SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Samsung Galaxy S21 Ultra 5G na Sifa Zake Muhimu (2022)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

May 4, 2022

Simu ya Samsung galaxy S21 ultra 5g ni samsung ya mwaka 2021 ambayo uwezo wake unazizidi simu nyingi mpya za android

Kwenye hii post utaweza kuelewa sababu ya bei ya samsung galaxy s21 ultra kuwa kubwa zaidi ya milioni mbili

samsung galaxy s21 ultra

Utaweza kujua sifa kubwa muhimu ambazo zinaifanya galaxy s21 kuzipita simu nyingi za 2022

Lakini kabla ya yote ni vizuri ukaijua bei yake kwa mikoa ya Tanzania hasa Dar Es Salaam

Bei ya Samsung Galaxy S21 Ultra Tanzania

Bei halisi mpya ya samsung galaxy s21 ultra 5g duniani ni shilingi 1,716,959.84/=

Hii ni bei ya galaxy ya GB 128 na RAM ya GB 12

Ila kwa maduka ya simu kariakoo samsung galaxy ya GB 256 na RAM ya GB 12 ni shilingi 2,700,000/=

Kwa baadhi ya watu huwa wanashangaa kwa nini simu inauzwa zaidi ya milioni

Ukitaka kuzijua sababu basi inabidi uzielewa sifa za galaxy s21 ultra 5g

Sifa za simu ya Samsung Galaxy S21 Ultra

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Exynos 2100
  • Core Zenye nguvu sana(1) – 1×2.9 GHz Cortex-X1
  • Core zenye nguvu (3)- 3×2.80 GHz Cortex-A78
  • Core Za kawaida(4) – 4×2.2 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G78 MP14
Display(Kioo) Dynamic AMOLED 2X, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 11
  • One UI 3.1
Memori UFS 3.1, 256GB,128GB,512GB na RAM 12GB,16GB
Kamera Kamera nne

  1. 108MP,PDAF, Laser AF(wide)
  2. 10MP dual pixel pdaf(periscope telephoto)
  3. 10MP(telephoto)
  4. 12MP dual pixel pdaf(ultrawide)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-25W
Bei ya simu(TSH) 1,716,959.84/=

Upi ubora wa samsung galaxy s21 ultra 5g

Samsung galaxy s21 ultra ina ubora kwenye sehemu karibu zote

Lakini kubwa ni utendaji mkubwa wa simu

samsung galaxy s21 ultra summary

Na uwezo wake mzuri wa kupiga piacha nzuri nyakati za usiku na mchana

Samsung galaxy s21 ultra haipitishi maji

Lakini pia ni samsung ya daraja la juu inayokaa na chaji masaa mengi

Uwezo wa Network

Galaxy s21 ultra ni simu ya 5G ambayo inakubali pia 5G aina ya mmWave

mmWave ni aina ya 5G yenye kasi na inayosafirisha data katika masafa ya 30GHz mpaka 300GHz

Ina masafa mengi ya 4G

Na 4g yake ni aina ya LTE Cat 24

LTE Cat 24 spidi yake ya juu kabisa ya kudownload ni 3000Mbps

Inachukua sekunde tisa tu kudownload faili lote la ukubwa wa 1200MB

Ila ni ngumu kuipata spidi hii Tanzania

Ubora wa kioo cha samsung galaxy s21 ultra 5g

Kioo cha samsung s21 uktra 5g ni aina ya dynamic amoled 2x

Dynamic amoled 2x ina rangi nyingi zaidi kuliko super amoled

Pitia kurasa huu kuona utofauti wa amoled na dynamic amoled

Dynamic inaonyesha kwa rangi zilizo kolea zaidi

Ubora wake unaongezwa na kutumika kwa HDR10+ na refresh rate ya 120Hz

Hivyo ubora wa kioo kuonyesha picha ni mzuri kwa kiasi kikubwa

Na pia kioo kina uangavu unaofikia 1500 nits hivyo kwenye jua utaweza kuona vitu kabisa

Nguvu ya processor Exynos 2100

Simu ya samsung galaxy s21 inatumia chip ya Exynos 2100

Exynos 2100 ni processor ya simu yenye core nane

Kwenye app za kupima nguvu ya processor yaani geekbench exynos ina alama nyingi zinazofikia 1082

Kiuwezo inazidiwa na chip ya iphone 13 pro max apple a15 bionic

Ni chip ambayo imegawanyika mara tatu amapo kiuwezo zinatofautiana

Uwezo wa core kubwa

Kuna core nne kubwa zipatazo nne

Core yenye nguvu sana ipo monj na inatumia muundo wa Cortex X1

Na core zenye nguvu kubwa kiasi zipo tatu na zinatumia muundo wa Cortex-A78

Cortex X1 na Cortex A78 zinaifanya simu kuweza kucheza gemu  kama la Call Duty Mobile kwa ubora wa ultra hd bila shida

Hizi ni core hutumika pale simu inapofanya kazi kubwa au nyingi kwa wakati mmoja

Uwezo wa core ndogo

Kuna jumla ya core ndogo zipatazo nne

Core hizi hutumia umeme mdogo na zina spidi isiyozidi 2.2 GHz

Muundo wake ni cortex a55 ambao kwa utunzaji wa chaji unazidiwa na muund wa Cortex A510 uliopo kwenye samsung galaxy s22

