halisi

Na kioo cha amoled kinakuwa bora zaidi kama kinawekewa teknolojia ya HDR10+ au Dolby Vision

Nguvu ya processor

Hakuna taarifa zinazoonyesha processor inayotumiwa na simu ya tecno spark 8C

Ila kwa kutazama aina ya memori simu inayotumia na bei ya simu inatosha kusema kuwa processor yake ina nguvu ndogo

Hata mfumo endeshi wa Android Go Edition unawekwa kwenye simu zenye nguvu ndogo ya kiutendaji

Mara nyingi memori za eMMC hutumiwa na chip ambazo hutumia nguvu ndogo katika kufanya kazi zake

Na hata memori upande wa RAM zinafafanua pia utendaji wa chini wa chip

Uwezo wa betri na chaji

Kutokana na simu kuwa na betri kubwa na chip inayotumia umeme mdogo inafanya simu kukaa na chaji muda mrefu.

Betri yake ukubwa ni 5000mAh

Pia hakuna taarifa zinazoanisha spidi ya kuchaji

Lakini bila shaka chaji yake itakuwa inapeleka umeme mdogo

Hivyo tarajia masaa mengi ya kuchaji mpaka simu ijae

Ukubwa na aina ya memori

Kuna matoleo matatu ya Tecno Spark 8C yanayotofautiana ukubwa wa RAM pekee

Kwani matoleo yote yana memori ya ukubwa wa GB 64

Kasoro moja iliyopo kwenye upande wa memori ni kitendo cha Tecno kutumia memori za eMMC 5.1

eMMC 5.1 husafirisha data kwa kasi ndogo

Kitu kinachoweza kuifanya simu kuwa nzito ikizingatiwa na RAM zake ni ndogo 2GB na 3GB

Uimara wa bodi ya Tecno Spark 8C

Simu imetengenezwa kwa bodi za plastiki

Si kitu cha kushangaza ikizangitiwa ni simu ya bei nafuu

simu ya tecno spark 8c bodi

Kwani simu inapotengenezwa kwa glassi hasa za gorilla huongeza gharama inayopelekea simu kuuzwa bei ya juu

Kutokana na hilo itakulazimu utafute kava inayoendana na kimo cha spark 8C ambacho ni inchi 6.7

Na vizuri pia ukaweka screen protector kama utainunua hii simu

Ubora wa kamera

Tecno spark 8C ina kamera mbili tu ambazo ubora wake ni mdogo

Kamera kubwa ina ukubwa wa 13MP

Lakini haina teknolojia yoyote ya ulengaji ikiwemo PDAF

simu ya tecno spark 8c kamera

Hivyo ufanisi wa kupiga picha si mkubwa

Kamera ya pili ni aina ya QVGA (320 x 240 pixels)

QVGA ni kamera za kizamani ambazo huwa na resolution ndogo

Kitu kinachoifanya kamera kutoa picha mbaya

Kwenye kurekodi video, simu inarekodi video za full hd pekee kwa fremu 30 kwa sekunde

Ubora wa Software

Hii simu inakuja na Android 11 toleo la Go Editon

Go Editon ni aina ya mfumo endeshi ambao umetengenezwa kwa ajili ya simu zinazotumia processor zilizo na uwezo wa chini na RAM ndogo

simu ya tecno spark 8c software

Mfumo huo unasaidia kuongeza ufanisi wa simu kiutendaji

Bila hivyo tecno spark 8c ingekuwa ni nzito zaidi

Yapi Madhaifu ya Tecno Spark 8C

Simu Tecno Spark 8C ina madhaifu kwenye idara karibu zote

Hatutogusia kila kitu ila tutajikita kwenye udhaifu wa utendaji na kamera

Hii tecno haiwezi kurekodi video za 4K

Na inatumia memori ambazo kasi yake ya kusafirisha taarifa sio kubwa

Usafirishaji wa data taratibu unaifanya simu kufungua app taratibu

Neno la Mwisho

Hii simu inamfaa mtu ambaye hapendi mambo mengi

Kwa mtumiaji anayetembelea zaidi mitandao ya kijamii na kupiga simu au sms Spark 8C inaweza mfanikishia mahitaji hayo

Na ikizingatiwa bei ya Tecno Spark 8C inahimilika kwa Watanzania wengi

Ila zipo simu za bei nafuu nzuri zaidi ya hii kwa bei rahisi.

Pitia baadhi ya simujanja za pixel: simu nzuri za pixels zikiwezo zile za chini ya laki nneĀ 

Maoni 14 kuhusu “Bei ya Simu ya Tecno Spark 8C na Sifa Zake Zote

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

display

[VIDEO]: Simu za tecno zenye kamera nzuri zaidi

Tazama ubora wa picha zilizopigwa na simu za Tecno Camon 30, Camon 30 Premier, camon 20 premier na nyininezo

tecno camon premier 30

Ubora wa simu za Tecno Camon 30 na bei zake(Pro, Premier)

Tangu mwezi wa nne kampuni ya walitoa matoleo ya Tecno Camon 30 Matoleo ya Camon 30 yapo matatu ambayo ni ya daraja la kati yaani mid range Ubora wa kiujumla […]

tecno camon 30 thumb

Bei ya Tecno Camon 30 Pro na Sifa Muhimu

Simu ya Tecno Camon 30 Pro ilitangazwa mwezi februari ila imetoka rasmi mwezi wa nne 2024 Ni simu ya daraja la kati(midrange) hivyo bei yake sio sawa na Tecno matoleo […]

tecno camon 30 premier thumbnail

Bei ya Tecno Camon 30 Premier 5G na Sifa zake muhimu

Kwenye matoleo bora ya simu kutoka Tecno, matoleo ya Tecno Camon huja na ubora katika vipengele vingi Hata bei za matoleo ya Camon huzizidi bei za Tecno Spark na Tecno […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company