Uwezo wa betri na chaji

Samsung galaxy s21 ultra ni moja ya simu inayotunza chaji muda mrefu

Galaxy s21 ultra ina betri kubwa lenye ujazo wa 5000mAh

Kiasi kinachochelewa kuisha hata simu ikiwa imewasha data masaa mengi

Kwani simu inakaa na chaji masaa 15 ikiwa inatumia intaneti masaa yote mfululizo

Ina chaji inayojaza betri kwa spidi kubwa ya 25W

Kwa mujibu wa majaribio ya GSMArena, betri ya galaxy s21 ultra inajaa kwa 100% ndani ya dakika 71

Ukubwa na aina ya memori

Galaxy s21 ultra 5g inatumia memori zenye kasi kubwa kusafirisha data aina ya UFS 3.1

UFS 3.1 inaongeza uwezo wa simu kiutendaji

Na galaxy ipo za matoleo manne

Kuna ya ukubwa wa 128GB na ram ya 12GB

Kuna yenye memori ya 256GB na RAM ya 12GB

Nyingine ina memori ya 512GB na RAM ya 12GB

Na kubwa zaidi ina ujazo wa 512GB na RAM ya 16GB

Nafasi kubwa inakupa uwezo wa kuweka vitu vingi

Ram kubwa inaisaidia simu kufungua apps nyingi kwa urahisi

Uimara wa bodi ya samsung galaxy s21 ultra 5g

Simu zote za samsung za daraja juu huundwa kwa bodi imara na ngumu kupasuka

Galaxy s21 ultra imengenezwa kwa vioo vya Gorilla Glass Victus

Hivi ni vioo ambavyo vinaisadia simu kutopasuka hata ikiwa imeanguka kwa urefu wa mita mbili.

Tazama majaribio ya kuangusha simu ya samsung galaxy s21 ultra yanavyostahmili kupasuka

Pia kioo chake ni kigumu hata kuchubuka na mikwaruzo

Kiuhalsia ukiwa na galaxy s21 hutohitajika kununua kava ya simu

Ubora wa kamera

Samsung galaxy s21 ultra ina kamera nne.

Kamera mbili zinatumia teknoljia ya dual pixel pdaf kitu kinachofanya simu kupiga picha vizuri kwa sababu ya ulengaji wa haraka na uilio sahihi ukilinganisha na pdaf

Samsung inaweza kupiga kitu cha mbali kwa kutumia kamera yake aina ya Telephoto

Kamera yake ya periscope telephoto inaza kuzoom mara 10 bila kupoteza ubora wa picha na pixels

samsung galaxy s21 ultra camera

Galaxy pia inatoa picha kwa ubora wa juu wakati wa usiku na mchana

Yaani texture ya kamera yake inaonyesha kwa kiasi kikubwa kila kitu ambacho kimepigwa.

Angalia hapa, namna ya kutambua simu yenye kamera nzuri kiufasaha

Simu inaweza kurekodi video za 8K kwa kiwango cha 24fps

Video za 4k kwa kiwango cha 60fps na full hd kwa kiwango cha 240fps na  video za 720p kwa kiwaango cha 960fps

Ubora wa Software

Simu inakuja na android toleo la 11 lakini simu inakubali android 12

Na software ya One UI 3.1 inaweza kubadilishwa na kuwekewa One UI 4.1

Kwenye One UI 3.1 kuna ongezeko la vitu vingi ikiwemo sehemu ya inayoonyesha google discover

Google discover ni mfumo wa google unaonyesha habari za vitu ambavyo unapendelea kutafuta kutumia google

Kuielewa zaidi One UI pitia, one ui ya samsung

Yapi Madhaifu ya samsung galaxy s21 ultra 5g

Udhaifu mkubwa samsung galaxy s21 ultra ni kitendo cha kutokuweka dual pixel pdaf kwenye kamera kubwa

Pia ukaaji wa chaji unazidiwa na iphone 13 pro max yenye betri dogo ukilinganisha na samsung

Neno la Mwisho

Kama unatafuta orodha simu zinazoongoza kwa ubora duniani basi simu ya Samsung Galaxy S21 Ultra ipo

Hivyo kama unaweza kununua ni vizuri ukaimiliki hii simu ya mwaka 2021

Kwa sababu ina uwezo wa kupokeo matoleo mapya ya android kwa miaka mingi

Maoni 6 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy S21 Ultra 5G na Sifa Zake Muhimu (2022)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

samsung a06

[VIDEO]-ubora wa picha na kiutendaji wa Samsung Galaxy A06

Hii ni video inayokupa nafasi kushuhudia sifa za ziada za samsung galaxy a06 hasa upande wa kamera Kama hujui, Galaxy A06 NI simu mpya ya daraja la chini ambayo imetoka […]

No Featured Image

Simu Mpya za Samsung 2024 (za bei rahisi na ghari)

Kuna simu zaidi ya tisa zilizotengenezwa na kampuni ya Samsung kutoka Hapa kuna orodha ya simu kumi mpya za samsung ambazo zimetoka mwishoni mwa mwaka 2023 hadi mwaka 2024 Ni […]

Bei ya Samsung Galaxy A25 na Sifa zake

Simu ya Samsung Galaxy A25 ilitoka rasmi mnamo mwezi desemba 2023 Ni simu ya daraja ambayo bei yake kwa Tanzania ni shilingi laki saba (700,000/=), hii ikiwa ni bei ya […]

samsung galaxy a15 thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A15 na Sifa Muhimu

Mwezi wa desemba 2023 ni mwezi ambao Simu ya Samsung Galaxy A15 ilizinduliwa Ni simu ya daraja la kati ambayo ina vitu vichache vinavyopatikana kwenye samsung za bei kubwa Ndio […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company